Uimamu wa Mwanamke kwa Wanaume kati...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uimamu wa Mwanamke kwa Wanaume katika Swala

Question

 Je, unajuzu Uimamu wa mwanamke kwa wanaume katika Swala?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swala ni nguzo katika nguzo za Uislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameifaradhisha kwa Waislamu, na Mtume S.A.W. amebainisha namna ya utekelezaji wake akasema: “Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali, pindi inapoingia Swala, basi mmoja wenu aadhini na asalishe aliye mkubwa zaidi kwenu”( ).
Kuswali Swala kwa pamoja ni bora zaidi kuliko mtu kuswali akiwa peke yake, amesema Mtume S.A.W. “Swala ya pamoja ni bora zaidi kuliko Swala ya mtu peke yake kwa tofauti ya daraja ishirini na saba”( ), na Swala ya pamoja inahitaji uwepo wa Imamu atakayeongoza, na kuongoza ni kuunganisha Swala ya mwenye kuswali na Swala ya mwingine kwa masharti yaliyowekwa na Sharia.
Hakuna tofauti kati ya Wanachuoni katika Uimamu wa mwanamume kwamba unafaa kwa Waumini wanaume na wanawake katika Swala ya lazima na Swala ya Sunna. Ama uimamu wa mwanamke kwa wanaume ni jambo lisilofaa, iwe ni katika Swala ya lazima au ya Sunna, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Fahamuni, mwanamke asiwe Imamu wa mwanamume, wala Mwarabu wa majangwani asiwe Imamu kwa mtu aliyehama Makka, wala mtu mwovu asiwe Imamu wa Waumini”( ), katazo lipo wazi, vilevile Uimamu unahitaji kuwatangulia maamuma, na mwanamke ni mwenye kuamrishwa kuwa nyuma ya safu za wanaume kwenye ibada ya Swala kama ilivyokuja kwenye Hadithi ya kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Safu bora ya wanaume ni ya kwanza, na safu mbaya ni ya mwisho, na safu bora kwa wanawake ni ya mwisho na safu mbaya ni ya kwanza”( ). Hadithi hii inahimiza wanawake kuwa nyuma, ikiwa mwanamke atawaongoza wanaume, basi atakuwa amekiuka maelekezo haya ya Mtume S.A.W. kwa sababu nafasi ya Imamu ni kutangulia mwingine, na Mtume S.A.W. amehimiza wanawake wawe nyuma, hivyo haifai mwanamke kuwa imamu kutokana na yanayofungamana na uimamu ikiwa ni pamoja na kutangulia kunakopingana na yaliyokuja kwenye Hadithi( ).
Mwanamke ikiwa atawaongoza wanaume kwenye Uimamu, basi hili halitaepusha kutendeka yaliyo haramu, kwa sababu ibada ya Swala inahitaji unyenyekevu wa moyo na utulivu wa nafsi pamoja na mazingatio ya fikra na akili katika kuteta na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hekima zake zimepelekea kuumba mwili wa mwanamke kwa umbile tofauti na mwili wa mwanamume, na akafanya ndani yake vitu vyenye kuibua hisia kwa mwanamume na kutikisa hisia zake za ndani, ili kuepusha fitina ya aina yoyote ile na kuzuia sababu ya maasi Sharia imefanya jukumu la uimamu usomaji adhana na kukimu Swala ni la mwanamume, na akafanya safu za wanawake kuwa nyuma ya safu za wanamume, katika hili Sharia Tukufu imetoa shime kubwa ya kuwalinda wanawake kutokana na fitina na kuibua hisia kwa kuzuia sababu zake zingewezesha hilo, na hasa katika nyakati za kuabudu na kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na haya ambayo tumeyaeleza ndiyo madhehebu ya Jamhuri ya Wanachuoni wema waliotangulia na waliopo, nayo ndiyo yaliyotekelezwa na madhehebu yote manne yanayofuatwa.
Kuna kundi dogo la Wanachuoni walio na mtazamo tofauti na huu, miongoni mwao wapo waliopitisha uimamu wa mwanamke katika Swala za Sunna na si za lazima, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad kwenye upokezi wake, yamekuja katika kitabu cha Ibn Muflihi Al-Hanbaly: “Wala haifai mwanamke kuwa Imamu kwa wasiokuwa wanawake wenzake na yamejengewa maelezo hayo katika kitabu cha Muntakhab: Haifai kuwaadhinia wasiokuwa wanawake wenzake, na kutoka kwenye maelezo hayo: Inafaa katika Swala ya Sunna, na maelezo mengine: Katika Swala ya Taraweh”( ).
Baadhi ya wengine wakapitisha mwanamke kuwa Imamu katika Swala za lazima kwa maana ya Swala za faradhi na hata zile za Sunna, limeelezwa hili kutoka kwa Abi Thaur na Ibn Jarir At-Tabary na Al-Muzny( ), nao ni mtazamo wa Muhydeen Ibn Al-Araby kutoka dhehebu la Dhwahiriyah( ).
Hawa wakachukua dalili yaliyopokelewa kutoka kwa Ummu Waraqa binti Abdillah Ibn Harith kuwa Mtume S.A.W. alimfanyia muadhini aliyemuadhinia na kumwamrisha Ummu Waraqa kuwaswalisha watu wa nyumbani kwake, amesema Abdurahman Ibn Khalad - mpokezi: Mimi nimemwona muadhini wake ni mtu mzima( ), dalili hapa ni kuwa: Ruhusa ya Mtume S.A.W. kwa Ummu Waraqa kuwa Imamu inafanya kazi katika Swala zote za faradhi na Sunna, wala haifai kuainisha Swala za Sunna tu, kwa sababu Swala za Sunna hazina adhana, na muadhini wake ataswali nyuma yake naye ni mwanamume - kama ilivyokuja kwenye Hadithi - hili limeonesha juu ya kufaa mwanamke kuwa Imamu kwa mwanamme katika Swala za faradhi na Swala za Sunna.
Jamhuri ya Wanachuoni wakajibu kuhusu Hadithi ya Ummu Waraqa kuwa upokezi wake sio sahihi, katika upokezi wa Waliid Ibn Jumaii nao ni dhaifu. Na kama ingethibiti kwa Ummu Waraqa, basi ingekuwa ni maalumu, kwa dalili kuwa haikuwekwa Sharia hiyo kwa mwanamke mwingine yeyote ya kuadhini wala kukimu Swala, kunahusisha uimamu kwake kwa kuhusishwa adhana na kukimu( ).
Miongoni mwa yanayopaswa pia kufahamika kwenye sehemu hii ni kuwa hakuna yeyote aliyesema inafaa kwa mwanamke kuadhini na kutoa hotuba ya Ijumaa kwa watu pamoja na kuwasalisha, kwani hili linakwenda kinyume na makubaliano ya Waislamu, wala haifai kuwa nje ya makubaliano haya kwa hali yoyote ile, wala haifai kuchanganya kati ya masuala mawili kuwangoza wengi na masuala ya kutoa hotuba ya Ijumaa, kama ilivyotokea ndani ya baadhi ya nchi za Kimagharibi hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa makundi ya fikra zenye shaka shaka.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas