Hatua na njia sahihi ambazo tukizifuata tutamaliza au kutokomeza fikra za Khawariji katika jamii zatu
Question
Ni zipi hatua na njia sahihi ambazo tukizifuata tutamaliza au kutokomeza fikra za Khawariji katika jamii zatu?
Answer
Fikra za Kikhawariji zinaangamiza jamii; kwa sababu zinaharaibu ustaarabu na maendeleo na zinasababisha dhiki na uharibifu, ni fikra haribifu zinazopingana na ufahamu sahihi wa Qurani na Hadithi, hapana budi kufuata Minhaji ya urekebishaji sahihi ya ukati na kati, ili kupambana na uharibifu wa fikra na Uhalifu wa Khawariji, na njia hii ipo katika kulingania Mwenyezi Mungu kwa Hekima na mawaidha mazuri, na kusambaza misingi ya ukati na kati, ustahamala na kuishi kwa pamoja, pia katika kusimamia wajibu wa kubainisha na kurekebisha dhana na fikra za kimakosa, sawasawa kwa wafuasi wa kundi hili au waliowahadaa, na kufanya kazi ya kuujenga vizuri ufahamu wa mwanadamu unaoendana na Minhaj ya kielimu yenye nguvu mbali na uzushi, pia njia hii inapatikana katika mchango wa nchi katika mpango wake wa tamaa ya maendeleo; kwa sababu Uduni wa maendeleo, ujenzi, kusambaa kwa maradhi katika jamii na ukosefu wa ajira ni kutokana na kusambaa fikra potofu, na mwishowe kupelekea kushika silaha na kuua watu wasio na hatia, hakuna dawa isipokuwa kufuata katiba na sheria kwa kutumia vyombo vinavyohusika na jeshi bora Duniani “Wamisri”.