{Basi waulizeni wenye kumbukumbu (z...

Egypt's Dar Al-Ifta

{Basi waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya Mwenyezi-Mungu vya kale) ikiwa nyinyi hamjui}.

Question

  Uzushi kwa Maswahaba na Imamu Al Bukhariyy.

Answer

Kuna gazeti linaitwa Al-Fajr toleo la 96 la tarehe 9/04/2007 likiwa limeandika makala katika ukurasa wake wa kumi na mbili ndani yake kukiwa na dharau ya wazi katika maandiko yake anuwani zake na madhumuni yake kwa Sahaba Mtukufu Abi Hurairah R.A. na kwa Imamu Al Al Bukhariyy mwenye kitabu cha Sahihul Al Bukhariy, nimepatwa na pigo kubwa mimi na jopo la wasomaji, kwa kuguswa mambo thabiti ya Dini ya msimamo wa kati na kati yenye thamani ya hali ya Juu sana kwangu kuliko roho yangu familia yangu na mali zangu, na umeambatanishwa ukurasa huu wenye maneno machafu, upi mtazamo wa sheria katika hilo? Na ipi hukumu ya Dini kwa mwenye kufanya hayo?
Jibu:
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, swala na salamu ziwe kwa Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Masahaba zake na wale wote wanaomfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho na baada ya utangulizo huo:
Kwa kupitia makala iliyoelezewa katika swali hilo na imeambatanishwa na kujiridhisha na ukweli wa yaliyokuja kwenye swali tumekuta kuwa mwandishi wa makala katika gazeti tajwa amenukuu katika makala yake yaliyomo kwenye kitabu kilichojaa dharau kwa Sahaba Mtukufu Abi Hurairah R.A. na mwandishi huyo amekipata kitabu hiki toka kwa baadhi ya rafiki zake pasi na kujiridhisha na yaliyomo, na bila ya kuuliza majibu mengi ambayo yamejibiwa hapa nyuma na wanachuoni kuhusu kitabu hiki, yamefupishwa yaliyonukuliwa na mwandishi katika vipengele kadhaa:
• Sehemu ya kwanza ya makala imeelezea yaliyomo kwenye makala iliyopita kuhusu kuwepo Hadithi za kutungwa ndani ya kitabu cha: [Sahihul Al Bukhariy.
• Kisha akaanza kunukuu kitabu kilichoashiriwa mfululizo wa dharau na ukosoaji kwa Sahaba Mtukufu Abi Hurairah R.A. mpaka kufika khaibar kwa kuwa kwake ni mwenye kuzama kwenye ujinga ili awe ni kasoro kwa Mtume S.A.W.
• Miongoni mwake ni kutokufahamika jina lake ndani ya zama za ujinga na hata zama za Uislamu, na kauli yake: Ni wazi kuwa huyu paka bado alikuwa anaishi naye.
• Pia hafahamiki chochote juu ya maisha yake, isipokuwa alikuwa ni mtu masikini sana na kuajiriwa na binti wa Ghazwan, na ni mtu alikuwa mjinga asiyejua kusoma wala kuandika, kisha baada ya hapo akataja kuwa alikuwa akichunga mbuzi.
• Pia madai yake kuwa alipokea Hadithi kutokana na Jafar Ibn Abi Twalib R.A.
• Kisha kurudi kwake mpaka siku ya khaibar pamoja na kisa chake na Aban Ibn Said Ibn Al-Aas, na yanayoonekana, na Mtume S.A.W. hakuwa ni mwenye kumtetea pindi alipodharauliwa na Aban.
• Kuhamia kwake Madina, na kutajwa baadhi ya mapokezi yaliyopatikana wakati wa njaa yake na dalili ya kuwa alikuwa ni mtu mwenye kuombaomba watu kwa kero.
• Kudaiwa kwake kuwa alikimbia kwenye vita vya Muutah.
• Madai yake kuwa alikuwa anafahamu utabibu, kutokana na yaliyonukuliwa na Thuaaly katika kitabu cha: [Thimar Al-Kulub fii Al-Mudhaaf wal Mansuub]
• Kutaja kwake kisa cha Al-Mudhirah “Nayo ni aina ya chakula” ili kufanya dalili kuwa alikuwa ni matu mwenye kupenda sana kula na woga wake wa vita.
• Ametajwa kupenda kwake sana utani, na kisa chake katika masuala ya ukhalifa na kupenda kwake utani na watoto, na kumalizia kwenye matokeo ya ajabu.
• Ametajwa Mtume S.A.W. alimtuma Abi Hurairah R.A. pamoja na Alaa Al-Hadhramy kwenda kwa Al-Mundhir Ibn Saawy na madai yake kuwa hilo alimkatalia.
• Alipewa usimamizi na Omar R.A. kwenye nchi ya Bahrain ndani ya mwaka wa ishirini na moja, kisha kumuhukumu kwenye mali zake, na madai yake kuwa alitumwa huko kwa sababu alikuwa ni katika Masahaba wadogo.
• Ametaja Omar R.A. alimtaka kutopokea Hadithi na akampiga na aina ya kiatu, na alikuwa akisema baada ya kifo cha Omar: Hakika yangu ikiwa nitazungumza Hadithi lau nitaiongelea Hadithi hiyo basi atanitikisa kichwa changu.
Inapaswa kufahamu kuwa makala - Kama asili ambayo inatumiwa na muandishi - haina undani wa usahihi wa kunukuu, lakini mambo mengi yaliyonukuliwa ni kutoka ndani ya vitabu vya fasihi, mfano kunukuu kutoka kwa Zamakhshariy ndani ya kitabu Rabii Al-Abraar na kutoka pia kwa Ibn Abi Al-Hadid kwenye sherehe ya [Nahaj Al-Balagha], pasi na kuchunga upokezi wa kisa, pamoja na kuwa upokezi katika dini, ndio kipimo cha hukumu ya mapokezi mbalimbali, na watunzi wengi wa fasihi hunukuu mapokezi bila ya upokezi unaoweza kuangaliwa juu ya usahihi wake au udhaifu wake, hii ni pamoja na kuwa ambao walionukuliwa ni watu wa Muutazilah na mwingine akituhumiwa kuwa ni mwenye kukanusha, hivyo basi majibu ya matini ambayo mwandishi anaitumia kwa kuchafulia ni ya kushushwa kwenye ukweli wa mapokezi, na inapaswa kufahamika pia mwandishi analeta kisa kisha anafuatia na uchambuzi wa ajabu usioonesha usahihi kwa mbali wala karibu.
Kabla ya kujibu kwa kina inapaswa kufahamika kuwa Masahaba wote ni watu wenye wingi wa uadilifu, uadilifu wao umepokelewa na kuelezewa kwenye Aya nyingi za Qur`ani Tukufu, miongoni mwa Aya hizo ni kauli ya Mola Mtukufu: {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wastani} na kauli yake tena: {Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu} na wanaozungumzishwa ni wale waliokuwepo wakati huo kama ilivyokuja kwenye kitabu cha: [Tadreeb Raawy” 2/214].
Imepokelewa kutoka vitabu vya Sunna ambavyo vinakubalika na Umma katika historia, na wanachuoni wamejengea uelewa wao wa dini ya Kiislamu milango waliyoigawa watu wa elimu katika kuelezea ubora wa Masahaba wote na katika ubora wa baadhi ya Masahaba, miongoni mwake ni pamoja na yaliyopokelewa na Tirmidhy kuhusu ubora wa Sahaba Abi Hurairah R.A.: “Alikuja Mtume S.A.W. na tunda za tenda, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ziombee dua kwa Mwenyezi Mungu azibariki, Mtume akazikusanya mkononi kisha akaniombea baraka kwenye tende zile na akaniambia: “Zichukue na uziweke kwenye chombo hiki, kila unapotaka kuchukuwa basi ingiza mkono wako na uchukue pasi na kuzisambaza”, nikazichukuwa tende zile na kuzitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu tulikuwa tunakula na kulisha wengine mpaka siku aliyouwawa Othman ndipo zikakatika”. Amesema Tirmidhy: Hadithi hii ni hasan na gharib. Na nyingine pia: “Mtu mmoja alikuja kwa Twalhah Ibn Ubeidillah na akasema: Ewe Aba Muhammad, je umemuona huyu Myemeni – kwa maana ya Aba Hurairah – ni mjuzi zaidi wa Hadithi za Mtume S.A.W. kuliko nyinyi! Tunasikia kwake ambayo hatusikii kwenu, akasema: Ama kuwa amesikia kutoka kwa Mtume S.A.W. yale tusiyoyasikia mie sina shaka kuwa amesikia kutoka kwa Mtume S.A.W. ambayo sisi hatujayasikia, na hilo ni kwa sababu alikuwa ni masikini asiye na kitu, alikuwa mgeni wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. mkono wake ulikuwa pamoja na mkono wa Mtume wa Mungu na sisi tulikuwa ni watu wa majumbani mwetu wenye kujitosheleza tulikuwa tunakuja kwa Mtume S.A.W. nyakati za mchana hivyo simtilii shaka kuwa amemsikia Mtume S.A.W. yale ambayo sisi hatukusikia, wala hakuna yeyote anayesemsemea Mtume wa Mwenyezi Mungu ambayo hajasema”. Amesema Tirmidhy: Hadithi hii ina Hukumu ya Hasan na Ghariib. Na nyingine pia kutoka kwa Omar R.A. kuwa amesema kumwambia Abi Hurairah R.A.: “Ewe Aba Hurairah wewe ulikuwa zaidi na Mtume S.A.W. kuliko sisi, na mwenye kuhifadhi zaidi Hadithi zake”. Amesema Tirmidhy: Hadithi hii ni hasan. Na pia kuna Hadithi nyingine kutoka kwa Abu Hurairah R.A.: “Nilisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ninasikia kwako vitu lakini si hifadhi. Akasema: “Kunjua kitambaa chako” Nikakikunjua, akazungumza Hadithi nyingi sikusahamu Hadithi yoyote aliyoniambia”. Amesema Tirmidhy: Hadithi hii ni hasan na sahihi.
Katika kitabu cha: [Tuhfat Al-Ahwadhy]: Amesema mwanachuoni wa Abi Hanifah...tamko lake: Kuwa Abi Hurairah si mwenye elimu si jambo sahihi, bali usahihi ni kuwa alikuwa ni katika wanachuoni ambao walikuwa wakifutu masuala katika zama za Mtume S.A.W. kama alivyosema Ibn Humam katika kitabu cha: [Tahrir Al-Usuul] na Ibn Hajar katika kitabu cha: [Al-Isabah fii Ahwaal Sahabah]. Na katika baadhi ya Hawaashy kitabu cha: [Nur Al-Anwaar] kuwa Aba Hurairah alikuwa ni mwanachuoni, ameelezea pia Ibn Humam katika kitabu cha: [Tahrir], na alikuwa akitoa Fatwa zama za Masahaba na alikuwa akipingana na Masahaba Watukufu kama vile Ibn Abbas aliposema: Muda wa eda ya mwanamke mjamzito aliyefiliwa na mume wake ni zaidi ya miezi miwili, Abu Hurairah akamjibu na kutoa Fatwa kuwa eda yake inaisha pale anapojifungua, hivyo ndivyo ilivyosemwa”. Nikasema: Abu Hurairah alikuwa ni mwanachuoni katika Masahaba na ni miongoni mwa wasomi wakubwa wa kutoa Fatwa, amesema Hafidh Dhahabiy katika kitabu Tadhkiratul-Huffaadh: Abu Hurairah Duusiyy Al-Yemeny muhifadhi wa Hadithi ni mwanachuoni mtu wa karibu wa Mtume S.A.W. alikuwa ni miongoni wa wana elimu ni katika Maimamu wakubwa wa Fatwa pamoja na utukufu, wingi wa ibada na unyenyekevu. Na amesema Al-Haafidh Ibn Al-Qayyim katika kitabu cha: [Al-iilaam Al-muwaqqeen]: Kisha alifanya kazi ya kutoa Fatwa baada ya Mtume S.A.W. ni radi ya Uislamu mzito wa Imani kambi ya Qur`ani na askari wa Mwingi wa rehema, hao ndio Masahaba wa Mtume S.A.W. walikuwa kati ya wenye wingi wenye uchache na wenye uwastani, lakini saba miongoni mwao walikuwa ni wenye mapokezi mengi akiwemo: Omar Ibn Khatwab, Ally Ibn Abi Twalib, Abdillah Ibn Masuud, Aisha Mama wa Waumini, Zaidi Ibn Thaabit, Abdillah Ibn Abbas na Abdillah Ibn Omar, waliokuwa na mapokezi ya wastani miongoni mwa vijana ni: Abubakri Swiddiq, Ummu Salama, Anas Ibn Malik, Abuu Said Al-Khudry, Abu Hurairah na wengine.... hakuna shaka kuwa Aba Hurairah R.A. alikuwa miongoni mwa wanachuoni katika wanachuoni Masahaba na miongoni mwa wanafatwa wakubwa.
Zimepokelewa Hadithi nyingi zinazokataza kuwatukana Masahaba R.A. kutoka kwa Abi Said amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Msimtukane yeyote katika Masahaba wangu, kwani mmoja wenu lau atatoa dhahabu kubwa sawa na mlima wa uhudi hatofikia kutoa kwa mmoja wao wala nafasi yake”. imepokelewa na Imamu Al Bukhariy na Muslim na kupokelewa kwa njia nyingi toka kwa Mtume S.A.W.: “Mwenye kumtukana Sahaba wangu basi juu yake imshukie laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika pamoja na watu wote”. Na inafahamika kuwa laana ni katika alama za madhambi makubwa. Imepokelewa na Ahmad katika upokezi wake na Tirmidhy – na amesema ni Hadithi yenye Hukumu ya Hasan na Gharib – kutoka kwa Abdillah Ibn Mughaffal R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “ Chondechonde kwa Masahaba wangu, chondechonde kwa Masahaba wangu, wala msiwafanye kuwa ni lengo baada yangu, basi mwenye kuwapenda kwa kunipenda mimi amewapenda wao, na mwenye kuwabughudhi kwa kunibughudhi mimi amewabughudhi na wao, mwenye kuwafanyia kero basi atakuwa amenifanyia kero mimi, na mwenye kuniudhi mimi basi atakuwa amemuudhi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mwenye kumuudhi Mwenyezi Mungu basi inahofiwa kuchukuliwa”.
Kama vile si katika heshima ambayo ametufundisha Mtume S.A.W. kujeruhi Masahaba zake, hasa kwa jambo lisilothibiti kwao. Amesema Al-Kadh Iyyaad: Katika kumuheshimu Mtume S.A.W. na kumfanyia wema ni pamoja na kuwaheshimu Masahaba zake na kuwafanyia wema pamoja na kufahamu haki zao na kuwafuata pamoja na kuwasifu kwa sifa njema kuwatakia msamaha kushikamana katika yale waliyovutana kati yao na kuwafuata waliowafuata na kupinga habari za wanahistoria na ujinga wa wapokezi na upotoshaji wa kundi la shia na wazushi kwa yeyote kati yao, na kushikamana nao kwa yale yaliyonukuliwa toka kwao mfano wa hayo ni pamoja na yale yaliyokuwa kati yao miongoni mwa fitina kwa maelezo mazuri, na kuwatoa kwenye matoleo mazuri, kwani wao ni watu wa hivyo, wala asitajwe yeyote miongoni mwao kwa ubaya, wala kuashiriwa jambo, isipokuwa hutajwa mazuri yao na yaliyobora kwao pamoja na kutajwa kwa wema mwenendo wao na kunyamaziwa yale yaliyo nyuma yao. Kitabu cha: [As-Shafaa 2/53].
Amesema Imamu Ghazaliy: Fahamu kuwa Kitabu chake ambacho kimekusanya ndani yake sifa za [Muhaajirin” Masahaba] waliohamia Madinah pamoja na wenyeji wao “Answaar”, na kuwa na mapokezi mengi ya habari za Mtume S.A.W. kwa matamshi mbalimbali...kila mm kuwatakasa oja imepokelewa sifa yake binafsi katika haki yake, inapaswa imani hii katika haki zao iende sambamba bila kuwadhania vibaya kama inavyoelezewa hali za kwenda kinyume na muktadha wa dhana njema, mengi yanayonukuliwa kwao ni uzushi wa kibaguzi katika haki yao wala hayana asili yeyote, na yaliyothibiti kunukuliwa toka kwao kumekuwa na maelezo, lakini akili haikuweza kuonesha makosa, na kubeba vitendo vyao kwa makusudio mazuri hata kama hawakufikia. Kitabu cha: [Al-Iqtisaad fii Al-Iitikaad uk 79]. Na anasema Al-Ghazaliy pia katika kitabu cha: [Al-Ahyaau] katika maelezo yanayapaswa kwa Muumini kuamini:....na kufanya dhana njema kwa Masahaba wote ikiwa ni pamoja na kuwasifu kama vile walivyosifiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na Mtume wake S.A.W. yote hayo ni katika yaliyopokelewa habari zake na kushuhudiwa athari zake, basi mwenye kuamini yote hayo akiwa na yakini nayo basi anakuwa ni katika watu wa haki na Sunna, na yupo tofauti na upotevu na kundi la uzushi wa dini”.
Hii ni kwa Masahaba wote, ama maelezo kuhusu Abi Hurairah R.A. amesema Imamu Abu Bakr Muhammad Ibn Is’haq Ibn Khuzaimah: Anazungumzia habari za Abi Hurairah ili kuzisukuma mbele habari zake kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa upofu wa mioyo yao wala hawafahamu maana ya habari, wanamtukana Abu Hurairah na wakimtuhumu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amemvua nayo ikiwa ni wito kwa wajinga kuwa habari zake hawawezi kuzithibitisha kwa hoja zao, ama kwa nje wanaona upanga kwa Umma wa Muhammad S.A.W. hivyo hawaoni utiifu kwa Khalifa wala Imamu, pindi wanaposikia habari za Abi Hurairah R.A. toka kwa Mtume S.A.W. tofauti na madhehebu yao ambayo ni upotovu wanakosa hila kuondoa habari zake kwa hoja na dalili, pindi tunapoangalia habari za Abu Hurairah ambazo zimepokelewa toka kwa Mtume S.A.W. katika kuthibitisha nafsi yake wanakosa hoja ya kuthibitisha usahihi wa makala yake ambayo ni ukafiri na ushirikina, lakini hoja ndani ya nafsi yake ni kwamba anaona kuwa habari za Abu Hurairah hazikubali hoja, na kujenga hoja kwa yule anayetofautiana naye na kukubaliana na yule anayekuwa habari za Abu Hurairah zinakubaliana na madhehebu yake, baadhi wamepinga tofauti hizi juu ya Abu Hurairah kwa kuwa hao hawajafahamu maana ya habari zake. Yameelezwa haya na Hakim katika kitabu cha: [Mustadraku 3/586].
Ama hukumu ya kifiqihi katika hilo: Hakuna tofauti kati ya wanachuoni kuwa ni haramu kumtukana Sahaba R.A. kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Wala musiwatukane Masahaba wangu, kwani mmoja wenu ikiwa atatoa sadaka dhahabu yenye ukubwa wa mlima wa uhudi hawezi fikia kiwango kilichotolewa na mmoja wao wala nafasi yake”. Wamekubaliana jopo la wanachuoni kuwa mtu huyo anakuwa ni fasiki na miongoni mwao wapo waliomkufurisha.
Amesema Ibn Hajar Al-Haitimy: Wamesema Masheikh wawili na wengineo kuwa kumtukana Sahaba ni katika dhambi kubwa, amesema Al-Jalal Al-Bulqiny: Naye akiwa tofauti na wengi, ni uzushi wenye dalili ya kuacha Sunna, yeyote mwenye kumtukana Sahaba atakuwa amefanya dhambi kubwa bila ya mvutano wowote”. Kitabu cha: [Zawaajir 3/332].
Amesema Ibn Taimiya: Ama mwenye kuwatukana Masahaba hatawafedhehesha kwenye uadilifu wao wala kwenye dini yao mfano kuwaelezea baadhi yao kuwa na sifa ya ubahili au woga au kuwa na elimu chache au kutokuwa na hali ya kuipa nyongo dunia na mfano wa hayo, kwa haya ndio anayostahiki mtu kutiwa adabu au kuadhiriwa, wala hatumuhukumu kuwa amekufuru kwa kuwazungumzia hivyo tu, na katika hili inachukuwa na maneno ya wasiokufurishwa na wasomi”. Kitabu cha: [Swaarim Al-Masloul uk 590].
Al-Khatwib Al-Baghdadiy ameweka somo ndani ya kitabu chake cha: [Al-Kifaayah uk 46, 49] ametaja baadhi ya maandiko yanayoonesha uadilifu wa Sahaba, kisha akakamilisha mlango kwa yale yaliyopokelewa kwa upokezi Imamu Aby Zur’aa Raazy – naye ni katika wazungumzaji wakubwa wa Hadithi – amesema: Pindi ukimuona mtu anamchafua Sahaba yeyote wa Mtume S.A.W. basi fahamu kuwa huyo ni zindiki, na hilo ni kwakuwa Mtume S.A.W. kwetu sisi ni Mtume wa kweli, na Qur`ani Tukufu ni haki, lakini imetufikia sisi Qur`ani na Sunna kupitia Masahaba wa Mtume S.A.W. lakini wanaotaka kuwajeruhi mashahidi wetu ili wapate kubatilisha Qur`ani na Sunna basi kuwajeruhi wao ni bora zaidi kwani wao ni mazindiki”.
Ama jumla ya uchambuzi wa kina juu ya madai ya mwandishi na majibu yake ni haya:
• Ama kumchafua kwa sifa ya umasikini, ni katika jambo kubwa la kumuheshimu mtu masikini hasa masikini katika Masahaba ambao wametangulia katika Imani, kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake S.A.W.: {Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake}, na kisha Mtume S.A.W. alikuwa akiwatukuza sana watu masikini na akiwakirimu hasa watu wa Suffah, nao ni masikini waliohama na Mtume S.A.W. ambao walikuwa wanakuja kwenye maeneo ya kivuli ya Msikiti wakifikia hapo na kuungana na kila aliyekuja hapo na wakawa wengi, walikuwa ni wenye umasikini mkubwa na subira, walipewa umuhimu sana na Hafidh Abu Nuaim mwanzoni mwa kitabu chake cha: [Huliyatu Al-Auliyaau].
• Ama kumchafua kuwa alikuwa akichunga mbuzi, hii ni sifa kwake, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenyezi Mungu hakutuma Nabii isipokuwa alikuwa akichunga mbuzi”. Wakamuuliza Masahaba wake na wewe pia? Akasema: “Ndio nilikuwa nachunga mbuzi kwa watu wa Makkah”. Imepokelewa na Al Al Al Bukhariyyy. Kwa sababu kazi hiyo ya kuchunga mbuzi hulainisha moyo na kumuandaa mchungaji kuwa na upole mzuri kwa wananchi wake, na hili ndio lililotokea kwake pindi alipokuwa kiongozi Madina kama maelezo yatakavyo kuja.
• Ama madai yao kuwa alidharauliwa katika mazungumzo baada ya vita vya Hunain, jambo hili lilikuwa ni kati ya Abaan na Abi Hurairah, Abaan hakuzungumza isipokuwa baada ya kuongea Abu Hurairah, huyu ni Kaatil Ibn Kaukal mmoja wa Sahaba na alikuwa katika vita vya Uhud, na wala hakuwa kwa sababu ya mgawira, ama kutaka mali ya ngawira kumekuwa na tofauti kwa wapokezi, baadhi yao wanasema alikuwa ni Abu Hurairah, na wengine wanasema alikuwa Abaan, na akawajumlisha Ibn Hajar wote kuwa walitaka mali ya ngawira, na wote wawili hawakupewa chochote, basi ni kwanini wanamshambulia Abu Hurairah pasi na Abaan, kama vile mtu kutaka mali ya ngawira kwa dhana kuwa anaona na yeye ana haki si jambo la kumuaibisha, wametofautiana vijana na wazee katika ngawira mpaka Mwenyezi Mungu akateremsha kauli yake: {Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini}, na watu wa badri ni miongoni mwa Masahaba bora kabisa.
• Ama madai yao kuwa alisilimu kwa sababu ya chakula, ni kuingia kwenye usafi wa nia ya Masahaba watakatifu, na kuwachafua katika ukweli wao na uzuri wa Uislamu wao, na hii ni katika utovu wa adabu na kukosa haya, inafahamika kuwa kuacha nchi kwenda kwa mtu Waarabu wote wamemrushia mishale kwa upinde mmoja si katika jambo la udhalilifu bali ni katika mambo ya kuazimiwa.
• Ama kumuaibiasha kuwa jina lake halikuwa lenye kufahamika lakini alifahamika kwa jina la kutungwa hili halina maana yoyote, kwani ni wangapi katika Masahaba na wanachuoni wasiofahamika majina yao isipokuwa wanafahamika kwa majina ya kupewa au ya kutungwa au kwa uchache walipata umaarufu kwa sababu hiyo ambapo walikuwa wakitajwa kwa majina yao hawakufahamika.
• Ama kumuaibisha kuwa paka alikuwa anaishi naye, hii inaonesha ujinga wa mwandishi na kupoteza mizani, ambapo ameizingati sifa ya huruma kuwa ni aibu na tuhuma, na Uislamu hivi haujatoa umuhimu kwa wanyama na kuwafanyia huruma iwe ni aibu, jambo hili haliwezi kupingwa na mtu mwenye akili.
Usahihi katika hilo ni Hadithi iliyopokelewa na Tirmidhy na kuifanya ni Hadithi yenye Hukumu ya Hasan katika yale aliyokuwa akihadithia masiku ya utoto wake: “Nilikuwa ninachunga mbuzi wa ndugu zangu, nilikuwa nina paka mdogo, nilikuwa usiku namuweka kwenye mti pindi unapoingia mchana alikuja akawa ananifuata na nikicheza naye, ndipo wakaniita baba wa paka”, ama tofauti na hivyo si sahihi, na Mtume S.A.W. huenda alikuwa anamwita kwa jina hili la kupachikwa ikiwa ni kumsifu kwa huruma yake na upole aliokuwa nao.
• Ama kumdhilisha kuwa kwake mjinga asiyejua kusoma wala kuandika, sifa hii ilikuwa kwa waarabu wote kwa mujibu wa andiko la Qur`ani, na Masahaba wengi walikuwa na hali hiyo, bali Tirmidhy anapokea kuhusu Abi Hurairah R.A. katika suna yake Hadithi anaisema kuwa ni Hadithi hasan na sahihi: “Hakuna mtu mwenye upokezi wa Hadithi nyingi toka kwa Mtume S.A.W. zaidi ya Abdillah Ibn Omar, kwani alikuwa akiandika na nilikuwa mimi si andiki”.
• Madai kuwa Omar alimtuma huko Bahrain kwa sababu ni katika Masahaba wadogo, na kuwa alimhukumu kwa mali yake na kumpiga. Jibu ni kuwa Omar R.A. hakuwa akiwatumia isipokuwa waja wema, na hakuwa akimsisitiza kwa nguvu Abi Hurairah R.A. ikiwa ni kumfanyia hiyana, lakini ilikuwa ni jitihada kwao wote wawili katika jambo la mali, na dalili ya hilo ni kuwa Omar R.A. alimtaka Abi Hurairah afanya kazi baada ya hapo Abu Hurairah alikataa – kama ilivyokuja kwenye kitabu Al-Istiiaab – na hii inaonesha ni ufuataji ule ule usio na mtazamo, na dalili ya mkazo huo haukuwa kwa Abi Hurairah bali ilikuwa Omar anafanya kwa watu wote, na hili linafahamika sana kwake Omar, inatutosha katika uzushi huu kisa cha Muadh pindi alipokuwa na mlimbikizo wa madeni ikiwa ni matokeo ya ukaribu wake na wema wake, Mtume S.A.W. alimtuma kwenda Yemen ili kwenda kukusanya mali, pindi aliporudi Muadh Madinah Omar pia alimtilia mkazo pia mpaka akaingilia kati Abubakri Siddiq na alikuwa ni Khalifa, kisha baada ya hapo pindi Omar alipochukuwa Ukhalifa na alipofairiki Abu Ubaidah kiongozi wa Shamu, Omar alimpeleka Muadh huko Shamu, lau ingekuwa msukumo wa Omar kwa viongozi ni kuwafanyia hiyana basi asingempa uongozi Muadh kuongoza Shamu baada ya kutokea hayo wakati wa utawala wa Abubakari.
• Kumchafua kuwa alikuwa ni mfanyakazi wa binti wa Ghazwan ili apate kujaza tumbo lake, inatosha kufanya kazi kuwa ni jambo la fahari kwani Nabii aliyezungumza na Mungu Musa A.S alifanya kazi ya kuajiriwa, kama alivyosema Mola Mtukufu: {Akasema: Mimi nataka kukuoza mmoja wapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi khiari yako}, kisa kizima kimenukuliwa kwenye kitabu cha: [Al-Iswabah cha Hafidh Ibn Hajar] kwa umuhimu zaidi, anasema Hafidh: Na katika kitabu cha [Historia ya Abi Abbas As-Siraaj] kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Mudharib Ibn Hazan: Nilikuwa natembea usiku mara akatokea mtu akitoa takbeer, nikakutana naye na nikamuuliza: Ni nini hii? Akasema: Ni kufanya wingi wa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu nilikuwa ni mwenye kuajiriwa kwa Busra Bint Ghazwan kwa kulisha kipando changu na kulisha tumbo langu, pindi wanapopanda nina waendesha na wanapokuwa wameteremka basi nina wahudumia basi Mwenyezi Mungu akaniruzuku kumuoa, hivi sasa mimi ninapanda na nikiteremka nina hudumiwa. Angalia unyenyekevu wake na kutambua kwake fadhila za Mwenyezi Mungu kwake, na wala hakufanya vitendo vya watu wenye kiburi.
• Madai yao kuwa ameweka Hadithi kwa msaada wa jafar, kwa sababu Abu Hurairah alikuwa akimfanyia sana wema, inaonesha wazi juu ya ujinga mkubwa, kwa sababu Aba Hurairah hakunasibishwa hivyo kwa Mtume S.A.W. lakini ni rai ilionekana kama walivyo Masahaba wengine, lakini mwandishi ameingia katika hili kutokana na kutokuwa na uelewa wa tofauti kati ya Hadithi iliyoinuliwa mpaka kwa Mtume S.A.W. na Hadithi iliyosimamishwa, kisha baada ya hapo anakuja na kuzungumzia ya Abi Huraira na Al Bukhariy.
• Ama kutaja kisa cha njaa yake na kuulizwa na Omar maana ya Aya, ili apate chakula, ndani yake kuna uchukuaji wa maneno, Aba Hurairah hakuomba chakula isipokuwa ni hali yake ya kutokuwa na matamanio ya vitu nalo ni jambo halali hasa kwa aliyefikwa na hali ya njaa, au huenda hakuwa na chakula na aliona haya kuomba na hili si jambo geni, isipokuwa hili limetokea kwa Omar na Abubakri, bali hata kwa mja bora wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kama ilivyokuja katika Hadithi iliyopokelewa na Muslim: Siku moja Mtume S.A.W. alitoka tahamaki akakutana na Abubakri na Omar akasema: “Ni kitu gani kilichokutoeni nyinyi majumbani kwenu ndani ya wakati huu? Wakasema: Njaa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Na mimi naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake kilichonitoa mimi ni kile kilichokutoeni nyinyi, simameni” wakasimama na Mtume mpaka akaja mtu katika wa Maanswaari Madinah. Akataja Hadithi, hivyo anasemaje mwandishi wa hili?.
• Ama kisa cha kutumwa yeye na Alaa kumlingania Mundhir Ibn Sawy Uislamu hakuna kinachofahamika katika hilo isipokuwa ni ubora wa muhusika, ama kutumwa kwake pamoja na ujumbe kwa umuhimu huu inaonesha juu ya imani iliyopo kwake, ama wasia wake kwa Amir ni kuna heri na nimsisitizo kuwa anampenda na wala sio kinyume, na kumteua Abi Hurairah kusoma adhana huko inaonesha juu ya ubora wake, na imetokea kutumwa Masahaba wengi kama vile Muadh, Khaalid na Abi Mussa, basi ni kutoka wapi anamuhusisha mmoja tu miongoni mwao kwa nia ya kukanusha, lau angetaka Mtume S.A.W. kukataa kitendo kama alivyokataa Hakam Ibn Abi Al-Aas kwenda Taif, pamoja na kuwa kwake ni mwenye nguvu zaidi ya Abi Hurairah, na kisa cha kukataa Hakam kimethibiti katika kitabu cha: [Al-Iswabah] na vitabu vyengine.
• Ama kuwa mwenye wingi wa utani, asili katika utani ni jambo halali, na kisa cha utani wake kwa watoto kinaonesha ubora wake, kwa sababu hakufanya hivyo isipokuwa na yeye alikuwa ni kiongozi wa Madinah, na hii inaonesha juu ya ukubwa wa unyenyekevu wake na uzuri wa kujumuika kwake. Na asili ya kucheza na watoto imepokelewa katika Sunna kwenye Hadithi ya kucheza kwa Mtume S.A.W. na mmoja wao pindi alipofariki ndege wake akamwambia: Ewe Baba wa Umair amefanya nini kinda wa ndege wako? Na Mtume S.A.W. alikuwa akifanya utani lakini hasemi isipokuwa ni jambo la kweli.
• Ama kauli kuwa yeye anadai kuwa na ufahamu wa masuala ya utabibu, haikuja kutoka kwake isipokuwa kauli moja, na hilo ni maalumu zaidi ya madai, kama vile mtu kunukuu maneno ya watu wa tiba kwa utamaduni wa zama zake hakuna ubaya katika hilo. Hii kwa kuchukulia limethitibi hilo kwake.
• Ama kukimbia kwake vita ya muutah, ni jambo la ajabu, jambo linalofahamika ni kuwa jeshi la Kiislamu kwa ukamilifu liliondoka eneo la bahilah kutoka kwa Khalid Ibn Al-Waleed baada ya vita vikali, ikiwa mwandishi anaona hivyo ni kukimbia basi iweje amemuhusisha Abu Hurairah pasi na wapiganaji wengine kwenye hili?
