Tafsiri ya Ibara Isemayo Dini ni ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tafsiri ya Ibara Isemayo Dini ni ya Mwenyezi Mungu na Nchi ni ya Wote.

Question

Katika ibara zilizoenea hivi sana kupitia vyombo vya habari ni ibara isemayo “Dini ni ya Mwenyezi Mungu na nchi ni ya wote”, na baadhi ya watu huiita ni kanuni ya lazima. Ni kwa upeo gani msemo huu ni sahihi kwa upande wa Sheria? Na upi uhusiano wa umoja wa kitaifa na kupenda nchi na Dini? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Neno dini katika lugha maana yake ni: Malipo, na dini pia maana yake ni: Hesabu, dini ina maana ya: Utiifu, dini kwa maana ya: Uislamu, dini pia ni: Desturi. Na katika Hadithi Mtume anasema: “Mtu mwenye akili ni yule mwenye kuihesabu nafsi yake na akafanya matendo yatakayomfaa baada ya kifo, na mtu mjinga ni mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake na kutarajia mema kwa Mwenyezi Mungu”. Amesema Abu Ubeid kwenye kauli yake Mtume ya kuihesabu nafsi yake kuna maana ya: kuidhalilisha na kuilazimisha. Na ikasemwa tena: ni mtu kuihesabu nafsi yake. Na katika Qur`ani: {Hakuweza kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme} [YOUSUF, 76]. Amesema Qatada: Katika hukumu ya umiliki. [Rejea kamusi ya Lisan Al-Arab, 13/170, Ch. Dar Sadir]
Miongoni mwa maana zake katika msamiati ni kuwa: Ni utaratibu wa Mwenyezi Mungu unawaongoza watu wenye akili kwa uchaguzi wao mzuri kuelekea kwenye heri – [Kitab Tuhfat Al-Muhtaj, 1/20, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Na neno nchi (taifa) katika maana ya lugha ni: Ni nyumba anayoishi mtu, nayo ni makazi ya mwanadamu na sehemu yake.
Wanachuoni wamefafanua maana ya taifa au nchi na vigawanyo vyake, hii ni kutokana na kufungamana kwa maana yake na masuala ya safari na Swala ya Ijumaa, hivyo wakagawa nchi kwenye nchi asili, nchi ya muda na nchi ya makazi, anasema Imam Al-Sarkhasiy: “Jibu ni kuwa nchi au taifa kuna aina tatu, nchi asili: Nayo ikiwa mtu atazaliwa kwenye nchi hiyo au kukulia humo, basi anakuwa ni mkazi wa hiyo nchi, aina ya pili: Ni nchi ya muda: Nayo ni kunuia msafiri kuishi nchini humo kwa muda wa siku kumi na tano hali ya kuwa yupo mbali na nchi yake asili, na aina ya tatu, nchi ya kuishi: Nayo ni msafiri kunuia kuishi katika chini hiyo kwa siku kumi na tano naye akiwa karibu na nchi yake asili [Kitabu Al-Mabsout cha Al-Sarkhasiy, 2/252 Ch. Dar Al-Maarifa].
Nchi katika zama zetu hizi hukusudiwa nchi ya kisasa yenye mipaka yake kijiografia yenye kufahamika, na kukusanya ndani yake wananchi wa nchi hiyo, na huitwa uzalendo wa utaifa. Na kila mwenye kubeba utaifa wa nchi hiyo basi huyo anazingatiwa ni mwananchi wake ni sawa awe anaishi humo au nje ya nchi hiyo.
Ibara ya “Dini ya Mwenyezi Mungu na nchi ya wote” inakadiriwa maana nyingi miongoni mwa maana hizo ni pamoja na ile yenye kukubalika Kisheria, na maana nyingine isiyokubalika Kisheria, miongoni mwa maana isiyokubalika Kisheria: Ni kukusudia msemaji wake kuwa Dini haina uhusiano na mfumo wa nchi, na hilo ndilo linalolinganiwa na watu wa mfumo wa Kisiasa usiotambua Duni.
Ikiwa atakusudia msemaji wa ibara hii kutenganisha Dini na mfumo wa kimaadili na kijamii na sheria ya nchi, na kuwa na uhusiano wa mtu na Mola wake, basi maana hii ni yenye kupingwa na Sheria, kwa sababu Mwenyezi Mungu Ameteremsha Kitabu na kutuma Mitume ili kudhihirisha Dini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia}.
Na Madhehebu yanayopingana hivyo ni madhehebu batili, kwa sababu yanalingania kujiepusha na utekelezaji wa amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu na Kuacha makatazo yake, na jambo hili ni katika Madhambi makubwa kwani ndani yake kuna kujiengua katika masharti ya Uislamu na misingi yake na kunapelekea uharibifu mkubwa wa mjengeko wa jamii hii na mshikamano wake.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu} [AN NAHL, 89].
Usilamu umewekewa Sheria na Mwenyezi Mungu Mtukufu haukuacha upande wa maisha isipokuwa ameuwekea Sheria na maelekezo, kwani Uislamu umekusanya pande zote za maisha, kiroho na kimwili, iwe ni kwa mtu mmoja mmoja au kwa mjumuiko wote wa kijamii.
Qur`ani Tukufu ambayo inasema: {Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu} [AL BAQARAH, 184]. Ni maneno hayo hayo ameyasema ndani ya sura hiyo hiyo: {Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa} [AL BAQARAH, 178] Nayo Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema ndani ya Sura hiyo: {Mmeandikiwa mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza} [AL BAQARAH, 180]. Na Anasema kwenye Sura hiyo tena: {Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachosha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu} [AL BAQARAH, 216]. Qur`ani imeelezea ulazima wa mambo haya yote kwa ibara moja: {Imelazimishwa kwenu}.
Mambo haya yote ni katika yaliyolazimishwa kwa Waumini kwa maana wamelazimishwa kufunga ikiwa funga ni katika mambo ya ibada, na kisasi ni katika mfumo wa kanuni ya uhalifu wa jinai, na usia kama unavyoitwa ni hali za mtu binafsi, na kupigana vita katika uhusiano wa kimataifa.
Sheria ya Kiislamu ni yenye kuhukumu matendo yote ya watu wanaolazimika kutekeleza, hakiepukani kitendo wala tukio katika matukio isipokuwa yana hukumu katika hukumu tano za Sheria (lazima, kupendelewa, uharamu, kuchukiza na kufaa).
Imam Al-Haramain amesema katika kitabu cha: [Ghiyath Al-Umam, Uk. 310, Ch. Dar Al-Daawa]:
“Na kinachotegemewa ni kwamba haitarajiwi kutokea kitakachotokea pamoja na kuendelea kubakia Sheria ikionekana kwa wanaoibeba isipokuwa katika Sheria hiyo kuna mwenye kushikamana na Hukumu zake Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Sheria hiyo”.
Mwenendo wa Mtume S.A.W. wote ulikuwa katika mambo mbalimbali ya maisha, kuanzia mambo ya uchumi, siasa, jamii, na Ibada na mengine mengi katika mambo ya maisha.
Madhehebu yoyote yanayolingania mbali na Kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na Sunna za Mtume wake Muhammad S.A.W, hayo ni madhehebu batili na wala haifai kwa Muislamu kufuata madhehebu hayo au kuyahamasisha au hata kuyalingania.
Ikiwa mzungumzaji wa ibara hii anataka kusema kuwa kutofautiana kwa Dini yao watu wa taifa moja hakutakiwi kuathiri umoja wa kitaifa, na kukutana watu katika masilahi ya taifa, basi maana hii inakuwa nzuri, kwa sababu nidhamu ya Kiislamu haimaanishi kuwa haiwazingatii wasiokuwa Waislamu ndani ya taifa moja, au kuwa inazuia moja kati ya haki za mwananchi yeyote, au ni nidhamu inayomlazimisha zaidi ya wajibu wake bali Uislamu upo pamoja na sera inayolingania umoja wa kitaifa na kutoa wito katika hilo siku zote, na unawaangalia watu wote kwa kuwazingatia kuwa ni jamii moja, kwani Amesema Mola Mtukufu: {Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Kiongozi} [AL BAQARAH, 30].
Wamadamu wote ni familia moja inayotokana na baba mmoja, na watu wote ni warithi wa uongozi huo katika ujenzi wa ardhi na kueneza usalama na amani. Qur`ani Tukufu imeweka misingi ya wazi ya familia hiyo ya wanadamu misingi ambayo inasimama juu ya ukweli wa wazi nao ni asili ya binadamu ni moja. Amesema Mola: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwake mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni} [AN NISAA, 01].
Watu wote katika mtazamo wa Uislamu ni watoto wa familia hiyo ya ubinadamu, na wote wana haki ya kuishi na kuheshimika, bila yoyote kubaguliwa au kutengwa.
Binadamu anaheshimika kwa mujibu wa mtazamo wa Qur`ani Tukufu, pasina kuangalia dini yake au utaifa wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} [AL ISRAA, 70].
Katika tofauti za watu kwa rangi zao, utaifa wao, lugha zao na dini zao ni alama katika alama zinazoonesha ukubwa na uwezo wa Mtukufu Muumba. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi} [AR RUUM, 22].
Na Muislamu katiba yake inamwongoza kwenye mahusiano mazuri na yule asiyekuwa Muislamu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL MUMTAHINAH, 08]
Ambapo Aya inalingania ushirikiano wema na usawa pamoja na ndugu zetu wananchi wenzetu hata wakiwa na dini yoyote ile.
Jambo la kupenda nchi ni katika Imani, na limekuwa ni lenye kuzingatiwa kwa Mtume S.A.W. pamoja na Masahaba zake, pamoja na kuwa nchi yao ilikuwa ni nchi ya washirikina ambapo Waislamu walionja humo aina mbalimbali za adhabu, ndipo Sunna za Mtume pamoja na historia yake vimeelezea kauli yake Mtume S.A.W. pale alipokuwa anahama kutoka Makka maneno ambayo yamepokelewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake. Amesema Mtume S.A.W.: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika mji wa Makkah ni ardhi iliyobora kwa Mwenyezi Mungu na ni ardhi yenye kupendwa sana na Mwenyezi Mungu lau mimi nisingetolewa kwako basi nisingetoka” .
Na katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari pamoja na Imamu Muslimu kuwa, Masahaba wa Mtume pindi walipofika Mji wa Madina baadhi yao walipatwa na homa na walikuwa wanamapenzi na Mji wa Makka na walipenda warudi, wakati huo Mtume S.A.W. ndipo aliposema: “Ewe Mwenyezi Mungu tupe mapenzi ya kuupenda Mji wa Madinah kama vile tunavyoupenda Mji wa Makkah au zaidi ya hapo, Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika mshikamano wetu na turekebishie pamoja na kuondoa madhara yake”.
Pindi Mtume alipotulia kimaisha pamoja na Masahaba zake Radhi za Mola ziwe kwao ndani ya Mji wa Madina na kuwa Mji huo ndio makazi yao, Mtume S.A.W. aliupenda Mji wa Madina na baadhi ya wanachuoni wakatoa dalili kuwa kupenda nchi ni katika Imani lakini pia ni katika mwenendo wa Mtume S.A.W. na mapenzi yake kwa Mji wa Madina.
Amesema Ibn Hajar kauli yake katika mlango unaoelezea katika haraka ya ngamia wake pale alipofika Madina ... kisha ikaendelea Hadithi na akasema: Hakika Mtume S.A.W. alikuwa pindi anapofika safari, basi huangalia vigingi vya Madina na kumfunga ngamia wake, na akiwa juu ya mnyama humuendesha kutokana na upendo wake mpaka pale aliposema. Katika Hadithi hii kuna dalili ya ubora wa Mji wa Madina na uhalali wa kupenda nchi. Kitabu cha; [Fat-h Al-Bariy cha Ibn Hajar Al-Asqalaniy, 3/621, Ch. Dar Al-Maarifa]
Akasema sehemu nyingine kauli yake kwenye mlango wa kufanya haraka kwenye kutembea- kwa maana wakati wa kurudi nchini. Kitabu cha: [Fat-h Al-Bariy cha Ibn Hajar Al-Asqalaniy, 7/253, Ch. Dar Tiba].
Na akaelezea Ibn Hajar katika yale yaliyoelezewa na Waraqa Ibn Nufal kwa Mtume S.A.W. kuhusu kutolewa kwake ndani ya mji wake katika yaliyoelezewa na Suheily pale aliposema: Huchukuliwa uzito wa kutenganishwa na nchi kwenye nafsi, kwani Mtume S.A.W. alisikia kauli ya Waraqa kuwa wanamfanyia kero na kumpinga, wala hakuonekana kukasirika kwa hilo, lakini ilipotajwa kuondoka, basi nafsi yake ilitikisika kwa amri hiyo, na hii ni kutokana na kupenda kwake mji wake, na mji unaoashiriwa hapa ni mji Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu na nyumba yake kuwa karibu na nyumba yake Mwenyezi Mungu lakini pia ni mji wa baba zake tokea zama za Nabii Ismail Amani iwe kwake. Kitabu cha: [Fat-h Al-Bariy, 16/289, Ch. Dar Tiba].
Kwa maelezo hayo: Ibara inayosema “Dini ni ya Mwenyezi Mungu na nchi ni ya wote” ikiwa msemaji wake anakusudia kuiondoa dini katika uhusiano wa mtu na Mola wake, basi maana hii inakataliwa na Uislamu na kupingwa. Na ikiwa msemaji anakusudia kuwa tofauti za wananchi katika dini hazifai kuwa ndio sababu ya kutofautiana, basi maana hii ni nzuri na inakubalika katika Uislamu na inalinganiwa pia. Kwa hivyo inapaswa kwa mwenye kubeba maneno ya Waislamu kuwa na maana nzuri, ikiwa ni kufanyia kazi dhana njema kwao kwani asili kwa Muislamu ni Amani na Usalama.
Amesema Ibn Is-haaq: Mtume S.A.W, aliandika makubaliano baina ya Wahamiaji na Wenyeji, na kuwaita pia Mayahudi pamoja na kuwaahidi na kutambua dini yao, na akawekeana nao masharti. Kitabu cha: [Sira cha Ibn Hisham, 1/501 Ch. Mustafa Al-Halaby]
Na vile vile watu wa nchi moja kuungana na kuwa pamoja kwa ajili ya masilahi ya nchi yao ni jambo lenye umuhimu mkubwa na Uislamu unalitolea wito. Na kuipenda nchi na kuyaogopea masilahi yake ni sehemu ya Imani kama yalivyothibitika hayo katika Mapokezi ya Kauli zilizonukuliwa kutoka kwa Wema waliotutangulia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas