Watoto wa tube/bomba
Question
Je, inaruhusiwa kuzaa kupitia watoto wa bomba?
Answer
Kuzaa kwa kuweka vichevushaji/virutubisho vya mume na mke nje ya mfuko wa uzazi, kisha kuvirejesha kwenye tumbo la uzazi la mke, hakuna pingamizi la kisheria juu yake ikiwa yai limetoka kwa mke na manii ni kutoka kwa mumewe, na utungishaji mimba hufanyika nje ya tumbo la uzazi la mke kupitia mirija, na yai lililorutubishwa hurudishwa kwenye tumbo la uzazi la mke huyo, bila kubadilishwa au kuchanganyika na maji ya uzazi ya mtu mwingine au yai la mwanamke mwingine, na kuna hitaji la matibabu kwa hili; hii lazima ifanyike na daktari maalumu.