Kwa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu Al...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu Aliahidi Kulipa Kisasi kwa Ami yake Hamza?

Question

Matni ya shaka:
Hamza Ami yake Mtume S.A.W. alipouwawa katika vita vya Uhud, Mtume alikasirika sana na akaapa kulipa kisasi kwa kuwaua Maqurysh sabinii kwa kumlipizia.
Na sisi tunauliza: Vipi inakuwa kwa anayeazimia kulipa kisasi kwa maadui awe Mtume? Na je, kulipa kiasasi ni katika tabia za mitume?
 

Answer

Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mtume S.A.W. aliahidi kuwaua waliomwua Hamza hasa wale waliomchezea na kupasua tumbo na kukata pua yake na sikio na wakatoa ini lake, Mtume alisikitika sana mpaka akalia kwa sauti, na akasema: “ Sitopatwa na msiba mkubwa kama msiba wako”
Kati ya ghadhabu na athari zake:
Kunatakikana mtu atofautishe kati ya ghadhabu ya kimaumbile ambayo mtu hawezi kuepukana nayo hata awe Mtume, na ghadhabu zinampelekea mtu kutoka katika misingi ya kitabia, ama ghadhabu za kawaida hili ni jambo la kawaida mwanadamu hawezi kuepukana nalo, awe atakavyokuwa hata Mitume, mwanadamu yeyote ana tabia na maumbile na mihemko ambayo Mwenyezi Mungu Amemwekea, na Mwenyezi Mungu Akafanya kurekebisha kwake kwa kuwajibishia ulazima wa kutenda na kulipwa kwa thawabu au adhabu, ama ghadhabu zinazomtoa mtu katika hali ya kawaida na kupelekea kutoka katika misingi ya kitabia iliyo sawa, hili kwa Mtume S.A.W. ni jambo la kawaida halivunji cheo chake, wala halipunguzi subira yake.
Na kuepushwa na mabaya (Isma) haina maana kwamba wao hawapatwi na matukio ya kibinadamu, vipi iwe hivyo na hali Mwenyezi Mungu Amewafanya kuwa viongozi wa muongozo tunaoufuata kwao katika yale yanayotushukia katika hali za kibinadamu, bali maana yake ni kwamba Mtume kikimpata chochote katika mambo ya kibinadamu, hakipelekei kufanya jambo baya.
Litakapothibitika hili inafaa kwa kwa mtu kufuata – mfano- wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. na kama mtu atashindwa kuzuia hasira zake wakati wa huzuni au ghadhabu kwa kutofuata ghadhabu zake na kutotekeleza aliyoazimia wakati wa huzuni akiono kwamba yanaweza kuleta madhara.
Maelekezo ya Kiungu:
Baada ya kushuka Aya ikambainikia Mtume S.A.W. kulipa kisasi kwa kilekile wala asizidishe akasema: tunasubiri wala hatuadhibu, ndio alifikwa na huzuni kubwa kwa alichokiona miili ya watu wake akiwemo Ami yake, akishuka Aya inayoelekeza kuwa adhabu yawe kwa kiwango cha kosa: {Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa} [AN NAHL: 126].
Kisha ananyanyua katika dara za miamala kwa kiwango cha juu, akasema: {Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri}katika Aya hii kuna kuchagua kati ya kisasi na kusubiri, kisha ikahamia katika jambo la subira lakini kuhama huku kukali na nafsi ya kibinadamu inahitaji msaada wa kiungu, akasema: {Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya Mwenyezi Mungu tu} [AN NAHL: 127].

 

Share this:

Related Fatwas