Kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Uanaume au Uanamke

Question

 Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasifiwa kwa Uume au Uke?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swali hilo sio sahihi, kwani swali kuwa sahihi lazima kuwepo uhusuiano baina ya maneno yake; uhusiano wa kiakili, kimatamshi na kiuhalisi, yaani kwa akili na kwa maneno na katika uhalisi wa nje unaotazamiwa. Na kwa ajili ya kueleza matamko tunataja mfano huu:
Kama mtu atakwambia kwamba hii ni kabati ya mbao iliyopo ndani ya chumba chako cha kulala, je, linahisi joto au baridi? Hakika wewe huwezi kumjibu kwamba kabati linahisi joto au baridi kwa sababu Kabati sio la kuhisi joto au baridi kwa kuwa sifa zake ni tofauti na zile za Watu ambao wanahisi joto na baridi.
Basi majibu sahihi ambayo anajibiwa mwenye swali hilo kwamba swali hilo silo sahihi, kwani kabati halihisi joto au baridi.
Kwa hiyo tunasema kuwa swali si sahihi, na kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu mfano wa juu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu siye kama watu, awe mwanmume au mwanamke, na maana hiyo ni aliyoyataja Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitakatifu aliposema: {Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona} [ASH SHURA 11]
Kinachokusudiwa katika Aya Tukufu ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hawakilishwi na chochote katika viumbe vyake na kwa hivyo Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamuwakilishi yeyote katika viumbe vyake katika Sifa hizi zote za Kuumba, kuanzia Umbile, Jinsi lilivyo, Sifa zake Maalumu, Uume au Uke na sifa zingine mbalimbali; kwa hivyo, Mola Mlezi ni Mola Mlezi, na Mja ni Mja na kuna tofauti kubwa baina ya Kiumbe na Muumbaji.
Na Ishara iliyopo katika Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Sema Yeye Mwenyezi Mungu ni Mmoja} sio kinyume cha Kiwakilishi Jina cha Kike bali hakika mambo yalivyo kinachokusudiwa katika Aya Tukufu ni kuwafahamisha Viumbe juu ya Mwenyezi Mungu kwa namna akili zao zinavyofahamu na wala haikusudiwi kamwe Uanaume kinyume cha Uanamke.
Kwani Matumizi ya Kiwakilishi Jina cha Mtu wa Tatu ni "Ishara ya Upweke wa Kike, na zote hizi ni katika sifa maalumu za lugha ya Kiarabu zinazohusika na kuwasemesha Watu lakini Lugha katika Utambulisho wa Mwenyezi Mungu haiendani na Sifa hizo. unaweza kurahisisha maelezo haya kwa Kujibu swali lililo karibu na la kweli.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas