Uzushi wa Qur`ani Kisa cha Ibrahim...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uzushi wa Qur`ani Kisa cha Ibrahim na Namrud

Question

 Uzushi wa Qur`ani Kisa cha Ibrahim na Namrud 

Answer

  Matni yenye shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mola: {Hukumuona yule aliye hojiana na Ibrahim kuhusu Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua Mashariki, basi wewe lichomozeshe Magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu} [AL BAQARAH: 258].
Imekuja katika tafsiri ya Aya hii kuwa maana ya Aya ni kushangazwa na hoja za Namrud na ujinga wake.
Hapa Qur`ani imekwenda kinyume na maelezo ya kihistoria yanayofahamika, na imekwenda kinyume na yaliyokuja ndani ya Vitabu Vitakatifu kwa sababu Namrud alimtangulia Nabii Ibrahim kwa miaka mia tatu hivyo ni vipi yalitokea mahojiano haya?
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hii Tukufu imekuja kama dalili na mfano wa Aya iliyoitangulia ambayo ndani yake kuna kauli ya Mola: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashetani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani} [AL BAQARAH: 257].
Mwenyezi Mungu akaja na simulizi ambayo haikuwepo kwa Nabii wake Ibrahim Amani ya Mungu iwe kwake pindi alipogombana na huyu mtu mwovu kwa Mwenyezi Mungu na ilikuwa muhimu kwake pamoja na kupewa na Mwenyezi Mungu ufalme kutofanya hilo.
Qur`ani Tukufu imetaja jina lake kwa sababu Qur`ani katika visa inaangalia madhumuni ya mahojiano au hoja yenyewe na mazingatio yake, kutajwa jina la mfalme hakutangulizi wala kuchelewesha katika madhumuni na mazingatio.
Ama kutajwa kuwa jina lake ni Namrud hao ni baadhi ya Wanachuoni wa tafsiri na baadhi yao mfumo wao ni kukusanya kila kilichosemwa katika maana ya Aya, wanataja mitazamo yote, na wanataja kabla ya kusema neno: “Imesemekana” neno ambalo linaonesha na kumaanisha udhaifu, na walichokifanya katika kutaja majina ambayo Mwenyezi Mungu hakuwataja kwa majina yao ni jitihada zao tu ikiwa wamepatia basi wana malipo ya aina mbili, na ikiwa hawajapatia wana malipo ya aina moja.
Ama kauli kuwa Namrud alimtangulia Nabii Ibrahim kwa miaka mia tatu, katika historia iliyohakikiwa na kupitishwa hakuna yanayothibitisha au kukanusha kuwa jina la mfalme ambaye alifanya mahojiano na Nabii Ibrahim kuhusu Mola wake ni huyu Namrud bali hicho ni kisa cha kihistoria kinahitaji utafiti zaidi.
Mwisho kabisa: Ikiwa ni sahihi yaliyosemwa kuhusu Namrud kuwa zama zake zilitangulia zama za Nabii Ibrahim Amani ya Mungu iwe kwake kwa miaka mingi, inaweza kuwa ni kwa upande wa kujirudia majina, wala hakuna kinachozuia kujirudia jina kwa mfalme zaidi ya mmoja kwa zama na historia mbalimbali.

 

Share this:

Related Fatwas