Sheria ya Kiislamu ni taaluma yenye misingi yake.
Question
Je, Sheria ya Kiislamu ni taaluma iliyo na misingi ama ni fikra za kawaida zinazoweza kujadiliwa na kubadilishwa na mtu yeyote?
Answer
Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuzungumzia Sheria na kuijadili isipokuwa wataalamu wabobezi wa Sheria, ambapo sheria ya kiislamu ni taaluma inayo misingi na kanuni zake mahususi zinazotokana na Qur`ani Takatifu na Sunna za Mtume (S.A.W.) na uelewa wa maswahaba watukufu (R.A.) kutokana na waliyoyajifunza kutoka kwa Mtume (S.A.W.), misingi iliyoandikwa na Maimamu na Wanazuoni na kuainishwa katika vitabu vyao, pia, wanazuoni wa Fiqhi waliainisha mbinu ambayo Muislamu huweza kujifunza elimu ya sheria na misingi yake kupitia kwake atakapotaka hivyo, hali atakaeshindwa kufanya hivyo, basi awajibike kwa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} [An-Nahl: 43], lakini ni miongoni mwa maovu ya wenye fikra kali kuwa wanajiingiza katika masuala wasiyoyajua, halafu hawatosheki kwa hayo, bali wanawalazimisha wengine kufuata maoni na mitazamo yao potofu, isitoshe, bali wanaenda kinyume na kuwashutumu wanazuoni wa haki wakidai kuwa wataalamu hawa wamependelea dunia wakaipoteza dini, na kwamba Wanazuoni hao wangesoma Sheria kwa misingi yake na njia zake zilizo thabiti tangu zama za watu wema mpaka zama za kisasa wasingekosa kufuata Wataalamu walioongoka, na wangetambua fadhila na nafasi ya Wanazuoni hao.