Je, Mtu Anaweza Kutumia Mali zake W...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je, Mtu Anaweza Kutumia Mali zake Wakati wa Uhai wake kwa Mabinti zake vyovyote atakavyo?

Question

 Sisi watatu ni ndugu wa baba na mama, na tuna ndugu zetu wawili wa kike wa baba mmoja, na baba yetu Mungu amrehemu alikuwa ameniandikia mimi na ndugu zangu wawili shamba lenye ukubwa wa hekari 11, na aliacha pia eneo lingine lenye ukubwa wa hekari sita lakini hakuliandika kwa yeyote, eneo hilo limeweza kugawanywa kwa warithi baada ya kifo chake, vile vile alinihusisha mimi na ndugu zangu wawili – bila ya ndugu zetu wawili wa kike wa upande wa baba – kiasi cha pesa paundi 1000 kwa kila mmoja kati yetu, pamoja na sisi kufahamu kuwa wakati anatuandikia hayo bado tulikuwa wadogo lakini dada zetu wawili wa upande wa baba mmoja wao walikuwa wameshaolewa.
Swali ni hili: Je mtu anaweza kutumia mali zake wakati wa uhai wake vyovyote atakavyo? Pamoja na kufahamu kuwa mimi nimesikia mara nyingi mitazamo na rai za Wasomi mbalimbali wa Sharia za Kiislamu katika maswala kama haya; baadhi yao wakiharamisha kilichofanywa na baba na kulazimisha kurudisha haki, na baadhi yao wanaharamisha kilichofanywa na baba na wanasema kurudisha haki ni jambo la kujitolea si lazima, wengine wanapitisha kilichofanywa na baba na hawatulazimishi kufanya chochote, ukweli ni upi kwenye mitazamo hii? Na je inafaa kwangu mimi kufuata rai na mtazamo wowote katika hili? Na je maana ya Hadithi inayosema: “Uulize moyo wako ukiwa utakwambia haki fuata, wema ni kile kinachoridhisha moyo, na uovu ni kinacholeta shaka na wasi wasi moyoni” kuwa mwanadamu anaposikia mitazamo na rai nyingi hivyo rai ambayo imeridhisha moyo wake na akili yake ndiyo inakuwa sahihi Kisharia? Na hapa ni ipi hukumu ya karibu na uhakika? Ambapo mimi nimechukuwa tahadhari na kurudisha baadhi ya haki kwa wenyewe, na nikawataka wanisamehe kwa kilichobaki na wamenisamehe.

Answer

 Shukrani ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehma na amani ziwe juu ya Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na Maswahaba zake na wale waliomfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho.
Asili kisharia ni kuwa mwanadamu yupo huru kutumia anachomiliki ima kukiuza kukitoa zawadi kukiweka waqfu kukikodisha au yasiyokuwa hayo katika matumizi ya Kisharia ambayo ni sehemu katika miliki, imepokelewa na Dar Al-Qutwubiy na Baihaqiy kutoka kwa Habban Ibn Aby Jabalah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Kila mmoja ana haki kwa mali yake kwa wazazi wake watoto wake na watu wote” Hadithi hii inatambua asili ya uhuru wa mwanadamu kutumia mali yake.
Pamoja na hayo lakini Sharia Tukufu imetaka kwa mtu aliyepewa amri kufanya usawa katika kuhusisha kujitolea kwake kwa watoto wake, imepokelewa na Saad Ibn Mansour katika Sunani kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Fanyeni usawa kati ya watoto wenu katika kuwapa, na kama ningekuwa mwenye kuathirika na yeyote basi ningewapendelea wanawake zaidi kuliko wanaume”, lakini kilichopitishwa Kisharia kwenye swali hili kuchukuliwa ni Sunna na wala si wajibu, ikiwa mzazi amempa mmoja wa watoto wake kitu kama zawadi na akakihusisha kwa mwanawe huyo bila ya watoto wake wengine, wakati huo mzazi huyu anakuwa ameacha kwa kupenda na wala si kwa wajibu, na kuacha kwa kupenda hakufangamani na dhambi yeyote, tafauti na kuacha kilicho wajibu, wakati huo hupata thawabu mtendaji wake na kupata dhambi mwenye kuacha.
Na kauli kuwa kufanyeni usawa kwa watoto katika kuwapa kitu ni katika mambo yanayopendeza na wala si katika jumla ya wajibu ndio kauli ambayo imekubaliwa na Jamhuri ya Wanachuoni kuanzia Imamu Abu Hanifa Imamu Maliki Imamu Shaafi na wengine.
Imekuja kwenye kitabu cha: [Al-Bahri Ar-Raiq] ni miongoni mwa vitabu vya Imamu Abu Hanifa 288/7 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Islamy: “Inachukiza kutanguliza baadhi ya watoto dhidi ya watoto wako wengine katika kuwapa kitu bure au zawadi isipokuwa katika hali ya ubora zaidi katika dini”.
Amesema Mwanachuoni Al-Kharashy katika sherehe yake ya kitabu cha: [Mukhtasari Khalil katika Fiqhi ya Imamu Maliki 82/7 chapa ya Dar Al-Fikri]: “Ama mzazi kutoa zawadi kwa baadhi ya watoto wake mali yake yote inachukiza”.
Ama kwa upande wa Imamu Shaafi amesema Sheikh Al-Islamy Zakaria Al-Ansariy As-Shafiy katika kitabu cha: [Asna Al-Matwalib” 483/2 chapa ya Dar Al-Kitabu Al-Islamiy]: “Inachukiza kwa wazazi wawili na walio juu yao kutoa mali kama zawadi kwa mtoto yeyote akiwa na watoto wengi”.
Jamhuri ya Wanachuoni kwa maelezo hayo wakachukuwa dalili miongoni mwa dalili hiyo Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhary na Muslimu katika Sahihi zao ni Hadithi inayotokana a An-Nuuman Ibn Bashir R.A kuwa amesema: “Baba yangu alinichukuwa mpaka kwa Mtume S.A.W akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu shuhudia kuwa mimi nimempa Nuuman hiki na hiki, akauliza Mtume: “Je watoto wako wote umewapa kama ulivyompa Nuuman? Akasema: Hapana, akasema Mtume S.A.W: Basi mshuhudishe mwingine kwenye hili, kisha Mtume akamuuliza: Hivi unapenda watoto wako wawe sawa kwenye wema kwako? Akajibu: Ndio. Mtume akasema: Basi ni kwanini isiwe hivyo”.
Ikiwa alichofanya Bashir ni haramu basi Mtume S.A.W asingemuamrisha kumshuhudisha mwengine kwa sababu Mtume S.A.W hawezi kuamrisha jambo la haramu.
Pia wakachukuwa katika moja ya mapokezi ya Hadithi ya Nuuman Ibn Bashiri kukiwa na kauli ya Mtume S.A.W kwa Bashiri: “Je utafurahishwa katika wema kwako watoto wako wawe sawa? Akasema: Ndio, akasema Mtume basi ni kwa nini isiwe hivyo”.
Na katika mapokezi mengine: “Hivi watoto wako wote umewapa kama hivyo? Akasema: Hapana, akasema Mtume S.A.W: “Hivi sio unataka kwao katika mema mfano wa unavyotaka kwa huyu? Akasema: Ndio, akasema Mtume S.A.W basi mimi sishuhudii”.
Hadithi hizi mbili zinaonesha kuwa jambo la usawa ni Sunna na si wajibu, ili kuunganisha hilo na kufanya wema kwa watoto wake sawa sawa, na usawa katika wema haukuwa ni jambo la lazima kwa watoto bali ni jambo linapendeza, haikuwa usawa katika kutoa ni jambo la lazima kwa wazazi bali ni jambo la Sunna kufanya hivyo, hii imeonesha kuwa Mtume S.A.W anawazindua Maswahaba zake kwa hilo ili kuchunga lililo zuri zaidi.
Vile vile imepokewa kutoka kwa baadhi ya Maswahaba kuwa wao walipendelea baadhi ya watoto wao bila ya kupingwa kufanya hivyo na Maswahaba waliobaki, kwa mfano Abu Bakari alimpendelea sana binti yake Bibi Aisha R.A, vile vile Omar alimpendelea mwanawe Aswima kwa kumpa kitu, na Abdulrahman Ibn Aufu R.A alimpendelea mtoto wa Ummu Kulthuum, na ikasemwa kuwa: Alimpendelea binti yake kwa Dirham elfu nne, na Ibn Omar R.A alichinja wanyama watatu au wanne kwa baadhi ya watoto wake bila ya wengine.
Wameelezea Wanachuoni wa Imamu Hambali na wengine ulazima wa kufanya usawa kwa watoto kwenye kuwapa kitu au vitu, wakitolea ushahidi yaliyokuja baadhi ya mapokezi ya Hadithi ya An-Nuuman Ibn Bashir R.A, na ndani yake ni kuwa Mtume S.A.W. alijizuia kushuhudia kutoa kwa bashir kumpa mtoto wake akasema kumwambia “Sitoi ushuhuda wa makosa”.
Lakini dalili hii inajibiwa kuwa makosa ni kuelekea kwenye kukusudia, hivyo yenyewe kwa mazingatio haya hukubalika yanayochukiza kama yanavyokubalika yaliyo haramu, kwani yanayochukiza ni yenye kuelekea tofauti na usawa, na yapo nje ya usawa, na kila kilicho nje ya usawa hicho ni makosa ni sawa sawa kikiwa ni haramu au chenye kuchukiza, na kukusanya kati ya dalili kunaleta maana ya kuchukiza.
Ikiwa uharamu utageukia kupendelea kati ya watoto na ikathibiti hali ya kuchukiza basi kuchukiza huku kutakataliwa ikiwa upendeleo kwa maana inayozingatiwa kwa mtoto anayependelewa kutapalekea kuhusishwa, kama vile kuhusishwa kitu kwenye hali ya ugonjwa au kuwa na watoto wengi au kushuhurishwa na mambo ya elimu na mfano wa hayo, vile vile ikiwa kunyimwa mtoto kwa sababu za kiakili au falsafa hakuchukizi kunyimwa kwake, angalia kitabu cha: [Hashiyatu cha Mwanachuoni Ibn Abideen 444/4 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], ni sherehe ya kitabu cha [Al-Muutwii cha Imamu Al-Baajy 94/6 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Islaamiy], kitabu cha [Mughny Al-Muhataaj cha Shaikh Al-Khatib As-Sharbiny 56/3 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah], pia kitabu cha [Al-Isaaf cha Mwanachuoni Al-Mardawy 139/7 chapa ya Dar Ihayaau Turathi Al-Arabiy], na hilo ni pale ilipoelezwa kuwa kuchukiza kunaondoka kwa uwepo wa haja, kitabu cha [Ghidhaau Al-Bab cha Mwanachuoni As-Safaariiny 323/1 chapa ya Taasisi ya Qurtwubah].
Kama walivyotafautiana Wanachuoni katika hukumu ya usawa kati ya watoto katika kuwapa zawadi ambapo wametafautiana pia katika sifa ya usawa huu unaohitajika, Wanachuoni wa Abu Hanifa Imamu Shafi na wengine wamesema kuwa usawa unaohitajika kati ya watoto unakuwa kwa kuwapa kila mmoja katika watoto mfano wa alichopewa mwingine, hakuna tafauti katika hili kati ya mtoto wa kiume na wa kike, kwani hupewa mtoto wa kike mfano wa alichopewa mtoto wa kiume, angalia kitabu cha: [Badaai As-Swanaai 127/7 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Islaamiy], na kitabu cha [Rawdhatu At-Twalibiin 279/5 chapa ya Al-Maktabu Al-Islaamiy] na kitabu cha [Al-Isaaf 136/7].
Wakaelezea Wanachuoni wa Imamu Maliki na Hambali kuwa usawa unaotakiwa unakuwa kwenye kugawa zawadi kati ya watoto ni kwa mujibu wa mgao wa Kisharia wa mirathi, hugaiwa mtoto wa kiume mara mbili ya mtoto wa kike. [Angalia sherehe ya Mwanachuoni Al-Kharshy 82/7, pia kitabu cha Kas-Shaaf Al-Qanaai 310/4 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah].
Kauli iliyopitishwa kwetu ni kauli ya kwanza, kwa sababu Mtume S.A.W alimtaka Bashir kuwapa watoto wake kile alichompa Nuuman, na akasema kumwambia: “Je watoto wako wote umewapa sawa na ulichompa Nuuman? Akasema: Hapana. Mtume S.A.W akasema: Sitokuwa shuhuda juu ya chochote, hivi haufurahishwi kwenye kufanyiwa wema na watoto wakiwa sawa? Akasema: Ndio. Mtume S.A.W akasema basi ni kwanini isiwe hivyo” wala hakutaka ufafanuzi zaidi kutoka kwake kuhusu watoto waliobaki ni wakiume au wakike? Hii imeonesha kuwa hakuna tafauti kati ya watoto wa kiume na wale wa kike katika kufanya usawa unaohitajika kwa watoto katika kutoa au kuwapa, na kanuni inasema: “Kuacha ufafanuzi katika hali halisi pamoja na kuwepo uwezekano kunateremsha kwenye ujumla wa kinachosemwa” ni kitabu cha Hashiyatu Al-Atwar sherehe ya kitabu cha [Jamuu Al-Jawaamii 24 – 25/2 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]. Na maana ya kanuni hii ni kuwa: “Kadhia ya matukio ikiwa italetwa kwenye Sharia basi inategemewa kuwa moja ya sura mbili, na Sharia kuacha ufafanuzi kwenye sura hizo basi kuacha kwake kuna dalili kuwa hukumu imeungana katika sura hizo mbili” kitabu cha [Hashiyatu Ibn As-Shatw 88/2 chapa ya Aalam Al-Kutub].
Watu wa madhehebu ya pili wamechukua dalili kuwa kilichobora kufuatwa kwanza ni mgawanyo wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amegawa kati yao na kufanya mtoto wa kiume kuchukuwa mara mbili ya mtoto wa kike. Kitabu cha [Al-Istidhkar 228/7 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah, Al-Mughny 388/5 chapa ya Dar Ihyaau At-Turath Al-Arabiy].
Lakini linajibiwa hilo kwa kuwepo tafauti kati ya mirathi kwa upande mmoja na utoaji wa zawadi wakati wa uhai kwa upande mwingine, ambapo upande wa mirathi inahusu baada ya kufa, na kila hali ina hukumu zake, na kwa vile utoaji wa zawadi ni jambo la kujitolea na wala sio la lazima kama mirathi, kama vile mtoto wa kiume na wa kike wanatafautiana kwenye mirathi, ama kwa undugu wa tumbo moja wanakuwa sawa sawa kama vile kaka na dada wa mama mmoja.
Mitazamo yote iliyotangulia imepokelewa kutoka kwa Maimamu wa dini na Wanachuoni wenye jitihada, na sisi ikiwa tutachukuwa mtazamo mmoja wapo ili kutolea Fatwa kutokana na kukubaliana na hali za watu basi hilo halipingani kulitumia na ni katika jumla ya kauli zinazozingatiwa, na kutokana na hilo mwenye sifa ya chini ya mwana jitihada inafaa kwake kufuata mtazamo wowote katika mitazamo hii na kwa hilo anakuwa na udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amelazimisha kwa mtu asiyejua kumuuliza msomi bila ya kuainisha msomi huyu na sio yule, kwani Amesema Mola Mtukufu: {Basi waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya Mwenyezi-Mungu vya kale) ikiwa nyinyi hamjui}. [An-Nahl:43].
Imeelezwa kwenye elimu ya msingi wa dini kuwa, mtu asiyejua hana madhehebu, ni kitabu cha [Al-Bahri Al-Muhitwu cha Imamu Zarkashy 375/8 chapa ya Daru Al-Kutub]. Kutokana na hilo ni kuwa halazimiki na madhehebu fulani, na ana haki ya kuteua kufuata madhehebu yeyote yale katika madhehebu yanayokubalika, vile vile ana haki ya kuhama kutoka madhehebu moja kwenda madhehebu nyingine, amesema Imamu An-Nawawy katika kitabu cha [Rawdha 117/11]: Jambo ambalo linahukumiwa na dalili ni kuwa – Mtu yeyote aisiyejua – halazimiki kufuata madhehebu, bali atatafuta Fatwa kwa yeyote anayemtaka au anayekubaliana naye bila ya kuchukuwa ruhusa.
Mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haitamy As-Shafiy amesema katika kitabu chake cha [Fatwa 315/4 chapa ya Maktabatul-Islaamiyah]: Kauli sahihi zaidi ni kuwa – kwa maana ya mtu asiyejua – kuwa na hiyari ya kumfuata amtakaye akiwa bora kwake pamoja na kuwepo mwingine bora zaidi.Ama kuchukuwa tahadhari ni jambo zuri, kutokana na uwezekano wa kutoka kwenye tafauti, kwani Wanachuoni wameelezea kuwa kujitoa kwenye tafauti ni jambo lenye kupendeza, kitabu cha [Al-Ashbah wa An-Nadhwahir cha Imamu As-Suyuutwy ukurasa wa 136 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], na Imamu Taaj As-Sabaky amesema katika kitabu chake [111 – 112 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: Imefahamika kwenye maelezo ya Maimamu wengi, na inakaribia kuzingatiwa kuwa ni makubaliano, kisha akaleta sababu ya kanuni kuwa: Kufadhilisha kwake – kwa maana ya kujitoa kwenye tafauti – sio kwa kuthibiti mwenendo maalumu bali ni ujumla wa tahadhari na kutoihusisha dini kwenye makosa, nalo ni jambo lenye kuhitajika moja kwa moja Kisharia, kauli ikawa kujitoa ni bora zaidi na imethibiti kwa upande wa ujumla, na kupitishwa kwake katika jambo lenye kuhitajika”.
Ama Hadithi iliyotajwa katika swali imepokelewa na Imamu Ahmad katika musnadi yake kutoka kwa Wabiswah Ibn Maabad Al-Asady R.A kuwa amesema: “Nilipita kwa Mtume S.A.W na mimi nikiwa nataka kutoacha kitu chema na kiovu isipokuwa nimuulize, na pembezoni mwa Mtume kulikuwa na kundi la Waislamu wakimuuliza mambo mbali mbali, nikiwa ninawavuka wale watu, wakasema: Una nini ewe Wabiswah kwa Mtume S.A.W nikasema: Niacheni nimsogelee kwani ni mtu nimpandaye sana kuwa karibu naye, akasema Mtume S.A.W mwacheni Wabiswah, sogea karibu ewe Wabiswah” alisema mara mbili au mara tatu, nikamsogelea mpaka nikakaa karibu naye na akasema: Ewe Wabiswah nikupe habari au utaniuliza? Nikasema: Hapana, bali nipe habari, akasema S.A.W: “Umekuja kuniuliza kuhusu wema na uovu” nikasema: Ndio, basi akakusanya vidole vyake akawa anavichezesha kifuani kwangu na anasema: “Ewe Waswibah uulize moyo wako, uulize moyo wako” akaniambia mara tatu, “Wema ni kinachotuliza nafsi, na uovu au dhambi ni kinachojenga shaka kwenye nafsi na wasi wasi na hofu moyoni, ikiwa watu watakwambia kuwa hii ni haki basi usiyachukuwe maneno yao”. Amepitisha Imamu An-Nawawiy katika kitabu chake Ukurasa wa 96 chapa ya Dar Al-Ghauthany.
Hadithi haina maana kuwa kiwango cha kufahamu hukumu za Kisharia na kubainisha usahihi ni kwa hisia za nafsi na moyo; kwani Wanachuoni wana njia mbili katika maelekezo ya Hadithi, miongoni mwao wameifanya ni Hadithi maalumu kwa Wabiswah R.A kwa lengo la maana maalumu aliyoifanya, na kwa hilo hukumu haiwezi kuhama kwenda kwa mwingine, na Hadithi wakati huo inakuwa kwenye tukio maalumu na si matukio ya jumla, amesema Imamu Ghazaliy katika kitabu cha [Ihyaau Uluumu deen 117/2 chapa ya Dar Al-Maarifah]: “Mtume hakumjibu kila mtu bali alisema hilo kwa Wabiswah kwa vile alifahamu hali yake”.
Wengine wameifanya kwa Muumini ambaye ameifikia nuru ya Imani na kufikia viwango vya ucha-Mungu pale anapofikwa na jambo lenye kuchanganya kwenye uhalali wake au kufaa kwake na wala hakukuta kauli ya yeyote isipokuwa kauli ya yule asiye aminika elimu yake au dini yake. Al-Hafidh Ibn Rajabu Al-Hambaly amesema katika kitabu cha [Jaamii Al-Uluum wal-Hikam 103/2 chapa ya Taasisi ya Risalah]: “Ama yasiyokuwa na Maandiko yatokayo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W wala kauli ya wafuasi wa kauli yake miongoni mwa Maswahaba na waja wema wa Umma waliotangulia, pindi yanapotokea kwenye nafsi ya Muumini mwenye kutulia moyo wake kwa Imani, kifua chake kikifunguka kwa nuru ya maarifa na uyakini, na kifua chake kuwa na hofu kwa shaka shaka zilizopo, na wala hakupata mtu wa kutoa Fatwa ya kuruhusu isipokuwa mwenye kuelezea mtazamo wake naye ni miongoni mwa asiyeaminika kwa elimu yake na dini yake, bali ni anafahamika kwa ufuataji wa matamanio, hapa Muumini anarudi kwenye hofu ndani ya kifua chake hata kama watafutu hawa wenye kufutu”.
Amesema Al-Mulaa kwenye kitabu cha [Mirqat Al-Mafaatih 1901/5 chapa ya Dar Al-Fikri]: “Ikasemwa: Maana kwenye jambo hili kuna mitazamo ya watu wa mitazamo na fikra zilizonyooka na watu wenye nafsi zenye kuridhia na nyoyo salama, hivyo nafsi zao kikawaida huelekea kwenye kheri na kujitenga na shari, kwani kitu chenye kuvutia kwenye kile kinachoendana sawa nacho na kuwa mbali na kile kilicho kinyume, na kuwa mwenye umuhimu mkubwa wa usahihi katika hali nyingi. Amesema At-Taurishty R.A na kauli hii hata kama itakuwa haijatupwa lakini kauli ya kubeba kwake ujumla wa mambo kwa wale wanaokusanywa na neno la Ucha-Mungu na kuzungukwa na wigo wa dini iliyo kweli zaidi na uongovu”.
Kwa maelezo hayo na kwa mujibu wa swali: Kitendo alichokifanya baba yako ni halali Kisharia na wala hakuna ubaya wowote na hasa kwa kuwa amefanya kwenu hilo kwa upendeleo nao ni utoto na kutokuoa, na kitendo hicho kinaendana na athari zake zote kuanzia uthibiti wa umiliki kwako na ndugu zako katika kile alichowapa bila ya kuwapa ndugu zako wengine wawili wa kike, hivyo hakuna ubaya kwenu kunufaika na kilichotolewa, ama ukiwa unataka kupita mapito ya kujitolea kwa kumrudishia dada yako kwa upande wa baba kile mlichokuwa mkichukue la kama mzazi wa kiume asingekupeni kama zawadi basi unaweza kufanya hivyo hata kama ni sehemu ndogo ya hiko, lakini kwenye sehemu yako, na hilo linakuwa kwako kwa njia ya kujitolea na wala si kwa njia ya wajibu na ulazima, lakini hata hivyo huna haki ya kuwalazimisha ndugu zako kufanya hivyo katika mafungu yao bali jambo hilo linarudishwa kwao wenyewe wakiwa watapenda watatoa na kama hawatapendezewa basi watabaki nayo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas