Kuoa kwa Mtume S.A.W Bibi Aisha.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuoa kwa Mtume S.A.W Bibi Aisha.

Question

 Swali: Ni vipi Mtume alimuoa Bibi Aisha?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu.Baada ya utangulizi:
Wamepokea kundi la watu wa usahihishaji wa Hadithi kuwa Mtume S.A.W alifunga ndoa na Bibi Aisha akiwa ni binti wa miaka sita na kukutana naye kimwili akiwa binti wa miaka tisa, haya yamepokelewa na kundi kubwa la wapokezi kwa njia tofauti, baadhi yao wamepokea kwa Hisham Ibn Ur’wa Kiongozi wa watu wanaoaminika na baadhi ya wengine wamepokea kwa wengine.
Ama shaka inayozunguka kwenye hilo:
Ni utafiti kuhusu sababu ya kuoa Mtume S.A.W Bi Aisha akiwa na umri huu ambao unaonekana kwa vigezo vya zama za leo ni umri ambao haifai kwa binti kuolewa kwa umri huu.
Msukumo sahihi wa swali hili ni kutofahamu tofauti kubwa kati ya mazingira tofauti na staarabu ambazo zinatenganisha kati yake kwa miaka mingi, na utekeleza wa mila na desturi za zama za sasa na zama za zamani pamoja na kuondoa tofauti kubwa inayotokana na zama pamoja na mazoea ya watu.
Ni mazoea mangapi yalikuwa yamechukuwa nafasi kwa watu na mwishowe yamebadilika kwa watu wengine, na desturi ngapi zilizoeleka kwa watu na wala hakuna athari zake kutokana na tofauti za desturi na mazoea kutoka zama moja kwenda zama zingine.
Kwa sababu hiyo watu wa “Makka” wala hawakushangaa pale ilipotangazwa habari ya kuoa na wala hakupatikana mtu yeyote katika maadui wa Mtume S.A.W aliyeichukulia ndoa ya Mtume kwa Bibi Aisha pingamizi au mlango wa kujeruhi na kutuhumu, nao ndio ambao hawakuacha njia ya kumpinga isipokuwa waliitumia hata kama njia hiyo itakuwa ni uwongo na uzushi….na Qur'ani Tukufu imeelezea hilo katika hukumu za Aya zake.
Je wanapinga kuchumbiwa msichana mdogo kama Bibi Aisha ambaye hajavuka umri wa miaka saba?
Lakini alishawahi chumbiwa kabla ya kuchumbiwa na “Muhammad Ibn Abdillah” na “Jubeir Ibn Matwam Ibn Adey” ambapo “Abubakri” hakuweza kumpa neno lake kwa Khaula Binti Hakeem, mpaka ukapita muda na kutekeleza ahadi yake kwa Abi Jubair.
Je wanapinga kuwa ndoa kati ya binti mdogo kwa umri wake na kati ya mtu aliyefikia umri wa miaka hamsini na tatu?
Kuna la kushangaza lipi kwenye hali kama hii, na hakuwa binti mdogo wa kwanza akiolewa kwenye mazingira hayo na mtu wa umri wa baba yake, na wala hilo halitakuwa ndio tukio la mwisho, kwani alishawahi kuozesha “Abdulmutwalib” binti wa baba mdogo wa “Amina” siku ambayo alioza Abdillah mtoto wake mdogo wa kike mfano wa Aisha naye ni “Amina Binti Wahab”
Na “Omar Ibn Khattab” alioa binti wa Ally Ibn Abi Twalib akiwa na umri zaidi ya umri wa baba wa mwanamke.
Na “Omar” akimuelezea “Abibakri” kumuoa binti yake kijana “Hafswa” na kati yao wakiwa na tofauti ya umri mfano wa umri wa Mtume na Aisha…
“Lakini ndoa hii ya Mtume S.A.W imewashuhurisha baadhi ya wanahistoria na wameiangalia sawa na mtazamo wa jamii ya sasa ambayo wao wanaishi, wala hawakukadiria kuwa ndoa mfano wa hizo imekuwa na imeendelea kuwa ni kawaida kwa nchi za Asia, wala hawajafikiria kuwa desturi hii bado ipo eneo la nchi za Mashariki mwa Ulaya, na ilikuwa asili ya Uhispania pamoja na Ureno mpaka miaka ya hivi karibuni, na yenyewe hii leo imekuwa si ndoa ya kawaida ndani ya baadhi ya maeneo nchini Marekani” ( ).
Ama kuhusu hoja zilizokuja katika ujumbe zenyewe zinakosa uhakiki:
Maneno ya Ibn Hajar yaliyotajwa yenyewe kwa asili ni kauli mbili, ya kwanza ni kuwa Fatuma ni mkubwa zaidi ya Aisha kwa miaka mitano, na kauli ya pili ni kuwa amezaliwa na umri wa Mtume S.A.W ni miaka thelathini na mitano, yakinukuliwa yote hayo na Ibn Hajar kila moja peke yake kisha akayachanganya yote mwenye kuuliza, angalia kitabu cha Iswaabat fii yamyiizi swahabah 8/54.
Vile vile yaliyotajwa kuhusu kumchumbia Matwam Bibi Aisha, hili linaegemezwa na desturi za Kiarabu walikuwa wanachumbia binti kwa walii wake akiwa na umri mdogo mpaka pale anapokuwa ndio huolewa.
Na yaliyotajwa kuwa Bibi Aisha alishiriki vita vya badri ili kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi uthibiti wake hauna nguvu kisha si dalili ya madai ikilinganishwa na umri imekuwa ni kama mpiganaji na si msaidizi wa wapiganaji.
Yaliyotajwa kuwa Suratul-Qamar imeteremshwa kabla ya Kuhama kwa miaka minane kuna uwezekana yakakosa dalili pia.
Kukomaa kwa mwili kunatafautiana kwa kutafautiana mazingira kwani katika hali ya mazingira ya joto kuimarika kwa mwili kunakuwa haraka sana na kubaleghe pia ni haraka na hasa kwa upande wa wanawake.
Kwa ujumla mitazamo hii sio dalili kwa mwenye madai, lakini mtazamo sahihi ni ule uliyoelezewa na Maimamu na maelezo yaliyopokelewa kwenye Athari kuwa umri wa Bibi Aisha wakati wa kuoelewa kwake ulikuwa ni miaka sita na wakati wa kukutana na Mtume S.A.W ulikuwa ni miaka tisa, na jitihada ambayo ameiwasilisha muhusika huyu ina upungufu wa dalili.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas