Zaka ya mali iliyohifadhiwa kwa aji...

Egypt's Dar Al-Ifta

Zaka ya mali iliyohifadhiwa kwa ajili ya kununua nyumba.

Question

Je inafaa kutoa zaka mali iliyohifadhiwa kwa ajili ya kununua nyumba?

Answer

Ikiwa mwanadamu hana makazi ya kuishi yeye na familia yake, akawa na fedha benki kwa ajili ya kununua nyumba, basi fedha hizi hazina Zaka, na hilo ni kwa sababu ana aminika kuwa anajiandaa kwa jambo la msingi na wala si kwa mambo ya starehe, na fedha zinafanya kazi kwa mahitaji ya asili, hivyo fungu la zaka ni kama hakuna, fedha hizo hazina zaka kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi} Al-Baqarah: 219. Na Mtume S.A.W amesema “Hakuna zaka isipokuwa kwa tajiri” imepokewa na Ahmad.

Ama mali inayozidia thamani ya nyumba hiyo itawajibika kutolewa zaka ikiwa itafikia kiwango cha kutolewa zaka pamoja na kufikisha mwaka, na hilo ni kwa kiwango cha robo ya fungu la kumi (2.5%) katika jumla ya hizo fedha.

Share this:

Related Fatwas