Kuwezesha dini ya Mwenyezi Mungu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwezesha dini ya Mwenyezi Mungu

Question

Makundi ya kigaidi na wenye fikra potofu wanadai kuwa wanafanya juhudi za kuiwezesha sharia na dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu na kuondoa dhuluma za jamii zigeuke kwa mwangaza, je, madai haya yako sahihi?

Answer

Neno la "Tamkiin" kuwezesha limetumika katika Qur`ani Takatifu katika Aya nyingi, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu: {Jee, hawaoni vizazi vingapi tulivyo viangamiza kabla yao? Tuliwaweka katika nchi tusivyo kuwekeni nyinyi} [Al-Ana'am: 6], na kauli yake (S.W.): {Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote} [Al-Hajj: 41], na {Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao} [An-Nuur: 55].

Kwa kuangalia Aya zilizotajwa hapo juu tunaona kuwa Mwenyezi Mungu Ametumia neno "Tamkiin" kwa maana ya kuwezesha na kusimamisha dini kwa muumini na asiye muumini na kwa umma waliotangulia, na kwamba mtendaji wa kitenzi katika Aya zote ni Mwenyezi Mungu (S.W.), ambapo Mwenyezi Mungu Amefanya kuwezesha na kusimamisha dini ni kazi yake mwenyewe siyo hukumu ambayo mwanadamu anaweza kuifanya mwenyewe kupitia kuhakikisha sababu zake.

Na ukiwaza kidogo kuhusu hali yetu ya kisasa tutaona kuwa kutokuwa na mbinu ya kitaaluma kumewapelekea baadhi kufahamu kuwa maana ya kuwezesha na kusimamisha dini ni harakati za kumwezesha mtu kufikia madaraka kupitia kuzihukumu jamii ukafiri, na kudai kuwa wao ndio waumini peke yao na kuwa wao ndio wamiliki wa Uislamu wakidai kuwa hali hii inahitaji kujitahidi kwa ajili ya kufikia malengo haya kwa kurudisha mambo kama yalivyokuwa zamani.

Share this:

Related Fatwas