Taasisi ya Kidini Nchini Misri

Egypt's Dar Al-Ifta

Taasisi ya Kidini Nchini Misri

Question

 Istilahi ya (Taasisi ya Kidini) husikika mara kwa mara. Je, nini makusudio yake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Taasisi ya Kidini Nchini Misri inamaanisha Asasi Kubwa Nne, nazo ni: Azhar Sharifu, Chuo Kikuu cha Azhar, Wizara ya Waqfu, na Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri; nazo ni Taasisi ambazo zinafuata mifumo ya Nchi, Katiba, na Sheria zake.
Na Taasisi hizi ingawa zinafuata mifumo ya nchi lakini hazifuati Serikali isipokuwa Wizara ya Waqfu ambayo Mkuu wake ni Waziri wa Waqfu, naye ni mmoja wa Mawaziri wanaounda Serikali.
Na tofauti kati ya Nchi na Serikali ni maarufu tena mashuhuri. Nchi ni yenye kuendelea na kubakia, ingawa Serikali hubadilika na kufuatiwa na nyingine.
Na Taasisi ya Kidini Nchini Misri inalazimika na ina wajibu ambao lazima utekelezwe, na nyadhifa ambazo lazima zitekelezwe, pamoja na historia ambayo tutaionesha.
Na taarifa hii ambayo huenda kuwa kwake wazi kwa mawazo ya baadhi ya watu, inaingiliana na makosa mengi wengine. Na inadhaniwa kuwa wenye mawazo na waandishi wakubwa wameshajua ukweli huu, pamoja na kujua dhima ya Taasisi ya Kidini nchini Misri, na juhudi zake inazoitekeleza ndani ya Ulimwengu wenye mabadiliko na pia maingiliano, lakini inaonekena kuwa baadhi ya waandishi wakubwa wameshaanza kufuata mawazo ya waenezaji wa fitna, na wakawaomba msamaha, na kuwafanya kama wahanga badala ya kuwa waovu, na wengine walikuwa wakiwachanganya, hata msimamo wao unamfanya mtu akishangaa kutokana na ukosefu wao wa uhakika wa Taasisi ya Kidini, wakati yakichochewa maswali ambayo tunalazimika kuyazungumzia kwa uwazi na udhahiri, miongoni mwake ni:
1- Je, jambo lililo kati yetu na waenezaji fitna kuwa: Sisi tunasimama pamoja na mwenye madaraka, na wao wanasimama dhidi yake? Hakika tofauti kati yetu na wao ni katika njia ya uthibitishaji, kuleta dalili, makubaliano, kujibu, kuelewa, na matumizi. Kisha je, Sisi ni wenye utawala au washiriki ndani yake, au Sisi ni karibu na mwenye madaraka kuhusu azimio lake au mengine, na ziko wapi Fatwa zilizotolewa na Taasisi ya Kidini ili kumsaidia mwenye madaraka, na je, kuyaangalia mambo ya umma na kushirikiana katika masuala ya nchi ni jambo linalomsaidia mwenye madaraka?
Na Je, wale waenezaji fitna wanaohifadhiwa ndani ya Taasisi za Mashirika ya Kidini, kisha kupitia njia yake wakafikia hali ya uenezaji wa fitna? Hakuna yoyote miongoni mwa waliojifunza ndani yake anayeshiriki katika umwagaji damu, na Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu wote.
Je, Hawa waenezaji fitna hawakutunzwa huko London kwa mujibu wa mafunzo ya kimagharibi ambapo kuna migongano, kwa hiyo walifanya kila walichoweza kukifanya na kuchukua kila walichoweza kuchukua katika mawazo yasiyo ya tamaa na hayahusiani na Sharia ya Kiislamu, na hii ilisababisha pigo kubwa kote Uingereza?
Na je, waenezaji fitna wengine hawakulelewa kwa mujibu wa mafunzo ya kimagharibi, na miongoni mwao kuna Mhandisi, Daktari, na Mhasibu, wakati hakuna yoyote miongoni mwao aliyehitimu katika Chuo cha Sharia mahali popote? Na je, Bwana Blair hakueleza kuwa Kiasi cha asilimia 99,9 kati ya Waislamu ni raia wema Ulimwenguni kote, na kuwa matendo kama haya siyo ya kawaida kwa Waislamu?
Na je, Taasisi ya Kidini, hasa baada ya kuizembea na kuitupilia mbali na kuwa kwake kitovu cha kutoa maazimio muda wa miaka mia mbili, imeshindwa kubakia imara, pamoja na kutayarisha wanazuoni wanaonukulu Dini mahali popote duniani, kwa utulivu na kwa mujibu wa madhehebu ya Watu wa Sunna Wal-Jamaa na bila kugongana na yeyote, kupitia karne ya kumi na Tisa na Karne ya Ishirini, mpaka Vita ya 1973, ambapo bei ya Petroli iliongezeka kutoka Dola moja kwa Pipa hadi Dola arobaini?
Kisha tuelewe vipi dhima ya Taasisi ya Kidini imepungua huko nje kutokana na upungufu wa uwezo wa kifedha, na ghafla upungufu huu unapelekea mgongano mkubwa wa Tarehe 11 Septemba, ambao mpaka sasa tunajaribu kuzifuta athari zake, na ikiwa umefanywa na Waislamu au wasio Wailamu.

Na je, Inafaa katika hali hii kuwa sisi tunaiona punje ndani ya jicho la Taasisi ya Kidini wakati tunashindwa kuliona tawi la mtende ndani ya jicho la aliyekubali kuiitupilia mbali Taasisi ya Kidini na hakujali ushirikiano wake?
Na je, Inafaa kuita kwa ziada ya kutupilia mbali baada ya ushindi huu mkubwa kwa upande wa taasisi nyingine, na kuwapa waenezaji fitna pasipoti ya kufikia kwa watu?
Na kuwa watu wanakatishwa tamaa na Wanazuoni Wafuasi wa Sultani, na hili ni jambo linalochekesha na kuliza, bila kuchunguza sababu za kweli za tatizo ambalo linadhibitisha uhalisia, na bila kujaribu kutatua tatizo hili.
Na je, Bwana Blair ndiye aliyeitambua maana hii, kama walivyodai baadhi yao? Ni wazi kuwa yeye alitambua kinyume chake. Na Ujumbe wa Wizara ya Waqfu wa Shirika Rasmi ulipokwenda London, Baron Simmons Waziri wa Mambo ya Kigeni, pamoja na Lord Kyrie Askofu wa Kanisa la Canterbury, ambalo ni maarufu zaidi Uingereza; walikubaliana pamoja kuwa ushirikiano Taasisi ya Kidini ya Misri ni lazima, lakini kwa sasa inadaiwa kuwa wao walivunjika moyo wa kushirikiana nayo.
2- Kuna makundi ya maswali, ingawa ni wazi lakini tunahitaji tena kutilia maanani nayo. Taasisi ya Kidini imekubali Katiba, nayo inataja katika kifungu chake cha kwanza kuwa: (Dini Rasmi ya Misri ni Uislamu), na kifungu cha pili: (Sharia ya Uislamu ni chimbuko la msingi la kutunga Sheria). Hapa tunauliza swali muhimu tena la msingi: Nani ni pamoja na Katiba na nani ni dhidi yake?
3- Na Taasisi ya Kidini inaamini Masuala ya Nchi, na haiwezi kukubali au kufikiri kuomba msaada kwa Mgeni au kushirikiana naye dhidi ya nchi yetu au watu wetu kutokana na sababu, lengo, au masilahi yoyote yawayo.
Nadhani kuwa misingi hii haiambatani na Kiongozi mwenyewe, lakini imeanzishwa kwa hisia ya kimaumbile ya kuipenda Nchi, na maono ya kidini ambayo huimarisha hisia hii na kuibariki, nadhani pia kuwa hii inaendelea katika nyakati zote, na haiambatani na wakati wetu wa sasa au hali yetu tu.
