Siku ni kama miaka elfu na miaka el...

Egypt's Dar Al-Ifta

Siku ni kama miaka elfu na miaka elfu hamsini

Question

Samahani, sikumbuki kwa hakika, lakini katika Qur’ani ilisema kwamba mwaka mmoja kwa Mwenyezi Mungu ni kama miaka elfu katika Aya moja na kama miaka elfu hamsini katika Aya nyingine? Tafadhali nisaidie ili kujiepusha na minong'ono ya Shetani. 

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi.} [AL HAJJ: 47]
Na Mola Mtukufu akasema: {Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi} [As-Sajdah 5]
Vile vile Mwenyezi Mungu akasema: {Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!} [AL MA'AREJ: 4]
Aya hizi tukufu zinazungumzia hali mbalimbali. Katika ulimwengu wa Akhera na Kiyama kuna matukio mengi na hali mbalimbali. Kwa kuzingatia wingi wa hali na matukio haya, wakati wa kila hali na mandhari hutofautiana kutoka kwao, kama vile wakati wa siku ya Kiyama ulitofautiana na siku za dunia katika muda wake na masharti mengine. Siku hizi zina viwango vingine vinavyotofautiana na viwango vya maisha tunayoishi. Kwa hivyo wafasiri wakasema kwamba siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu ni siku ya Saa ya Kiyama, au siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini ni siku ya kupaa kwa roho na malaika kwa Mwenyezi Mungu, na hii ni siku tofauti na siku iliyopita ambayo ufufuo utatokea.
At-Tahrir Wa At-Tanwir (Juz 11 / uk. 161)
Na siku ile kutokana na kauli yake {Kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu} ndiyo ni siku iliyotajwa katika Aya ya Surat Al-Hajj (47) kwa kusema: Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi} Na maana ya kupima kwake katika miaka elfu: Inapatikana ndani yake kutokana na vitendo vya Mwenyezi Mungu katika viumbe vya mbingu na ardhi lau ingekuwa kutokana na vitendo vya watu, mfano wake ungetokea katika miaka elfu moja, basi unaweza kukadiria hilo kwa idadi ya matendo, au kwa kukata umbali, na uwezekano kadhaa umewekwa katika hilo.
At-Tahrir Wa At-Tanwir (Juz 11 / uk. 162)
Maana ya hivyo ni: kuonya juu ya ukuu wa uweza na ukuu wa ufalme wa Mwenyezi Mungu na usimamizi wake. Inaonekana kwamba siku hii ni siku ya Kiyama, yaani saa ya kuharibika kwa ulimwengu wa dunia, na siku iliyotajwa hapa sio Siku ya Kiyama iliyotajwa katika Surat Al-Maarij, kasema Ibn Abbas. Hakubainisha mojawapo, na wala sio lengo la wasomaji kubainisha mojawapo ya siku hizo mbili, bali ni somo lilipatikana kutokana na mambo ya kutisha.
At-Tahrir Wa At-Tanwir (Juz15 / uk. 307)
{Malaika na Roho hupanda kwendea kwake}, maana yake ni roho za watu wa Peponi kwa daraja tofauti katika mbingu. Kupaa huku kutakuwa Siku ya Kiyama, ambayo ni siku ambayo urefu wake ni miaka elfu hamsini. Haya ni makadirio ya mwisho wa ukuu wa nyumba hizo, kupaa kwa watu mashuhuri wa ulimwengu kwao, na ukuu wa siku iliyotokea.

 

Share this:

Related Fatwas