Namna za kisasa za Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
Question
Ni ni zipi namna za kisasa za Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu?
Answer
Jihadi inawezekana kuwa kwa namna na hali za kisasa zinazoambatana na muktadha wa haki ya wakati na maendeleo yake, ambapo wajibu wa kwanza kabisa unatakiwa kutoka kwa jamii ya Waislamu; wajibu ya kuitetea nchi ikishambuliwa na maadui kwa sababu yoyote, na kuendelea kuwa wacha Mungu, kushirikiana, kufanya juhudi na kutumia mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kujiandaa kwa mambo haya, pia, kujitahidi kulinda mipaka na maeneo muhimu kutokana na maadui, na kwa watu binafsi basi miongoni mwa aina za kisasa zilizo wazi za Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kujiunga na majeshi ya nchi kwa kutambua kuwa hayo ni wajibu wa dini na nchi, vile vile, tunapaswa kujua vema kwamba sisi yaani; Waislamu wa zama za kisasa hatuna haja ya kwenda kwa majeshi kwa nchi zisizo za Kiislamu kwa lengo la kufikisha daawa, zaidi ya kusafiri na kuzunguka kutoka nchi hadi nyingine kwa mujibu wa kanuni za kimataifa zinazotoa dhamana ya kuhakikisha na kuheshimu uhuru wa kuchagua dini na itikadi na kukataza ubaguzi kati ya watu kwa sababu ya dini au kabila, vipindi vya satalaiti na mitandao imeenea sana na kuunganisha nchi zote duniani takriban, hivyo, kueneza ujumbe fulani upande wowote ulimwenguni huwa ni jambo rahisi.