Upigaji picha

Egypt's Dar Al-Ifta

Upigaji picha

Question

Upigaji picha

Answer

Jengo la sharia ya Kiislamu limejengwa juu ya msingi wa kuondoa aibu na kurahisisha ibada, na Mujtahidi ndiye anayezingatia kwa makini, kutafiti, kuchunguza, kutafakari na kusawazisha mambo - baada ya kutimiza zana za Ijtihadi - Ijtihadi na kufanya upya mambo hayo hayamaanishi mwelekeo wa kuharamisha kwa ajili ya matukio tu, na kauli ni kwa uhalali wakati hakuna matini iliyokataza ni muhimu zaidi kuliko kauli ya kukataza au kuharimisha; Kwa sababu asili ya mambo ni halali.

Kuna mitazamo mingi kuhusu hukumu ya picha, wako wanaosema kuwa ni halali na wale wanaosema kuwa ni haramu. Mtazamo sahihi ni kwamba hukumu ya upigaji picha wa kisasa iwe inajuzu au haramu haitokani na ukweli kwamba inaitwa upigaji picha, lakini badala yake inafuata  kuelewa ukweli wake kwanza; kuhukumu jambo ni sehemu ya utambuzi wake.

Huu ni utafiti kuhusu suala hilo na kuunga mkono kauli ya kuliruhusiwa, pamoja na uwasilishaji wa maoni ya wale wanaosema kuwa ni haramu, na kujadili hivyo kwa mbinu ya kielimu, kama inavyotakiwa na maadili ya utafiti.

Maana ya upigaji picha na picha katika lugha na matini za kisharia

Kwanza: Maana ya upigaji picha na picha katika lugha:

Swahib Taj Al-Arus alisema: “Picha ni umbo, ukweli, na sifa”.

Kisha akasema: “Picha hiyo imetumika kwa maana ya umbo na sifa, na kutoka maana hii hii kuna Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W) : Mola wangu Mlezi alinijia usiku huu kwa umbo bora kabisa”.

Kisha akasema: “Mkusanyaji – akimaanisha Al-Fayrouzabadi, mtunzi wa kamusi – amesema katika Al-Basaa’ir: Picha ni hutofautisha nayo na vingine, nayo ni aina mbili:

aina inayoonekana ambayo watu binafsi na umma huona, kama vile picha ya binadamu, farasi na punda.

Ya pili: Inapatana na akili na kutambulika kwa umaalumu na sio kwa ujumla, kama vile picha ambayo ni ya kipekee kwa mwanadamu kutokana na akili, maono, na maana anazotofautishwa nazo. Mwenyezi Mungu akaashiria picha mbili hizo kwa kusema: {Na akakutieni sura, na akazifanya nzuri sura zenu} [Ghafir: 64] {Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga} [Al-Infitar: 8] {Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo} [Al-Imran:6] Na kauli yake Mtume (S.A.W): “Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu kwa umbo lake”. Alikusudia kwa hayo Aliyomhusishia mwanadamu katika umbo linaloonekana kwa macho, na kwa hilo Mwenyezi Mungu alimtukuza  zaidi ya viumbe vyake vingi.

Kisha akasema: “Na sura ni: uso, na kutokana na  maana  hii ni Hadithi ya Ibn Muqrin: “Je, hukujua kwamba sura hiyo ni haramu”, na kinachokusudiwa ni kumzuia mtu asipigwe kofi usoni, na Hadithi nyingine isemayo: “Inachukiza kujua picha” yaani, kuweka pasi au alama kwenye uso. Vile vile ina maana ya niliwazia sura yake. Na picha maana yake pia ni: sanamu.

Al-Fayoumi amesema katika Al-Misbah Al-Munir: “(Picha) ni: sanamu:, na wingi wake ni picha pia, kama vile: nyumba katika umoja na nyumba ni wingi, niliona jambo hilo, yaani nilifikiri sura na umbo lake akilini. Umbo hilo linaweza kutumika kumaanisha sifa, kama wanavyosema: umbo la jambo ni hivi na hivi, yaani, sifa yake ni hivi, na kutoka maana hii wanasema: sura ya jambo fulani ni hivi na hivi. yaani: sifa yake ni hivi.

Picha hiyo inaitwa umbo la kitu, uhalisia wake, sifa yake, na aina yake, na inaitwa: uso, na inaitwa: umbo na sifa ambayo mtu anafikiria juu ya kitu ndani ya akili yake, kama inaitwa: sanamu.

Upigaji picha: Ni kutoa kitu umbo lake, sura yake, sifa yake, na aina yake.

Pili: Maana ya upigaji picha na picha katika matini za Kiislamu:

Maana ya upigaji picha na picha katika Qur’ani:

1- Mwenyezi Mungu anasema: {Yeye ndiye anayekuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo} [Al-Imran:6]

Imamu Al-Razi amesema: “Ama kauli yake: {Yeye ndiye anayekuundeni} [Al-Imran: 6] Al-Wahidi amesema: Kupiga picha ni kufanya kitu katika umbo, na umbo ni: umbo lililopatikana kwa kitu wakati wa kutunga baina ya sehemu zake.

 Mwanachuoni Al-Alusi anasema: “Kupiga picha ni: kuweka kitu katika umbo ambalo hakikuwa juu yake, na sura ni: umbo ambalo ndani yake kitu kinaundwa kwa utunzi.

2- Mwenyezi Mungu anasema: {Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura} [Al-A’raf: 11].

Mwanachuoni Al-Tahir bin Ashour alisema: “Kupiga picha maana yake ni: kukifanya kitu kuwa sura, na sura maana yake ni: umbo ambalo mwili umeumbwa kwake, kama vile udongo pia huundwa kwa namna fulani.

3- Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura} [Al-Hashir: 24].

Imamu Al-Qurtubi amesema: “Na mpiga picha: mpiga picha na mjumuiko wa picha katika maumbo tofauti, hivyo kupiga picha hupangwa kwa mujibu wa uumbaji na huufuata. Maana ya upigaji picha ni: kupanga na kutengeneza sura, na Mwenyezi Mungu akamuumba mwanadamu katika matumbo ya mama kwa njia tatu: Akamfanyia pande la damu, kisha donge, kisha akamfanyia sura, na ni umbile ambalo ndani yake ana sura. sura hivyo ambayo kwayo anajulikana na kutofautishwa na wengine kwa tabia yake, basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

Inaweza kufupishwa kutokana na hayo yaliyotangulia kwamba upigaji picha katika Qur'ani Tukufu ulitajwa kwa maana: kukifanya kitu kuwa na sura, na kwa maana ya upangaji na uundaji ambao kitu kina sura na umbo ambalo kwayo kitu kinatofautishwa na vengine. Na picha ilitajwa kwa maana: umbo ambalo kitu hupata kwake wakati wa kuunga baina ya sehemu zake, au umbo ambalo mwili umeundwa, au umbo ambalo kitu kinajulikana nacho na kutofautishwa na vingine.

Maana ya upigaji picha na picha katika Sunna:

1- Imepokewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Abu Talha, (R.A), amesema: Mtume (S.A.W) amesema: “Malaika hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha”.

Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalani alisema katika Fath Al-Bari: “Al-Khattabi amesema: Malaika hawaingii ndani yake nyumba ambayo ndani yake ipo picha inayoharamishwa kumilikiwa, ambayo ni moja ya picha ambazo ndani yake nafsi ambayo haijakatwa kichwa, au haijadhalilishwa”.

Katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Dawood kwa upokezi wake: “Malaika hawaingii nyumba ndani yake kuna mbwa au picha au mwenye janaba”.

Mwanachuoni Al-Saharanafuri amesema kuhusu kufanya Ijtihadi katika kuifafanua Hadithi ile: “Maana ya picha: ni sura ya mnyama ikiwa imetundikwa ukutani, au kwenye nguo iliyovaliwa, au kwenye kilemba, na kadhalika, miongoni mwa mambo ambayo hayadhalilishwi, tofauti na kile kilicho katika zulia lililokanyagwa, au mto, au kitu kama hicho kinachodhalilishwa, basi Malaika hawazuiliwi kuingia”.

2- Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas, (R.A), kwa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) alisema: “Mwenye kutengeneza picha anaadhibiwa na atalazimishwa kuzipulizia roho naye si mwenye kupuliza humo abadan”

Ibn Hajar amesema: “Hadithi hii ni dalili ya kwamba inajuzu kupiga picha isiyo na roho kama vile miti, au jua, au miezi. Abu Muhammad Al-Juwayni alifikisha katazo hilo, kwa sababu baadhi ya makafiri walikuwa wakiviabudu vitu hivyo”.

Maana ya hili ni kwamba anaombwa kuzipulizia roho ndani ya picha yake, na amri hii ni kwa ajili ya kutoweza na kulaumiwa tu.

3- Picha hiyo imekuja na maana (sanamu) katika Hadithi ya Wahb Ibn Munabbih kutoka kwa Jabir kwamba Mtume, (S.A.W), alimuamuru Umar Ibn Al-Khattab, (R.A) wakati wa kufungua, alipokuwa kwenye mtaa wa Bathaa kutoka Makka, kuja kwenye Al-Kaaba na kufuta kila sura ndani yake, basi Mtume, (S.A.W), hakuingia humo mpaka ikafutika kila picha ndani yake.

Mwanachuoni Al-Saharanafuri alisema katika maelezo yake: “Yaani kila sanamu katika sura ya nabii au malaika, au mfano wa hayo, iliyochongwa ukutani au yenye mwili au kitu kingine ambacho kina roho. ”.

Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Aisha, (R.A) katika Sura ya “Kilichokanyagwa miononi mwa picha” kwamba alisema: “Niliifunika kwa nguo nyepesi, ndani yake kulikuwa na masanamu”.

Ibn Hajar alisema katika maelezo yake ya Hadithi: “Kauli yake: “kuna masanamu”: Na ndicho kitu kinachopigwa picha, nacho maana yake kwa ujumla zaidi kuliko kutiwa nakshi, au kuchongwa, au kupakwa rangi, au kusuka katika vazi. Na katika upokezi wa Bukair Ibn Al-Ashaj kutoka kwa Abdul Rahman Ibn Al-Qasim katika Muslim, Aisha, (R.A) aliweka nguo ambayo ndani yake kuna picha”.

4- Picha vile vile imetajwa kwa maana ya (uso) katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Umar kwamba alichukia sanamu hiyo ioneshwe, na Ibn Omar, (R.A.), akasema: Mtume (S.A.W.) amekataza kupigwa picha.

Katika Fath Al-Bari amesema: “Kinachomaanishwa na picha ni uso”.

5- Picha imetajwa kwa maana ya (Sifa) katika Hadithi ailiyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Abu Hurairah (R.A), kutoka kwa  Mtume (S.A.W.). alisema: “Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu kwa picha yake” Yaani kwa sifa zake.

Ibn Hajar amesema katika kitabu cha Fath Al-Bari: “Kulikuwa na tofauti ya rai juu ya kile kiwakilishi kinarejelea nini, ikasemwa: kinarejelea Adam, maana yake: Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kwa sifa ambazo aliendelea nazo, mpaka akashuka na mpaka alikufa, ili kuwaepusha na upotofu wa wale wanaodhania kuwa Adam alipokuwa Peponi, alikuwa kwa sifa tofauti.. Mpaka akasema: “Kinachokusudiwa na picha ni sifa, na maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba kwa mujibu wa sifa zake za elimu, maisha, kusikia, kuona na mambo mengine, hata kama sifa za Mwenyezi Mungu si kama hizo.”.

Na amesema katika kauli yake Mtume (S.A.W): “Kila atakayeingia Peponi atakuwa katika picha ya Adam”: “yaani atakuwa kwa sifa za Adam”.

6- Picha pia ilitajwa kwa maana ya mfano wa mwili uliochorwa kwenye kitambaa cha hariri.

Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy kutoka kwa Abu Mulaika kutoka kwa Bi. Aisha, (R.A) kwamba.: “Jibril alikuja kwa sura yake akiwa katika vazi la hariri ya kijani kibichi kwa Mtume (S.A.W) na akasema: huyo ni mke wako katika dunia na Akhera”.

Amesema katika Tuhfat Al-Ahwadhi: “Kauli yake: “Jibril alikuja” yaani: katika ndoto “katika sura yake” yaani: kwa sura ya Aisha, na katika Hadithi nyingine kutoka kwa Bi. Aisha (R.A) kwamba: (Jibril alishuka kwa sura yangu katika kiganja chake cha mkono, wakati Mtume (S.A.W.), alipoamrishwa kunioa.” Upokezi wa Al-Tirmidhiy na upokezi huu umeunganishwa na maana: kwamba sura yake Aisha ilikuwa kwenye kitambaa, na kitambaa hicho kilikuwa katika kiganja chake cha mkono.

Iliyokusudiwa kwa picha ni picha ya kitu chenye roho, iwe ni mtu mwenye kivuli, au mchongo, au rangi, au mfumo katika vazi, na kwamba kiko ndani ya matini zinazokataza hivyo maadamu ina sifa ambayo mtu aliye hai anaweza  kuishi nayo. Lakini ikikatwa kichwa cha picha hiyo au viungo vyake vimekatwa, kwa mfano, matini zinazokataza haziishughulikii picha ile.

Na inajuzu kuiweka picha hiyo ikiwa ni kwa njia ya kudharau, kama ikiwekwa juu ya mto au zulia linalokanyagwa, au ikitumika katika vyombo.

Picha hiyo ilitajwa kwa maana ya uso na maana ya sifa, umbo na mwili. Vile vile upigaji picha una: maana ya kupiga picha ya kitu fulani.

Hukumu ya Upigaji Picha

Upigaji picha wa kisasa au upigaji picha: ni sanaa ya kurekodi picha za kuona na kuzihifadhi kwa njia ya zana (Kamera) inayojulikana. Zana hii hurekodi watu, vitu, mahali na matukio, na kumwezesha mtu kuhifadhi alichokiona, kukiandika na kukifurahia kwa kuendelea, na kukirudishia wakati wowote anapotaka.

Kamera inafanana zaidi na jicho la bandia, na mfumo wake wa kupiga picha unafanana -kwa kiasi fulani- na mfumo wa kuona kwenye jicho. Zana huona vitu na kuhifadhi ilichoona ili kukuwezesha kukitazama wakati wowote unapotaka.

Kwa hivyo upigaji picha hauendi zaidi ya ile ya kufunga kinyume chake, kama kioo. Vitu huakisi mwanga wao kwenye kioo, kwa hiyo inaonesha kinyume cha umbo lake, hivyo ndivyo vinavyotokea kwenye kamera ambavyo ni kuakisi.

kuakisi au kinyume chake inamaanisha: kitu kilichosafishwa (kioo na kadhalika) hupokea mwanga unaoakisiwa juu yake kutoka kwa kitu kilicho kinyume chake, hali ambayo hufanya sura ya kitu kinaonekana juu yake. Kiwango cha uboreshaji na usafi wa kitu hiki cha kuakisi, ndivyo kinavyoeleza kwa usahihi zaidi umbo la kitu kilicho kando yake. Kamera ni kama kioo, hupokea mwanga unaooneshwa juu yake kutoka kwa vitu vilivyo kinyume chake kupitia lenzi yake ili kuanguka kwenye filamu, lakini athari za vitu vilivyooneshwa kwenye kioo hupotea haraka baada ya kugeuka kutokana na kukutana na vitu hivi, au vitu vinageuka kutoka kwao, ikiwa mmoja wa watu aligundua kitufe cha kubonyeza wakati wa kusimama mbele ya kioo ili kuhifadhi sura yake na kuifunga mahali pake na kuiacha, na picha hiyo ilipigwa kwenye kioo, wakati hakuna mtu aliyesema kwamba hali hii ni haramu, vinginevyo ni haramu kuangalia kwenye kioo; kwa sababu ni haramu kutazama kile kisichojuzu, huku athari ikiwa imewekwa kwenye filamu kwenye kamera, kwa hivyo haitofautiani na kioo isipokuwa kwa athari ya tukio linaloakisiwa juu yake, ambalo linaoneshwa na hatua ya kemikali inayoitwa (kusafisha picha).

Ikiwa ni sawa kufikiria kusimama mbele ya kioo na kuonesha mwili wetu kwenye ukurasa wake kama taswira hii ambayo matini za kisheria zimeitaja, basi ni sahihi kuzingatia tafakari ya fomu yetu kwenye filamu kupitia kinachojulikana kamera kama upigaji picha kwa maana hiyo hiyo.

Inajulikana kuwa kusimama mbele ya kioo hakuzingatiwi upigaji picha kwa maana iliyotajwa hapo juu, na ndivyo ilivyo kwa yale ambayo filamu zimehifadhi na kuoneshwa kwenye kadibodi ya kile tunachokiita (picha).

 Upigaji picha wa kisasa haujumuishi kukionesha kitu fulani; sura yake, au umbo lake, au sifa yake, kama kwamba haijumuishi upangaji au uundaji unaopelekea kukionesha kitu hicho kuwa na umbo ambalo linalojulikana, kama kwamba hakihusishi kuiga, nayo ni kufananisha kitu na kitu kingine, na kupigwa kwa picha kwenye filamu au kioo si kazi ya mwanadamu hapo kwanza, bali ni sifa mojawapo ya nyenzo ambazo Mwenyezi Mungu aliumba; Picha na sura ya takwimu zinazofanana zimewekwa juu yake, ambayo inaongoza kwa kuibuka kwa mfano wake au kivuli chake juu yake.

(Majadiliano ya wale wanaopiga marufuku upigaji picha):

Baadhi ya wanachuoni wametoa hoja kwamba kupiga picha ni haramu, na wakataja dalili zifuatazo:

Kwanza: Picha imejumuishwa katika jina la picha, kilugha na kiistilahi. Ama katika lugha; picha katika lugha ni fomu, basi ni picha ya lugha.

Ama kuhusu istilahi: kwa sababu hivyo ndivyo watu wanavyofahamiana wao kwa wao bila pingamizi, kila mtu anaita sura kwa picha na anayepiga picha anaitwa “mpiga picha.” Bali, watu husema: Tulikwenda kwa mpiga picha, na akatupigia picha, wahusika wa idara za serikali husema katika hali zao kwa wale wanaokubaliwa: Ni muhimu kuwa na picha ya kivuli au ya rangi ya ukubwa fulani na vile, na hili ni jambo linalojulikana sana ambalo hakuna mtu anayekataa; kwa hivyo picha hiyo inaitwa upigaji picha, na imejumuishwa katika Hadithi za jumla zinazoashiria uharamu na mkazo wa upigaji picha, na hakuna ushahidi wa kisheria wa kutofautisha kati yake hata kidogo. Kulingana na hili, ni lazima iwe haramu  kwa ujumla, kwa sababu imethibitishwa kuwa picha imejumuishwa kwa jina la picha, kwa lugha na istilahi pia.

Jibu kwa hilo ni kwamba hatukubali kuingizwa kwa picha chini ya jina "picha" katika lugha au istilahi; Kwa sababu kile kinachoitwa upigaji picha leo ni istilahi tu isiyo na maana ya upatanisho wa semantiki, kwani haikumaanishwa na picha iliyoharamishwa iliyotajwa katika Hadithi za bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.), Kwa hakika, kuita jina la upigaji picha kunaangukia katika aina fulani ya ufananishi. Kwa hiyo, hukumu ya uharamu haitumiki kwake, kama kwamba hukumu ya uharamu wa kuvaa hariri ya asili haitumiki kwa kile kinachoitwa leo hariri, ambayo imeundwa na viwanda vya kisasa tu, kwa sababu ya kufanana nayo kwa jina lake la kiistilahi.

Hukumu ya kisheria inayohusiana na kitu fulani inahusu tu kitu hicho na sio kile ambacho kinashiriki kwa jina na inapingana nacho katika ukweli na asili.

Na uhusiano baina ya picha katika maana ya kilugha, kisheria na kiistilahi ni katika jina tu, na hauingii katika Hadithi zinazoashiria uharamu wa kupiga picha kwa viumbe hai.

Ushahidi una neno la "kupiga picha" na "mpiga picha", yaani: kufanya kitu hiki katika umbo maalumu, kwa hivyo kidahizo cha (kupiga picha) kinahitaji kuwa na kitendo katika picha ile ile, na inajulikana kuwa uhamishaji wa picha kwa mashine haikusababisha kitendo chochote kutoka kwa mpiga picha katika picha hii. Hakupata mpango wowote ndani yake, wala kuchora, wala kuongeza, wala kupungua ili awe sawa na uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Badala yake, aliweka mashine (kamera) mbele ya kitu kinachopigwa picha, hivyo aliweka picha ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu juu ya sifa ambayo Mwenyezi Mungu aliumba juu yake, kwa hiyo akifungwa kwa kuakisi tu, kwa hiyo hali hii haijajumuishwa katika ushahidi wa jumla wa kuharamisha.

Pili: Sababu ya kuharamishwa kupiga picha ni kuiga kwa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, yaani, kufananisha kwa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, kama ilivyotajwa katika matini ya Hadithi ya Bibi Aisha, (R.A.): “Ewe Aisha, mwenye adhabu kali zaidi katika Siku ya Kiyama ni watu wanaofananisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu.” Mwenye hekima anajua kwamba kupiga picha kwa kamera hakupatani zaidi na uumbaji wa Mwenyezi Mungu kuliko kutengeneza masanamu kwa mkono. Kwa hiyo kupiga picha na mashine ni marufuku zaidi kuliko kutengeneza masanamu kwa mkono, kwa sababu ya uwiano mkubwa kati ya picha na iliyopigwa picha.

kufananisha ni kuiga la kitu na kitu kingine, na hali ya kupiga picha iliyoharamishwa ni kutengeneza sanamu ambayo haikuwepo au iliyotengenezwa hapo awali ambayo ingelinganishwa nayo na mnyama aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu, na maana hii haipo katika kupiga picha na mashine.

Tatu: Hakuna chochote katika Qur`ani wala katika Sunna kinachoashiria kuwa inajuzu kupiga picha kwa kutumia mashine (Kamera).

Jibu lake ni kwamba kuruhusiwa hakuhitaji dalili, asili ya vitu ni kuruhusiwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amedhalilisha kila kilichomo katika ardhi kwa ajili ya manufaa ya mwanaadamu, Mwenyezi Mungu amesema: {Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi.} [Al-Baqarah: 29]

(Hitimisho):

Kwa kumalizia, ikiwa upigaji picha ulitumiwa katika kutekeleza wajibu, na ilikuwa ni njia ya kutekeleza wajibu huo, basi upigaji picha unakuwa ni wajibu, kama vile kupiga picha kwenye uwanja wa jeshi ili kuepusha hatari ya adui na kuweza kukabiliana na. kupigana naye, na upigaji picha katika uwanja wa ufunzaji wa sayansi ambao unachukuliwa kuwa ni wajibu au utoshelevu au kwa ajili ya kutambua hali ya ugonjwa na majeraha, vile vile upigaji picha kwa ajili ya utambulisho wa kibinafsi au pasipoti, na kama kuwapiga picha wahalifu ili kuwakamata na kuwajua kwa ajili ya kukamatwa ikiwa watafanya uhalifu na kuamua kukimbia.

Na ikiwa upigaji picha utatumiwa kwa ajili ya kueneza maovu, kueneza uchafu na kuharibu maadili na wema na jamii iliyoharibika, basi kupiga picha ni haramu, na kuzitazama picha hizi ni haramu pia.

Na ikiwa upigaji picha ukitumika kwa jambo linaloruhusiwa, basi kupiga picha kunajuzu isipokuwa hali hii iwe ni kisingizio cha jambo lililoharamishwa. Kama upigaji picha ukitumiwa katika jambo linaloruhusiwa, lakini kwa sababu fulani inaongoza kwenye uovu uliokatazwa, basi upigaji picha unachukua hukumu ya matokeo yake.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mjuzi Zaidi.

Kusoma katika sheria ya kuishi na Mwingine

Katika Madhehebu ya Shafi

Utafiti uliowasilishwa katika kongamano:

Sheria ya kuuangalia Ulimwengu na kuishi ndani yake katika Madhehebu ya Kifiqhi na uzoefu wa kisasa.

uliofanyika nchini Oman

Kuanzia tarehe 25-28 Jumada Al-Ula 1434 BH, na 6-9 Aprili 2013 BK

Imeandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini katika Nchi ya Oman

Share this:

Related Fatwas