Kitenzi Ata “Kimekuja” kwa Kiwaki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kitenzi Ata “Kimekuja” kwa Kiwakilishi Jina cha Mtendaji Pamoja na Kuwepo Mtendaji

Question

 Aya ya Qur`ani: {Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo * Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi mnaona!}{AL ANBIYAA: 2, 3}.
Swali: Nini amesema mjenga hoja?

Answer

 Kufutwa kwa kiwakilishi jina cha mtendaji katika neno Assarruu kwa maana ya “Kuongea kwa siri” kwa kuwepo mtendaji wa wazi naye neno Alladhina kwa maana ya “Wale ambao”( ).
Kuondoa shaka
1. Muulizaji amekosa uelewa katika hii shaka kuwa Qurani Tukufu imeteremka kwa lugha zote za Waarabu( ) na matumizi yaliyokuja kwenye Aya Tukufu ni katika lugha za Waarabu( ).
2. Lugha hii ambayo imekuja kwenye Aya Tukufu ni lugha ya fasihi ya Kiarabu imekuja na Aya za Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume S.A.W. bali na mashairi pia ya Kiarabu, katika Aya za Qurani ambazo zimekuja na kanuni hii ni kauli yake Mola Mtukufu: {Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona hayo wayatendayo}[AL MAIDAH: 71] na katika Hadithi Tukufu ambazo zimekuja kwenye kanuni hii ni pamoja na kauli yake Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Abi Huraira R.A.: “Munalindwa na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana”( ).
3. Aya Tukufu imekuja na mifumo ya kina inayokubaliana na kanuni za lugha na kuruhusu upanuzi wa maana na kuelezea siri za ubainifu, kwani Wanachuoni wametoa maelezo mbalimbali ya Aya Tukufu na kila maelezo yanafungua maana mpya pasi na kusumbua maana ya Aya, na hii ni ufasaha wa lugha ya Kiarabu ambayo haifahamiki kwa kina isipokuwa na wasomi.
4. Kauli za Wanachuoni katika kuelezea Aya Tukufu zimejikita katika pande mbili kwa ujumla:
1- Ni kuifanya herufi ya Waw ndio kiwakilishi cha mtendaji wa kitenzi Assarruu “Wamefanya siri” na kwa maelezo haya kuna maelekezo mengi ya mambo ya silabi.
Maelekezo ya Kwanza: Neno “Hakika wale waliodhulumu” badala ya wote katika wote na herufi ya Waw katika neno Assarruu kwa maana ya “Wamefanya siri” kwa sababu herufi ya waw ni ya wingi.
Maelekezo ya Pili: Ni kuwa imekuja kwenye lugha ya baadhi ya makabila ya Kiarabu ambayo yanakusanya kiwakilishi jina pindi anapotokea mtendaji na kile kinachofasiri.
Maelekezo ya Tatu: Kuwa sehemu ya silabi ya fat’ha katika kulaumu, ambapo makadirio ya kitenzi yamefutwa ambayo ni: Lawama maalumu kwa wale waliodhulumu.
Maelekezo ya Nne: Kuwa ni Kiima na yaliyokuja kabla yake ni kielezi chake, kwa maana ya wale ambao wamedhulumu wamenong’ona kwa siri.
2- Ni kufanya maneno {Ambao wamedhulumu} ndio mtendaji wa kitenzi cha Assarruu kwa maana ya “Waliongea kwa siri” ama herufi ya Waw yenyewe ni alama ya wingi wa watendaji na si vyengine, na Waarabu walikuwa wakifanya hivyo hata kwa upande wa wawili.
3- Muulizaji hakutaja wajibu wa kufutwa kwa dhamiri katika neno Assarruu kwa maana ya wameongea kwa siri, inampita maana hii kubwa na kuharibu mifumo ya Aya Tukufu na kupoteza yaliyomo kwenye Aya miongoni mwa mambo ya ufasaha na muujiza.

 

 

Share this:

Related Fatwas