40- Zaburi Iliyotajwa Ndani ya Qur’...

Egypt's Dar Al-Ifta

40- Zaburi Iliyotajwa Ndani ya Qur’ani Tukufu

Question

 Je! ni kitabu gani cha Zaburi kilichotajwa ndani ya Quran Tukufu? Je, ni sawa na Taurati, Injili, na Qur’ani, na juu ya nani iliteremshwa? Na ikiwa kuna tofauti, tofauti hii ni nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Zaburi: jina la jumla ya maneno ya Nabii wa Mwenyezi Mungu, Daud, (A.S.), ambayo baadhi yake aliteremshiwa na Mwenyezi Mungu na baadhi ambayo alimpa katika maombi na dua. Leo kinajulikana kama Kitabu cha Zaburi kutoka katika vitabu vya Agano la Kale la Biblia.
Na Daudi, (A.S.), alikuwa ni Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kuwasaidia Wana wa Israili katika zama fulani. Na kitabu hiki kiliteremshwa kwake na kina khutba na mithali, na wana wa Israili walikuwa wakiiimba katika sala zao.
Na Qur’ani Tukufu inapozungumzia vitabu vitakatifu ambavyo Mwenyezi Mungu aliviteremsha kwa mitume waliotangulia -kama vile Zaburi, Taurati na Injili - inazungumzia asili ya vitabu hivi vilipoteremshwa, na wala haina maana ya vile ambavyo sasa viko mikononi mwa watu, kwa sababu vitabu vingi vya zamani vimekuwa vilipotea katika nyakati za kale na vimepotoshwa, na hakuna hati inayojulikana ambayo kutegemea usahihi wa maambukizi yao. Mbali na mabadiliko ya lugha yake katika lugha kadhaa, na tafsiri haitoi maana katika hali yake kamili.

 

Share this:

Related Fatwas