4- Shirika la Kidini la Misri lina mfumo wake, nao ni kunukulu Madhehebu ya Kisunna na Madhehebu zake nne zilizo maarufu na mashuhuri: (Madhehebu ya Hanafi, Madhehebu ya Maliki, Madhehebu ya Shafi, na Madhehebu ya Hanbali), pamoja na kukubali madhehebu zingine ambazo wanazifuata Waislamu Ulimwenguni, kimsingi na kimatawi kwa mujibu wa njia ya ufahamu sahihi, nazo ni: (Madhehebu ya Jaafari, Madhehebu ya Zaidi, Madhehebu ya Ibadhi), pia Madhehebu ya (Dhahiri) ambayo makundi ya wanazuoni waliitegemeza huku na kule.
Hivyo Taasisi hii kuhusu chaguo lake la kidini, mara nyingi huwa inapanua mazingira ya kutoa dalili kwenye madhehebu ya wanaojitahidi wakubwa kama vile; Al-Awzai’iy, At-Tabariy, Al-Laith Ibn Saad, na wengineo, idadi ya wanaojitahidi ni zaidi ya themanini kupitia Historia ya Kiislamu.
Ili kupata maoni yao, na huenda kuyatilia nguvu zaidi, kwa mtazamo wa nguvu ya dalili yake, au kwa masilahi ya watu, au kwa kuleta makusudio ya Sharia Tukufu, na huo ni mfumo ambao kundi la wataalamu liliukubali katika enzi yetu hii kimashariki na kimagharibi, kwa maoni ya wenye akili miongoni mwa madhehebu zote za Waislamu. Na Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.
5- Na Taasisi ya kidini kwa upande wa kuelewa kwake Sharia Tukufu na kuelewa uhalisia uliopo, linaelekea mwelekeo wa Uthibitishaji ambao ni mmojawapo wa misingi ya Dini yetu. Na Mtume S.A.W, katika ilivyopokelewa na Muslim katika Utangulizi wa Sahihi yake, alisema: “Yatosha mtu kuwa ni muongo, anapozungumza kila alilolisikia” .
Kutokana na hayo, waislamu walianzisha Elimu ya Visomo vya Qur`ani Tukufu, kukinukulu Kitabu cha Mwenyezi Mungu bila mabadiliko wala makosa; na Elimu za Hadithi Tukufu kimapokezi na kimaudhui, ambapo wakinukulu maneno ya Mtume S.A.W, kwa mujibu wa mfumo wa kitaaluma usio wa mfano; na Elimu ya Misingi ya Fiqhi, na Elimu za lugha ya Kiarabu, kwa ajili kufahamu, kupitia elimi hizi, ufahamu madhubuti kwa matini ya Sharia ambayo tuliipokea kwa Lugha ya Waarabu.
Na mfumo huu uliwaathiri chanya kuhusu kuelewa uhalisia wao, ambapo matendo yao ya uhalisia huu yamejengeka kwa matokeo yaliyothibitishwa, na siyo kwa habari zilizodhaniwa, au kwa maoni ya huku na kule.
Na huenda wengi wa watu walidhani kuwa Taasisi ya Kidini inachelewa kwa kutekeleza wajibu wake, na baadaye inadhihiri mbele ya wote kuwa haikuchelewa, bali ni Taasisi yenye busara, na kujua vipi kuthibitisha habari, na vipi kuzithamini, na vipi kutendeana nazo.
6- Taasisi ya Kidini imeshatekeleza wajibu wake, na bado iko, na haitaacha wajibu huu kupitia hali yenye ugumu mkubwa, na inajaribu siku zote kuwa yenye uaminifu kwa Dini, Taifa, na Historia yake.
Na kama watu wakitaka kupata faida ya ujuzi wake na jitihada yake, basi ni tayari sana kufanya hivyo, na haikuchelewa, na haitafanya kinyume cha hivyo, lakini wasipotaka na wakaipa mgongo, basi wao watapoteza mema mengi kwa nafsi zao, na kama wakasisitiza kuipa mgongo, basi wao ni wenye hasara.
Ama kujaalia Taasisi hii kama kibanio cha kubandika juu yake makosa ya wengine, na yanayopita na kuchochea ndani nafsi zao, basi hayo si miongoni mwa tabia njema, wala semi za kweli, bali ni kasoro ya uungwana, na kuzuia ufahamu mwingi.
7- Hakika kulikuwa, mwishoni mwa Karne ya Kumi na Tisa na mwanzoni mwa Karne ya Ishirini, hujuma kali dhidi ya Taasisi ya Kidini ya Misri, na kulikuwa na misimamo ya kuchekesha ambayo huonesha lililo nyuma yake. Lakini Taasisi ya Kidini iliendelea kuutekeleza wajibu wake wa kidini na wa kijamii, pia baadhi ya watu hawa waliendelea kuihujumu, bila kuelewa kuwepo kwake, kuendelea, na kupanuka kwake, na bila kuelewa kuwa: hujuma dhidi ya Taasisi ya Kidini inajengeka kwa mawazo na habari tu, bila kuelewa kisahihi uhalisia au uchanganuzi halisi.
Jambo linaloonesha kuwa: Leo inafanana kabisa na jana. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyopiga mifano ya Haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano}.
1- Muhammad Ali Basha baada ya kuitenganisha Taasisi ya Kidini na maisha ya kiraia, na Kumuondoa Omar Makram, na kutuma ujumbe kwenda Ufaransa, kwa ajili ya kuingiza fikra ya kuwa na Nchi ya kisasa, na akaambatanisha sambamba na Mfumo wa Elimu, basi tukawa na mifumo miwili: Elimu ya Kiraia na Elimu ya Kidini.
Na bila kujali maoni ya kimalezi na athari ya kijamii kuhusu usambamba wa Elimu, hakika hali hii bado inaendelea kuwepo mpaka leo, pamoja na fumbuzi nyingi zilizopatikana, ambazo tunaweza kuzijadili baadaye.
Nasema kuwa Muhammad Ali baada kufanya hivyo, kisha kutokea Ukoloni wa Uingereza Nchini Misri, kwa athari zote za kinafsi na kijamii, tuliona hujuma kali dhidi ya Imamu Muhammad Abdo, na hapo kulikuwepo Gazeti liitwalo (Himarat Minetiy) yaani (Punda wa mtu aitwaye Minetiy), ambalo lilikuwa likimshambulia Imamu katika machapisho mengi, hata muuzaji wa Gazeti hili naye alimshambulia Imamu – kama walivyotuambia Masheikh wetu walioona hivyo kinaganaga kwenye Mlango wa Al-Muzayinin, mmoja kati ya milango ya Msikiti Mtukufu wa Al-Azhar – Sehemu ya kutokea Imamu huyu pamoja na wanafunzi wake, baada ya kumaliza masomo, basi muuzaji wa gazeti alikuwa akipaza sauti na kusema: (Al-Mufty wal Himara), yaani (Mufti na Punda).
Hapo Imamu alikuwa akitabasamu na kumpa Pauni moja ya dhahabu kama bei ya Gazeti, ambalo bei yake wakati huo haikuzidi senti chache, baada ya kupita muda, muuzaji huyu baada ya kuitumia hii Pauni – ambayo ilikuwa na thamani kubwa wakati huo – kisha baada ya mwezi mmoja au miezi miwili, muuzaji alikuwa akipaza sauti tena, hapo Imamu akawa anamwambia: je, mali imeisha? Na kumpa pauni nyingine, hali ya kuwa ni mwenye kutabasamu.
Na ingawa Imamu alikuwa rafiki wa Mtawala wa Misri (Al-Khidewiy) lakini Kiongozi huyo alizuia Imamu asipewe sehemu ya mali ya Waqfu – Imamu alikuwa Msimamizi wa Mali ya Waqfu ya Kiislamu – kwa hiyo Magazeti yalimhujumu Imamu Muhamad Abdo, ole wao mwishoni! Sasa magazeti haya yalikwenda wapi? Na Kuna anayesikia habari zake? Lakini Muhammad Abdo alibaki kuwa Imamu, mwenye mwelekeo wa Marekibisho na Matengenezo, na watu bado wanamkumbuka na kumsherehekea mpaka leo, na sasa hivi tunaadhimisha miaka mia ya kifo chake.
2- Na Mwandishi Ahmad Amin katika kitabu chake kizuri Hayaty (Maisha yangu) anataja kuwa: Amepata maudhi mengi kutoka kwa watu kutokana na kuvaa vazi lake ka Kiazhari, wakati alipokuwa mdogo, na akaeleza: namna watu wa kawaida wanavyowashambulia wamazuoni hata wakitembea barabarani.
Na ingawa hali hii ipo lakini Taasisi ya Kidini bado inaendelea kuwa na subira na kutafuta thawabu na kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu, na haitaki thawabu wala kushukuriwa na mtu yeyote.
Mpaka kutokea Mapinduzi ya Mwaka 1919 ya Misri, na wote waliporejea kwenye hali ya upole, ambayo ilichochea mapinduzi mara mbili zaidi dhidi ya Wafaransa wakoloni, na mmoja wa Wafuasi wa Taasisi za Kidini ndiye aliyemuua Generali Kleber, kisha Generali wa Tatu wa uongozi Menou (Abdullahi Menou) akasilimu, na akamuoa Zubaida Al-Bakry; na kupitia Mapinduzi ya Mwaka 1919, watu wote walisahau msimamo wao dhidi ya Taasisi ya Kidini, hali kadhalika Taasisi ya Kidini nayo pia ikausahau msimamo wa watu dhidi yake, na ikaungana nao.
3- Na tukisoma Kazi kamili za Mshairi Beram At-Tunisiy tukano laana za wazi dhidi ya Sheikh Muhammad Bakhit Al-Muttii’iy katika matamshi mabaya, ambayo hatuwezi kuyataja hapa, pia tunaona matusi na laana dhidi ya Azhar na Sheikh wake, ambayo pia hatuwezi kuyataja, kwa sababu yanauchupa mpaka wa adabu, pamoja na uhalifu wake dhidi ya Mfumo na Mila na Desturi za umma, ambao unajenga kosa la jinai kwa kuyakiuka hayo yote, na inaweza kurejelewa huko.
Lakini nini kilichotokea baadaye? Kilichotokea baadaye ni kuwa: Beram At-Tunisiy alitubu, akaitangaza toba yake hadharani, na akawakataza wengine wasiyasimulie yale aliyoyasema na kusababisha uchochezi ndani yake, hapo aliyetubu basi Mwenyezi mungu aikubali toba yake. Hata yeye alianzisha kasida yake, iliyoimbwa na Mwimbaji Mashuhuri Ummu Kulthum: (Aliniita, na mimi nilimuitika hadi katika Mlango wa Nyumba yake).
Na toba yake ilikuwa ya kweli, ambapo Beram alirejea kwa Mola wake Jamii yake, na Dini yake, na akayamalizia maisha yake kwa mwisho mwema wenye faraja.
4- Kwa maneno mengine, kuna wanaoikosoa Taasisi ya Kidini, na sisi tunahusiana na hao waliojuliwa kwa uzalendo, mageuzi, na mawazo yaliyonyooka, wakati tunaachana na wale wasio na sifa hizi, ambapo hatuna kabisa mazungumzo nao. Na kuhusu waaminifu miongoni mwao, tunajua kuwa maneno yao yametoka kwa madhumuni ya kutaka mageuzi na siyo kwa kutaka uchochezi, na kwa manufaa na siyo kwa madhara. Na tunajadili nao kwa madhumuni ya kufikia lengo linalowanufaisha watu katika siku hizi na zijao.
Mwandishi Mkubwa Salama Ahmad salama aliandika makala, Alhamisi ya tarehe 14/7/2005 katika Gazeti la Al-Ahraam, na andiko lenyewe ni: (Kwa maoni yangu kuwa Wanazuoni wa Waislamu, au kwa maneno mengine Wanazuoni wa Utawala katika Ulimwengu wa Kiislamu hawakuwa tena na sifa ya kukabiliana na upotovu na mabadiliko ambayo yanauathiri Uislamu. Na hasa baada ya kutokea maambatano kati ya Taasisi ya Kidini na Mashirika ya Taifa, hapo Waislamu walijinyimwa kusikia Fatwa zao, hali kadhalika makatazo yao kwa kuwa na misimamo mikali kwa Jina la Dini, hayakupata tena wa kuyasikia. Na Taasisi ya Kidini inapotoa Fatwa kwa mujibu wa maombi fulani na kwa malengo ya kisiasa, basi huleta msukosuko unaoporomosha uaminifu wake chini kwa chini).
Maneno haya huenda yakatolewa kwa moyo unaobeba machungu ya Waislamu, lakini yana matokeo ambayo tunalazimika kuyatanabahisha; kwa sababu yanatumiwa kinyume na kusudio lake, na sisi sote tunalazimika kusimama dhidi ya matokeo haya, pamoja na mwandishi wake.
Na je, ni kweli kuwa maoni haya ya mwandishi yapo? Twende tukajadili suala hili kwa mujibu wa uhalisia, na siyo kwa maoni binafsi au maamuzi ya mapema.
5- Kupitia Historia ya Kiislamu yamedhihiri makundi mengi katika Mashariki na Magharibi ya Dunia, na yameupotosha ukweli, yameeneza fitna, na kusababisha mauaji; na wakati huu Wanazuoni Waislamu walikuwa ngome ambayo haya makundi yote hayakufanikiwa kwa kuwepo kwa wanazuoni hawa, na hali hii ilitokea kwa sababu mbili:
Kwanza: Maneno ya Wanazuoni hujengeka kwa mfumo sahihi wa kitaalamu. Pili: Maneno ya watu wa matamanio na bidaa ni kinyume cha maumbile sahihi, pia ni kinyume cha kanuni ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe vyake.
Na kwa kufuatana na wakati, upotovu huu haukutulia wala kumalizika na hautaisha, na hivyo si kwa sababu ya ushindi wa Wanazuoni wote, kama alivyodhani mwandishi, na pia si kwa sababu kuwa Wanazuoni ni wa utawala, au kuwa Dini haisemi kitu katika Siasa, wala kuwa Taifa linatumia Wanazuoni katika misimamo ya kisiasa; hayo yote ni maelezo ya kasoro juu ya suala zima.
Na upotovu huu umejitokeza kwa sababu ya kupinga marejeo, na sababu ya hii ni mielekeo, matamanio, na masilahi mbali mbali ambayo yamo mikononi mwa Viongozi wa Makundi, au watu wa kawaida ambao hawajui pa kuichukulia Dini yao.
Na makundi haya kupitia Historia, ama yanawabagua watu na Machimbuko ya Sharia (Qur`ani na Sunna) au kuwabagua Wanazuoni wao. Kwa hiyo maneno ya mwandishi huchochea maudhui nyingine yenye hatari, nayo ni yeye kuwaita watu na Wanazuoni pia watangaze upinzanj kwa Utawala, ili wathibitishe hali ya upinzani kwa upinzani tu, au kupinga kwa Nidhamu na Jamii, ili pasemwe kuwa fulani ni mwanazuoni jasiri, na watu wasikie maneno yake, na yeye ni miongoni mwa waliodhihirisha haki mbele ya mtawala dhalimu, jambo ambalo huleta faraja kwa mwanadamu. Lakini je, hii inakubalika?
Hakika Wanazuoni wanatekeleza wajibu huu siyo kwa njia ya kutangaza kuwepo tu, au kuiomba Dunia, bali wanasema haki pamoja na kutoa dalili yake, na kuomba radhi zake Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kutekeleza makusudio ya Sharia na masilahi ya watu, na wanazungumzia mambo ya nchi kwa maana pana zaidi, na hapo kuna anayehisi uchungu, kwa sababu Mwanazuoni analazimika kubaki misikitini tu, na jambo hili hasa ndilo lililosababisha fikra ya Ugaidi, pamoja na sababu zingine ambazo tutazijadili kwa mfululizo.
Tumuulize mwandishi: Zipi Fatwa zilizotolewa kwa mujibu wa ombi, na Waislamu wakazuia kuzisikia? Na je, wauaji ndio Waislamu? na mwandishi anakusudia nini kwa usemi huu wa jumla (Waislamu walizuia)? Je, hii sio kinyume cha kweli? Ayaite makundi ya waenezaji fitna pamoja na wengine wanaopotosha kwa kauli kama (Waislamu), wakati neno hili ni la jumla.
Hebu, tumuombe mwandishi mkubwa ayarejee maoni yake, na ataje Fatwa moja au mbili miongoni mwa zile zilizotolewa kwa mujibu wa maombi. Na inatakiwa watu wote wajue tofauti kati ya Fatwa, mawaidha, na maoni binafsi, na inatakiwa pia watu wajue kuwa kutoa kauli kiholela, bila kuthibitisha, na kuichukua pasipo na vyanzo vyake, na kutegemea habari zinazoenea kama chimbuko, hayo yote ni kinyume cha Uthibitishaji ambao ni njia ya kuielewa Haki yenyewe.
6- Na uhalisia wa Taasisi ya Kidini ni kwamba bado inatekeleza wajibu wake wa Kitaifa, Kijimbo, na Kiislamu, na daima iko na uongozi tangu mwanzoni, kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu. Haturidhishwi na uhalisia wetu, na hatujitoshelezi kwa mafanikio yetu, lakini hakika inalazimika ijulikane hivyo, hasa kwa kuwa sisi tuko katika Ulimwengu wa kubadilika, na kuwa lugha ya tarakimu pamoja na lugha ya maudhui ni dalili ya hayo.
7- Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri ilianzishwa Mwaka wa 1895, na Mufti wake wa kwanza alikuwa ni Mheshimiwa Imamu Mkuu Sheikh wa Azhar katika wakati huo, Sheikh Hassuna Nawawiy, kisha akafuatiwa na Imamu Muhammad Abdo, kuanzia mwaka wa 1899 mpaka 1905 alipofariki kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu.
Na kupitia miaka hii sita, Imamu Muhammad Abdo alitoa idadi ya Fatwa 964, ambazo ziliandikwa katika Kumbukumbu za Ofisi ya kutoa Fatwa, na idadi ya wakazi wa Misri kwa wakati huo ilikuwa haizidi milioni kumi.
Na baada miaka mia mpaka sasa, bado Taasisi ipo inatekeleza majukumu yake katika Jengo jipya ambalo ndani yake kuna vyombo vyenye teknolojia ya kisasa, k.v. tarakilishi, na vyombo mbalimbali vya maendeleo ya mawasiliano, pia Ofisi hii ililihama Jumba la Riyadh Basha, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Misri, lililoko katika Jumba la Mahakama za Abbasiya kwenye Jengo kuu lililo karibu na Ofisi za Sheikh Mkuu wa Azhar, Barabara ya Salah Salim, Kairo.
Na Msimamizi wa kutayarisha jengo hili jipya, na aliyetoa msukumo wa kazi hiyo alikuwa Mheshimiwa Imamu mkuu Prf Dkt Muhammad Sayed Tantawiy, Sheikh wa Azhar, alipotawala kazi ya Umufti, Mwaka wa 1986, na ujenzi wa jengo hili Mwaka wa 1992.
Idadi ya Fatwa zinazotolewa kila mwezi siku hizi na Ofisi ya Kutoa Fatwa ni marudufu zaidi ya idadi ya zile zilizotolewa miaka sita, wakati wa Imamu Muhammad Abdo, na kwa kuzingatia kuwa Idadi ya wakazi imeongezeka mara zaidi, basi ni dhahiri kuwa idadi ya Fatwa elfu moja zilizotolewa ndani ya muda wa miaka sita wakati wa Imamu Muhammad Abdo, itakuwa Fatwa elfu saba, kwa kuzingatia kiwango cha idadi ya wakazi, hivyo kuchukuliwa kuwa maambatano ya watu na Taasisi yao ya Kidini ni kutokana na idadi.
Lakini kama idadi ya Fatwa itakuwa elfu nane kila mwezi, je, jambo hili bado linahitajia dalili ya uwajibikaji wa Taasisi ya Kidini? Na dalili yenye nguvu ya mwambatano wa Waislamu na Taasisi ya Kidini? Na dalili ya kosa la anayefikiri kuwa Waislamu wanajinyima marejeo yao ya Kidini?
8- Na Ofisi ya kutoa Fatwa inaziandika Fatwa zote inazozitoa, na hakuna Fatwa hata moja miongoni mwa Fatwa hizo, iwe inatokana na maombi, au imefasiriwa kwa yeyote, kwamba haikujali Qur`ani na Sunna, na radhi za Allah na Mtume wake, na njia ya Wema waliotangulia, au masilahi ya watu, au makusudio ya Sharia.
Na inawezekana kuzipitia Fatwa zote. Na Fatwa hizi zote za miaka mia iliyopita, isipokuwa zilizokaririwa, ndizo zilizosajiliwa katika Diski iliyouzwa kwa bei ya Pauni kumi ya Misri katika Maduka ya Mauzo ya Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu. Na Fatwa hizi zimechapishwa katika juzuu 23 mpaka sasa.
Pia tuna tovuti ambayo Fatwa mpya huchapishwa kwenye tovuti hiyo, pia tunazifasiri Fatwa hizi kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, na Kijeumani, hasa zile zinazohusu Maisha ya Mwislamu katika Nchi za Magharibi, ili kumrahisishia maisha yake, na kumpa jukumu la Uwakilishi wa Uislamu Sahihi, na Mlingaiaji wake kupitia mwenendo wake kabla maneno yake, kwa ajili ya Dini hii Tukufu. Na Ofisi ya kutoa Fatwa inapokea mamia ya Fatwa na maswali kila mwezi kwa njia ya Baruapepe na Tovuti, kutoka Ulimwenguni kote, kisha kuyajibu maswali yote na kuzijadili Fatwa hizo.
9- Na Mwislamu anaweza kurejea Tovuti ifuatayo:
www.dar-alifta.com na kutafuta Fatwa yoyote katika tovuti hii, ya kuzichukua huku na kule. Na Mtume S.A.W, anasema: “Yatosha mtu kuwa ni muongo, anapozungumza kila alilolisikia” . Na kufikisha Fatwa ni ushahidi, kwa hiyo Mtume S.A.W, anasema: “Je, umeona Jua, basi kwa mfano wake utoe ushahidi” .
Kwa hivyo habari nyingi zinazoenea zimehusishwa na Mheshimiwa Mufti, ama kwa lengo uzuri au baya, k.v. Eti, Yeye ameharamisha maandamano, amehalalisha rushwa, kumuua Balozi wa Israil hapa Kairo, Quiz, Uchi, Pombe, dawa za kulevya, n.k. Miongoni mwa mfululizo wa upuuzi wa kuchekesha na kuliza, tuliyoyakanusha, na kujibu, lakini bado kuna baadhi yao hupenda kuchochea. Na kutothibiti na kutothibitisha ndiyo wenyewe ndani ya mazingira ya uongo unaoharamishwa kisheria.

