Mashaka juu ya marejeleo ya Kiislam...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mashaka juu ya marejeleo ya Kiislamu

Question

  Mashaka juu ya marejeleo ya Kiislamu

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Marejeleo: Ni chanzo kinachotokana na maana ya Asili ya Kitu na chanzo kimetengenezwa ili kuonesha sifa ya kitu nacho ni uwezekano wa kutokea na kupinga na wakati huo huo kina sifa ya usimamizi wa binadamu na jamii.
Marejeleo ni fikra kuu ambayo inatengeneza msingi wa fikra zote ndani ya mfumo maalumu na ndio msingi wake thabiti wa mwisho ambao mitazamo ya dunia haiwezi kufanya kazi bila kuwepo kwake… na chanzo kimoja ambacho ndio marejeleo ya mambo yote na kunasibishwa kwake na wala chenyewe hakirejeshwi upande wowote wala kunasibishwa… chenyewe kinajitegemea na kutegemewa na watu wote na vitu vyote na ndio ambacho kinaupa ulimwengu mshikamano wake na mfumo wake na maana yake na kuuainishia halali yake na haramu ( ), na kwa kurejelea asili ya mada kwa upande wa lugha na katika matumizi ya Qur`ani utakuta maana ya mzunguko huu ambao wenyewe ndio msingi na ndio mwelekeo.
Kurejelea: Ni kurudi mwanzoni au kukadiria mwanzo wa sehemu au kitendo au kauli, na kurejelea kunakuwa ni kukirudia chanzo au sehemu ya chanzo au kwa kufaya kitendo katika vitendo vyake, hivyo kurejelea ni kurudi na marejeleo ni kurudia ( ).
Kisha ufahamu wa ukaribu zaidi na ufahamu bora wa kimaarifa ambao unasimamia matendo na tabia ni ufahamu unaosimamia mfumo wa ufahamu na maadili.
Umma wetu umeishi ukiwa na historia ndefu wala hakujawahi jitokeza swali kuhusu nini marejeleo yake kwa uharaka kama huu ambao unatambuliwa na mfuatiliaji wa maarifa ya sasa ambapo jambo lenyewe kwa uhalisia halikuhitaji kuuliza swali.
Ni kama vile uelewa wetu mwingi unaishi kwenye kuhitaji marejeleo kwenye hali ya uwepo wa mvutano wa kimaarifa na kiuelewa na mvutano wa haki kwa upande mmoja na batili kwa pande zingine.
Tawheed kwa maana ya upwekeshaji – kwa sifa yake ya msingi mkuu na uelewa mkubwa pamoja na akida kuu kwa upande wetu – inasimama ndani ya ufahamu huu ( ) ambapo inasimamia uhalali wa kuwepo na kuendelea, na kuimarisha kiwango cha uelewa na kufahanya juhudi za kuufanyisha kazi na kuuboresha, na kuonesha ukati na kati wa chanzo hiki na kushuhudisha kwenye marejeleo na vyanzo mbalimbali.
Kwa hivyo ndio maana Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja Muumba na Muendeshaji wa mambo ambaye kwake ndio msingi wa – kuumba na kuwepo – na kwake ndio sababu ya kuendelea uwepo na mwendelezo ufalme ni wake kisha kwake - Mola Mtukufu – ndio marejeleo na mafikio kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake} [AR RUUM 11] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Na kwa nini nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa?} [YASIIN 22] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema tena: {Yeye ndiye Mola wenu na kwake mtarejeshwa} [HUUD 34].
Madamu Mola ndiye Muumba na Msimamizi wa mambo yote ya ulimwengu na walimwengu, hivyo hakuna nafasi kwa mwanadamu ambaye amepokea kwenye jukumu la kutekeleza amri na kupewa jukumu la kubeba Amana isipokuwa ni kurejelea kwa Muumba wake kwa hiyari akiungana na ulimwengu wenye kumsujudia Mola Mtukufu kwa hiyari na kwa lazima:
{Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumtii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?} [AALI IMRAA 83] Kisha unakuja mtazamo wa Muislamu wa marejeleo yake kuwa ni sehemu ya imani yake kuwa yeye ni mja wa Muumba wa ulimwengu na yeye amepewa amri ya kutekeleza yale aliyepewa kusimamia ndani ya ulimwengu katika ibada ujenzi na utakasifu, na haya ndio yanayofaa kuita “Ibada kwa kufuata marejeleo” kama vile marejeleo ya kiupwekeshaji yaliyo nje ya mwanadamu yaliyobainishwa kwake yanasimamia uadilifu ambao mwanadamu hawezi kuupata kwa kurudi kwa mwanadamu mwenzake “Ibada ya moja kwa moja”.
Na hufungamana maana ya marejeleo ya kati ambapo yanaendana na marejeleo ya kiupwekeshaji na ibada kiuelewa na kimsingi ( ), huendana na kuleta kuumbwa na ibada nayo ni hekima “Iliyopinga upuuzi” ( ) au kujituliza na kuridhia:
{Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?} [AL MU'MINUUN 115] . Mola Mtukufu Amesema:
{Ewe nafsi iliyo tulia * Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha * Basi ingia miongoni mwa waja wangu * Na ingia katika Pepo yangu} [AL FAJER 27-30].
Haya hayapo kabisa kwenye marejeleo yasiyorejea kwa Muumba mwenyewe wala hayapatikani tu wala kukanushwa tu kisha yakapoteza kwenye matamanio na kuingiza kwenye njama chafu na shaka.
Mwanadamu kumuabudu Mwenyezi Mungu – Mtukufu – na kumpa jukumu kwa yale aliyomteremshia Sharia inayozuia upotevu wake na kuhisi kwake kupoteza Muumba wake: {Hapana! Hakika mwanadamu bila ya shaka huwa jeuri * Akijiona katajirika * Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo} [AL A'ALAQ 6-8].
Marejeo na Hoja:
Yaliyopokelewa ndani ya Qurani na Hadithi ni chanzo pekee cha Sharia kupitia kazi za jitihada ambazo hufanywa na wenye kujitahidi ambao wamekamilikiwa masharti na vigezo maalumu vilivyoelezewa na elimu ya misingi ya Sharia.
Na katika alama za vitu fikra watu na taasisi – katika wigo wa marejeo – hupatikana sehemu ya marejeo huongezeka na kupungua kwa kiasi cha kufaa kujinasibisha kwa Muumba Mtukufu, na ambapo kwake mwanadamu unaweza kuteremka ubainifu wa Mungu kwa njia ya ufunuo unaosomeka na ikawa kujengea hoja ufunuo ambao ni Qur`ani kumezuiliwa na kukakubalika kujengea hoja kwenye Hadithi ambayo ni chanzo cha marejeleo ya Kiislamu.
Na vipengele vilivyopitishwa ndani ya Sharia visivyo na tofauti kwa Muislamu yeyote huitwa makubaliano ya Wanachuoni, nayo ni maswala yasiyokubali kuleta jitihada, na wakati huo huo huitwa ni Uislamu, na amri si ya lazima moja kwa moja bali inaweza kukunjuliwa ili kuchunga masilahi ya mwanadamu na kufanya ufunuo – Qur`ani na Sunna – ni amri moja kwa moja na amri ya kudhaniwa, hivyo Qur`ani yote ni ya amri za moja kwa moja zilizothibiti na baadhi yake ni zenye maana ya kidhana, kwa upande wa Sunna baadhi yake ni amri ya moja kwa moja na zingine ni kidhana kwa mujibu wa ufafanuzi wake katika elimu ya Kiislamu ( ).
Katika alama za ukati na kati katika hili ni kuwa eneo hili linakubali kuleta hoja na kujibu ikiwa ni kufanyia kazi ulazima wa jitihada ambayo mwenye kufanya jitihada atakuta mlango mpana pamoja na uwepo wa mabadiliko ya mambo ya kudhaniwa, hii ni kwa upande wa vyanzo.
Ama kwa upande wa watu pamoja na kuchunga kuwa kuzuiliwa kufanya makosa hakuna kwa zaidi ya Manabii na kwa mujibu wa Tawheed katika Uislamu ambapo hakuna mwandamu yeyote anachukuwa sehemu ya Mungu na wala hakuna miongoni mwao yeyote mwenye kustahiki jina la marejeleo isipokuwa kwa kiwango wanachohifadhi kwenye vyanzo vyetu fikra zetu alama zetu na wanafanya jitihada na wanapatia kisha kuna ishara mbili:
Ishara ya Kwanza: Ni kuwa hakuna zama katika zama au kundi lenye sifa ya kuwa marejeleo kama mfano wa zama za waja wema waliopita, na hawa hawakuwa hoja wao wenyewe isipokuwa ni kwa kile kiwango walichofaulu katika utekelezaji wa kurudi kwenye vyanzo vikuu Qu`rani na Sunna na kufanya vizuri kwenye jitihada pamoja na kupanua katika kufungua sababu zenye kufikia makusudio ya Sharia na kuzuia sababu zitakazo leta madhara.
Ishara ya Pili: Ni kuwa uelewa wa marejeleo unafungamana zaidi na uelewa wa watu wa elimu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafanya:
{Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} [AN NAHL 43] watu waliopewa ufumbuzi wa kusimamia waja kwenye masilahi ya mustakabali wao na maisha yao.
Marejeleo na Mfumo wa Uelewa:
Ufahamu wa marejeleo unafungamana sana na mfumo wa makusudio ya Sharia ambapo utakuta fahamu zote mbili zinakwenda sawa kama mwenendo wa maji.
Kulinda marejeleo au vyanzo inakusanya pamoja na kulinda dini kulinda umma na kulinda ustaarabu maalumu, na hayo ni matakwa ya kibinadamu si ya Kiislamu tu, kisha kulinda marejeleo ni kulinda vinasaba vya maarifa kuchanganyika kisha kuyayuka asili yetu kwa wenzetu.
Ikiwa mfungamano kati ya marejeleo na makusudio ni mkubwa kwa kiwango hiki hivyo marejeleo yanafungamana njia ambazo lazima zichukuliwe ili kulinda marejeleo, na huongezeka umuhimu wa kuchukuwa njia muhimu hasa zile zenye kuhudumia misingi mikuu ya umma kisha zinafuata kwa hatua vipaombele vya njia hizi na kufikia kiwando cha mjenga hoja kisha mboreshaji sawa na kiwango cha njia hizi kuleta maslahi ya mtu na jamii au kuzuia uharibifu wa mtu na jamii.
Miongoni mwa njia muhimu ni pamoja na kutengeneza katiba sheria za kimarejeleo kwa misingi yetu na uelewa wetu na mifumo yetu mikuu ( ) na kuchunga taasisi za kimarejeleo zilizo lazima kuwepo na kufanya kazi ili kuchunga marejeleo yetu kwa upande wa usimamizi shirikishi kwa upande wake wa kinadharia au kuzungumziwa au kuenea ( ).
Kama vile marejeleo hulinda asili yetu hivyo ni lazima taasisi zenye kulinda marejeleo na kuyasimamia kusimamiwa na watu wenye utambuzi na hoja ya kimaarifa.
Katika ufahamu wenye mfungamano mkubwa zaidi na ufahamu wetu ni ufahamu na maana ya malezi kwani yenyewe ni njia ya kukusudiwa katika jumla ya mfumo wa lazima wa kulinda marejeleo kwani mti unaotunzwa hauleti matunda yake isipokuwa ni baada ya kurudiwa mara kwa mara, na subira ya mtunzaji ni subira ya mwenye kutegemea matunda yake kwa muda mrefu kwani mwenye kufanya haraka ya kitu kabla ya wakati wake basi ataadhibiwa kwa kukikosa.
Hivyo ni lazima pande za kimalezi ya kimaarifa kukutana kwa ukaribu na upande mwingine maarifa ya kimalezi na kuimarisha mizizi ya kimarejeleo ndani ya nafsi za umma kwa wote wadogo na wakubwa na hasa kwa watoto wadogo kwa nafasi kubwa kwenye haya malezi kisha mmea huu humwagiwa maji na kutibiwa maradhi yake, na miongoni mwa malezi ni mafunzo endelevu na uelewa wake pamoja na njia zake hivyo hatutakuwa mbali pindi tukisema kuwa kuheshimu marejeleo yetu na ishara zetu pamoja na taasisi zetu ni kutukuza ishara za Mwenyezi Mungu: {Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo} [AL HAJ 42] na katika muundo huu jitihada hutoa mafunzo ya kufikiri kiuchambuzi kiubunifu na kimkakati vinavyotumikia marejeleo na yale yanayozunguka na kukwamisha utukuzo na heshima kwa watabiri na makuhani.
Vile vile maana ya ulinganiaji inafungamana na maana yetu kwa mfungamano wa roho na mwili, kwani mwenye kulinda marejeleo anapaswa kuyafanya ndio mnara wa kujilinda na kuondolea mambo yenye kuleta shaka yanayoletwa na watu wenye kujenga shaka shaka.
Bila ya kuchukuwa njia za kulinda marejeleo basi uhalisia utazalisha maradhi ya kimarejeleo na kupatwa mwili wa umma wa kiustaarabu, hivyo bila ya uelewa mzuri wa marejeleo kundi kwenye umma litafikwa na kile kinachoweza kuitwa Udanganyifu wa Kimarejeleo hivyo umma kuletewa marejeleo yaliyo katika nasaba kwetu ya ajabu na asili yetu ya maarifa ya kiustaarabu.
Bila ya kuchukuwa juhudi za kuboresha upya marejeleo na njia zake basi umma utafikwa na hali ya Kuliwa Kimarejeleo ambapo hakuna shaka kutachangia kuleta hali ya udhaifu kwa mashahidi ya ustaarabu au Kupuuzwa Marejeleo asili na kusambaa marejeleo machache ambayo yanasifika kuwa ni mageni na ya ajabu, na huenda yakaelezewa kuwa yenyewe yameng’olewa hayana maamuzi na huenda yakafikia kuwa yenyewe malisho ya walinganiaji ambapo ndani ya umma wetu yakawa hayana nasaba.
Imekuwa wazi – kwa yale ninayoyazingatia – kuwa maana na uelewa huu ni tawi katika mti wa uelewa wetu linapanua uelewa na kuimarisha pamoja na kuulisha wala halijitengi nao bali huudhihirisha na kuuweka wazi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas