Mipaka ya Mamlaka ya Baba Juu ya Bi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mipaka ya Mamlaka ya Baba Juu ya Binti yake.

Question

Ni ipi mipaka ya mamlaka ya baba juu ya binti yake? Je, ana haki ya kumzuia kujifunza, au kufanya kazi kwa mujibu wa ulinzi wake juu ya binti yake? Na unakuwaje msimamo wa baba kuhusu ndoa, matibabu, n.k.? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salaamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya aali zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa Wema mpaka Siku ya Malipo.
Maana ya neno la Wilaya katika lugha ni utawala, na neno la Walaya maana yake ni ulinzi, Mwenyezi Mungu amesema katika Qur`ani: {Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora wa malipo, na mbora wa matokeo} [AL KAHF:44]. Yaani: ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu pekee yake tu.
Maana ya neno la Walaya katika istilahi: mojawapo ya maana bora ambazo zimesemwa kuhusu maana ya neno hili: ni "Mamlaka halali inayomwezesha mmiliki wake kufanya mwenendo sahihi ambao unatumiwa kwake au kwa wengine kwa nguvu au chaguo."
Uwiano kati ya maana ya kilugha na maana ya kiistilahi ni wazi, kwa sababu mlinzi yuko karibu na wale walio chini ya mamlaka yake, msaidizi wake, na anayemwangalia masuala yake.
Ulinzi umegawanywa kulingana na maudhui yake kwa: utunzaji juu ya nafsi, na ulinzi juu ya mali.
Ulinzi juu ya nafsi ambapo mlinzi anasimamia masuala ya kibinafsi ya wale walio chini ya mamlaka yake, kama vile: kufundisha adabu, kuelimisha, kutibabu, kuozesha, na kufanya kazi.
Sababu za kusimamia ulinzi wa nafsi ni nne: utoto, uwazimu, utumwa, na uke.
Kwa upande wa ulinzi juu ya mali, mlinzi atasimamia masuala ya mali ya wale walio chini ya mamlaka yake, kama vile matumizi, kukamilisha mikataba, na kutekeleza kile kinachohusiana na haki za mlinzi mbele ya wengine na zinazohusiana na haki za wengine, kuhifadhi mali zake, uwekezaji wake na maendeleo yake.
Mamlaka ya serikali ni ya asili; inathibitisha kwa uthibitisho wa mwenye mamlaka bila haja ya uthibitisho kutoka kwa wanadamu, na mmiliki wake hawezi kujitenga na hiyo, kwa sababu hayakuthibitisha kwake kwa uwezo wake, nayo yameainishwa katika ulinzi wa baba kwa mali za mtoto wake mdogo.
Au pengine ni mamlaka ya uwakilishi; mmiliki wake huyapata kutoka kwa mtu mwingine, kama vile mlinzi ambaye mamlaka yake yametokana na baba, babu au jaji, na wakala ambaye huchukua mamlaka yake kutoka kwa mteja wake, na kadhalika. Na hali hii inaendelea mradi sifa yake inaendelea, kama ikiondolewa mamlaka yanaondolewa pia.
Sababu ya uhalali wa aina hizi mbili za ulinzi ni kutunza masilahi ya aliye chini ya ulinzi huu. Na kufanya baba ni asili katika ulinzi huu sababu yake ni kwamba ubaba unazingatia kabisa haki ya yule aliyekabidhiwa; kwa ajili ya huruma yake, naye anaweza kufanya hivyo; kwa utimilifu wa akili yake, na yule mtoto mdogo hushindwa kutafuta masilahi yake mwenyewe, na uthibitisho wa ulinzi ili mwenye busara kutafuta masilahi halali ya yule asiye na uwezo wa kufanya hivyo; Kwa sababu ni kutokana na suala la msaada juu ya haki, na kutokana na suala la hisani, na kutaka kusaidia wanyonge na kutoa misaada kwa anayeihitaji, na yote haya ni mazuri kwa upande wa akili na sheria.
Kwa hivyo, ikiwa mwenendo wa baba pamoja na binti yake kwa mujibu wa ulinzi wake hupingana na huruma, shauku na masilahi ya sasa na ya baadaye ambapo anasababisha madhara kwa binti yake, au ana lengo la kufikia masilahi ya udanganyifu au ya chini ambayo hayaendani na shida anayopata kwa sababu yake, basi katika hali hii baba anatumia haki yake vibaya. Kwa sababu haki katika sharia ya Kiisilamu haikuachwa bila kuwekewa mipaka - kama uhuru - na hakuna udhalimu wala utawala unaotumiwa na mmiliki wake kila anapotaka, wala kwa namna anavyotaka, lakini haki zimefungwa ili kufikia malengo yake ya kuleta masilahi na kuondoa madhara.
Msichana anayo haki juu ya baba yake ya kumfundisha, na imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika kitabu cha: Al-Sunan Al-Kubra] kutoka kwa Abu Rafe R.A., kwamba alisema kwa Mtume S.A.W.: Ewe Mtume wa Mungu, je! Mtoto ana haki kama ilivyo haki yetu juu yao? Mtume S.A.W. alisema: “Ndio, mtoto ana haki juu ya baba ya kumfundisha kuandika.” Ikiwa baba anataka kumzuia binti yake kutojifunza na binti akataka kinyume cha matakwa ya baba yake, basi halazimiki kumtii baba yake kwa hilo, na ukiukaji wake katika hali hii sio uasi, kwa sababu utii kwa baba, hata ukiwa utii ni lazima, masharti yake ni kutomdhuru mtoto.
Ibn Taimiyah alisema: “Mtu analazimika kuwatii wazazi wake isipokuwa katika dhambi, hata wakiwa wapotovu ... na hii ni kwa ajili ya faida yao na hakuna madhara, na ikiwa hali hii imekuwa ngumu kwake na haijamdhuru, inakuwa wajibu, na vinginevyo haitofaa” [Al-Fatwa Al-Kubra 5/381- Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ibn Taimiyah alisema pia – miongoni mwa yaliyopokelewa kutoka kwake, kutoka kwa Mwanachuoni Ibn Muflih katika kitabu chake cha: [Al-Adaab Asha-Riyah]: - na kwamba wanavyofaidika navyo - anakusudia: wazazi - na hakuna madhara kwake – yaani kwa: mtoto - kwa kuwatii wazazi wake, hapa kuna sehemu mbili: sehemu ambayo inawadhuru kuiacha, kwa hivyo ni wajibu kuwatii katika sehemu hii, lakini kwa sisi hali hii ni lazima kwa jirani, na sehemu ambayo ina manufaa kwao na haimdhuru mtoto pia, utii wao uko kulingana na muktadha ya maneno yake, lakini kwa ile ambayo inamdhuru kuwatii wazazi, kuwatii kwa hivyo sio lazima kwake katika hali ile, lakini ikiwa ni ngumu kwake na haimdhuru, basi kuwatii ni lazima kwake. [1/436, Ch. ya Alam Al-Kutub].
Madhara ya kuacha kujifunza kwa msichana ni wazi, hayaondolewi; kwa sababu ikiwa kuachwa kwake ni kabisa, basi ni hiki kitu kinachomkosesha mambo mengi, ambayo anaweza kuyapata katika maswala ya dini yake na mambo ya kidunia, na hufanya ufahamu wake kuwa duni kuliko ule wa wenzake wengine waliosoma, na kuathiri vibaya fursa yake ya ndoa kwa kiasi na kwa namna yoyote, na hali hii inazuia uwezo wake baadaye juu ya malezi ya watoto wake vizuri, na hakuna shaka kwamba ufahamu wa mwanamke aliyeelimishwa huongezeka kwa kiwango cha masomo aliyopokea, na hupungua kwa kiwango cha kupungua kwa mafundisho yake.
Na kile kinachothibitisha tulichoamua: ni kile kilichotajwa na wanavyuoni ni kwamba inaruhusiwa kumkiuka baba ikiwa mtoto wake amezuiliwa kutafuta elimu, hata ikiwa elimu hii sio ile ya lazima kwa mtoto apate, mradi tu hajamdhuru baba yake kwa hilo.