• Ama kunukuu kwake kuwa ilikuwa katika masiku aliyokuwa swiffain akiswali nyuma ya Imamu Ally na kukaa kwenye meza ya Muawiyah na kula naye, pindi alipoulizwa hilo akajibu: Kula chakula kwa Muawiyah ni sehemu bora, na kuswali nyuma ya Ally kuna ubora, na ubora una ukamilifu zaidi, kwa sababu hiyo alipata umaarufu kwa jina la sheikh wa chakula, na yeye hakushiriki kwenye vita na makundi mawili, kisa hiki kinapatikana ndani ya baadhi ya vitabu vya fasihi bila kuwa na mapokeo, kama alivyosema Zamakhshariy katika kitabu Rabii Al-Abraar na Ibn Abi Al-Hadeed katika cha: [Sherehe ya Nahaji Al-Balaaghah] wakiwa wamenukuu kutoka mapokezi mbalimbali yanayo kubaliana na madhehebu yao hata bila ya mapokezi, kama vile hakuwa maarufu kwa hili isipokuwa kwa watu wenye kupenda matamanio, ikiwa tutapitisha usahihi wa kisa kwa mfano basi hakuna mapungufu wakati wa kukizingatia na kuleta uadilifu, ama kunukuu kwake kati ya makundi mawili wakati wa vita, hii inaonesha kuwa ikiwa ni katika watu wa kuaminika basi lisingekuwa kundi lolote na woga ujasusi wake kwa kundi lingine, ama kauli yake “Swala na Ally ni yenye ukamilifu” na chakula kwenye meza ya Muawiyah inaonesha juu ya nguvu ya haiba, lau angekuwa anataka chakula basi angefanya udanganyifu katika hilo, lakini wakati huo alishakuwa ni mwenye uwezo. Ama kutoshiriki kwake vita hakuoneshi woga, bali inaonesha kuwa alichagua kusimama kupigana na vita na moja ya makundi mawili, na hili lishafanywa na Masahaba wengi, miongoni mwao ni Abdillah Ibn Omar, Saad Ibn Abi Wiqaas naye ni mmoja kati ya kumi na mbili waliobashiriwa Pepo.
• Ama nukuu yake kuwa Omar alimzuia kupokea Hadithi, na kauli yake kuwa anazungumza Hadithi lau atasikia Omar basi angemtikisa kichwa chake, jibu ni kuwa kisa hiki hakifai, lakini kunapatikana kwa mfano kwenye kitabu cha Ibn Abi Al-Hadeed, kama tutachukulia kwa mfano ni kisa sahihi, basi jambo linalofahamika ni kuwa ukali wa Omar katika kuzuia kupokea Hadithi basi kungekuwa kwa Masahaba wote, na kisa chake na Abi Musa katika Hadithi ya kutaka ruhusa iliyopo kwenye kitabu cha Hadithi cha Muslim, amri haikuambatana siku zote kwa Abi Hurairah peke yake, lau itakuwa ni sahihi basi lingechukuliwa kwenye Hadithi zilizokuja katika mambo ya ruhusa au fitina jambo ambalo linapaswa kufahamika hekima katika kupokelewa kwake.
• Ama aliyo yaashiria mwanzoni mwa makala kuwa ameondoa stara ya Imamu Al Bukhariy na kitabu chake, Imamu Al Bukhariy ni Imamu wa wazungumzaji wa Hadithi na waandishi wake sahihi, kitabu chake ni sahihi zaidi baada ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ilivyotajwa katika kitabu cha somo la mustalah, ama kukichafua kitabu chake kwa sababu ya baadhi ya Hadithi ambazo hazifahamiki kwa baadhi ya akili za hawa hakubadilishi ukweli, na jibu ya hilo ni lile alilojibu Imamu wa Maimamu Muhammad Ibn Is’haqa Ibn Khuzaimah katika maelezo yake aliyoyatoa katika kumtetea Abi Hurairah R.A.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia na kwa mujibu wa swali, mwenye kuwazumgumzia vibaya Maswahaba ni fasiki ambaye lazima kumrudi kwa ushahidi wake. Vilevile vile mwenye kumzungumzia vibaya Imamu Al Bukhariy, kwa sababu anazungumza katika Dini ya Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na elimu, na kuwa mwenye kuwachafua Maimamu wanukuu wa Hadithi kutoka kwa Masahaba na waliokuja baada yao ni kana kwamba anataka kukusanya sheria katika zama za kwanza pasina kuzipeleka ndani ya zama zingine, naye anakuwa ametanguliwa na mwenye kupitia njia hii na anakuwa ni kama mwenye kumuelekea mfuta historia, na mwenye kuwa hivyo basi ni haki yake kuadhiriwa, ikiwa sheria zinatoa adhabu kwa msambazaji maneno yasiyokweli kwa lengo la kueneza mfadhaiko kwa watu na kuwaletea mgongano kati yao, basi adhabu ya mtetereshaji wa Imani za Waislamu na mwenye kuleta mambo ya uongo na uzushi katika haki ya vithibiti vya dini yao na alama zao za dini basi ni bora zaidi adhabu hizo.
Basi yupo huru yule mwenye kuuza dini yake kwa dunia – bali huenda kwa dunia ya mwingine – na mwenye kutaka kupata umaarufu kupitia misingi ya dini na vitu vyake muhimu isipokuwa anatuchukuwa katika adhabu yake na kuchukuwa kwa mikono yake lawama za mwenye kulaumu, ili iwe fundisho na onyo kwa mwingine yule anayeingiza nafsi yake kwenye kutikisa amani ya jamii.
Fitina imelala, laana ya Mwenyezi Mungu imfikie yule atakaye iamsha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas