Kugeuza Maelezo Kutoka Nafsi ya Pi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kugeuza Maelezo Kutoka Nafsi ya Pili Kwenda Nafsi ya Tatu Kabla ya Kukamilika Maana

Question

Aya yenye kuleta shaka:
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
 

Answer

{Yeye ndiye anaye kuendesheni nchi kavu na majini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo humuomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru} [YUNUS 22]
Nini amesema mlalamikaji.
Ni kwa nini maelezo yamegeuzwa kutoka nafsi ya pili ambayo ni wewe kwenda nafsi ya tatu ambayo ni yeye kabla ya maana kutimia? Sahihi ni kuendelea kumzungumzisha anayeambiwa ( ).
Msukumo wenye kuleta shaka:
Muulizaji amekosa kufahamu vigezo vya muundo wa kugeuza maelezo katika lugha ya Kiarabu ambao umeletwa na Qur`ani Tukufu, miongoni mwa faida za kugeuza maelezo katika Aya hii Tukufu.
Ni kuwa baada ya kutaja neema ukaja mfumo wa kuzungumza ili kuenea kwa wote wanaoambiwa na Qur`ani Tukufu mpaka siku ya Kiyama katika kauli yake:
{Yeye ndiye anaye kuendesheni nchi kavu na majini. Hata mnapo kuwa majahazini} baada ya maelezo kuhama kutoka kwa washirikina na kuelezea uwongo wao maelezo yakabadilika na kuzungumzia watu wa mbali au nafsi ya tatu Mwenyezi Mungu Akasema:
{Na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande} ili kuwazindua juu ya ubaya wa matendo yao na kupinga kwao katika Aya Tukufu ambayo inafuata kauli yake Mola Mtukufu: {Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki} [YUNUS 23]
Ugeuzaji wa mazungumzo katika Aya ya kwanza ukaleta faida kuwa upingaji huu ni wenye kuelekea kwa washirikina tu na si kwa wengine katika Waislamu ambao mazungumzo yao yanakuja kwenye Aya Tukufu na kuendelea mpaka kusimama Kiyama, “Aina hii ya kugeuza mazungumzo haijaelezewa na watu wa elimu ya lugha nayo ni kuhusisha kwa njia ya alama” ( ). Na ikaanza kuleta dhamiri ya mtu wa mbali mwishoni mwa kutaja neema kwenye kauli yake Mola Mtukufu: {Na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakafurahia} ili kuelezea kuwa neema imewaenea wote, na ishara ya kuja kwa upepo mkali imekuja katika hali ya furaha kusudio lake na kuwapa mtihani na kuwatisha, ikiwa ni maandilii ya kauli yake Mola Mtuufu: {Yakawajia mawimbi kutoka kila upande} utumiaji huu ni wa Qur`ani Pekee nao ni katika ubunifu wake ( ).
Aya hizi zimeleta mifano mingi ya kubadilisha maelezo kutoka kuambiwa nafsi ya pili kwenda nafsi ya tatu ili kufanya dhamiri ya kuambiwa kuwa kwa washirikina na kufanya pia dhamiri ya nafsi ya tatu kuwa ni wao.
Imamu Zamakhshary anasema “Ikiwa utasema ni nini faida ya kutumia maneno kutoka dhamiri ya kuzungumzishwa nafsi ya pili kwenda nafsi ya tatu utasema: Utasema ni katika ufikishaji, kana kwamba anataja hali zao kwa wengine ili ziwashangaze, na kupelekea miongoni mwao kupinga na kufanya ubaya”.
Maelezo haya yanahitaji ufafanuzi zaidi nao ni kama ufuatao:
Hawa ambao Mwenyezi Mungu amewazungumzia katika Aya hii wameneemeshwa kutembea nchi kavu na majini, wakapewa mtihani wa upepo na kimbunga baada ya chombo chao kuanza safari na wakajielekeza kwa Mwenyezi Mungu wakimtaka uokozi, wakimuahidi Mwenyezi Mungu ikiwa atawaokoa basi watamshukuru na kufahamu fadhila zake, lakini baada ya kuokolewa wakasahau walichomuahidi Mwenyezi Mungu na wakarejea kumuasi kama Mola Mtukufu Alivyosema: {Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki}.
Ikiwa miongoni mwa faida za kugeuza maelezo kutoka kuwambiwa moja kwa moja kuwa “Mulikuwa kwenye chombo” mpaka kuelezea wengine hali yao ya ajabu ili kuibua hasira zao kwao na kuona ubaya wa matendo yao kwa Mwenyezi Mungu.
Ama watu wa elimu ya matumizi ya lugha baada ya Zamakhshary, wameongezea mitazamo mingine ya kilugha inayokubaliana na uelewa wa Imamu Zamakhshary bila kupingana naye, wakasema: “Siri ya kugeuza maelezo kutoa kuambiwa nafsi ya pili kwenda nafsi ya tatu ni kuwa nafsi ya tatu inakubaliana na kitendo cha “Kutembea kwa chombo” wao wakawa fukweni na jahazi likiwa limetia nanga pembezoni mwa fukwe watu wakawa wanapanda kwenye jahazi au chombo mpaka walipokamilika chombo kikang’oa nanga na kuanza kutembea kwa haraka mpaka wakawa hawaonekani, wao hawapo mpaka ili wazungumzishwe moja kwa moja, lakini kutokuwepo kwao mazungumzi yakaendelea kuhusu wao sawa na kuzungumzia asiyekuwepo”.
Hali zote mbili za kilugha zinatokana na maelezo haya “Na vyombo vikawa vinakwenda nao” bila ya hata kimoja kuachana na chingine.

 

 

 


 

Share this:

Related Fatwas