Msomi Al-Saffariniy alisema katika maelezo yake juu ya kitabu cha: [Mandhumatul Adab kwa Ibn Abd Al-Qawi Al-Hanbali]: “Ni lazima kuwatii wazazi (isipokuwa katika) kufanya kitu (marufuku), kwa hivyo usiwatii wao katika hali hii, kwa sababu Mwenyezi Mungu, aliyeumba uumbaji, anatiiwa zaidi, kwa hivyo haasiwi kwa utii wao (au): (kwa ajili ya suala) kutokana na maswala ya dini ... (yaliyosisitizwa) kufanywa, kama vile Swala za Sunna ... kwa maana ya amri na makusudio yake sio lazima, ikiwa wakimkataza kutokana na hilo, basi sio lazima kuwatii wao, lakini lazima achukue hatua ya kwanza kufanya jambo lililosisitizwa na hajali makatazo yao. Ndio, yeye hukaa nao kwa wema duniani, kama vile katika hali ya kutafuta elimu ambayo haiwadhuru na kutoa talaka kwa wake kutokana na maoni (kama) ikiwa wakimkataza (kutafuta elimu) sio lazima kwake, ambapo (haiwadhuru) Wazazi (kuitafuta), elimu hii (1/382, Muasasat Qurtuba].
Katika hali nyingine, kujifunza somo maalumu katika suala la Sunna na Faradhi Al-Kifaya (kujitosheleza) kulingana na asili yake, lakini somo hili linategemea mtu ambaye alilosoma, hivyo, kwa mujibu wa kile kilichoamuliwa na kundi la wachunguzi wa Fiqhi kwamba (Inapaswa) Faradhi Al-Kifaya (kwa kuianzia); alisema katika kitabu cha [Jamii Al-Jawamii na maelezo yake kwa msomi Al-Mahali]: ((Na Inapaswa) Faradhi Al-Kifaya (kwa kuianzia); hiyo: inakuwa Faradhi Ain (lazima), ambayo inamaanisha vivyo hivyo katika umuhimu wa kutimiza (kwa usahihi zaidi) kwa faradhi hii” (1/240), pamoja na kitabu cha: [Hashiyat Al-Atwar. Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah], na Ibn Al-Shat Al-Maliki alisema katika maelezo yake juu ya Fruuq Al-Qarafi: “Inapaswa Faradhi Al-Kifaya inakuwa Faradhi Ain (lazima), kwa kuianzia kufuatana na mtazamo ulio sahihi zaidi, hata kutafuta elimu kwa yule anayekuwa na busara” 1/163, pamoja na Al-Fruuq. Alam Al-Kutub].
Na kama elimu ni kazi, ikiwa mahitaji ya kibinafsi au ya umma yanajitokeza, na ilikuwa kazi halali ambayo haina marufuku ya kisharia, na mwanamke anaweza kujihifadhi mwenyewe, heshima yake, na dini yake, pamoja na kuifaa kwa muundo wa mwili wake na kisaikolojia, basi utokaji wake nje ya nyumba hauna aibu kwa haki, wala haupingani na ulinzi wa mwenye mamlaka juu yake.
Na Sharia Tukufu haikuzuia kazi ya yule mama inayotekeleza masharti haya. Miongoni mwa dalili ni: Hadithi ile iliyopokelewa kutoka kwa Imam Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Jabir Bin Abdullah, R.A., alisema: “Mama mdogo/mkubwa’’ alitalikiwa, akataka kuenda kukata mitende yake, mtu mmoja akamkanya asitoke. Akamuendea Mtume S.A.W. Akasema: “Nenda ukate mitende yako kwani pengine ukatoa Swadaqah au ukafanya wema.”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim katika kitabu cha: [Al-Mustadraka na Al-Tahawi katika kitabu cha Mushkil Al-Athar] - na asili ya Hadithi hii iko katika Sahihi Al-Bukhariy – kutoka kwa Aisha, R.A., alisema: Mtume wa Mungu, S.A.W., aliwaambia wake zake: “Atakaye fariki baada yangu ni yule mwenye mkono mrefu” Aisha alisema: “Kama tukikutana Pamoja katika nyumba ya mmoja wetu baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. tunapima mikono yetu ukutani, na tumeendelea hivyo mpaka Zainab binti ya Jahsh, mke wa Mtume, S.A.W., alikufa na alikuwa mwanmke mfupi, na hakuwa mrefu kuliko sisi. Basi tulijua kwamba Mtume, S.A.W., alikusudia tu kwa mkono: Mtowaji sana Swadaka. Alisema: “Zainab alikuwa mwanamke ambaye akifanya kazi kwa mikono yake kushona na kupaka rangi ngozi na kutoa swadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Na serikali inaweza kuwalazimisha wenye mamlaka wasiwadhuru wale ambao wako chini ya mamlaka yao kutokana na wanawake wenye uwezo katika kazi yao ambayo inatekeleza masilahi na kuzuia ufisadi wa kibinafsi na wa umma, kama kazi hii imezungukwa na usalama na amani, na msingi wa kifiqhi unasema kwamba mtawala ana mamlaka ya kufunga jambo linaloruhusiwa kwa masilahi yanayozingatiwa, na kwamba vitendo vyake kwa raia vinategemea masilahi, Wakati wowote ambapo hakuna masilahi ya umma, basi vitendo vya mtawala vinategemea Sharia sahihi ambayo watu wanalazimika kuitekeleza na kuifanyia.
Mwanamke tangu zamani hakuwa mbali na kushiriki kikamilifu katika jamii ya Waislamu, lakini alikuwa na mchango mzuri katika nyanja mbali mbali; alikuwa mpiganaji, muuguzi na mwanasayansi, katika maisha ya Mtume S.A.W. na baada yake pia.
Miongoni mwa michango yake katika Jihadi: iliyopokelewa kutoka kwa Sahihi Muslim kutoka kwa Anas, R.A. ni kwamba Umm Salim katika siku ya Hunain alichukua kisu akawa nacho, na Abu Talha akamwona, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu ni Ummu Salim aliye na kisu, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alimwuliza; “Kisu hiki umetoa wapi?” Alisema: Nimekichukua ikiwa mmoja wa washirikina atanikaribia nitampasua tumbo lake. Akamfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., acheke.
Na imepokelewa kutoka kwa Sahihi Muslim kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alikuwa vitani na Ummu Sulaim na kikundi cha wanawake kutoka Al-Ansar walikuwa wanatoa maji kwa wapiganaji ili kunywa na kuwatibu waliojeruhiwa.
Vile vile imepokelewa kutoka kwake kuwa: Siku ya Uhud, watu miongoni mwa Maswahaba walishindwa, na Abu Talha alikuwa mbele ya Mtume (S.A.W.), akizungukwa kwa ngao – ili kujilinda na silaha za makafiri -. Alisema: Abu Talha alikuwa mtu hodari sana wa kutupa mishale, na akavunja siku ile pinde mbili au tatu. Alisema: Mtu mmoja alikuwa akipita ana kasha la mishale akasema: Isambaze kwa Abu Talha. Alisema: Na Mtume S.A.W., anaangalia watu, Abu Talha anasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa baba yangu na mama yangu nakufidia, usiwasimamie watu; ili usipate mshale kutoka mishale ya watu, nakufidia, Alisema: Nilimuona Aisha bint Abu Bakr na Ummu Sulaim na hakika, wameshamiri naona vikuku vya miguu yao wanavyo kimbilia mbio kubeba viriba – na watu wengine wamesema: Wanapeleka viriba huku wamevibeba migongoni mwao kisha wanawamiminia vinywani watu kisha wanarudi wanavijaza tena kisha wanakuja navyo wanavimimina vinywani mwa watu.
Vile vile imepokelewa kutoka kwake, kutoka kwa Ummu Atiyah Al-Ansariyah alisema: “Nilipigana pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.) Vita saba nafuata misafara yao ili nitengeneza chakula kwao, kuwatibu waliojeruhiwa, na kuwaponya wagonjwa”
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Sa'd kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alisema kuhusu Ummu Imarah Nasibah Bint Kaab kwamba katika siku ya vita vya Uhud Mtume hakugeuka kulia wala kushoto ila alimuona Ummu Imarah akipigana vita kwa ajili yake.
Kuhusu suala la ushiriki wa mwanamke katika maarifa: wanawake walikuwa wakihudhuria mabaraza ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. na wakajifunza kutoka kwake, hata aliwahusishia baraza peke yao. Imepokelea kutoka kwa Al-Bukhari na Muslam kwamba Abu Said Al-Khudriy alisema kwamba wanawake hao walimwambia Mtume S.A.W.: Wanaume wametushinda kwako, kwa hivyo utuainishie siku ya kuwa sisi tu, akawaahidi siku ya kukutana na wao, akawahubiria, na akawaamuru.
Aisha, R.A., alikuwa akitoa Fatwa kwa Waislamu mbele ya Maswahaba, na hurejelewa katika shida.
Ibn Al-Qayyim alisema: “Kwa Aisha, aliwatangulia katika elimu ya Mirathi, hukumu ya halali na haramu, na miongoni mwa wale waliochukua kutoka kwake ambao hawazidi kusema zaidi kuliko maneno yake tu ni: Al-Qasim Bin Muhammad Bin Abi Bakr, mpwa wake, na 'Urwah bin Al-Zubaiyr, mtoto wa dada yake Asmaa. Masruuq alisema: Nimewaona baadhi ya Maswahaba wakubwa wa Mtume S.A.W. wanamuuliza juu ya Mirathi, na Urwah bin Al-Zubaiyr alisema: Sikuona yeyote aliyejua juu ya hukumu au hali ya ujahili au kusimulia ushairi, na Sikuona yeyote aliyejua juu ya Faradhi au matibabu zaidi kuliko Aisha.” [Ilaam Al Mwaqiin 1/17, 18 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Baada ya hapo historia ilirekodi idadi kubwa ya wanawake ambao walifanya kazi katika elimu na kuwa maarufu katika Hadithi, Fiqhi na elimu zingine za Sharia, hata kikundi cha wanavyuoni wakubwa– wa kisasa na wa zamani- walitaja miongoni mwa Masheik wao idadi ya wanawake wasomi waliopokea maarifa na kusimulia Hadithi, miongoni mwao ni: Imam Malik bin Anas, Ahmed bin Hanbal, Al-Samani, Ibn Asaker, Ibn Al-Jawzi, Ibn Hazm, Ibn Al-Qayyim, Al-Thahabiy, Al-Mundhiri na Ibn Hajar Al-Asqalani.
Kati ya wanawake hawa ni wale ambao waliitwa wanachuoni wa kisasa, na wengine wao waliitwa wanachuoni wa ulimwengu, na wengine wao wameitwa manachuoni wa Asban, wengine wao waliitwa wanachuoni wa Iraqi, wengine wao waliitwa wanachuoni wa Kairo, na wengine wao waliitwa wanachuoni wa Sham.
Kuhusu habari ya ushiriki wa wanawake katika maisha ya kisiasa: Imepokelewa kutoka kwa Al-Tabaraani katika kitabu chake Al-Mujam Al-Kabiir kwamba Samarra binti Nahik Al-Asadiyya, alikuwa amewahi kumwona Mtume S.A.W. na alikuwa akitoka na ngao nene na kitambaa cha kichwani kizito, na mkononi mwake mjeledi; anawaelimisha watu adabu, kuwaamuru mema na kuwakataza maovu. Al-Haythamiy alisema katika kitabu cha: [Al-Mujama']: "Wanaume wake ni waaminifu" [9/264, Ch. ya Dar Al-Rayyan Lilturath – Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Arabiy].
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abi Asim katika kitabu cha Al-Ahd Wal-Muthani kwamba Umar Bin Al-Khattab R.A., alimtuma Ash-Shifa Binti Abdullah Al-Adawiyah, kwenye soko.
Al-Hafiz Ibn Abd Al-Barr alisema katika kitabu cha Al-Istiiaab: “Mwanamke anayeitwa Ash-Shifa binti Abdullah Al-Adawiyah alisilimu kabla ya Hijra kwa sababu yeye ni mmoja wa wahamiaji wa kwanza, na akafungamana na Mtume S.A.W. Alikuwa mmoja wa wanawake wenye busara na wema wao ... na Omar akawa akimtanguliza kwa maoni na akamridhisha na akampendelea, na labda amemfanya awe na mamlaka katika suala moja la soko.” [4/1868, 1869- Ch. ya Dar Al-Jiil]
Historia imeandika kwetu mamlaka ya baadhi ya wanawake juu ya mambo kadhaa ya serikali na utawala wao kwa mafanikio, miongoni mwao: Shagaratu Dur Ummu Al-Khalil Al-Salihiyya huko Misri, Radhiyah Sultana Bint Sultan Shams Al-Din Al-Tamsh kutoka wafalme wa India na ndiye mfalme wa tano wa jimbo la Mamalik nchini India, na Sikandar Beykum binti Nadhar Muhammad Bin Waziri ametawala Bahubal, nchini India, na baada ya kifo chake Binti Shah Jahan Beykum alitawala nchi - naye ni mke wa Sayyid Hassan Khan Al-Qanawji Al-Bukhari - na kisha Binti yake Sultan Jehan Beykum alichukua madaraka baada yake.
Kama mamlaka ya baba katika kumuozesha Binti yake, Sharia Tukufu imethibitisha haki hii, na maana ndani yake ni kwamba: ndoa ni mkataba hatari, na uzoefu wa baba – kwa mujibu wa kawaida - na kuthamini kwake kwa watu na hali huzidi uzoefu wa binti yake, ambayo - kwa mujibu wa kawaida pia - anaweza kudanganywa kwa urahisi, na mara nyingi hisia zake hushinda akili yake. - tofauti na baba yake – licha ya kuwa baba pia ni mwenye kukabiliana na mumewe ukitokea mzozo au kutokubaliana kati yao baadaye, kwa hivyo ilikuwa sahihi kumkabidhi jambo lake.
Wasomi walitofautiana kuhusu mamlaka ya baba juu ya binti yake katika kuozesha: je! Mamlaka hayo ni ya lazima - ambapo mlinzi anatimiza ndoa ya msichana bila ya kuzingatia idhini yake - au mamlaka hayo ni ya chaguo - kwa hivyo ni lazima achaguliwe kabla ya ndoa yake? Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi - ambayo imechaguliwa kwa Fatwa - wanaamini kwamba mamlaka ya lazima ni kwa msichana mdogo sio msichana mzima ambaye amebaleghe ambapo mamlaka ya baba yanazingatiwa kama mamlaka yanayopendekezwa.
Ibn Najim alisema: “Mamlaka katika ndoa yako\ aina mbili: mamlaka yanayopendekezwa, ambayo ni: mamlaka juu ya msichana mzima mwenye busara, akiwa mjane na mwana wari, na mamlaka ya lazima, ambayo ni: juu ya msichana mdogo, akiwa ni mjane na mwana wari.” [Al-Bahr Al-Raeq 3 / 117 Ch. Dar Al-Kitab Al-Islami]
Lakini ikiwa baba anakataa kumwozesha mtu ambaye anamtamani kutokana na watu wema, basi mamlaka yake huondolewa juu yake kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni wote, kwa sababu asili ya shearia ya mamlaka ni masilahi, sio madhara, na hii ndiyo inayoitwa “Dhuluma ya mwenye mamlaka”.
As-Shafiy alisema: “Dhuluma ni kutakiwa - kwa mwanamke - kwa kuolewa na mwanamume kama yeye au ni bora kuliko yeye, lakini mwenye mamlaka anakataa” [Al-Um 5/14- Ch. ya Dar Al-Maarifa].
Ibn Qudamah alisema: “Maana ya dhuluma ya mwenye mamlaka ni: Kumzuia mwanamke kuolewa na mwanamume ambaye ni mwema akiomba hivyo, na kila mmoja wao anatamani rafiki yake.” [Al-Mughniy 7/24. Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Na mtakapo wapa wanawake Talaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema.” [AL BAQARAH: 232], na hii ni marufuku kwa wenye mamlaka juu ya mwanamke kwamba hawamkatazi kuolewa na anayemtamani miongoni mwa watu wema, wakifanya hivyo hali hii ni dhuluma inayokatazwa.
Imam As-Shafiy alisema: “Katika Aya hii kuna dalili kwamba ndoa inafanywa kwa idhini ya mwenye mamlaka, bibi harusi na bwana harusi, na kwamba mwenye mamlaka hapaswi kuwa na dhuluma, na akimdhulumu, basi mtawala atamwozesha msichana yule, kwani anayezuia haki basi mtawala anaruhusiwa kuchukua haki hii na kumpa mwenye haki” [Al-Um 5/178].
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy katika Sahihi yake kwamba dada ya Maqal Bin Yasar alimuachana na mumewe, na akamwacha hadi eda yake ilimalizika, akamposa, naye Maqal Bin Yasar akakataa, kwa hivyo Aya hii ikashuka:{basi msiwazuie kuolewa na waume zao} .
Wanafiqhi wamegusia suala hili katika vitabu vyao. Baadhi yao walisema kwamba dhuluma ya mlinzi hufanya mamlaka yake huhamishiwa kwa mtawala, na baadhi yao walisema kuwa huhamishiwa kwa wenye mamlaka wengine ambao ni mbali zaidi.
Alisema katika Badai Al-Sanai kutoka kwa vitabu vya Madhehebu ya Hanafi: “Mshichana mwenye busara na huru, akiomba kuolewa na mtu mwema, basi ni lazima kwa mwenye mamlaka yake amwozeshe; kwa sababu ni kukataza dhuluma, na kukataza jambo maana yake ni kuamrisha kinyume chake, na ikiwa anakataa, amemdhuru msichana yule, na mtawala amesimamishwa ili kuondoa madhara. Basi mamlaka huhamishwa kwa mtawala”. [8/252. Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Alisema katika kitabu cha Al-Iqnaa na maelezo yake kwa msomi Al-Buhutiy: “(Ikiwa mtu wa karibu hafai kuwa mwenye mamlaka) (au yule mwenye mamlaka amemdhulumu msichana, basi mamlaka yake huhamishwa kwa aliyemfuata) yaani mtu mwengine anayefuata mwenye mamlaka wa karibu anamwozesha msichana yule, kwa sababu mamlaka hayathibitishwi kwa karibu aliye na sifa ya dhuluma, kuwepo kwake ni kama kutokuwepo kwake, kama kwamba alikuwa na wazimu. Ikiwa mtu aliyemfuata mwenye mamlaka alimdhulumu msichana pia, basi mtawala ndiye atakayemwozesha, kwa sababu Mtume S.A.W. alisema: "Ikiwa wamegombana, basi mtawala ndiye mwenye mamlaka kwa wale wasio na mwenye mamlaka” (Na dhuluma ni: kumuzuia kuolewa na mtu mwema akimtamani hivyo na kila mmoja wao alitamani mwenzake) kwa mahari au (hata) ilikuwa (bila ya mahari ya wenzake” [Kashf Al-Qinaa 5/54. Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Kwa msingi huu, hairuhusiwi kwa wazazi kuwa wakali katika suala la kuolewa kwa msichana wakati wa kuwepo kwa mposa anayefaa bila ya sababu pamoja na hamu ya msichana kwa kuolewa. Kwa sababu hali hii ya ukali wao ni dhuluma kwake na kufungua milango ya ufisadi katika jamii. Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy kutoka kwa Ali bin Abi Talib, R.A., kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akamwambia: “Ewe Ali, mambo matatu usiyacheleweshe: Swala ikiwa wakati wake umeshafika, na mazishi ikiwa yakihudhuria, na wasichana wakipata mifano yao”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abu Hurairah, R.A. kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., amesema: “Atakapoposa kwenu mnaemridhia dini yake na tabia yake (kuwa ni njema) basi muozesheni msipofanya hiyo kutatokea fitna katika ardhi na uovu mkubwa”.
Al-Minawi alisema: "Inamaanisha ni: msipoozesha wale ambao mnaemridhia dini yake na tabia yake (kuwa ni njema), na ukiangalia mtu ambaye ana pesa au utajiri, wanawake wengi hubaki bila mume na wanaume bila mke, kwa hivyo uzinzi unazidi na aibu inatolewa, mauaji hufanyika kati ya wale ambao wametajwa kuwa na aibu, na dhiki zinafadhaisha na dhiki zinaibuka. [Faidh Al-Qadir 1/243-i. Ch. ya Maktaba Al-Tujaria Al-Kubra-Egypt]
Vivyo hivyo, baba hana haki ya kumzuia binti yake kwa matibabu kama akitaka kutibiwa, kwani hali hii ni kuondoka kutoka mahitaji ya mamlaka yake na huruma yake na utunzaji wake kamili, lakini badala yake, kama mwenye mamlaka ana uwezo anaweza kumlipia msichana dawa na matibabu yake, muda tu msichana yuko chini ya uangalizi wake na udhamini wake; Kwa sababu ni lazima kwa baba kubeba jukumu la ulezi wa binti yake kwa kila njia, na wasomi wamesema kwamba hii inajumuishwa katika suala la matumizi yaliyo ni lazima juu ya baba kwa mtoto wake.
Imam Ar-Ramliy alisema katika kitabu cha: [Nihatul Muhtaj]: "(Analazimishwa), akimaanisha: tawi la uhuru ... (matumizi), akimaanisha: mahitaji ya maisha - hata: dawa na malipo kwa daktari - (baba ... na babu ... (na) asili ya huru anatakiwa kuleta mahitaji ya maisha kwa mtoto na mjukuu. hata akiwa ni wa kike vile vile.” [7/2188. Ch. ya Dar Al-Fikr]
Wazazi na wenye madaraka wanatakiwa kumcha Mwenyezi Mungu katika binti zao na kutendeana nao kulingana na matakwa ya masilahi yao ya umma na ya kibinafsi, na kile kinachohitajika kwa kuelezea uke uliopo na wa kudumu katika utunzaji wao, na kukumbuka thawabu kubwa inapopatikana, na ahadi ya uhakika wakati wa kukiuka.
Imepokelewa kutoka kwa Masheikh wawili Al-Bukhariy na Muslim katika Hadithi zao za kweli kutoka kwa Ibn Omar, R.A. kuwa alimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akisema: “Kila mmoja wenu ni mchunga (dhamana) wa raia zake na ataulizwa juu yao, basi Imamu ni mchunga na ni dhamana juu ya raia zake …”
Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika Sunnah yake kubwa, kutoka kwa Anas, R.A., kwamba Mungu, S.A.W., amesema: “Mwenyezi Mungu atauliza kila mchunga (dhamana) kuhusu raia zake, je, alitunza raia au alipoteza hata mwanamume ataulizwa kuhusu familia yake.”
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy kutoka kwa Aisha, R.A., kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Mwenye kutahiniwa na mabinti hawa kwa chochote, naye akawafanyia ihsani, watakuwa ni kinga kwake na Moto.”
Imepokelewa kutoka kwa Abu Burdah kutoka kwa baba yake kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alisema: “Wanaume watatu watakuwa na malipo mara mbili. “Kisha akasema kati yao: “Mtu ambaye alikuwa na mjakazi amemfundisha adabu nzuri, na akamfundisha vyema, akamwacha huru akamuoa basi ana malipo mara mbili.” Al-Bukhariy alisema: Mlango wa kumfundisha mtu mjakazi wake na familia yake.
Imamu Ibn Hajar alisema katika kitabu cha: [Al-Fath]: "Msemo wake: Mlango wa kumfundisha mtu mjakazi wake na familia yake ni kulinganisha na Hadithi kwa tafsiri ya mjakazi kwa matini na katika familia kwa kupima, hali ya kuwajali familia huru katika kufundisha faradhi za Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mjumbe wake inasisitizwa zaidi kuliko kutunza wajakazi” [1/190- Ch. ya Dar Al-Maarifa - Beirut].
Wasichana pia wanatakiwa kuwa wenye fadhili katika kuomba haki zao kutoka kwa wazazi wao, na kuzifikia kwa upole kadri iwezekanavyo, kwa sababu ikiwa kutimiza haki hiyo ni jukumu la wazazi kwa watoto, basi hairuhusiwi kwa wale ambao wana haki juu ya wazazi kuwadhuru wazazi wakati wa kutimiza haki hiyo.
Mwenyezi Mungu amesema: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima (23) Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.(24)}. [AL ISRAA: 23, 24]. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisisitiza kuwatendea wazazi wema, ambapo wema kwao walikuwa baada ya kumpwekesha Allah, na akaamuru kuwaheshimu wao na kuwafanyia wema kwao na kusema nao kwa msemo wa heshima, laini inayotakiwa na tabia njema, na kwamba hakuidhinisha hata kwa neno dogo linalotokana ubaya.
Mwenyezi Mungu amesema: {Na tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wake.} [AL ANKABUUT: 8]. Mwenyezi Munu amesema pia: {Lakini kaa nao kwa wema duniani} [LUQMAAN: 15], yaani: kukaa nao kwa wema, na tabia nzuri, upole, subira, kuwafanyia wema, na kuunganisha koo zao.
Imepokelwa kutoka kwa Al-Tirmidhiy – na imethibitishwa – kutoka kwa Abu Al-Dardaa, R.A., kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Baba ndiye ni Pepo ya kati kati, kwa hivyo ikiwa ukipenda poteza mlango huo au utunze.”
Imepokelwa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abu Imamah, R.A., kwamba mtu alisema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni ipi haki ya wazazi juu ya mtoto wao? Mtume S.A.W. alisema: Wao ni Pepo yako na moto wako.”
Sufyan At-Thawriy alisema: “Yeyote mwenye kuwaangalia wazazi wake vibaya hakuwafanyia wema.”
Hii yote ni taarifa kubwa inayohusu haki ya baba juu ya mtoto wake, na kwamba tabia inayofaa ni lazima ifunzwe kwa binti huyo mpaka kupata haki bila kuathiri hali yake au kuharibu akili yake.
Na Mwenyezi Mutngu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas