Kitenzi Ata “Kimekuja” na Kiwakili...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kitenzi Ata “Kimekuja” na Kiwakilishi cha Umoja Kinachorejea kwa Wawili

Question

 Aya ya Qur`ani: {Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni nyinyi, hali ya kuwa wanao stahiki zaidi kuridhishwa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake, lau kama wao ni Waumini}{At-Tawbah: 62}.
Swali: Ni nini alichokisema mjenga hoja?

Answer

 Ni kwanini kiwakilishi jina hakikuja kwa maana ya wawili jina la Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kingesema kuwaridhisha hao wawili? ( ).
Kuondoa shaka
1. Muulizaji ameshindwa kufahamu ni ipi yenye kufaa zaidi kwenye sifa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kufanyiwa uwingi na mwengine yeyote katika waja wake ndani ya muundo mmoja hata kama huyu mja ndio mja bora wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye Muhammad S.A.W. kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenyezi Mungu na mja ni mja na kuna tafauti kati ya kiumbe na Muumba.
2. Muulizaji pia ameshindwa kuelewa kuwa katika Aya Tukufu kuna kitu kinachoitwa mfumo bora nao ni katika uzuri wa elimu ya fasaha au elimu ya lugha, na muulizaji hakufahamu bali amefanya umoja wa kiwakilishi jina katika kauli ya Mola Mtukufu: {Kuridhishwa} pamoja na kuwa kimerejea kwa wawili kwa sababu kimetakiwa kiwakilishi jina kurejea kwa jina la kwanza katika majina mawili, na kuzingatiwa kiunganishi ni katika viunganisha vizuri ambapo inakadiriwa: Mwenyezi Mungu ndio mwenye haki zaidi kuridhishwa na Mtume wake pia, hivyo maneno yanakuwa ni sentensi mbili kama Siibawayhi alivyosema. Na kiwakilishi jina katika neno “Kuridhishwa” kinarudi kwenye jina Takatifu la Mwenyezi Mungu, kwa sababu ndiyo muhimu zaidi katika habari, na kwa sababu hiyo ndiyo kimeanza nalo.
Na mfano wa Aya Tukufu kauli yake Mola Mtukufu: {Kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina}.
3. Hakusema: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote wawili hao kwa washirikina, kwa sababu sifa ya Mwenyezi Mungu kutokuwa na jukumu kwa washirikina ni sifa ya kiupwekeshaji kwa mmoja peke yake ambaye hana wa mfano wake katika uwepo wote, kwa sababu hiyo ndio maana Amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina} kwa maana na Mtume wake hana jukumu kwao, na kitu kinachojulisha hili ni yale yaliyotajwa kwanza kwa upande wa Mwenyezi Mungu.
4. Kama vile kuridhia Mtume ni katika kuridhia Mwenyezi Mungu na kupatikana utafauti kati yao wawili ni jambo halipo hivyo Mtume amekuwa ni sehemu ya kuridhika kwa Mola wake, hivyo imetosha kutajwa mmoja wao.
Huu ndio upwekeshaji ndani ya Qur`ani, undani zaidi na hukumu ya kina na ufikishaji zaidi katika kumtenga Mwenyezi Mungu na usawa pamoja na mfanano hata tamko tawheed au upwekeshaji ni safi lenye kuepukana na mfanano wa kimaana na kuepukana na mfanano wa kimatamshi.
Ndani ya Qur`ani Tukufu halijapokelewa jina la pili yake linakuwa la Mwenyezi Mungu, wala kupokelewa jina la tatu linakuwa la Mwenyezi Mungu si kwa upande wa maana wala matamshi na huo ndio Upwekeshaji halisi, ni Ujumbe wa Mitume yote na Manabii wote.
Kwa Ufupi
Katika Aya kuna mfumo wa muujiza wa kina kwa sababu maana yake ambayo hawakuongoka nayo ni: “Na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye haki zaidi ya kuridhishwa na Mtume wake ni mwenye haki zaidi ya kuridhishwa hivyo “likaondoshwa” neno mwenye haki zaidi ya kuridhishwa kwenye jina la kwanza kwa dalili ya jina la pili “Na Mtume wake ni mwenye haki ya kuridhishwa”. Na huu ndio utaalamu wa elimu ya balagha ambapo huitwa: “Mfumo”.
Tafsiri:
Na sharti katika neno: {Ikiwa ni Waumini} limetumika ili kuhimiza na mategemeo ya imani yao, kwa sababu yaliyoelezewa kuhusu wao kutokana na hali mbalimbali hakutabakia uwezekano ndani ya imani zao, hivyo likatumika sharti la mategemeo na kuhimiza Imani, na ndani yake pia kuandika ikiwa watarudia mfano wa matendo yao basi watakuwa ni makafiri kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake, na ndani yake pia kuna mafunzo kwa Waumini na tahadhari kutokana na hasira za Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Miongoni mwa njia za maelezo ya Qurani wakati wa kutajwa Mtume na kutajwa jina Tukufu la Mwenyezi Mungu:
Ndani ya Suratul-Tawbah yenyewe vilevile imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na laiti wao wangeli ridhia kile alicho wapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu Anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila zake na pia Mtume wake; hakika sisi ni wenye kumtaka Mwenyezi Mungu}
Uzuri wa imani ya upwekeshaji katika mifumo ya Qurani kwenye maeneo matatu:
Eneo la Kwanza: {Alichowapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake} ambapo ameunganishwa Mtume na jina la Mwenyezi Mungu pasi na kuwepo Kiwakilishi Jina cha wawili.
Eneo la Pili: {Mwenyezi Mungu Anatutosheleza} pasi na kuunganishwa Mtume na jina la Mwenyezi Mungu, kwa sababu kutosheleza hakuwi ispokuwa na Mwenyezi Mungu.
Eneo la Tatu: {Mwenyezi Mungu Atatupa katika fadhila zake na pia Mtume wake} pasi na kuletwa Kiwakilishi Jina cha wawili na kusema kwa mfano kutokana na fadhila zao bali limeunganishwa neno na “Mtume wake” baada ya kukamilika sentensi ya kwanza.
Kisha likafutwa katika sentensi ya pili neno “Na Mtume wake” inajulisha kwenye maelezo yaliyopita, kwa maana: Atatupatia Mtume wake kutokana na fadhila zake.
Mfumo upo wa aina mbili
Mfumo wa Kwanza: Ni kufuta maneno ya sentensi ya kwanza na kuoneshwa katika sentensi ya pili iliyokuja baada yake moja kwa moja, mfano wa Aya ambayo wameifanya chanzo cha hii shaka.
Mfumo wa Pili: Ni kufuta maneno sentensi ya pili yanayojulisha kutajwa katika sentensi ambayo imetangulia, na mfano wake ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu: {Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana kuangaza .. }
Na maana yake ni kuwa: Mchana kuwa mwangaza ili wapate kufanya mihangaiko yao, hivyo likafutwa neno kwa sababu “ili watulie” ni dalili yenye nguvu kwenye hilo.
Na unaweza fahamu ufutwaji wa kwanza, vilevile ni kutokana na dalili ya pili nayo ni neno “Kiza” kwa maana tumeufanya usiku kuwa ni kiza au giza, na kufutwa kwa sababu yaliyokuja kwenye sentensi ya pili nayo ni “Muangaza” ni dalili ya hilo.

Share this:

Related Fatwas