Na baadhi yao walisema kuwa: kuna vitu haiwezekani kuvitoa ispokuwa kwa upande wenu, kwa sababu vimechapishwa mara nyingi. Na akili hii imepigwa marufuku, kwa msingi wa kuwepo watu wengi wasiothibitisha vilivyo, namna tuliyojifunza wakati Qur`ani iliponukuliwa, na mfano wake ni Sunna, Fiqhi, Elimu ambapo zilinukuliwa kwa waliotutangulia. Na uthibitishaji ni utamaduni ambao lazima uenee, mpaka tufikie akili ya kitaalamu ili tuepukane na akili ya ngano na maoni ya binafsi yaliyo dhaifu.
10- Kuhusu Chuo Kikuu cha Azhar kwa sasa ni Chuo Kikongwe kabisa kuliko vingine vyote Duniani, baada kupita miaka elfu moja ya kazi endelevu, na ni Chuo kikubwa kabisa kuliko chochote Duniani. Na idadi ya Wanafunzi wake kwa sasa ni laki nne kwa ujumla, na walimu elfu saba, na ina vitivo sabini. Kwa hiyo ni Chuo kikubwa kuliko chochote nchini Misri na Duniani, k.v. Chuo cha Harvard Nchini Marekani, Chuo cha Cambridge London, Uingereza, na Chuo cha Tokyo Nchini Japani.
Nacho kinatekeleza wajibu wake, ambapo huweza kuendeleza mbinu za kufundishia kupitia miaka mia iliyopita, mpaka kufikia kuwa na Utambulisho wake duniani. Kama kupanua masomo yake, ambapo bado hakijatosheka na Ufundishaji wa Elimu za Sharia pekee, bali pia hufundisha Elimu mbalimbali za Kiraia.
Na mwanafunzi baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Azhar ambacho huhifadhisha Qur`ani – nayo ni sifa ambayo Misri bado inaongoza Kimataifa –, kutoka kwa Mashekhi, waliohifadhi Qur`ani, na wanafunzi wao. Na mashindano ya kimataifa bado yanahitaji Mahakimu kutoka Misri, na zaidi ya hayo, Wamisri wamekuwa wakijipatia tuzo mbalimbali za Kwanza kwa miaka mingi.
Na Misri bado ni Kitovu cha Qur`ani na usomaji wake ndani ya Ulimwengu wote wa Kiislamu, na bado Misri ni sababu ya heri na kuhifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Ulimwenguni kote.
Na Chuo kikuu cha Azhar bado ni Kitovu cha Masomo bobezi ya Kiakademia kwa ngazi za juu, na Waalimu wake bado wanaendelea kusomesha sehemu mbalimbali za Ulimwengu wa Kiislamu na Ulimwengu wa Kimagharibi, na wao ni Wakuu wa Vitengo, pamoja na kupata Viti vya Ualimu ndani ya Taasisi na Magharibi. Je, uhalisia huu wa kuonwa na kuhisiwa bado unahitajia dalili yoyote ile? kama ilivyosemwa:
Hakisihi kitu cho chote akilini
Ikiwa mchana utahitajika dalili.
11- Kuhusu Wizara ya Waqfu ndiyo inasimamia Ulinganiaji wa Kiislamu kupitia zadi ya Misikiti elfu tisini hapa Misri, na kupitia wahitimu elfu arobaini, miongoni mwa wahitimu wa Al-Azhar Sharifu, ambao watu wanawahitajia. Na Wizara hii inafanya mafunzo ya kiwango cha juu, kwa madhumuni ya kuwaunganisha walinganiaji hawa kwa mazingira yanayoendelea, na kwa Mtandao wa Tovuti ya Kimataifa, na zana za uchanganuzi kwa ajili ya kuelewa yaliyomo ya kila upande, na katika ufasiri na uchapishaji kwa njia ya Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu, na kamati zake.
Pia Wizara iliweka mfumo unaozuia kuchezea Ulinganiaji, au kufanya kazi hii asiye na uwezo, kwa hiyo iliweka sharti lililo ni: anayepanda Membari lazima awe Mhitimu wa Azhar au Kitivo cha Darul U’uluum, au mwenye uhodari unaomuwezeha kufanya hivyo, kwa njia ya kumpa Mhutubu ruhusa inayotolewa na Ofisi za Wizara, na hayo yote ni kutokana na mwitikio kwa maombi ya watu, kwa madhumuni ya kudhibiti mambo ya Ulinganiaji, na kuzuia asiye na uwezo katika kazi hii.
Hata hivyo, tuliona anayepinga taratibu hizi, ambapo anaona kuwa: Hivi ni vizuizi dhidi ya Walinganiaji, na haisihi kuwakumba, na kuwa hizi ni aibu juu ya Uso wa Ulinganiaji hapa Misri. Na swali linalotolewa ni: Mpingaji huyu anataka nini? Yeye anataka kupinga kwa ajili ya kupinga tu, kwa sababu yeye atapinga hali ya Taasisi ikifanya, na atapinga hali ya Taasisi ikiacha. Tumuombe Mola! Atupe ujira wetu mara mbili kwa msiba huu.
12- Kuhusu Baraza la Uchunguzi wa Kiislamu, limekwisha toa idadi ya juzuu kubwa ishirini na nane, ambazo zinakusanya tafiti zilizotolewa katika mikutano yake, na machapisho yake ya taaluma yalifikia mamia, na wanachama wake ni jopo la Wanazuoni na Wataalamu wa nyanja zote za Sayansi na Sanaa za ubobeaji.
Na ripoti za vikao vyake tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa zimesajiliwa, na mapendekezo, mikutano, maamuzi, Fatwa, maoni, mielekeo, yote yamesajiliwa, yamechapishwa, na yamepatikana.
Na Baraza lina uhusiano na Mabaraza mengine yaliyoliiga na kuifuata njia yake, ingawa yalianzishwa baadaye. Na bado linapokea masuala kutoka kwa dunia nzima kimashariki na kimagharibi, na linayadurusu ilivyo, na kuyajibu kwa elimu iliyojengeka na kweli, hivyo baada ya uchunguzi wa kina.
Nakumbuka kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar kimekwisha kubali kuanzisha Kituo cha Masomo ya Wakazi, kwa ajili ya kuchunguza masuala mapya k.v. Watoto wa Maabara na Mageuzi ya Jeni n.k., kisha wapingaji walieneza mengi dhidi ya kituo hicho na dhidi ya Al-Azhar, hata kuwa baadhi yao waliituhumu Al-Azhar kuwa ni kibaraka cha Marekani.
Na kituo hicho kwa uongozi wa Prof Dr Jamaludin Abu Surur kilichunguza masuala yanayohusu Wakazi, na Kufanya Semina kadhaa na Mikutano, kisha katoa idadi kubwa ya tafiti na maoni, ambayo yamewekwa mbele ya Baraza la Uchunguzi, ambalo limeyachunguza mnamo muda wa miaka miwili, pasipo kasi wala polepole. Na Baraza lilitoa maoni yake baada ya mwendo huu wa taaluma, na bado linafanya mpaka sasa kwa utulivu na bila ya kelele. Kisha wote walisahau mambo ya kutia mashaka na kupuuza yaliyotolewa kila mara. Na hii ni tofauti kati ya akili ya elimu, ambayo inalindwa na Taasisi ya Kidini, na akili ya ngano ambayo Taasisi iliipiga vita, na bado inaipiga vita.
13- Tunaendelea kuona kwa kweli hali ya Taasisi ya Kidini Nchini Misri na kutekeleza wajibu wake hata kufikia linalotarajiwa kutoka kwake na ndani yake. Tutaona Ujumbe wa Al-Azhar katika kila mahali, ambapo unashiriki katika kuinukulu Dini kwa watakaotufuata, kwa njia ya kufundisha, na njia ya Daa’wah katika Vituo mbali mbali vya kiislamu, kutoka katika Washington, London, Rome, huko Magahribi, na mpaka Ufilipino, Brunei, na Pakistani, huko Mashariki.
Al-Azhar ina Wajumbe wake katika kila mahali: Asia, Afrika, na Ulaya, na wote wakitekeleza wajibu wao, pia ina Wageni kutoka katika zaidi ya Mataifa sitini , wanaojifunza hapa Misri, na wanaporudi Nchi zao wanapata Vyeo vya Dini na Taaluma za ngazi ya juu kabisa, na miongoni mwao ni: Rais, Waziri Mkuu, na wengi wao wanapata Cheo cha Ukadhi, Mufti, Waziri huko nchini mwao, wakati wao ni wenye uwezo na mafanikio.
Na Al-Azhar iko popote, Watu wa Sunna na Jamaa walipo, na Uislamu kwa madhumuni yake ya ukati na kati mzuri pia upo, na ufahamu sahihi unaojengeka na njia makini ya taaluma kwa matini ya Dini, na ufahamu halisi kwa maisha na namna ya kuishi ndani yake, pia zote zipo.
Huu ni ukweli unaotangaza hakika hizi sahili, ambapo kukanusha kwake ni inda mbaya. Tunaweza kufikiri kuhusu kuendeleza linalotokea, kuliendesha hadi hutekeleza zaidi, au kulipa zana, ili kueneza na kupambana na mabadiliko mbali mbali. Lakini kulikosoa tu na kulielezea kwa kosa, kasoro, na upungufu, basi ni njia isiyo sawa, lakini husemwa:
Huenda jicho linakanusha mwangaza wa Jua kutokana na ila
Na huenda mdomo unazuia ladha ya maji kutokana na maradhi
14- Tukiongeza juhudi za Vyuo vya Al-Azhar, ambavyo idadi yake imezidi kuliko Vyuo elfu saba, na vyote vimejengeka kwa jitihada za kibinafsi, hakika vimegeuza hali ya watu kutoka katika giza hadi nuru, na kutoka katika ujinga hadi elimu. Na mfumo wa Al-Azhar ulijaribu kuhifadhi kitambulisho chake, pamoja na maendeleo makubwa kuzunguka kwake. Pia ulijaribu uwe sawa na mfumo wa elimu wa Umma, baada ya mapigano yalioendelea zaidi ya miaka thelathini mwanzoni mwa Karne ya Ishirini.
Idadi ya Vyuo ilikuwa vitano, na idadi ya wanafunzi wake haikuzidi elfu tatu, sasa vikawa Vyuo elfu saba, na wanafunzi ni milioni moja na nusu. Na kama idadi ya wakazi ilizidi mwanzoni mwa Karne ya Ishirini hadi mwishoni kwake kadiri ya maradufu tano, basi Vyuo vimezidi marudufu elfu moja na mia nne, na wanafunzi walizidi kadiri ya marudufu mia tano.
Na wanaohusika na Al-Azhar, miongoni mwa walio hai idadi yao imefikia watu milioni kumi kuizunguka Dunia, kati ya miaka 6 na miaka 96. Hali hii inabainisha kadiri Taasisi ya Kidini kutekeleza wajibu wake, na kadiri watu wanavyojiunga nayo.
15- Kama tukirejea tena kwa fikiri ya Taasisi ya Kidini mbele ya fikira ya
mgongano tutaona kuwa fikira ya mapigano inachukulia mambo
matatu, nayo ni:
Kwanza: Ulimwengu wote unachukia Waislamu, nao wapo katika hali ya vita daima kwa ajili ya kuwaangamiza, na hatari hii ni kutokana na pande tatu za maovu: Uzayoni (Mayahudi), Umisionari (Wakristo), na Usekyula (Ukanamungu). Na kuwa kuna njama inayofanywa dhidi ya Waislamu mara kwa siri na mara kwa dhahiri. Na kuwa kuna harakati kwa ajili ya kutuangamiza, ambapo tulisimama muda mrefu mbele yake bila ya kutenda tendo la kufaa.
Pil: Mgongano ni lazima na ulimwengu huu hata tuzuie uadui na ujeuri, na hata kulipiza kisasi kwa lililotokea katika Ulimwengu wa Kiislamu huko na kule. Na uwajibikaji wa mapigano utachukua sura mbili: Kwanza: ni kuwaua makafiri waliolaaniwa, na pili: kuwaua waliotoka katika dini wanaofanya ufisadi. Kuhusu makafiri waliolaaniwa, hawa ni wanadamu wote isipokuwa wanaoshuhudia Shahada Mbili, na walitoka katika dini waovu: Ni hawa wanaoshuhudia Shahada Mbili lakini wanahukumu kwa yale asiyoteremsha Mwenyezi Mungu, na wakaenda tofauti na fikira yao.
Na kama tunavyoona: Maneno haya yana uchangamano, uongo, na ujinga kwa kadiri nyingi, lakini yatavutia vijana wengi.
Tatu: Hakika fikira yao, inatakiwa kuwa aina ya fikira inayoenea kwa jumla, maana ya hao kuwa: Hayafanyi kupitia asasi au Taasisi ambayo inaweza kufuata mwendo wake, lakini yanafanya kama fikiri huru bila kigezo, ambapo mpokeaji wake anaweza kuyaridhia mahali popote, kisha atatekeleza namna anavyoweza, bila maagizo wala uhusiano na kituo au kiongozi.
Na kwa mujibu wa hayo fujo itaenea kwa kasi na kushamiri kwa kina, na nadharia hii inahusiana sana na Nadharia ya Machafuko ya Ubunifu, ambayo tutaijadili baadaye, nayo ni istilahi inayoenea katika matumizi ya kisiasa na kifasihi hivi karibuni, istilahi hii ambayo watu wengi hawaelewi asili yake, maana yake, na mfano wa utambuzi unaohusika.
16- Nguzo za fikira hii zinapinga njia ya Taasisi ya Kidini, na tukitaka kupambana na mabadiliko haya tunalazimika kusisitiza umuhimu wa Marejeo ya Taasisi ya Kidini, siyo kwenye Taifa tu lakini kwa kuzingatia kuwa ni mradi wa ustaarabu wa kibinadamu, na desturi ambayo Media, Waandishi, na Wenye fikira lazima waishike.
Na tunalazimika tusiwe bahili kwa mali ambayo ni mshipa wa maisha juu ya Taasisi hii wakati inapotekeleza wajibu wake.
Na Mtume S.A.W, aliwalingania watu wa Makkah, na idadi ya waumini haikuzidi watu mia mbili, kupitia miaka kumi na mitatu, kisha alipohama kwenda Madinah, na mali ikapatikana, watu waliingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi. Kwa hiyo tukisisitiza umuhimu wa Marejeo, na kuimarisha msimamo wa Taasisi ya Kidini kuhusu kupambana na mabadiliko, basi hali itageuka na kutulia.
Na Taasisi ya Kidini ina fikira wazi juu ya nguzo hizi tatu, tutazifafanua baadaye.
17- Kuhusu sifa kuu za fikiri hii, inaona- ikiwa ni makusudi au siyo- kuwa Uislamu ni Dini ya kijimbo, na kama kwamba imeteremshwa kwa Waarabu tu, au inalazimika kubakia ndani ya Nchi za Waislamu tu. Lakini fikiri ya Watu wa Sunna kuwa: Uislamu ni Daa’wah, na Daa’wah ni yenye sifa ya Ulimwengu. Na Mwenyezi Mungu amesema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote}. Na pia alisema: {Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui}.

Na ikiwa ni hivyo, basi mapigano hayafai kama msingi kwake. Kwa hiyo dhana ya Jihadi ilikuwa pungufu na yenye msukosuko kwa watu hawa, ambapo inaainishwa kwa kutoa dalili ya mapigano, kisha walifupisha dhana hata wakachanganya kati ya mapigano na mauaji.
Na Jihadi ni dhana pana ambayo inakusanya Jihadi kuu, yaani jihadi ya nafsi, na Jihadi ndogo, yaani jihadi ya mapigano, kwa ajili ya kuzuia uadui, na kuondosha Dhulma, na Mola wetu anasema: {Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur`ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa}.
Na Mtume SAW, anasema: “Mlikuja mjio bora, na mlikuja kutoka katika jihadi ndogo kwenye jihadi kubwa, nayo ni jihadi ya mtu kwa matamanio yake”. Na katika pokezi ingine: (Jihadi ya moyo).
Na Mola wetu anasema kuhusu desturi ya mapigano katika Suratul Baqarah: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui}.
Na ufupisho huu wa dhana ya kiroho ya Jihad kwa matumizi madogo tu, kisha kutoka katika mapigano mpaka mauaji, ni sifa kuu ya fikira hii, na kwa kuongezea, kuna sifa nyingine, nazo ni:
Kwanza: Kutoelewa uhalisia.
Pili: Mwelekeo mkali kuhusu kuelewa habari walizozijua. Lakini Watu wa Sunna hakika walielewa Kauli ya Mtume S.A.W: “Hakika Dini hii ina nguvu, basi ichukueni kwa upole” , na walielewa ile aliyomuelezea Bi Aisha Mtume S.A.W, ambapo alisema: “Mtume S.A.W, hakuwa na hiari ya mambo mawili ila alichagua lililo jepesi kuliko lingine, madamu halikuwa na dhambi, na Yeye alikuwa mbali na dhambi kuliko watu wote”.
Tatu: Ushinde, kukata tamaa, na kuhisi dhulma.
Nne: Fikira ya juu juu ikiwa ni kuhusu kuelewa matini, au kuutambua uhalisia, au uhusiano kati ya haya mambo mawili. Kinyume cha Taasisi ya kidini ambayo hushughulikia kuifundisha, kuizoea, kuilea, kwa kutegemea kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapowarejea, ili wapate kujihadharisha}.
Na kwa hiyo tunayaona maoni yao, mielekeo yao, mwenendo wao, misimamo yao, na hukumu zao juu ya vitu kuwa ni batili; na mambo matano haya ni lazima kwa wachunguzi wayazingatie katika kulichanganua suala hili.
18- Na Taasisi ya Kidini haitoi kauli kiholela, wakati inaposisitiza heshima yake, na wala haitaji yasiyo ya kweli, wala haizidishi au kuficha kitu, na inachukua Suratul Aa’sr kama desturi kuu katika kazi zake, ambapo Mwenyezi Mungu anasema: {Naapa kwa Zama! Hakika binadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Ila wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri}.
19- Na Taasisi ya Kidini Nchini Misri ina msimamo wa wazi kupitia historia yake na usasa wake juu ya maadui wa Uislamu; na wanaojidai kuwa wao ni Waislamu. Na maadui wa Uislamu – walio nje ya Waislamu – wao ndio waanzao uadui kwa Uislamu na wanakataa kutangamana nao, na wakawapiga vita, na kuwaudhi watu wake.
Na wanaodai kuwa wao ni Waislamu, na pia ni miongoni mwa watu wake, lakini wao ni katika makundi mawili: Wanafiki na waenezaji fitna.
Na Mwenyezi Mungu alitutahadharisha na makundi haya matatu, na akawalaumu. Na msimamo wa Taasisi ya Kidini unajengeka kwa kutii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake juu ya hawa wote.
Na tunaona misingi hii iko wazi kuhusu machimbuko ambayo Waislamu wanachukua Dini yao kutoka nayo. Na tunaona mpingaji kwa Taasisi ya Kidini anataka kupata njia nyingine, ambayo inayoonwa kwa kupitia maono au maoni yake, au kupitia utashi au matumaini yake, akiwa ni mwaminifu, au kupitia matamanio au masilahi yake, akichanganywa njiani.
20- Msingi wa kwanza ni kuzihakikisha habari, ukweli wake, na kuzielewa vizuri sana. Na Mtume S.A.W, anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kwenu mambo matatu: Habari za uvumi, kupoteza mali, na kuuliza sana”
Na anasema pia: “Tahadharini na dhana, hakika dhana ni maneno ya uwongo kabisa”
Na anasema pia: “Mazoea mabaya ya mtu ni kauli yake: kujigamba”.
Yaani: mazoea mabaya kabisa ya mtu atumie neno la (Walijigamba) kwa kuonesha muradi wake, na kunukulu habari bila kuthibitisha. Na habari nyingi zinazotumia njia hii zinajenga akili dhaifu, ambazo hazitegemei ukweli katika fikira, bali zinategemea tetesi, uongo, na matamanio.
21- Taasisi ya Kidini inafuata njia ya kuthibitisha habari, njia iliyosisitizwa katika Uislamu, na ambayo kupitia kwake, Dini imefikishwa kwetu, hivyo inatekelezwa kwa Maadili ya uvumilivu, upole, tabia njema, usamehevu, na hekima. Na Mtume S.A.W alimwambia Ashajj Abdu Qais: “hakika una sifa mbili, ambazo Mwenyezi Mungu anazipenda, nazo ni: Subira na upole”. Na katika Mapokezi ya Tabaraniy: “Mwenyezi Mungu na Mtume wanazipenda”.
Na hilo ndilo lililowapotea wale wapingaji wa Taasisi ya Kidini, ambao wanaiomba kila mara baada ya kutolewa maneno matupu kuyaelezea, na kuzifuata habari ili kushirikiana nazo zikiwa kweli au za uongo. Na Taasisi hii haikufanya hivyo kupitia maisha yake marefu, wala haitafanya hivyo inshaallah; kwa sababu kazi kama hii inaondosha heshima yake, pia ni kinyume na mafunzo yatokanayo na Dini ya Mwenyezi Mungu, ambaye anasema: {Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wangekurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapoleta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyafanya}.
Na pia anasema: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Kakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka}.
Na pia anasema: {Hapana kulazimisha katika Dini, kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu}.
Na pia anasema: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni kutokana na Dini, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale waliokupigeni vita kutokana na Dini, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhalimu}.
22- Taasisi yaKidini inajenga hukumu zake juu ya ufahamu kamili wa Qur`ani na Sunna, na wakati huo huo juu ya ufahamu wa kina kwa Machimbuko haya Mawili, na kuzuia ukamilifu na ukina ni marufuku. Mwenyezi Mungu anasema: {Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnaowatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa, Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake?}.
Pia anasema: {Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali mnajua?}.
23- Kwa hiyo Taasisi ya Kidini hutofautisha kati ya dhana ya mapigano, desturi yake, na dhana ya uuaji unaoharamishwa, na uenezaji wa fitna na wanaohusika nao. Na Mwenyezi Mungu anasema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wanazo uadui}.
Na pia anasema: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa. Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye kutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu zipo ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyo kuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda}.
24- Kuna anayekumbuka Taasisi ya Kidini wakati anapotaka kuzungumzia kasoro yake au kuitofaulu kwake. Na kwa hakika, Historia ya Taasisi ya Kidini ni kwamba, Taasisi hii imebobea katika kulinda Ibada, Ulinganiaji, na Elimu ya Sharia, tangu Wakati wa Muhammad Ali.
Na kwa hivyo, Elimu ya kiraia imejiendeleza yenyewe, na bila ya kuathiriwa na Taasisi ya Kidini. Na Vyuo Vikuu vimeanzishwa, kuanzia Chuo Kikuu cha Taifa, hata idadi ya Vyuo Vikuu imefikia kumi na viwili, chini ya uongozi wa Baraza Kuu la Vyuo Vikuu, na Chuo Kikuu cha Al-Azhar kiko chini ya uongozi wa Baraza Kuu la Al-Azhar.
Na hata hivyo, tunawaona baadhi ya Viongozi wa Usekyula wakilaumu Taasisi ya Kidini kuwa ni sababu ya kushindwa kwa kuwageuza watu kwenye fikra kamili ya Usekyula, ambao wanautaka vilivyo. Hapo jambo linachekesha na linastahiki kusikitikiwa na kuonewa huruma.
Na sisi tunawanasihi kuwa wajirejee, na kuchunguza Historia ya watu, na mahitaji ya Umbile la kibinadamu na hadhi ya Dini ndani yake, na waelewe kuwa majaribio ya kutangulizwa, yaliyofanyika kwa bidii na kuathiri kwa kiasi kikubwa, kwa mfano Uturuki, hayakuwatoa watu katika Dini, na kwamba Ufaransa inapitia masomo iliyojifunza, baada ya kushindwa kwa Usekyula wa kuiondosha Dini katika maisha ya watu. Na matokeo yalikuwa ni kuwepo vizazi vyenye hali mbaya.
Na huyu Rais (Bush) kwa sasa anatoa wito wa kufundishwa Nadharia ya (Ubunifu wa busara wa Ulimwengu na Maisha), nayo ni Nadharia ibayotegemea fikra ya kuwepo Nguvu ya kificho inayosimama nyuma ya maendeleo ya kibinadamu, na uumbaji wa Ulimwengu, sambamba na Nadharia ya (Maendeleo na Mageuzi), ambapo alisema usemi huu: (Hakika wanafunzi wa shule wanalazimika kujifunza Nadharia ya Ubunifu wa Busara kama nadharia ya kushindana na Nadharia ya Maendeleo na Mageuzi). [Yamenukuliwa kutoka katika Gazeti la Washington Post: Jumatano 3/8/2005].
Hivyo, maoni ya Bush yalizua ukosoaji mkali kwa upande wa wapingaji wa Nadharia ya (Ubunifu wa Busara), ambapo wanasema kuwa: hakuna dalili ya kitaalamu inayoitegemezwa, na hakuna msingi wa kielimu wa kuifundisha.
Na wengi wa wanasayansi wa Shirika la Uchunguzi wa kitaalamu unasema kuwa: Nadharia ya (Ubunifu wa Busara) haikuharibiwa, lakini ni jaribio tu linalotolewa kwa ustadi, kwa ajili ya kuingiza fikira ya Dini – hasa ya Kikristo – ndani ya Fikira ya wanafunzi.
25- Tunatumaini kuwa wao watayasoma Machimbuko yao huko Magharibi, na wasiishie kwenye Miaka ya Sitini ya Karne ya Ishirini, kwani kuna jaribio lililogeuza mawazo, mielekeo, na misingi. Na tunatumaini wasiokuwa mfano wa maneno ya Sartre katika utangulizi wake wa (Wanaoadhibiwa katika Ardhi), ambapo anasema: (Tukisema: hapa upo Undugu, walisena: undugu undugu, wakipaaza sauti bila kuelewa maana yake).
26- Hakika Taasisi ya Kidini hulinda Ibada kwa njia ya kufuata, na siyo kuzua, na Njia yake ni ya ukati na kati, ambayo inajengeka kwa hoja na dalili na Misingi ya kina ya Kitaaluma katika uwanja wa Uthibitishaji, Kuelewa, na zana za kielimu, vilevile Taasisi ya Kidini, inashughulikia Daa’wah, kwa Misingi ya Hekima na Mawaidha Mema, na hushughulikia Elimu kwa Msingi wa Njia, akili ya kitaaluma, na siyo Mwelekeo wala Ngano.
Na mambo hayo matatu ndiyo watu wanayahitajia katika maisha yao; Ibada yenye uaminifu, Daa’wah yenye mwangaza, na Elimu inayofaa ambayo hutakasa nafsi, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: {Hakika amefanikiwa aliyeitakasa, Na hakika amepata hasara aliyeiviza}.
Na yale anayotoa Mwislamu anayeistawisha ardhi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Yeye ndiye aliyekuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo}.
Na anamuabudu Mwenyezi Mungu kwa haki, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangachukia makafiri}.
27- Na Taasisi ya Kidini kupitia mfumo wake haishughulikii sana tuhuma, lakini inasikiliza sana nasaha, kwani: “Dini ni nasaha”.
Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu}.
28- Ikiwa hii ni hali ya Taasisi ya Kidini na fikra yake, na inaweza kunufaisha kikamilifu, basi tunajua kuwa: tuko katika ulimwengu usio na mipaka, na umekuwa ukiendelea na kasi yake na maendeleo yake, na kuwa tunahitajia kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuacha nyayo zetu ndani ya Ulimwengu huu, ili tuendelee katika kutekeleza jukumu tulilokabidhiwa.
29- Hakika sisi tunapoeleza uhalisia wa Taasisi ya Kidini, haimaanishi kuwa tumekwisha timiza wajibu wetu, na kutekeleza kazi yetu, bali tulilolijifunza katika Taasisi hii Muhimu, na Masheikh wetu, Mwenyezi Mungu awarehemu, kuwa: Elimu haina mwisho na hailitambui neno Mwisho, na mwanadamu analazimika kutekeleza wajibu kwa wakati – nao ni endelevu na wa kudumu – na pia kuwa: “Kazi zinazopendwa sana na Mwenyezi Mungu ni zile endelevu, hata zikiwa chache”. Na: “Hakika Mwenyezi Mungu anapenda yeyote atakayeifanya kazi aiboreshe”.
Ni kwamba: Kutafuta elimu na kazi, tangu kuzaliwa hadi kufa, pamoja na kuanzia kwenye Dawati hadi kaburini. Na tulilolitaja ni kwa ajili ya kurekebisha sura mbaya inayotolewa na watu wengi, bila ya elimu wala kuzingatia ukweli au uhakika. Hali hii inakusanya suala la kutwisha jukumu bila kutoa madaraka, pamoja na kusisitiza daima kwa kuzuia madaraka, na hofu ya kutisha kutokana na madaraka, na hii ni hali yao katika kupoteza madaraka, kwa hiyo, ewe ndugu yangu nasaha iliyo bora ni kwamba usimuulize aliyenyimwa madaraka.
30- Linalotarajiwa kwa Taasisi ya Kidini iingie katika mbinu za kisasa, na imekwisha anza kuingia, lakini hali hii inahitaji mali nyingi na juhudi kubwa kabisa, na hima endelevu. inahitaji kuwepo daima kimataifa kuhusiana na kitaifa, na uwakilishi wa Taasisi za Kimataifa, na inahitaji wote wayapitie Marejeo yake ambayo iliyatekeleza na bado kuyatekeleza.
Na haifai kwa aliyetaka kufaidika aiahirishe na hadhi yake, ambayo Mwenyezi Mingu alijaalia nayo.
Na Taasisi ya Kidini inahitajia Satalaiti, na kuimarisha Gazeti lake ambalo ilifanikiwa kulitoa, na kuchapisha Gazei hili mahali popote Ulimwenguni, na Gazeti hili limekuwa likitolewa tangu zaidi ya Miaka themanini. Pia linahitajia mazoezi daima juu ya maendeleo na mambo mapya.
Ewe Mola! Tuongoze kwa haki, na utupe mafanikio katika kila unachopenda na kuridhia, na uifanye mioyo yetu iwe thabiti na yenye upendo wa imani na matendo mema, na uziongoze hatua zetu, na ukubali matendo yetu mema, na utupe zawadi nzuri za wanaokujua, Amin.
Na Rehema na Amani ziwashukie Mitume wote, na Sifa Njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

 

Share this:

Related Fatwas