Mtoto wa Nabii Nuhu A.S.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtoto wa Nabii Nuhu A.S.

Question

 Mtoto wa Nabii Nuhu A.S. 

Answer

Swali:
Ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu imekuja: {Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamuita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri * Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama} [HUUD: 42, 43].
Kisa hiki hakifahamiki ndani ya Vitabu Vitakatifu, hivyo kitakuwa ni tofauti, mtoto wa Nabii Nuhu anayekusudiwa ndani ya Aya ni Kanaan – kama walivyosema Wafasiri – na Nabii Nuhu alikuwa na watoto watatu ambao ni: Sam. Haam na Yaafath, na wenyewe walioa wanawake watatu, hivyo waliokoka pamoja naye ni wanane, sasa kisa cha kuangamia Kanaan kipo wapi? – ambaye anatajwa kuwa ni mtoto wa Nabii Nuhu – na inafahamika kuwa Kanaan hakuwa ameshazaliwa, na Kanaan hakuwa mtoto wa Nabii Nuhu bali ni mtoto wa Haam ambaye ni mtoto wa Nabii Nuhu, naye Kanaan alizaliwa baada ya tukio la tofani.

Jibu la Swali:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Qur`ani Tukufu haikuelezea haiba ya huyu mtoto wala haikutaja jina lake wala jina la mama yake wala kitu chochote tofauti na ilivyotaja, kusudio la Qur`ani Tukufu kuelezea visa vya Manabii na waja wema ni kubainisha mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwao ikiwa ni pamoja na uwepo wa masilahi ambayo hayana mwisho, ama matukio ya kihistoria na udhibiti wa kutokea kwake muda wake uwezekano wake si katika makusudio ya Qur`ani.
Wafasiri wamefanya utafiti kuhusu jina la huyu mtoto na jina la mama yake, kuhusu kisa chake tegemeo lao ni mapokezi ya kihistoria, kama vile baadhi yao wanakusudia katika kukielezea kukusanya kila kilichotajwa, hivyo maelezo ya Wafasiri sio hoja ya Qur`ani bali ni jitihada zao ili kufikia kwenye kusudio la Qur`ani Tukufu, ikiwa watafikia basi Mwenyezi Mungu wa kushukuriwa kwani wana malipo ya aina mbili, na ikiwa hawatafikia basi wana malipo ya aina moja, mjadala wa maelezo kukubalika na kutokubalika yanaegemeshwa kwenye kilichoelezewa na Wafasiri pasi na kuelekezwa kwenye Aya ya Qur`ani.
Pili: Hakuna kizuizi cha huyu Kanaan – ambaye ametajwa na Wafasiri wa Aya – kuwa si Kanaan ambaye amemtaja muulizaji naye ni Ibn Haam, wanatafsiri wa zama za hivi sasa wameelezea kwa kina kuhusu Aya hii, lau muulizaji atarejea maelezo hayo basi asingekuwa na shaka kwenye kuifahamu Aya Tukufu. Wasomi wa Tafsiri wamesema: Mtoto huyu wa Nabii Nuhu ni mtoto wake wanne kutoka kwa mke wake wa pili ambaye alikuwa anaitwa Waailah alizama huyu mama na ametajwa mwishoni mwa Suratul-Tahriim, na ikasemwa: Jina la mtoto wake lilikuwa ni “Yamma”, na ikasemwa tena: Jina lake ni “Kanaan” naye sio Kanaan Ibn Haam babu wa watu wa Kanaan, kwa upande mwingine Taurati iliyopo hivi sasa haikutaja huyu mtoto na kadhia ya kuzama, je Nabii Nuhu alikuwa na mke au hana mke?( ).


*****


 

Share this:

Related Fatwas