Mwenyezi Mungu kunasibishwa na sehe...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwenyezi Mungu kunasibishwa na sehemu.

Question

Je! Watu wa Al-Ashaaira wanamnasibisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yupo sehemu zote?

Answer

Watu wa Al-Ashaara hawajasema kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yupo sehemu zote, na hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyesema hivyo, na inafahamika kuwa watu wa Al-Ashaaira wanachosema katika Madhehebu yao ni kukosekana sehemu na upande kwa Mwenyezi Mungu, wao ni watu wa utakaso kwa Mwenyezi Mungu, nao ni Ahlu Sunna wal-Jamaa ambao Akida yao inafuata Akida ya watu waliotangulia wa Umma huu, na Wanachuoni wao wanafahamika, hivyo ni vipi wahusishe sehemu ya Muumba wao, AbdulQaadir Al-Baghdadi amesema: “Wamekubaliana kuwa hapatikani sehemu wala kuhusishwa na wakati”.

Akida hii ya waja wema waliotangulia miongoni mwa Maswahaba – Radhi za Mungu ziwe kwao – Imamu Ally R.A. anasema: “Mwenyezi Mungu hana sehemu, Naye hivi sasa yupo kama alivyokuwa” kwa maana Mwenyezi Mungu hausishwi na sehemu iliyoibuka yenye kuumbwa, na mwisho wa mambo ni kuwa inaweza dhaniwa na mdhaniaji kuwa watu wa dhehebu la Al-Ashaaira wanasema hivyo kwa kauli yao: Yeye Mwenyezi Mungu elimu yake imezunguka vitu vyote, hivyo hakuna sehemu wala zama isipokuwa anafahamu, na hilo tofauti na kudhani kwao.

Share this:

Related Fatwas