Nabii wa Mwenyezi Mungu Hud na Watu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Nabii wa Mwenyezi Mungu Hud na Watu Wake Walirudi

Question

Matini ya Tuhuma:
Imetajwa katika Qur’ani Tukufu kwamba: {Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni wazushi tu} Mpaka kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi! Hakika kina A'adi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina A'adi, kaumu ya Hud.} [HUD: 50:60]
 

Answer

Vile vile Mwenyezi Mungu alisema: {Na kwa A'adi tulimpeleka ndugu yao, Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?} Mpaka kauli yake Mwenyezi Mungu: {Basi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mizizi ya wale walio zikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.} [AL A'RAAF: 65:72].
Na ikatajwa katika tafsiri yake: kwamba Hud ni mtoto wa Abdullah Ibn Rabah Ibn Al Khulud Ibn Aad Ibn Aws Ibn Iram Ibn Sam Ibn Nuh, na ikasemwa: Yeye ni Hud Ibn Shalah Ibn Arfakhshad Ibn Sam Ibn Nuh Ibn ami yake ndugu wa Aad. Na watu wa kabila la Adi walikuwa wakiabudu masanamu, basi Mwenyezi Mungu akawaletea Mtume wake Hud, lakini wakamkadhibisha na wakawa wakali zaidi, basi Mwenyezi Mungu akawawekea mvua kwa muda wa miaka mitatu mpaka wakafanya juhudi, ndipo Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa upepo wa kukata uzazi. Hud na Waumini walio pamoja naye wakaokoka, wakafika Makka na wakamwabudu Mwenyezi Mungu mpaka kufa.
Lakini katika Taurati kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu Hud pamoja na kaumu yake Aad hakikutajwa, na wala haikutajwa katika Taurati pia kuwa Hud alikuwepo baina ya Nuh na Ibrahim, na haikutajwa kuwa mmoja wa kizazi cha Nuhu ni mtu ambaye alikuwa jina lake ni Aad, na haikutajwa adhabu ya kukatika kwa mvua kwa muda wa miaka mitatu isipokuwa katika siku za Nabii Eliya.
Jibu la Tuhuma:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hizi zinataja kisa cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Hud, (A.S), na watu wake, na mwito wake kwao kwenye tauhidi, na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ahadi ya kwamba Mwenyezi Mungu atawapa malipo ya hayo kwa uwezo unaozidisha nguvu zao walizojipambanua nazo, na kukadhibisha kwake na kumshitaki, na mwisho wa hali baina yao kwa kauli kwamba amewafikishia ujumbe wa Mwenyezi Mungu alioutumwa nao. Na kwamba Sunna ya Mwenyezi Mungu ni kuwaangamiza wanaokadhibisha, na wokovu wa Hud na walioamini pamoja naye.
Ama kusema kwao kwamba Hadithi ya Hud na watu wake Aad haikutajwa katika Taurati, na kusema kwao: Hakuna Nabii katika Taurati baina ya Nuhu na Ibrahim, tunasema: Hiki si kitu pekee kisichotajwa katika Taurati. Kuna hadithi ambazo ni makhsusi katika dini yao pia hazikutajwa katika Taurati, kama vile kisa cha Zakaria kumfadhili Maryam, maneno ya Isa akiwa kitandani, na kuumba kwake ndege kutoka kwa udongo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kumpulizia kwake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na mengine mengi, wakati ambapo kutotaja Taurati kwa hadithi ya Hud sio dalili kwamba hadithi hii haijathibitishwa.
Ama kwamba hakuna nabii katika Taurati baina ya Nuhu na Ibrahim, jambo hili linashangaza. Na tunawaambia: Ikiwa mliyoyasema ni kweli, basi wako wapi Manabii wa Mwenyezi Mungu walio katika dhuria wa Nuhu?
Ama kwamba Taurati haikumtaja mtu mmoja aitwaye Aad katika kizazi cha Nuhu, basi hili ni jambo la ajabu. Je, inatakiwa kwa ajili ya kuthibitisha kuwepo kwa mwanadamu ni lazima kutajwa kwake katika Taurati? Wapi? Basi, walioishi katika kipindi hiki cha Taurati? Je, Taurati ilikuwa ni kumbukumbu iliyohesabu majina yote ya watu walioishi kabla ya kuteremshwa?!
Ama kwamba Taurati haikutaja adhabu ya kukatika kwa mvua kwa muda wa miaka mitatu isipokuwa katika zama za Nabii Eliya - basi tukichukulia kuwa haya ni kweli – tunasema kuwa: Qur'ani haikusema kuwa mvua ilikatika miaka mitatu kabla ya kunyesha kwa watu wa Hud. Bali ni ijtihadi ya baadhi ya wafasiri, na baadhi yao walijishughulisha na kukusanya kila kilichosemwa juu ya Aya hiyo, kwa hiyo hii ni miongoni mwa maneno ambayo baadhi ya wanavyuoni wa tafsiri wanayaeleza.

 


 

Share this:

Related Fatwas