Tuhuma za Kuwapendelea Wanaume Zai...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tuhuma za Kuwapendelea Wanaume Zaidi Kuliko Wanawake katika Akhera

Question

  Je! Wanaume watapendelewa zaidi kuliko wanawake katika akhera?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanaume hawapendelewi zaidi kuliko wanawake, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesawazisha baina ya wanaume na wanawake katika hukumu nyingi, Mwenyezi Mungu akasema: Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa. [AL-AHZAAB: 35].
Haya ni katika dunia na Akhera, na suala si lolote ila ni tofauti katika ubora wa starehe kufuatana na tabia ya uumbaji. Mwanaume ana starehe zinazotofautiana na starehe za mwanamke, na hili huzingatiwa duniani na kuzingatiwa huko Akhera, basi starehe ya wanaume ni nyingi kwa mitala, na kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaifanya starehe yao Peponi pamoja na Al-Hor Al-Ain, na starehe ya mwanamke pamoja na mwanamume mmoja, kwa hivyo, starehe ya mwanamke Peponi kuwa pamoja na mwanamume aliyempenda.
Na alipokuja mwanamke kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), ukmuuliza kuhusu mambo ya Dini na akamwambia kwamba wanaume wametupendelea zaidi kuliko sisi kwa kuhudhuria swala ya pamoja na, Mtume (S.A.W), akamjibu kuwa mwanamke anafanya jambo moja ambalo ni sawa na malipo ya yote hayo, nalo ni kumfanyia mume wake wema akasema kuwa jambo hilo ni saw ana malipo ya yote hayo. Uislamu ulizingatia hali, maumbile na udhaifu wa wanawake, hivyo ukawapa malipo makubwa kwa kazi ndogo.

Share this:

Related Fatwas