Kumuita Mama wa Mtume S.A.W. Neno la (Bibi).
Question
Nini hukumu ya kumuita Mama wa Mtume S.A.W, kwa neno la (Bibi)?
Answer
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Jamaa zake na Masahaba zake, na waliomfuata. Na baada ya utangulizi huo:
Jibu la swali hili linaambatana na kuzungumzia mwisho wa wazazi (Baba na Mama) wa Mtume S.A.W. ambapo wanazuoni walihitilafiana kuhusu mwisho wao, na kauli ya haki ni kuwa wao wawili wameokoka.
Na hii ni kwa mujibu wa madhehebu ya wengi wa wanazuoni wahakiki kati ya wanazuoni wa Umma, waliotangulia na waliowafuata; ambapo walieleza hivyo, na walivitunga vitabu kadhaa kuhusu jambo hili, na jumla ya vitabu hivi ni zaidi ya arubaini, na Imamu As-Sayutiy peke yeke ana vijitabu sita miongoni mwa hivyo, navyo ni:
1- Masalik Al-Hunafaa Fi Walidai Al-Mustafa.
2- Ad-Daraj Al-Manifah Fil Aabaa Ash-Sharifah.
3- Al-Maqamah As-Sundusiyah Fi An-Nisbah An-Nabawiyah.
4- At-Taa’dhim Wal Minnah Fi Anna Abawai Raulillahi S.A.W. Fil Jannah.
5- Nashrul A’alamain Al-Manifain Fi Ihiyaa Al-Abawain Ash-sharifain.
6- As-Subul Al-jaliyah Fil Abaa Al-A’aliyah.
Waliendelea katika kuthibitisha hukumu hii na kuitolea dalili kwa njia kadhaa, miongoni mwake ni:
Njia ya kwanza: kuwa wao wameokoka, kwa sababu hawakuwa na ushirikina, bali walikuwa na Dini ya Hanifiya, yaani Dini ya Babu yao Ibrahimu A.S., na kauli hii ni ya wengi wa wanazuoni, miongoni mwao Imamu Al-Fahkr Ar-Raziy.
Wenye njia hii walitoa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: {Ambaye anakuona unaposimama. Na mageuko yako (ya kuinama na kuinuka na kusimama katika Sala) pamoja na wale wanaosujudu (pamoja nawe)}. [ASH SHURA: 218-219], yaani: Hakika alikuwa akigeuka katika mifupa ya mgongo wa waumini wanaosujudu, na hii ni dalili ya kuwa wao hawakuwa washirikina.
Imamu Al-Fakhr Ar-Raziy katika Tafsiir yake [Mafatiihul Ghaib: 13/33, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy, Bairut] anasema: “Miongoni mwa dalili ya kuwa mmoja wa wazazi wake S.A.W. hakuwa mshirikina ni kauli yake Mtume S.A.W.: “Nimetokana na migongo ya wenye kutakasika kwenda kwenye matumbo ya uzazi ya wenye kutakasika”; na Mwenyezi Mungu alisema: {Hakika washirikina ni najisi}. [AT TAWBAH: 28], na hii inawajibika kusemwa kuwa: hakuna mmoja wa Babu zake alikuwa mshirikina”.
Na Imamu As-Sayutiy amejiunga na njia hii, iliyoelekewa na Imamu Al-Fakhr katika kitabu chake: [Masalik Al-Hunafaa Fi walidai Al-Mustafa, Uk. 40-41, Ch. ya Dar Al-Amiin, Kairo]; na akatoa dlili ambatishi ambayo ameichukua kwenye tangulizi mbili.
Kwanza: Hadithi Sahihi zimeonesha kuwa asili zote za Mtume S.A.W. kutoka kwa Adam mpaka Baba yake Abudullahi, wote ni bora zaidi kuliko watu wa karne zao; na miongoni mwa Hadithi hizi: ni ile liyotajwa katika Sahihi Bukhariy, kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kuwa Mtume S.A.W. alisema: “Nimetumwa kutoka katika karne bora zaidi kuliko karne zote za binadamu, mpaka nikiwa katika karne hii niliyopo ndani yake”.
Pili: Hadithi na Kauli pokezi huonyesha kuwa Dunia katika zama zote, kuanzia zama za Adam na Nuhu mpaka Siku ya Kiyama, haikuwa tupu na watu wenye umbile, wanaomuabudu Mwenyezi Mungu, kumpwekeshe , na kusalia kwake, na kwa ajili yao dunia inahifadhiwa, na pasipo wao dunia ingeangamizwa na vilivyopo juu yake.
Na miongoni mwa Hadithi na Kauli pokezi hizi: ni ile ilivyotajwa katika Musanaf Abdulrazaaq, kutoka kwa Maa’mar, kutoka kwa Ibn Juraij alisema: Ibn Al-Musayab alisema; Ali Ibn Abi Taalib alisema: Waislamu saba au zaidi hata sasa wakiishi duniani, na pasipo wao dunia ingeangamizwa na walio juu yake. Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha {Masalik Al-Hunafaa: Uk. 45-46] anasema: Hii ni Isnad Sahihi kwa Sharti la Maimamu wawili, na kauli kama hii si maoni tu, lakini ina hukumu ya kuendeleza kwa Mtume S.A.W.”. [Mwisho]
Kisha akasema: “Ukilinganisha kati ya tangulizi hizi mbili, itatokea kwa uwazi kuwa wazazi wa Mtume S.A.W. hawakuwa washirikina; kwa sababu imethibitika kuwa kila mmoja kati yao ni mbora zaidi ya karne yake, na kama ikikusudiwa kuwa watu wa umbile ni wao wenyewe basi hii ndiyo inatakiwa, lakini ikikusudiwa kuwa ni wengine na wao wenyewe ni washirikina basi kuna mambo mawili: ama mshirikina ni bora kuliko Muislamu na hii ni batili kwa kauli ya pamoja, au kuwa wengine ni bora zaidi kuliko wao wenyewe, na hii pia ni batili kwa kuzipinga Hadithi Sahihi; kwa hiyo inalazimika kwa uwazi kuwa wasio washirikina, ili wawe ni bora kuliko watu wote katika kila karne”. [Mwisho]
Njia ya pili waliyoipitia wale wanaosema kuwa wazazi wa Mtume S.A.W. waliokoka, kwa kuwa wao ni miongoni mwa watu wa kipindi kati ya Mitume; kwa sababu walikufa kabla ya kuja Utume wa Mtume, basi hawana na adhabu; na Maimamu wa Watu wa Sunna walieleza kuwa: aliyekufa na hali hakufikishiwa Utume basi ni mwenye kuokoka.
Imamu An-Nafarawiy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Al-Fawakih Ad-Dawaniy Ala Risalat Abi Zaid Al-Qairawaniy: 1/80, Ch. ya Dar Al-Fikr] alinukulu kutoka kwa Mtaalamu Al-Ajhuriy kauli yake:
“Baadhi ya walimu wetu walitoa dalili ya kuteua kuwa: watu wa kipindi kati ya Mitume ni wenye kuokoka, watakuwa peponi, vile vile wazazi wa mtume S.A.W. ni wenye kuokoka, na hawakuwa Watu wa motoni; kwa sababu walikufa kabla ya Utume, na hakuna adhabu kabla ya Utume; kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:
{Na sisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpaka tuwapelekee Mtume} [AL ISRAA: 15], na kuingia peponi hakupatikani kwa matendo, lakini ni fadhili halisi za Mwenyezi Mungu, na moto ni malipo ya kafiri na asi, na aliyekufa kabla ya Utume hazingatiwi kuwa asi, kwa hiyo wataalamu wa Elimu ya Maneno na Msingi Mkuu miongoni mwa madhehebu ya Asha’ariy walikubaliana pamoja kuwa aliyekufa bila ya kufikwa na Utume ni mwenye kuokoka, hatokuwa na adhabu wala thawabu”. [Mwisho]
Miongoni mwa walioeleza hivyo pia ni Imamu Sharafud- Diin Al-Munawiy, na aliinukulu pia As-Sibt Ibn Al-Jawziy, kutoka kwa kundi la wanazuoni, miongoni mwao ni Babu yake, na aliitilia mkazo Mtaalamu Al-Ubiy katika Sharh yake ya Sahihi Muslim, na aliikubali Al-Hafidh Ibn Hajar katika baadhi ya vitabu vyake, kama alivyotaja Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha: [Masalik Al-Hunafaa: Uk. 16-17].
Walitoa dalili yao waliielekeza katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpaka tuwapelekee Mtume}. [AL ISRAA: 15], na kauli yake pia: {Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako hakuwa wa kuiangamiza miji kwa dhulma, hali wenyewe wameghafilika (hawakujiwa na Mitume wa kuwaonya)}. [AL ANA'AM: 131], na Aya na Hadithi zingine.
Na Wazazi wa Mtume S.A.W. ni miongoni mwa watu wa kipindi kati ya Mitume; kwani walikufa bila ya kufikishwa Utume, kwa sababu zama zao ni mbali na zama za mwisho wa Mitume, naye ni Bwana wetu Issa A.S, na zama zao pia zilikuwa zama za ujinga, kwa hiyo hakuna mmoja aliyeupata Utume wa Mtume miongoni mwa Mitume wa mwenyezi Mungu isipokuwa wachache wa mapadre wa watu wa kitabu ulimwengini kote, kama vile Sham n.k., na haijulikani kuwa wao walikuwa na safari nyingi, na hawakuishi maisha marefu yanayowawezesha kuzichunguza habari za Mitume, na wao hawakuwa vizazi vya Nabii Issa A.S, wala miongoni mwa watu wake, na hayo yote bila shaka yanaonesha kuwa wao ni miongoni mwa watu wa kipindi kati ya Mitume.
Mwenye kusema kuwa: Hakika watu wa kipindi kati ya Mitume watahiniwe katika (Siraat), na kama wao walikuwa watiifu wataingia peponi, isipokuwa kinyume cha hayo, hapo wataalamu walitaja kuwa Wazazi watukufu wakitahiniwa hakika wao ni miongoni mwa watiifu, na Al-Hafidh Ibn Hajar aliyasema kuhusu alivyonukulu kutoka kwake Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha [Masalik Al-Hunafaa: Uk. 17] kauli yake: “Dhana yetu kuhusu wazazi wa Mtume S.A.W. waliokufa kabla ya Utume watatii kwenye mtihani kwa ajili ya kumuadhimisha na kumridhisha S.A.W.”. [Mwisho]
Imamu At-Twabariy alitaja katika Tafsiir yake [Jamiu’ul Bayan: 24/487, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah] kutoka kwa Ibn Abbas RA, kuwa alisema katika tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na Mola wako atakupa mpaka uridhike}. [ADU DHUHA: 5] kuwa: “Miongoni mwa maridhio ya Muhammad S.A.W. kuwa mmoja wa watu wa nyumba yake asiingie motoni”.
Njia ya tatu waliyoipitia wenye kusema ni wenye kuokoka ni kuwa: Mwenyezi Mungu anawafufua mbele yake S.A.W. mpaka wamuamini S.A.W. na njia hii waliielekea makundi mengi ya wanahadithi na wengineo, miongoni mwao; Al-Khatib Al-Baghdadiy, Ibn Shahin, Ibn Al-Munayir, Al-Muhib At-Twabariy, na Al-Qurtwubiy. Walitoa dalili ya njia yao kwa Hadithi dhaifu, lakini zinaendeleza kuwa ni Hasan kwa jumla ya mapokezi yake, na aliitaja hiyo Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha [Masalik Al-hunafaa; Uk. 85-86].
Na waliopita njia hii walijibu kuwa: Mtume S.A.W. amekatazwa kuwaombea msamaha kuwa: ufufuo wao ni baada ya kukatazwa, kwa hiyo una hukumu ya kulifuta katazo.
Imamu Al-Qurtwubiy katika kitabu cha [At-Tadhkirah Biahwal Al-Mautaa wa Umuril Akherah: Uk. 138, Ch. ya Dar Al-Minhaj, Riyadh] anasema: “Hakuna upingaji, walhamdu Lillahi, kwa sababu ufufuo wao ni baada ya katazo la kuwaombea msamaha kwao, kwa dalili ya Hadithi ya Aisha RA, kuwa huo ulikuwa wakati wa Hija ya kuaga, na Ibn Shahin aliijaalia kuwa ufutaji kwa habari zilizotajwa.
Kisha akasema [Uk. 140-141]: “Hivyo fadhila za Mtume S.A.W. na sifa zake kuu zinaendelezana na kufuatana mpaka wakati wa kufa kwake, na ufufuo huu ni miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake. Na ufufuo wao na imani yao si ngumu kiakili wala kisheria; kama ilivyotajwa katika Kitabu kuhusu ufufuo wa muuliwa wa Bani Israili na kuambia kuhusu muuaji, na Issa AS, alikuwa akiwafufua waliokufa, vile vile Mtume wetu S.A.W. Mwenyezi Mungu amewafufua, kwa mikono yake, makundi ya waliokufa.
Na hii ilipothbitishwa, basi kitu gani kinachozuia imani yao baada ya kufufuliwa kwao, kwa ajili ya kuzidisha heshima na fadhila yake, pamoja na habari zilizotajwa kuhusu hili”. [Mwisho]
Zilizotangulia ni njia za wanazuoni waliosema uokokaji wa wazazi wa Mtume S.A.W. nazo ni njia za nguvu zina dalili na hoja, na wengi wa wanazuoni wa Umma wanazikubali.
Na kati ya maoni wanayotoa ni dalili ya maudhui hii na ishara ya ukokaji wa wazazi wa Mtume, ilivyonukuliwa na Mtaalamu Ibn A’abidiin, mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy katika kitabu cha[ Al-U’uquud Ad-duriyah Fi Tanqiih Al-fatawa Al-Hamidiyah: 2/331, Ch. ya Dar Al-Maarifah] ambapo anasema: “Mtaalamu Al-Khafajiy alileta njia nyingine ambapo aliipangilia, na yenye usahihi, akisema :
Wazazi wa (Twaha) Mtume wana ngazi ya juu
Katika Pepo ya milele na nyumba ya thawabu
Na tone la fadhila yake ya ndani
Linaokoa na kuepusha adhabu kali
Basi vipi matumbo ya kumchukua
Yanaweza kuingia adhabu kali?
[Mwisho]
Na kauli ya kuokoka kwa wazazi wa Mtume S.A.W. ni rai ya Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri:
Sheikh wa Uislamu Al-Burhan Al-Baijuriy katika kitabu cha [Sharh Jawharat At-Tawhid: Uk. 68, Ch. ya Dar As-salaam] anasema:
“Ukijua kuwa watu wa kipindi kati ya Mitume ni wenye kuokoka kwa rai yenye nguvu, utajua kuwa wazazi wake S.A.W. ni wenye kuokoka, kwa sababu wao ni miongoni mwa watu wa kipindi kati ya Mitume, vile vile wazazi wake S.A.W. wote wanaume na wanawake ni wenye kuokoka na inahukumiwa kwa imani yao, na hawakuwa na kufuru, uchafu, aibu, wala kitu waliokuwa nacho Wajahili, kwa dalili kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na mageuko yako pamoja na wale wanaosujudu}. [ASH SHURA: 219], na kauli yake Mtume S.A.W.: “Nimetokana na migongo ya wenye kutakasika kwenda kwenye matumbo” na Hadithi zingine zenye sifa ya uhakika zaidi”. [Mwisho]
Na imetolewa Fatwa ya Mtaalamu Mufti wa Miji ya Misri ya zamani, Mtaalamu wa wakati wake Sheikh Muhammad Bakhiit Al-Mutii’iy, tarehe 2 Mfungo tatu 1338 H., sawa na 25 Novemba 1919; ambapo alisema mwishoni mwake kuhusu hukumu ya aliyedai kuwa wazazi wa Mtume S.A.W. sio miongoni mwa watu wa imani kuwa:
“Hakika amekosa kwa uwazi, huwa na dhambi, kwani alimuudhi Mtume S.A.W. lakini hahukumiwi kuwa kafiri, kwa sababu suala hili silo miongoni mwa misingi ya dini ambalo Muislamu analazimika kuifasili. Na hii ni haki ambayo inaashiria matini na wanazuoni wenye uhakiki” [Mwisho]
Na jumla ya kauli za wanazuoni huonya kwa kuthubutu hadhi ya Mtume S.A.W. na kumuudhi kwa kuwataja wazazi wake kwa upungufu, na kutanabahisha kuwa ni lazima kuwa na adabu mbele yake; na Imamu Abu Bakr Ibn Al-Arabiy, miongoni mwa Maimamu wa madhehebu ya Malik, aliulizwa kuhusu Mtu aliyesema kuwa: Baba ya Mtume S.A.W. ataingia motoni, akajibu kuwa: hakika aliyesema hayo ni mwenye kulaaniwa; kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:
{Kwa yakini wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu Amewalaani katika dunia na Akhera, na Amewaandalia adhabu ifedheheshayo}. [AL AHZAB: 57], akasema: “Hakuna adha mbaya kuliko kusemwa kuwa Baba wa Mtume ataingia motoni”. [Mwisho] [Taz. Masalik Al-Hunafaa, na Imamu As-Sayutiy; Uk. 88].
Na Imamu Al-Qastalaniy, mfuasi wa madhehebu ya Shafiy katika kitabu cha {Al-Mawahib Al-Laduniyah: 1/111, Ch. ya Al-Maktabah At-Tawfiqiyah, Kairo] anasema: “Tahadhari! Tahadhari! kutaja upungufu, kwa sababu hiyo itamuudhi Mtume S.A.W. na kwa kawaida wakitajwa wazazi kwa upungufu, au waelezwe kwa sifa ya upungufu, basi mtoto ataudhika kwa utajo huu wa mazungumzo, na Mtume S.A.W. alisema: “Msiwaudhi watu hai kwa sababu ya waliokufa”.
Ameipokea At-Twabaraniy katika kitabu cha: [As-Saghiir], na hakuna shaka kuwa kumuudhi Mtume S.A.W. ni kufuru, na mwenye kufanya hivyo auliwe, pasipo kutubu, kwa rai yetu’. [Mwisho]
Na Mtaalamu Al-Alusiy katika Tafsiir yake [Rohol Maa’aniy: 19/138, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] akitaja kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mageuko yako pamoja na wale wanaosujudu}. [ASH SHURAA: 219] kuwa: Imani ya wazazi wake S.A.W. ni kauli ya wengi wa wanazuoni wakubwa miongoni mwa watu wa Sunna; kisha akaongeza kuwa:
“Na mimi ninaogopa ukafiri wa huyu anayesema kwao RA, kinyume cha hayo, miongoni mwao Al-Qariy na wengineo” [Mwisho] Al-Qriy anakusudiwa: Mulla Ali Al-Qariy.
Tutazungumzia kwa urefu baadaye kijitabu chake kuhusu maudhui hii.
Mtaalamu Ibn A’abidiin mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy katika Hashiya yake [Radul Muhtar Ala Ad-Durul Mukhtar: 3/185, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Kwa ujumla kama walivyosema baadhi ya wahakiki kuwa:
Haitakiwi kulitaja suala hili isipokuwa kwa adabu sana, nalo si miongoni mwa masuala ambayo kutolijua kwake hudhuru, au litaulizwa kaburini, au kwenye Kisimamo, kwa hiyo kuuzuia ulimi usizungumzie isipokuwa heri ni bora zaidi. [Mwisho].
Ibn A’asakir katika kitabu cha: [Tariikh Dimashq: 45/222, Ch. ya Dar Al-Fikr] amepokea kuwa: “Kiongozi mmoja wa Bani Umayyah huko Sham alimkabidhi mtu madaraka ya mji huko, na baba mzazi wa mtu huyo alikuwa akipima kwa mizani mahali paitwapo Al-Mananiyah – ni kundi la watu wenye bidaa – na Umar Ibn Abdilaziz alipoijua habari hii ya huyo mtu, akasema: kwa nini ulimkabidhi mtu kama huyo madaraka ya Waislamu, ambapo baba yake alikuwa akipima kwa mizani huko Al-mananiyah, akasema mtu huyo: Ewe Kiongozi wa Waumini, kuna uhusiano gani baina yangu na baba yake Mtu yule, na Baba ya Mtume S.A.W, alikuwa mshirikina? na Umar akasema: Ah, kisha akanyamaza kidogo na kisha akainua kichwa chake, akisema: Je, niukate ulimi wake, mkono na mguu wake, au niikate shingo yake? kisha akasema: Je, unamlinganishaje mtu huyu na Mtume S.A.W? Hutanifanyia kazi yoyote kwangu muda wa maisha yangu” [Mwisho]
Kuhusu wale wanaopingana na wengi wa wanazuoni wa Umma, na hawakuelekea njia hizi zilizotangulia, hoja yao ni kama ifuatayo:
Ilivyopokelewa katika Sahihi Muslim, kutoka kwa Anas, kuwa: Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, baba yangu yuko wapi? Akasema Mtume: “Yupo motoni”, na alipoondoka, Mtume akamwita, akasema: “Hakika baba yangu na baba yako wapo motoni”.
Kuhusu Hadithi hii wanazuoni walizungumzia kwa pande mbili, nazo ni Isnadi yake na Matini yake.
Kwa upande wa Isnad: Imamu As-Sayutiy aliibainisha na kuihakikisha, ambapo alisema – na kauli yake inatosha, basi uwe na subira ingawa ni ndefu mno:-
Jawabu: Tamko hili la kauli yake: “Hakika babangu na baba yako wapo motoni” wapokeaji hawakuikubali pamoja, lakini ilitajwa na Hammad Ibn Salamah, kutoka kwa Thabit, kutoka kwa Anas, nayo ni njia yenyewe ya mapokezi ya Imamu Muslim, na Maa’mar, kutoka kwa Thabit alimpinga kutotaja tamko la: “Hakika baba yangu na baba yako wapo motoni” lakini alimwambia: “Ukipita kwenye kaburi la kafiri mpe habari mbaya za moto” na tamko hili halina kusudio la baba yake S.A.W. hata kidogo. Na Maa’mar ni mhakiki sana kuliko Hammad, na kuna maangalizi kuhusu kuhifadhi kwa Hammad, na mapokezi yake yana makosa ambayo yamewekwa na mtoto wa mke wake katika vitabu vyake, na Hammad alikuwa hakuhifadhi, na alipotoa Hadithi ya mapokezi haya aliyataja pamoja na makosa.
Kwa hiyo Imamu Bukhariy hakupokea kitu cha Hammad, vile vile Imamu Muslim katika misingi yake, isipokuwa Hadithi yake kutoka kwa Thabit. Na Al-Hakim katika kitabu cha: [Al-Madkhal] anasema: Imamu Muslim hakupokea kutoka kwa Hammad katika misingi isipokuwa Hadithi yake ni kutoka kwa Thabit, lakini amepokea kutoka kwake maelezo kutoka kwa baadhi ya wapokeaji.
Kuhusu Maa’mar hakuna maangalizo ya kuhifadhi kwake, wala kuyazuia mapokezi yake. Na Maimamu wawili walikubali kupokea kutoka kwake, na tamko lake ni Bora zaidi.
Kisha tumeona kuwa Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Saad Ibn Abi Waqqas, kwa mapokezi haya ya tamko la mapokezi ya Maa’mar, kutoka kwa Thabit, kutoka kwa Anas.
Al-Bazzar, At-Tabaraniy, na Al-Baihaqiy walipokea kwa njia ya Ibrahim Ibn Saad, kutoka kwa Az-Zhuriy, kutoka kwa A’amir Ibn saad, kutoka kwa Baba yake kuwa: bedui alimwambia Mtume S.A.W.: baba yangu yuko wapi? Akasema: Yupo motoni, akamwambia: Baba yako yuko wapi? Akasema: “kila unapopita kwenye kaburi la kafiri mpatie habari mbaya za moto”. Na Isnad hii imekubaliwa kwa masharti ya Maimamu wawili, kwa hiyo tamko hili linazingatiwa sana kuliko lingine, na la kipaumbele.
Na At-Twabaraniy na Al-Baihaqiy walizidisha mwishoni mwake walisema: Baadaye Bedui huyu alisilimu, akisema: Mtume S.A.W. alinikalifisha uzito, kwani kila nilipopitia kaburi la kafiri nimbashirie moto.
Na Ibn Majah alipokea kwa njia ya Ibrahim Ibn Saad, kutoka kwa Az-zuhriy, kutoka kwa Salim, kutoka kwa Baba yake alisema: Bedui mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W. akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika baba yangu alikuwa akiunga undugu, na alikuwa… yeye yuko wapi? Akasema Mtume: “Yupo motoni” na mtu huyu akahuzunika sana, na akasema; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Baba yako yuko wapi? Mtume S.A.W. akasema: “kila ukipita kwenye kaburi la kafiri mpe habari mbaya za moto”, na Bedui huyu baadaye alisilimu, na akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alinikalifisha jukumu, kila nilipopitia kaburi la kafiri nimpatie habari mbaya ya moto.
Bila shaka ziada hii ilibainisha kuwa tamko hili kuu lililotolewa na Mtume S.A.W, na Bedui, baada ya kusilimu kwake, aliliona kuwa ni wajibu kulitekeleza, na akitekeleza, lakini jawabu likikuwa kwa tamko la kwanza, halikuwa na amri yoyote, kwa hiyo inafahamika kuwa tamko la kwanza ni maelezo machache ya mpokeaji, aliyapokea kwa maana ya kutokana na kufahamu kwake.
Hivyo mapokezi ya aina hii yametajwa katika Vitabu Viwili Sahihi yana tamko la maelezo machache ya mpokeaji, wakati kuna tamko lingine lenye ubora. Kwa mfano: Hadithi ya Imamu Muslim, kutoka kwa Anas kuhusu kutosoma Bismillahi, na sababu iliyotangulia ni maoni ya Imamu Shafiy R.A, na akasema: mapokezi thabiti kwa njia nyingine ni kutoisikia, lakini mpokeaji alifahamu kutoisoma, na akaipokea kwa maana kutokana na ufahamu wake, na hilo ni kosa.
Na sisi tulijibu Hadithi ya Imamu Muslim katika maudhui hii kama alivyojibu Imamu wetu Shafiy R.A, Hadithi ya Imamu Muslim kuhusu kutoisoma Bismillahi, kisha ingechukulia kuna makubaliano ya wapokeaji kuhusu tamko la kwanza basi ingepingwa kwa dalili zilizotangulia, na Hadithi Sahihi ikipingwa kwa dalili zingine zenye nguvu zaidi basi inawajibika kuielezea kwa njia nyingine na kuzipa dalili hizi kipaumbele kama ilivyoamuliwa katika Elimu ya Misingi.
Na kwa jibu wa hili la mwisho inajibiwa na Hadithi ya kutoidhinisha kwa kumuombea Mama yake msamaha, pia inaweza kuelezwa kuwa hakuna uunganisho kwa dalili ya kuwa: mwanzoni mwa Uislamu kulikuwa katazo la kumsalia mwenye deni akiwa Muislamu, na huenda Mama yake alikuwa na mizigo mingine isipokuwa ukafiri, kwa hiyo alizuiwa kumuombea msamaha kwa sababu hizi, lakini jibu la kwanza ni la msingi, na haya ni maelezo kwa jumla.
Kisha niliiona njia nyingine ya Hadithi kama tamko la mapokezi ya Maa’mar ambayo ni wazi zaidi, ambapo alieleza kuwa: Mwenye swali alitaka kuulizia baba yake Mtume S.A.W. lakini aligeuza maoni yake kiheshima na kiadabu. Al-Hakim ameipokea katika Al-Mustadrak, na kuisahihisha, kutoka kwa Laqiit Ibn A’amir kuwa alitoka kuelekea Mtume S.A.W. na alikuwa na Nuhaik Ibn A’asim Ibn Malik Ibn Al-Muntafiq, akisema:
Tulikuja Madinah mwishoni mwa Rajabu, tukaswali Swala ya Alfajiri, hapo Mtume S.A.W. alisimama kuhutubu, alitaja Hadithi kwenye kauli yake: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, Kuna mmoja kati ya Majahili waliotangulia yuko katika heri? Na mquraish alisema: Hakika Baba yako Al-Muntafiq yupo motoni, hapo nilihisi joto kati ya ngozi ya uso wangu na nyama yangu kwa sababu alivyosema Baba yangu kwa uwazi, hapo nilitaka kusema: Na Baba yako Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Lakini niligeuza maoni yangu nikasema: na jamaa zako Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: akasema: “Kila ukipitia kaburi la Mshirikina wa Kiqureshi au wa A’amir, sema: Muhammad alinituma kwako , basi kuwa na bishara mbaya kwako”. Mapokezi haya hayana utata, na ni wazi kabisa kuliko yote. [Mwisho wa maneno ya Imamu As-Sayutiy].
Na kwa upande wa Matini: Hadithi hii kwa tamko lake la kwanza ikithibitishwa lazima ifahamike kisahihi, ambapo haipingani na Aya wala Hadithi zinazoonesha kuwa wazazi wa Mtume S.A.W. ni wenyekuokoka.
Kwa hiyo hakuna kosa kuwa kauli yake (Baba yangu) ni Ami yake Abu Taalib; kwa sababu Qur`ani ilitumia tamko la (Baba) kwa maana ya (Ami) katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Wakasema: “Tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahimu na Ismaili na Is-haka…”}. [AL BAQARAH: 133].
Hapo Ismaili aliitwa (Baba) ilhali alikuwa Ami yake Yaakubu, na mazoea ya Waarabu ilikuwa ikijaalia (Ami) ni kama (Baba) na Mpwa (Mtoto wa Ndugu) ni kama (Mtoto), hata washirikina wa Quraish walimwambia Abu Taalib: “Mwambie Mtoto wako asimame kuwatukana Waungu wetu”, wakati wanakusudia Mtume S.A.W. na kumuita Abu Taalib Baba ya Mtume S.A.W. ilikuwa jambo maarufu kwa Maqureshi; kwa sababu Yeye S.A.W, alilelewa na kutunzwa katika nyumba yake, na imethibitika kuwa Abu Taalib atakuwa motoni, kwa hiyo yeye anayekusudiwa kwa tamko la “Baba yangu na baba yako wapo motoni”.
Na miongoni mwa waliosema kuwa maana ya Baba katika Hadithi hii ni Ami- kwa kuchukulia kukubali tamko hili-: Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha: [Masalik Al-Hunafaa: Uk. 81].
Kadhalika: Mkuu wa wafuasi wa madhehebu ya Shafiy na Mufti wao Imamu Ibn Hajar Al-Haitamiy katika kitabu cha: [Al-Minah Al-Makkiyah Fi Sharh Al-Hamziyah: Uk. 102, Ch. ya Dar Al-Minhaj] anasema:
“Na Hadithi ya Imamu Muslim: Mtu alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Baba yangu yuko wapi? Akasema: “yupo motoni”, na mtu alipotoka, Mtume alimwita, akisema: “Hakika Baba yangu na baba yako wapo motoni”, kauli hii inalazimika kuielezwa, na maelezo wazi kwangu kuwa: alitaka kuwa Baba yake ni Ami yake Abu Taalib; kwa sababu iliyotangulia kuwa: Waarabu walikuwa wakimuita Ami Baba, pia kuna dalili ya majazi ndani ya Aya ifuatayo, yaani kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na sisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpaka tuwapelekee Mtume}. [AL ISRAA: 15], ambayo ina dalili kinyume cha Hadithi, kwa mujibu wa rai sahihi kabisa ya Watu wa Sunna, na kuwa Ami yake ni ndiye aliyemlea baada ya Babu yake Abdul Muttalib”. [Mwisho]
Kuna mwelekeo mwingine kwa Hadithi hii nao ni Ufutaji, kama alivyoutaja Imamu As-Sayutiy katika kijitabu chake [At-Taa’dhim Wal Minnah Fi Anna Abawai Rauslillahi Fil Jannah: Uk. 126, imechapishwa pamoja na Masalik Al-Hunafaa, Ch. ya Dar Al-Amin, Kairo] ambapo alibainisha kuwa Hadithi hii iliyotangulia inapinga dalili zingine sahihi, na kuna tofauti kati yake ambayo inapelekea kuwa dalili hizi zinaifuta Hadithi, na akataja mfano wa hayo, akisema:
“Suala hili-yaani suala la wazazi- lina mfano sahihi, na wanazuoni wanahitilafiana nalo, suala hili ni: watoto wa washirikina; ambapo ilipokewa katika Hadithi nyingi kuwa wao kwa yakini wapo motoni, na katika Hadithi chache kuwa wao wapo peponi, na wengi wa wanazuoni walisahihisha hivyo, miongoni mwao ni Imamu An-Nawawiy akisema: Hakika ni madhehebu sahihi yaliyochaguliwa ambayo wana uhakiki waliikubali; kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na sisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpaka tuwapelekee Mtume}. [AL ISRAA: 15], na mtu mzima haadhibiwi kwa sababu habari ya dini haikufikishwa kwake, basi mwingine ni mfano wake.
Na haya ni maneno ya Imamu An-Nawawiy, wakati wengine walitaja kuwa Hadithi zinazoonesha kuwa wao wapo motoni zimefutwa kwa Hadithi zinazoonesha kuwa wapo peponi”. [Mwisho]
Miongoni mwa dalili za wapingaji ambazo zilitajwa katika kauli za wanazuoni ni: iliyotajwa katika kijitabu kinachohusu Mulla Ali Al-Qariy juu ya Wazazi wa Mtume S.A.W. kilichoitwa: [Adillat Mua’taqad Abi Hanifa Fi Abawai Ar-Rasul S.A.W.”, na ndani yake kauli ya Imamu Abu Hanifa katika kitabu chake cha: {Al-fiqh Al-Akbar] kuwa Wazazi wa Mtume S.A.W. walikufa makafiri.
Na yaliyomo ya kijitabu hiki-kwa kuchukulia ni sahihi- yamekataliwa kwa ujumla wake, na yamejibiwa kuwa ni lazima tuwe na adabu zaidi mbele ya Heshima ya Mtume, na kutomuudhi kwa kupunguza hadhi ya Wazazi wake. Hapo juu zilitajwa matini za kauli za wanazuoni kuhusu suala hili, na maneno ya Mtaalamu Al-Alusiy juu ya mtungaji wa kijitabu hicho si mbali nawe.
Kwa hakika yaliyomo katika kijitabu hiki siyo sahihi, na tunayaonesha kama ifuatayo:
Sheikh Mustafa Abu Seif Al-Hamamiy aliandika makala katika kitabu chake cha: [An-Nahdah Al-Islahiyah, Ch. ya Al-Halabiy] kujibu kijitabu hiki, akilaumu kabisa aliyesaidia kukichapisha na kukitangaza; kwani kazi hii inamghadhibisha Mtume S.A.W. na kumuudhi, na baada ya kulichunguza jambo hili alisema Uk. 544:
“Hakika ghadhabu ya Mtume S.A.W. na kila muumini lazima imshukie mchapishaji wa kijitabu hiki kuliko mtungaji wake; kwa sababu mtungaji aliandika nakala yake tu, lakini aliyeichapisha hakika alitangaza maelfu ya nakala hii, na kuichapisha kupitia ulimwenguni kote, baada ya kuwa nakala moja tu imewekwa mahala pake, na kufahamika na watu mmoja mmoja, lakini baada ya kuchapishwa, watu wa dunia wataiona, hasa maadui wa Uislamu na maadui wa Mtume wa Uislamu S.A.W. na wao wakiiona nakala hii watafurahi sana, na watasema yasiyokubaliwa na Mwenyezi Mungu wala Mtume wake wala waumini.
Na kama kwamba mchapishaji katika hali hii anamuonesha Mtume S.A.W. binafsi na Wazazi wake kwa kauli hii, isitoshe bali anamuonesha hivi bila shaka, na hayo yote yanamuudhi Mtume S.A.W. kiasi kikubwa, na aliyesababisha hayo yote ni huyu mchapishaji aliyefanya kila kitu mpaka nakala hii imedhihirika”. [Mwisho]
Kisha Sheikh alibainisha kuwa: kuna kosa katika muswada wa kitabu cha: [Al-Fiqh Al-Akbar na Imamu Abu Hanifa], ambao mtungaji amekijenga kijitabu chake juu yake, na kuwa usahihi ni kinyume cha alivyotaja- kama katika nakala nyingine- ambapo alisema (Uk.545): “Hakika alivyosema mtu huyu- yaani Imamu Abu Hanifa- katika kitabu cha: [Al-Fiqh Al-Akbar] siyo yaliyotajwa, bali matini ya kauli yake ni: (Wazazi wa Mtume S.A.W. walikufa katika Umbile, na Abu Twalib alikufa kafiri).
Na hayo niliyoyaona kwa macho yangu katika kitabu cha: [Al-Fiqh Al-Akbar na Imamu Abu Hanifa R.A.], kwenye nakala ya Maktaba ya Sheikh wa Uislamu huko Al-Madinah Al-Munawarah, Rehema na Amani zimshukie Mwenyeji wake, na uandishi wa nakala hii unarejea Enzi ya mbali, hata baadhi ya wanaofahamu huko waliniambia kuwa imeandikwa katika Enzi ya Abasiya, na nakala hii ni miongoni mwa nakala nyingi na namba yake ni (220) katika sehemu ya Al-Majamii’ kwenye Maktaba hii. Na mwenye kutaka kuiona nakala hii ya kitabu cha: [Al-Fiqh Al-Akbr] chenyewe, basi aende Maktaba hii, na ataikuta huko kwa matini hii tuliyoinukulu hapa”. [Mwisho]
Kisha alitaja mwongozo mzuri ambao unafahamika katika muktadha wa ibara- katika nakala aliyoitegemea Mulla Ali Al-Qariy, nao ni: Wazazi wa Mtume S.A.W. walikufa makafiri- na kutia mkazo wa mabadiliko ya maneno ndani yake, akisema (Uk. 545-546): “Atayeichunguza atakuta matini iliyopo katika nakala ya Mulla Ali Al-Qariy ina makosa mawili:
Kwanza: ni uongo unaopinga nakala ya zamani iliyotajwa hapo juu. Pili: kuna uzushi ndani yake, kwa sababu aliyesoma kuwa (Abu Twalib alikufa kafiri) baada ya matini aliyoinukulu Mulla Ali, atasema kuna kikwazo: Wazazi wa Mtume S.A.W. wakikufa makafiri, na Abutwalib hivyo hivyo, basi usahihi wa maneno utakuwa: Wazazi wa Mtume S.A.W. na Abu Twalib walikufa makafiri wote, na wala hataji ukafiri wa Wazazi wake S.A.W. kisha akataja ukafiri wa Abu Twalib peke yake.
Ama kuhusu nakala yetu iko wazi ndani yake kutaja ukafiri wa Abu Twalib peke yake, ambapo kuna tofauti kati ya waliohukumu, kwa sababu inataja yanayoonesha imani ya Wazazi wake S.A.W. kisha kutaja ukafiri wa Abu Twalib”. [Mwisho].
Licha ya hayo, kuwa Sheikh, Mwenyezi Mungu Amrehemu, amepoza vifua vya waumini kwa alivyonukulu katika kijitabu hiki kuwa: Mulla Ali Al-Qariy amegeuza kauli yake juu ya Wazazi, na akafuata walivyosema wengi wa wanazuoni wa Uislamu, ambapo alisema (Uk. 546-547) kuwa: “Sheikh Mtaalamu Mkubwa Mulla Ali Qariy, Mwenyezi Mungu Amrehemu, ampe hisani, amzidishe nafuu yake, amegeuza yaliyoandikwa katika kijitabu hiki kwa yalivyoandikwa katika Sharehe yake ya kitabu cha: [Ash-Shifaa na Kadhi I’iyadh].
Hapo msomaji atafurahia sana habari hii njema kiasi kikubwa na kwa kila upande, naam, kila muumini atapata bishara na furaha kubwa anaposikia hivyo juu ya mtu mkubwa kama Mulla Ali Al-Qariy.
Nami nitaharakisha bishara kwa msomaji, nitayanukulu maneno ya Sheikh katika maelezo haya, ili mchunguzi ayaone kwa macho. Na maneno yake haya yapo katika mahali pawili pa maelezo yake. Kwanza; katika namba yake 601, pili: katika namba yake 648, Ch. ya Istanbul, ilyochapishwa Mwaka 1316 H.
Kwanza: Mtungaji wa Ash-Shifaa alitaja kuwa: “Abu Twalib alimwambia Mtume S.A.W. hali ya kuwa wamepanda pamoja kipandoni: Nilihisi kiu na sina maji, Mtume S.A.W. akashuka, na kuipiga ardhini kwa unyayo wake, hapo maji yakatoka, akamwambia: Kunywa”, na baada ya habari hii Mulla Ali Qariy alisema tamko hili: “Ad-Duljiy anasema: ni dhahiri kuwa tokeo hili lilikuwa kabla ya Utume, basi litakuwa miongoni mwa alama za Unabii, na si mbali kuwa lililopo baada ya Utume, ambapo litakuwa miongoni mwa miujiza, na inawezekana kuwa ni ishara ya kudhihirisha matokeo ya Utukufu na Baraka za unyayo ya Bwana wa Viumbe, zama za mwisho karibu maelfu ya miaka; chemchemi ndani ya Arafat, ifikayo Makkah na mzunguko wake kutokana na athari ya baraka hii; hivyo Abu Twalib hakusilimu, na kuhusu Wazazi kuna kauli kadhaa, na iliyo sahihi zaidi kuwa walisilimu, kama walivyokubaliana Watukufu wa Umma, na kama alivyobainisha hivi Imamu As-Sayutiy katika Vijitabu vyake Vitatu vilivyotungwa”.
Pili: Sheikh, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: “Kuhusu walivyotaja kuwa Mtume S.A.W. aliwahuisha Wazazi wake, rai sahihi zaidi ya suala hili kuwa lipo kwa rai ya wengi wa wanazuoni waaminifu, kama alivyosema Imamu As-Sayutiy katika Vijitabu vyake vitatu vilivyotungwa”. [Mwisho wa alivyonukulu Sheikh Al-Hamamiy]
Kisha Sheikh alitaja upingaji na akaujibu, akisema (Uk. 549): “Imebaki kusemwa kuwa mageuzi ya Mulla Ali rai yake katika kijitabu chake; Sisi hatujui yapi yameahirishwa ili yawe dalili; Je, ni kijitabu? Basi yeye amekwisha geuza rai yake kuhusu wokovu wa Wazazi R.A, au kauli yake katika Sharehe ya Ash-Shifaa? Hapo aligeuza rai yake kuhusu ukafiri wao, na akasisitiza kuwa wao ni waumini. tutazungumzia nukta hii, tukisema:
Jambo dhahiri kuwa maneno yake katika Ash-Shifaa ni ya mwisho, lakini kuchukulia kuwa maneno ya kijitabu ni ya mwisho inaonekena ni dhaifu, na mwenye kuchunguza maudhui hii ataiona nyepesi kabisa, kwa sababu Sheikh alieleza katika Sharehe yake ya Ash-Shifaa kuwa kauli ya kusilimu kwa Wazazi ni yenye kukubaliwa na Watukufu wa Umma, na ni rai ya wengi wa Wahakiki, yaani akigeuza rai hii kwa kauli nyingine ambayo ni ndani ya kijitabu, basi atayapinga yaliyokubaliwa na wengi wa Wahakiki, na basi vipi uzito wa kauli inayopinga walivyoikubali Watukufu wa Umma, ambapo kauli hii itakuwa ni kinyume na upande wa Watukufu wa Umma”. [Mwisho]
Kwa mujibu wa yote yaliyotangulia tunasema hivi:
Hakika kwa kauli ya kuwa Wazazi wa Mtume Mtukufu S.A.W. walikufa waislamu, na hawakuwa kamwe na ushirikina, au kuwa Mwenyezi Mungu Aliwahuisha mbele yake S.A.W. wakamuamini, basi inajuzu kuwaita tamko la ubwana juu yao; ambapo hakuna kizuizi cha kisheria cha kufanywa hivi, bali ni jambo linalotakiwa, kwa kuwa kuna heshima nyingi na Mtume S.A.W.
Na kwa kauli ya kuwa wao ni miongoni mwa kipindi kati ya Mitume, basi wao ni wameokoka katika Akhera, lakini hawatendewi kama waumini katika dunia; au kwa kauli inayowapinga wengi wa wanazuoni wa Uislamu kuwa wao kamwe sio miongoni mwa waumini, pia inajuzu kuwaeleza kuwa ni mabwana; yaani inajuzu kumwelezea Mama wa Mtume S.A.W.: Bibi Amina Bint Wahb; kwa sababu tamko la (Bwana) katika Lugha ya Kiarabu linamaanisha Mola, Mmiliki, na Muungwana, Mbora, Karima; na pia (Bwana): anayefanya heri sana kuliko wengine. [Taz. Lisaan Al-Arab, na Ibn Mandhuur: Kidahizo: (Sa Wa Da); 3/228-230, Ch. ya Dar Daadir].
Na tamko la (Bibi) huonesha mwanamke ajizuiliaye na machafu. [Taz. Al-Mukhassas Fil Lughah, na Ibn Sidah: 1/345, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy; Lisaan Al-Arab, na Ibn Mandhuur, Kidahizo: (A’a Fa Fa): 9/253].
Na bila shaka kumuelezea Mama wa Mtume S.A.W. tamko la (Bibi) kwa maana hii, haina kizuizi cha kisheria, na inaambatana na kweli, kwa sababu yeye ni mkuu kati ya watu wake, pasipo na shaka.
Na haisemwi: inakatazwa kumuelezea Mama wa Mtume S.A.W. (Bibi), kwa mujibu wa kauli kuwa Wazazi ni miongoni mwa kipindi kati ya Mitume, na wao ni wameokoka katika Akhera, lakini hawatendewi kama Waumini katika dunia, au kwa kauli nyingine inayowapinga wengi wa wanazuoni wa Uislamu kuwa wao kamwe sio miongoni mwa Waumini, na kwa kauli yake S.A.W. katika ilivyopokelewa na Ahmad katika Musnad yake, na Bukhariy katika kitabu cha: ([Al-Adab Al-Mufrad] , na Abu Dawud katika Sunan yake, kutoka kwa Qatadah, kutoka kwa Abdullahi Ibn Buraidah: “Msimwambie mnafiki kuwa Bwana kwa sababu akiwa hivyo, basi mmemghadhibisha Mola wenu Mtukufu”. Kwa sababu zifuatazo:
Kwanza: Hadithi hii ina hitilafu katika usahihi wake; na kama baadhi ya Wanahadithi wakiisahihisha, kama vile Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Adhkaar: Uk. 362, Ch. ya Dar Al-Fikr], na Al-Hafidh Al-I’iraqiy katika kitabu cha: [Takhriij Ahadith Al-Ihiyaa kwa tamko la (kwa fasiki): Uk.1056, Ch. ya Dar Ibn Hazm], na Imamu Al-Mundhiriy katika kitabu cha: [At-Targhib wat-Tarhib: 3/359, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah], isipokuwa baadhi yao waliielezea ukataji wa Isnad, kwa sababu haijulikani kuwa Qatadah alisikia Abdullahi Ibn Buraidah, kama alivyosema hivi Imamu Bukhariy katika [At-Tarikh Al-Kabir: 4/ 12, Ch. ya Dairat Al-Maa’arif Al-U’uthmaniyah, Haidarabad Ad-Dikin], na imenukuliwa na Imamu A-Tirmidhiy katika Sunan yake, kutoka kwa baadhi ya wanazuoni [Sunan At-Tirmidhiy: 3/310, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy, Bairut].
Na maneno ya Imamu Bukari ameinukulu Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Tahdhib At-Tahdhib: 8/3555, Ch. ya Matbaa’at Dairat Al-Maa’arif An-Nidhamiyah, Hindi], na maneno ya Imamu A-Tirmidhy ameinukulu Al-A’alaaiy katika [Jamii’ At-Tahsiil: Uk. 255, Ch. ya A’alam Al-Kutub. Bairut]; Ibn Al-Iraqiy na Abu Zura’ah katika [Tuhfat At-tahsiil: Uk. 625, Ch. ya Maktabat Ar-Rushd, Riyadh], na wote waliinyamazia.
Na Hadithi hii ameipokea Al-Hakim katika Al-Mustadrak, kutoka kwa U’uqbqh Ibn Al-Asamm, kutoka kwa Abdullahi Ibn Buraidah na akasema: “Hadithi hii Isnad yake ni sahihi, na Maimamu wawili hawakuipokea”, isipokuwa Imamu Al-Hafidh Adh-Dhahabiy ameielezea katika kitabu cha: [At-Talkhis] kwa kauli yake: “U’uqbah ibn Al-Asamm ni dhaifu”. [Mwisho]
Na katika [Mizan Al-Ii’tidal] alinukulu kauli za wanazuoni kuhusu U’uqbah Ibn Al-Asamm kuwa: Yahya alisema: Siyo kitu, na Abu Dawuud alisema: dhaifu, na Al-Fallas alisema: alikuwa dhaifu katika Hadithi, na si mwenye kuhifadhi, na An-Nasaiy alisema: si mhakiki”. [Mwisho]
Na maneno haya yanaonesha kuwa haifai katika dalili na ufuatano. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote.
Pili: Hii inalingana na kitendo cha Mtume S.A.W. na wasio Waislamu; ambapo aliwazungumzia makafiri ya wafalme wa Waajemi na wa Warumi katika barua zake kwao kwa kauli yake (Mheshimiwa) kama vile: Mheshimiwa wa Warumi, n.k., kama ilivyotajwa katika Kitabu Sahihi.
Imamu An-nawawiy anasema katika kitabu cha: [Sharh ya Sahih Muslim: 12/108, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Hakutaja neno la (Mfalme) tu, lakini alitaja yanayoonesha upole, akisema: Mheshimiwa wa Warumi, yaani ambaye wanamuadhimisha na kumtanguliza watu wake. Na Mwenyezi Mungu aliamuru ulaini wa maneno kwa wanaolinganiwa katika Uislamu, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema}. [AN NAHL: 125], na pia akasema: {Kamwambieni maneno laini}. [TWAHA: 44], na mengineyo”. [Mwisho]
Na bila shaka kumuita Mama wa Mtume S.A.W. kwa neno la (Bibi) kwa njia ya kuwa yeye ni Mtukufu kati ya watu wake na wakati wake, hapo hakuna ubaya.
Na inajulikana kati ya Waislamu wote kuwa: Bibi Amina binti Wahb ni Mtukufu kati ya Quraish, na wakati wake alikuwa Bibi kati ya watu wake na mwenye daraja bora zaidi, na Baba yake ni Wahb Ibn Abd Manaf Ibn Zuhra, Mkuu wa bani Zuhra.
Imamu Ibn Kathir katika kitabu cha: [As-Sirah An-Nabawiyah: 1/177, Ch. ya Dar Al-maa’rifah, Bairut] anasema: “Abdil-Muttalib Baba yake Abdullahi, Baba ya Mtume S.A.W. alitoka naye kwenda Wahb Ibn Abd Manaf Ibn Zuhra Ibn Kilab Ibn Murra Ibn Kaa’b Ibn Luaiy Ibn Ghalib Ibn Fihr, na wakati huo alikuwa Mkuu wa bani Zuhra kiumri na kiheshima, akamuoza Binti yake Amina Binti Wahb, ambaye wakati huo alikuwa Bibi wa wanawake wa watu wote”.
Kauli ya kuwa tendo la Mtume S.A.W. na wafalme hawa hakika lilikuwa kwa masilahi ya kuvuta nyoyo zao na kuwapa tamaa ya kuingia Uislamu, lakini tuliyo nayo hayakuwepo. Na hii siyo sahihi; kwa sababu kumuadhimisha Mama wa Mtume S.A.W. kumuita kwa neno la (Bibi) juu yake, kwa kuzingatia heshima ya Mtume S.A.W. na kutuliza nyoyo za Waislamu wanaoona kuwa Wazazi ni miongoni mwa waumini na waliookoka.
Tatu: Kwa upande wa makubaliano na mpingaji na kuchukulia kukubali usahihi wa Hadithi hii, na kutokupingwa kwa nyingine, hakika kuadhimisha asiye Muislamu au fasiki siyo haramu kwa uwazi, bali huenda iwe ni halali bila ya chukizo, ikiwa kuwepo udhuru hali ya kuiacha, na inachukiwa kinyume cha hivyo.
Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Adhkaar: Uk. 362, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Hakuna ubaya kumuita mtu fulani bwana, au ewe bwana wangu, n.k., ikiwa mwenye ubwana ni mbora, mwenye heri ya elimu, wema, au mengineyo, lakini ikiwa fasiki, au mwenye shaka ya dini yake, n.k., basi inachukiza kumuita Bwana”. [Mwisho]
Na Ibn A’allan As-Siddiqiy katika kitabu chake cha: [Dalil Al-Halihin Li Turuq Riadh As-Salihin: 8/193, Ch. ya Dar Al-kitaab Al-Arabiy, Bairut] anasema katika Sharhe ya Hadithi ya: “Msimwambie mnafiki kuwa: Bwana”, na mfano wake matamko yote ya kutukuza Watu, na mahali pa katazo: ikiwa kuna udhuru basi kuna hali ya kuiacha, juu ya nafsi yake, jamaa zake, au mali yake, na pasipo na hayo basi hakuna chukizo”. [Mwisho]
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: Inajuzu kisheria kumuita Mama wa Mtume S.A.W, kwa kutumia neno la (Bibi).
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.