Aliyeachwa na Aliyefiwa na Mumewe, ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Aliyeachwa na Aliyefiwa na Mumewe, Kubeba Jukumu la Kumlea Mtoto.

Question

 Je! Inaruhusiwa kwa mjane, mwanamke aliyeachwa au ambaye hajaolewa, na vilevile wanaume wenye hali kama hiyo, kubeba jukumu la kulea Mtoto?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Jumuia na Tasisi ambazo hushughulika kubeba jukumu la kulea watoto huomba watu wanaotaka kubeba jukumu la kulea mtoto kwa masharti maalumu na vyeti vinavyothibitisha usahihi wa kauli yao, masharti hayo ni lazima yatekelezwe kama hayaendi kinyume na sharia ya Kiislamu.
Na masharti haya yaliyowekwa na taasisi hizo yamekuja kufuatana na tafiti za kijamii za muda mrefu na za kina, na ndani yake pamechungwa mazingira maalumu ya nchi husika na mila na desturi zake na waliofanya tafiti hizo ni wabobevu kwa ajili ya kuweka masharti hayo ya malezi ya mtoto yanayompatia Mtoto huyo maisha mazuri, na ni lazima yafanyiwe kazi yale yote yaliyomo katika miongozo ya taasisi hizo; kumtii kiongozi katika hayo, ambapo taasisi hizo zimetoa kibali cha kufanyika kwa tafiti hizo na kuweka vidhibiti kwa mujibu wa matokeo yake.
Na tangu zamani, Wanachuoni wa Fiqhi waliweka masharti kwa mwokotaji wa Mtoto – ambaye ndiye anayesimamia mtoto anayeokotwa – masharti yafuatayo: Awe mwenye kukalifishwa kwa maana ya kuwa mtu mzima mwenye akili, aliye huru, aliyebaleghe, Mwislamu, mwadilifu, kwa sababu haifai Mtu huyo awe hajafikia umri wa kukalifishwa, au kuwa mwovu, na vilevile haifai kwa mtu tu kuwa mlezi wa Mtoto aliyeokotwa bila ya kuchunguzwa na kuteuliwa hali yake hata kama mtu huyo ataonekana kwa uwazi wake kuwa ni mwaminifu, na atapokonywa haki hiyo iwapo atataka kusafiri naye kwani haaminiki na anaweza kumfanya mtumwa na atachunguzwa pale alipo kwa amri ya Kiongozi tena kwa Siri bila yeye mwenyewe kujua – na hautakuwa uchunguzi na ufuatiliaji huo wazi wazi – ili asiudhike, na ili pia asijioneshe na kufanya udanganyifu, na ikiwa ataaminiwa kwa hilo kama vile kuwa kwake mwadilifu, basi hatanyang'anywa haki ya ulezi na wala hatachunguzwa. [Isniy Al Matwaleb 496/2, Ch. ya Dar Al Kitaab Al Islamiy]
Na baadhi ya Wanachuoni wa Fiqhi wanaona kuwa ni lazima kwa mlezi wa mtoto kutokuwa na ugonjwa wa mbaranga na ukoma na mfano wa magonjwa hayo magonjwa yote ambukizi na ya hatari, na hii ikiwa ameambatana nayo. [Rejeo lililopita]
Na Mlezi anapimwa juu ya Mtoto aliyepatikana kwa ujumla kwamba mlezi anayesimamia ulezi wa mtoto kwa ulezi, matunzo, na kuchanganyika naye, na vilevile Mlezi ataifanya kazi hii na kwa hivyo, lazima masharti yote yanayotakiwa yawepo kwa mlezi wa Mtoto
Na ikiwa Wanachuoni wa Fiqhi hawamshurutishi Mlezi – ambaye ndiye anayesimamia mtoto aliyeokotwa – awe mwenye familia au mwenye ndoa au mwanaume, na hivyo ndivyo ilivyo kwa Mlezi wa Mtoto, na iwapo Kiongozi -au taasisi zilizompa kiongozi madaraka ya kubeba majukumu yake katika jambo hili- zitaona umuhimu wa kuweka masharti haya, basi ni wajibu kumtii kiongozi huyo katika jambo hilo na wala haijuzu kumpinga kwani yeye ana uwezo wa kufungamanisha Uhalali wa kitu kwa ajili ya Masilahi ya Mtu.
Na masharti yanayowekwa na taasisi hizo, mara nyingi hayaendi Kinyume na Makusudio pamoja na Sababu kuu ambazo kwa ajili yake, wanachuoni wa Fiqhi wameweka masharti yao, na kwa ajili hiyo, kufuata masharti hayo ni Wajibu wa kisheria kwani Makusudio ya Sheria ni mamoja, na kinachobadilika ni hali mbalimbali na mila na desturi za watu, kwani hizo hubadilika kutokana na mabadiliko ya sehemu na muda (mahali na wakati).
Na kutokana na maelezo hayo: Hakuna kizuizi chochote kisheria na katika uwazi, kwa Mwanamke aliyefiwa na mumewe na aliyeachwa na yule ambaye hajaolewa, na vilevile wanaume wenye hali kama hizo, kubeba jukumu la kulea Mtoto, wanaweza kumlea mtoto, kama tu hawatavunja masharti yaliyotajwa katika miongozo maalumu inayohusu Suala hili na kama hayakwenda kinyume na sheria ya Kiislamu, kama vile kuwa kwake ulezi katika hali ya kubaleghe na anayelelewa ni tofauti na mlezi wake kijinsia, na kama hapatakuwepo mkinzano wa masilahi ambayo kwa ajili yake Wanachuoni waliyaweka masharti hayo baada ya kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa.

 

Share this:

Related Fatwas