Ukiritimba

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukiritimba

Question

Ni ipi adhabu ya kuzuia bidhaa zenye ruzuku na kuziuza katika soko la ulanguzi?

Answer

Kujipatia bidhaa za ruzuku kwa njia isiyo ya haki au kuzizuia kwa njia si ya kisharia au kuziuza katika soko la ulanguzi ni haramu Kisharia, nayo ni dhambi kubwa kwa sababu hilo ni kufanya madhara na uadui kwenye mali za wastahiki, na kwa mali za umma, lakini pia kula mali za watu kwa njia batili, na kwenda kinyume na kiongozi mkuu wa nchi ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya kumtii kwake katika mambo yasiyokuwa ya kimaasi ni sawa na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtii Mtume wake S.A.W. mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi} An-Nisaai: 59.

Wenye kufanya vitendo hivi viovu ikiwa pamoja na kushikilia bidhaa za ruzuku na kuziuza, Sharia Tukufu imewawekea adhabu ili waogope na watubu kwa uharibifu huu, kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Ewe Kaabi Ibn Ujrah, ni kuwa haitoingia Peponi nyama iliyoota kutokana na kula haramu, kwani moto ni bora kwake, Ewe Kaabi Ibn Ujrah: Watu ni wenye kutafuta: Yupo mwenye kuinunua nafsi yake kwa Mola wake huyo ni mwenye kuepushwa na adhabu kali, na yupo mwenye kuiuza nafsi yake huyo ameangamia. Imepokewa na Imamu Ahamd.

Mtendaji wa hilo anastahiki adhabu ya kisheria pamoja na ile iliyoandaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake siku ya Mwisho. 

Share this:

Related Fatwas