Miujiza ya Kuteremka Meza Kutoka Mb...

Egypt's Dar Al-Ifta

Miujiza ya Kuteremka Meza Kutoka Mbinguni Juu ya Marafiki wa Isa

Question

Matini ya shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe miongoni mwa wanao shuhudia. Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ilikiwe Siku kuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku. Mwenyezi Mungu akasema: Hakika Mimi nitakuteremshieni hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakaye kanya baadae, basi hakika Mimi nitampa adhabu nisiyopata kumpa yeyote katika walimwengu}. [AL MAIDAHA 112-115]
 

Answer

Na hii ambayo imetajwa na Qur'ani Tukufu kuhusu suala la kuteremka kwa meza ya chakula kutoka mbinguni kwamba ni jambo ambalo halijawahi kutokea, lakini kisa cha Meza ya chakula kimo ndani ya Qur'ani kimeanza kwa kutofahamu vyema baadhi ya Aya za Injili, kwani Injili haisemi kuwa wanafunzi wa Isa A.S, walitaka alama kutoka mbinguni, wala haisemi ya kwamba meza ya chakula iliteremka kutoka mbinguni, lakini waliomfuata Isa A.S, ili wasikie mafunzo mwituni waliishi naye kwa muda mrefu na Isa A.S, hakutaka kuwaacha waondoke hali ya kuwa wana njaa ili wasije kupotea (kuchoka) njiani basi akachukua mikate mitano na samaki wawili kisha akavibariki vyakula hivyo na akagawa kisha akawalisha wote na kikazidi kwa walaji kumi na mbili tu. [Matta 26: 20-29, Morqas 14: 17-25, Loqa 22: 14-30, Yohana 13: 1-30]
Kujibu shaka:
Kituo cha Tafiti za Kisheria katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ikiwa tutakubali ya kwamba kisa hiki hakikutajwa katika vitabu vitakatifu – kama wasemavyo wao – basi hii sio dalili ya kutosha ya kutotokea kwake; kwa kuwa kutotaja hakumaanishi kutotokea, na Yohana amesema wazi katika Injili yake, kwamba: Hakika Alama ambazo alizifanya Isa A.S, ni nyingi na kama zote zingeandikwa basi ulimwengu wa vitabu usingetosha, na hii ni dalili ya wingi wake, baadhi ya waandishi wa hizi Injili nne zinazotegemewa, wameandika yale ambayo hayakuandikwa na wengine. [Kitabu cha: Tafsiri Al Manar 216/7]
Pia inajuzu kuwa habari ya kisa hicho imetajwa katika baadhi ya Injili ambazo zimekataliwa na Kanisa na hazikuzingatiwa, halafu kisa hicho kilipotewa baada ya hayo. [Kitabu cha: Tafsiri Al Manar 216/7]
Au huwenda ukawa umeandikwa lakini umetajwa kwa njia ya istiara na hawakuweza kuitambua maana, na kinaweza kuwa kisa cha chakula cha mlo wa usiku kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu uliotajwa kwenye vitabu vyao. Na watu wa Injili wameweka wazi kwamba maneno mengi ya Mtume Isa A.S, yalikuwa mifano na alama na wanakihesabia kila kilichokuja kuhusu chakula na kinywaji katika ufalme wa Mwenyezi Mungu kuwa ni katika hizo alama.
Na vilevile baadhi ya Maandiko yanayohusu vyakula na vinywaji duniani nini kinachotujulisha kwamba wao waliashiria kisa hiki kwa baadhi ya usomaji kwa Mujibu wa ufahamu wao na Itikadi yao kwani walikuwa wakinukulu hayo kwa maana yake kisha yakanukuliwa kutoka kwao kwa kufasiliwa na mzizi wake ulishapotezwa na uhakika wake haujulikani [Kitabu cha: Tafsiri Al Manar 216/7]
Ama kauli ya kwamba aliyeomba ilikuwa ni alama kutoka mbinguni na wala haikuwa meza ya chakula kutoka mbinguni, tunasema: hakika hiyo Aya ni Meza ya chakula, na hakuna ukinzani wowote, na hii inaafikiana na yaliyokuja katika Injili ya Yohana: wakamwambia ni alama gani utaileta; tuione ili tukuamini? Utafanya nini? Wazee wetu walikula Manna katika Mwituni kama ilivyoandikwa: kwamba yeye aliwapatia mkate kutoka mbinguni waule. [Yohana 6: 30-31]
Na kauli yao: baba zetu walikula Manna katika nchi, wakitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu awateremshie meza ya chakula kutoka mbinguni ili wale kama walivyokula baba zao, na kauli yake: Hakika yeye aliwapatia mkate kutoka mbinguni ni dalili kwamba wao kweli walitaka meza ya chakula.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas