Kumwusia Mtoto Aliye Chini ya Ulezi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwusia Mtoto Aliye Chini ya Ulezi (Kafala)

Question

Je, inafaa kwa mlezi wa mtoto yatima au asiyefahamika ukoo wake kumuusia mtoto huyu anayemlea sehemu ya mali yake? Ikiwa inafaa basi ni kiwango gani kinachoruhusiwa na sharia katika hali hii? 

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, swala na salamu ziwe kwa Nabii wa mwisho ni Mtume wetu Muhammad S.A.W. na kwa Maswahaba zake na wale wenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya malipo, na baad ya utangulizo huo:
Wasia ni: Kutoa haki baada ya kifo, tofauti na zawadi ambayo ni: Umiliki wa kitu hivi sasa, ni kitu kinachotolewa wakati mtu bado yupo hai pasi na fidia yoyote, hivyo wasia na kutoa zawadi vyote hivyo ni katika aina ya vitu vinavyotolewa kwa hiyari, tofauti ni kuwa wasia ni umiliki unaopatikana baada ya mtu kufariki, na kutoa zawadi ni umiliki wakati wa uhai.
Mwanadamu anaweza akampa mwenzake zawadi wakati wa uhai wake mali yoyote aitakayo pasi na masharti yoyote madamu tu anavigezo kamili - kwa maana ni mtu aliyebaleghe mwenye akili yupo huru sio mwenye kuzuiliwa na mali hiyo - asiwe katika hali ya ugonjwa wa kifo, kwa sababu anayo haki ya kutumia mali yake kwa matumizi ya aina mbalimbali yaliyo halali kama anavyotaka kwa kiasi anachoona kuwa na maslahi, ikiwa atafanya hivyo kisha akafariki basi matumizi haya - ni sawa sawa yawe ni ya kutoa zawadi au kujitolea au mauzo au yasiyokuwa hayo - yanazingatiwa ni makubaliano halali yaliyo sahihi yametekelezwa na kufanyiwa kazi, vitu vilivyotolewa na mwenyewe havizingatiwi ni mali ya kurithi bali inakuwa ni haki ya yule aliyeandikiwa, hashirikishwi kwenye mali hiyo mtu mwengine mwenye haki ya kumrithi aliyetoa.
Vile vile anayo haki ya kutoa wasia kwa yeyote amtakaye - kwa mali yoyote - isiyozidi theluthi moja, kwa sababu yeye ndio mmiliki wa mali mwenye mamlaka ya kutumia atakavyo, na hilo ni kwa vile tu ana vigezo kamili, lakini kwa vile umiliki wa mali katika wasia umekuwa ni baada ya mtu kufariki basi mwenye mali amewekewa kiwango cha theluthi moja kama kiwango cha juu, haifai kuongeza kiwango hiko isipokuwa kwa ruhusa ya warithi: Kila mmoja na fungu lake, na kulinda haki ya warithi katika mali iliyoachwa, ikiwa marehemu ameusia zaidi ya theluthi ya mali yake basi kitatekelezwa kiwango hiko ama kilichozidia basi kitatekelezwa kwa ruhusa ya warithi.
Na dalili kuwa wasia ni jambo la kisharia unakuwa katika kiwango cha theluthi moja tu ya mali ya mtu ni Hadithi iliyopokelewa na Saad Ibn Aby Wiqaas R.A. amesema: Nilikuwa mgonjwa Mtume alinitembelea mwaka wa hija ya kuaga nikamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimekuwa na maumivu makali kama unavyoona, na mimi nina mali wala hakuna wa kunirithi isipokuwa ni mtoto mmoja tu, je nitoe sadaka theluthi mbili ya mali yangu? Mtume S.A.W. akasema “hapana” nikamuuliza je nitoa nusu yake? akasema: Ni theluthi moja ewe Saad, na theluthi ni nyingi, kwani ukiiacha familia yako wakiwa ni wenye uwezo ni bora kuliko kuwaacha wakiwa ni ombaomba kwa watu” imepokelewa na Muslimu: “Hakika ni bora kwako ukiwaacha warithi wako matajiri” [Amepitisha Al Bukhari 3/1431, na Muslim 3/1250].
Kwa maelezo hayo yaliyotangulia: Mlezi Kutoa wasia kwa Mtoto anayemlea ni jambo linalofaa kisharia kwa masharti yaliyotajwa kwa mtoa wasia, madamu mali inayotolewa wasia ni theluthi tu ya mali yote, na wasia utafanyiwa kazi kwa kiwango hiko pasi na kuhitajika ruhusa ya warithi. Ikiwa kiwango kilichotolewa wasia kitazidi zaidi ya theluthi basi watatakiwa ruhusa warithi kwa hicho kilichozidia, ikiwa watatoa ruhusa basi inafaa kutolewa zaidi ya theluthi moja, lakini ikiwa hawajaruhusu basi wasia hautatekelezwa kwenye kiwango hiki kilichozidi, ikiwa baadhi yao wameruhusu kinyume na wengine basi wasia utatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa tu, na kilichozidi kitarudishwa kwa warithi ili kigawanywe, ama mtoto aliyeusiwa atachukuwa theluthi moja tu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas