Kufufuliwa na Maisha ya Akhera kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufufuliwa na Maisha ya Akhera kwa Mayahudi

Question

 Assalaam Alaikum. Mwenyezi Mungu Anasema katika Suratul-Aala Aya ya 17 – 19:
{Lakini nyinyi mnapenda sana maisha ya dunia ¬* Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi * Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo * Vitabu vya Ibrahimu na Musa}.
Hii inaashiria kuwa maisha ya Akhera au maisha baada ya kifo kama ilivyokuja katika Vitabu vya Nabii Ibrahim miaka 16000 kabla ya Kristo, na Vitabu vya Musa miaka 1200 kabla ya Kristo.
Wasiokuwa Waislamu wanasema kuwa Mayahudi hawakuwa na elimu kuhusu maisha ya Akhera au hata uhai baada ya kufufuliwa mpaka ilipotokea hali ya mawasiliano kati yao na Wafursi takriba miaka 500 kabla ya Kristo.
Kama vile hakuna ishara yoyote ya imani hizi katika Agano la Kale kabla ya kuonekana athari za Wafursi, tunataka hoja ya Aya hii ya Qur`ani? Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema.

 

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Aya Tukufu inasema: {Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo * Vitabu vya Ibrahimu na Musa}. Na ishara ya Aya Tukufu katika kauli ya Mola Mtukufu {Haya} inakusudia kauli ya Mola Mtukufu: {Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa * Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali * Lakini nyinyi mnapenda sana maisha ya dunia * Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi}. Makusudio ni kuwa mazungumzo ambayo yamekusanya Aya Tukufu yamo ndani ya Vitabu vya mwanzo Vitabu vya Ibrahim na Musa ima kwa maana zake au matamshi.
Imepokelewa na Ibn Mardawiy kutoka kwa Abi Dharr amesema: “Nilisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je kuna chochote kimeteremshwa kwako katika vile vilivyokuwemo kwenye Vitabu vya Ibrahimu na Musa? Akajibu Mtume S.A.W.: {Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa * Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali * Lakini nyinyi mnapenda sana maisha ya dunia * Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi}.
Kuamini Siku ya Mwisho kwa kuzingatia asili yake ni nguzo katika nguzo za imani ya Dini ya Kiyahudi Kikristo na Uislamu pamoja na kuwa ufafanuzi wa imani hii hutofautiana kati ya dini na nyingine, lakini asili ya imani ni thabiti hata kama kutakuwa na tofauti ya ufafanuzi, kwani Dini ya Kikristo inazingatia kuhesabiwa Siku ya Kiyama ni kupitia kwa Masihi ndio ambaye atawahesabu waja, na Uislamu unazingatia mhesabu Siku ya Kiyama ni Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Muhammad S.A.W. ni mwombezi mkubwa.

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas