Kuhusu Utelelezaji Sheria Nchini Mi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhusu Utelelezaji Sheria Nchini Misri

Question

Kuhusu Utelelezaji Sheria Nchini Misri 

Answer

Waraka wa kazi uliowasilishwa katika warsha iliyohusu mahusiano kati ya Sharia na Katiba katika wigo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Misri.

 (Kikao cha pili – Sharia na sheria za kiraia za nchi)

Chuo cha Kijerumani cha masomo ya Kimashariki – Hotel ya Flaminco – Zamalekh Jijini Cairo Misri.

9/6/2012

Muwasilishaji Ni:

Ahmad Mamduh Saad

Katibu wa mambo ya Fatwa na mkurugenzi idara ya tafiti za Kisharia katika ofisi ya Mufti wa Misri.

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimuendee Mtume wa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba zake.

Baada ya Utangulizi:

Swali lililowasilishwa kwenye kikao hiki: Ni nini makusudio ya Sharia inayotakiwa kutekelezwa: Sharia kwa upande wa Hukumu au Sharia kwa upande wa Makusudio?

Kabla ya kuingia kwenye jibu, lazima kuelezea baadhi ya maana ya maneno na misamiati yenye uhusiano na kinachoulizwa ili taswira yake iwe ni sahihi kwenye kufahamika, kisha niingie kwenye makusudio kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa msaada wake.

Maana ya baadhi ya Misamiati yenye uhusiano:

Sharia:

Maana neno Sharia kwa upande wa lugha: Ni kuingia ngamia kwenye maji yanayotembea, husemwa: Amemuingiza ngamia wake, kwa maana amemuingiza kwenye maji, na pia imepokewa na Al-Baihaqy kutoka kwa Amiri wa Waumini Ally Ibn Abi Twalib R.A: “Hakika unyweshelezaji dhaifu zaidi ni kumpa maji” ([1]), kwa maana: Watu wenye ngamia kuwapatia ngamia wao maji ya kisima yasiyohitajika kuwanywesha, na Waarabu hawaiti sharia mpaka maji yawe mengi hayakatiki, na inakuwa hali maalumu isiyonyeshelezwa kwa kuyanunua,

Na huitwa Sharia kwa yale yaliyowekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake ndani ya dini na akaamrisha na kuwafaradhishia, kama vile Ibada ya funga, Ibada ya Swala, Ibada ya hija, Ibada ya zaka, ndoa na zingine, pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu} [AL JAASIYAH: 18]. Katadah amesema akiwa mwenye kuifasiri hii Aya: “Sharia ni mambo ya faradhi adhabu amri na makatazo” ([2]), na Al-Farraa amesema katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Sharia: Ni dini mila na mfumo.

Sharia imeitwa hivyo, ikiwa ni kufananishwa na kuingia kwenye maji, ambapo mwenye kuingia kwenye maji kwa hakika ataloa na kusafika ([3]), nayo ni sehemu ambayo watu huenda mara kwa mara ili kunywa maarifa ya kidini na hukumu za kielimu ambazo Mwenyezi Mungu amewapa jukumu la kutekeleza.

Katiba:

Katiba ni tamko au neno la Kifursi limeingizwa kwenye lugha ya Kiarabu, lilikuwa linatumika kwa maana ya kitabu kilichoandikwa ambacho ndani yake kinakusanya sheria za nchi.

Na Waziri mwenye kurejea yaliyoandikwa kuhusu hali za watu alikuwa akiitwa kwa jina hilo kwa kuwa kwake ndio mwenye hii kopi ya sheria, kuitwa kwa jina la katiba msimamizi wa amri za mfalme ni aina tu ya ukiukaji ([4]).

Kisha matumizi yake yakapanuka zaidi na hivi sasa inaitwa sheria kuu ya nchi, ambayo inakusanya sheria ambazo zina ainisha muundo wa nchi, na mfumo wa utawala pamoja na serikali tatu: Bunge, Serikali Kuu na Mahakama, hupangilia mipaka ya kila upande katika pande hizo tatu na uhusiano wa kila upande kwa mwengine, pia hubainisha haki kuu na uhuru wa watu ([5]).

Katiba huzingatiwa kuwa ni sheria muhimu sana zinazofanya kazi nchini, bali ndio msingi wa hizi sheria, na sheria zinapaswa kutokwenda kinyume na katiba.

Hukumu iliyotolewa na mahakama ya rufaa ni kuwa: “Kwa vile katiba ndio sheria mama iliyoundwa, yenye kuongoza basi sheria zingine zimekuwa zikiendana na hukumu zake, ikiwa kutakuwa na mgongano wa sheria na katiba basi kilichowajibu ni kufuata hukumu za katiba na kuachana na sheria zingine zisizo kuwa katiba, uwe mgongano huo umetangulia au umekutana na katiba, ikiwa kwenye katiba limekuja andiko lenye kufaa kufanya kazi bila ya kuwepo haja ya kutungwa sheria yeyote basi tamko hili la katiba litatekelezwa ipasavyo, na huzingatiwa hukumu iliyokinyume na katiba katika hali hii imefutwa madhumuni yake kwa nguvu ya katiba yenyewe” ([6]).

Hukumu:

Neno hukumu kwa upande wa lugha: Ni kuhukumu kitu kuwa ni hivi au sio hivi, ni sawa sawa kimelazimiana na hivyo au hapana ([7]).  

Na katika msamiati: Ni maelezo ya Mwenyezi Mungu yanayofungamana na vitendo vya waliopewa majukumu kwa kuamrishwa au kuhiyarishwa.

Maelezo: Ni kuelekeza maneno yenye manufaa kwa mtu mwingine ambapo atayasikia, na kusudio lake hapa: Ni kuambiwa, nayo ni maneno yenye faida yaliyoelekezwa kwa mtu mwingine, ni katika kutumia kitenzi kisoukomo na kukusudia jina la mtendewa, na maelezo kuambatanishwa na jina la Mwenyezi Mungu ni kuondolewa maeelezo yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu ambayo hayazingatiwi kama ni hukumu.

Na kufungamana: Maana yake ni mfungamano, na unakuwa mfungamano kimaana kabla ya kuwepo mpewa jukumu au baada ya kuwepo kwake.

Vitendo: Ni uwingi wa kitendo, kusudio lake: Ni mambo yaliyoletwa na mpewa majukumu miongoni mwa kauli au vitendo au imani.

Wenye kupewa majukumu: Ni uwingi wa mwenye kupewa jukumu, kusudio lake: Ni mtu aliyebaleghe mwenye akili timamu ambaye ujumbe umemfikia.

Kuamrishwa: Maana yake ni kupewa amri, ni sawa sawa ikiwa ni kwa kutekeleza kitendo au kutotekeleza, amri ya lazima au si ya lazima, hii inakusanya sehemu nne: Wajibu Sunna Haramu na kuchukiza.

Kuhiyarishwa: Maana yake ni kati ya kutenda na kuacha, nayo ni: Halali ([8]).

Kitendo cha muamrishwa: Ni maelezo yaliyopokelewa kitu kuwa sababu au sharti au kizuizi au usahihi au uharibifu, hilo linakusanya kitendo cha mpewa jukumu, kama vile kitendo cha uzinifu ni sababu ya uwepo wa adhabu, na kukosekana kwake ni sababu ya wajibu wa usafi, na uharibifu usio wa lazima kama vile ulevi ni sababu ya kuharibu kwake mali ya mtu mwingine wakati wa kulewa kwake.

Makusudio:

Maana ya Makusudio: Maana ya makusudio kwa upande wa lugha: Ni kukusudia. Na kukusudia kuna maana nyingi kwa upande wa kilugha. Miongoni mwazo: Ni Kunyooka kwa njia, husemwa: Njia yenye kukusudiwa: Nyepesi iliyonyoka.

Pia: Kukielekea kitu na kukileta, unasema: Nimekusudia Nyumba Tukufu, kwa maana: Nimeiendea ili kuifikia.

Miongoni pia: Ni kati na kati kutovuka mpaka, nayo ni fumbo, na pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:  {Kati yao yupo aliye jidhulumu mwenyewe, na yupo wa katikati} Fatir: 32 ([9]).

Ibn Janny zote hizo amepitisha kwa maana ya kuelekea kitu, akasema: Asili ya herufi hizi tatu (Kaaf, Swaad na Daal) katika maneno ya Kiarabu: Ni kudhamiria kuelekea kusimama na kuinuka kukielekea kitu, hii ndio asili yake, pamoja na wakati mwingine uhusishwa kwa maana ya kunyoka bila ya kupinda, hivi unaonaje wakati mwingine unakusudia uovu kama unavyokusudia uadilifu? Kuazimia na kuelekea yanakusanya yote mawili ([10]).

Hapa lengo la Makusudio: Ni makusudio ya Sharia, nayo kwa maana ya kimsamiati: Ni maana na hekima iliyowekwa na Sharia katika hali zote za uwekaji Sharia ambapo haihusishi uwekaji wake na aina maalumu ya hukumu za Sharia, katika hili inaingia sifa ya Sharia, malengo yake makuu na maana ambayo uwekaji Sharia hauachani na maelezo yake, na katika hili pia zinaingia maana nyingi za hukumu ambazo hazijaelezwa kwenye aina zingine za hukumu.

Mgawanyiko wa Makusudio:

Makusudio ya Sharia kwa upande wa umuhimu wake yanagawanyika sehemu tatu: Makusudio Muhimu, Makusudio ya kuhitajika, Makusudio yaliyo mazuri.

Sehemu ya Kwanza – Makusudio Muhimu:

Makusudio muhimu ya Sharia ni yale yanayofungamana na kulinda moja ya Makusudio matano ya Sharia ambayo: Dini nafsi akili heshima na mali.

Ibn Sabaky amesema: “Makusudio muhimu: Ni yale yanayolinda makusudio miongoni mwa makusudio matano ambayo dini zimekubaliana kuyalinda, nayo ni Nafsi dini akili mali na nasaba ([11]).

Makusudio haya yameelezewa kuwa ni muhimu, kwa sababu masilahi ya dini na dunia yanajengeka kwa kuyalinda makusudio hayo, ikiwa dini itakosekana basi mpangilio wa malipo yanayotarajiwa utakosekana, ikiwa atakosekana mtu wa kutekeleza basi atakosekana wa kutekeleza dini, ikiwa akili itakosekana basi ufuasi wa dini utaondoka, ikiwa kizazi kitakosekana hakutakuwa na kubakia, na ikiwa mali itakosekana hakuna maisha ([12]).

Mambo muhimu kuwa matano yaliyotajwa marejeo yake ni kufuatana. Na makusudio haya hayajahusisha Sharia bila ya Sharia bali yamekuja kwenye Sharia zote za mbinguni, Shatwiby anasema: “Uma umekubaliana – bali dini zote – kuwa Sharia imewekwa ili kulinda mambo muhimu matano, nayo ni dini nafsi kizazi mali na akili, na kufahamika kwa umma kama vitu muhimu, wala hilo kwetu halijathibiti kwa dalili maalumu, wala kushuhudiwa kwetu asili maalumu yenye sifa pekee ya kurejewa, bali umefahamu kuendana kwake na Sharia kwa mkusanyiko wa dalili zisizoishia kwenye mlango mmoja” ([13]).

Sehemu ya Pili - Makusudio ya Kuhitajika:

Makusudio ya kuhitajjika: Ni yanayokosekana kwa upande wa upanuzi na kuondoa tabu mara nyingi hupelekea shida na matatizo kwa kukosekana yanayohitajika, ambapo yenyewe ikiwa hayajaangaliwa vizuri basi watekelezaji wataingia kwenye matatizo ([14]).

Mambo ya kuhitajika yapo chini ya mambo muhimu, kwa sababu ambayo yanapelekea kukosekana kwake yenyewe yanaleta matatizo na uzito ambavyo havifikii kiwango cha kukosekana au kupungua moja ya mambo makuu matano.

Sharia ya Kiislamu imesimamia upande wa kufikiwa kwa makusudio yanayohitajika, na kuondoa uzito na matatizo kwa watekelezaji wa amri. Mola Mtukufu Amesema:

{Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} katika mlango huu: Kuna ruhusa iliyopokelewa katika hukumu za Sharia na misamaha ([15]).

Sehemu ya Tatu – Makusudio yaliyo Mazuri:

Imamu Al-Haramain Al-juwainy ameelezea makusudio yaliyo mazuri ni kuwa: “Kila kisichoendana na dharura maalumu wala haja ya jumla, lakini kinaonesha lengo la kuleta heshima au kupingana na kinyume chake” ([16]). 

Yenyewe inarejea kwenye mazuri yanayongezeka kwenye asili ya masilahi ya mambo muhimu au ya dharura na ya kuhitajika, wala kukosekana kwake hakupelekei kukosekana mambo ya dharura wala ya kuhitajika bali yanakuwa sehemu ya uzuri na kupendezesha ([17]).

Katika mifano ya sehemu hii: Ni pambo la vazi na uzuri wa muonekanao, adabu za kula kunywa na mfano wa hayo, pia: Kama vile uharamu wa kitu najisi, kwani ni ukiukaji wa asili unaendana na uharamu wake hata yenyewe ni haramu kujichafua kwa najisi bila ya kuwepo udhuru wa hilo ([18]).  

Migawanyiko hii mitatu iliyotajwa hakuna tofauti katika mpangilio wake kwa sababu mpangilio huu unakubaliana na nguvu ya mahitaji ya kila sehemu, nayo yamelezewa na Imamu Al-Ghazaly katika kitabu chake cha “Al-Mustasfy” kwa maana ya nguvu katika yenye masilahi, akasema: “Maslahi kwa kuzingatia nguvu yake yanagawanyika kwenye: Sehemu ya masilahi ya dharura, sehemu ya masilahi ya mahitaji, na sehemu ya masilahi yanayofungamana na uzuri na mapambo ([19]).

****

Kuhusu Utekelezaji Sharia.

Hakuna shaka kuwa suala la kuhukumu Sharia imekuwa ni maudhui inayongelewa sana na kushuhurisha mno kile kinachoitwa hii leo “Maoni ya Umma”.

Maelezo kuhusu utekelezaji wa Sharia yanatulazimu kuleta maana nyingi hakuna shaka kuwa kuzifahamu kwake kutamsaidia mtafiti kutengeneza muelekeo maalumu wenye muono na dalili, nao ni kama ifuatavyo:

Maana ya utekelezaji Sharia:

  Imelezwa kuwa Sharia hukusudiwa kila kilichowekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kwenye dini na kuamrisha kwao, na hilo linakusanya yote Mwenyezi Mungu aliyoyateremsha kwa waja wake katika Akida Ibada Mashirikiano Maadili na mengine, Mola Mtukufu Anasema:

{Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo} [AS SHURA: 13.] Sudayy amesema: Hiyo ni dini ([20]).

Lakini matumizi ya Sharia yaliyoenea sana ni kukusudiwa kila kisichokuwa Akida katika hukumu za vitendo, hivyo basi ibara imekuja: “Uislamu ni Akida na Sharia”.

Maana hii ni pana zaidi ya maana ya Fiqhi kwa maana yake ya kimsamiati, ambapo Fiqhi kimsamiati haizungumzii isipokuwa hukumu ambazo njia yake ni Jitihada, ama masuala yenye hukumu za moja kwa moja ambayo yanashirikiana katika maana yake maalumu na ya jumla na ambayo huitwa: Mambo ya dharura yanayofahamika katika dini, kama vile wajibu wa Ibada ya Swala Uharamu wa zinaa na mfano wake, wala haviitwi kuvifahamu kwake ni Fiqhi ([21]). Ama uitaji uliopita wa neno Sharia, wenyewe unazungumzia hukumu za mambo ya dharura na hukumu ambao maarifa yake yanasimama juu ya mtazamo na dalili.

Ama kuitwa neno Sharia katika kauli yao: “Utekeleza Sharia” lenyewe linakusudiwa maana maalumu katika zilizoelezewa ambapo hukusudiwa sharia ([22]) inayotawala, ambayo ni ibara ya mkusanyiko wa sheria ambazo zinaunda mahusiano ya watu katika jamii, na ambazo zinawalazimisha wafuasi wake wote kuzifuata kwa njia ya malipo yanayopitishwa na mamlaka kuu kwa mwenye kukiuka wakati inapohitajika, kutokana na maana hii mfumo linganishi umekuja katika mapendekezo ya kielimu na tafiti kati ya Sharia na sheria.

Na maana ya kuzitekeleza: Ni kuwa marejeo katika mambo ya sheria na kufuata masuala na kadhia mbalimbali ([23]).

Makusudio ya Sharia au hukumu za Sharia.

Nini makusudio ya Sharia inayotakiwa kutekelezwa: Je ni Sharia za hukumu au Sharia za makusudio?

Ukweli ni kuwa kugawanyika Sharia kwenye Sharia za hukumu na Sharia za makusudio kunaweza kufahamika kuwa makusudio yanaweza kujengewa maana iliyo nje ya sehemu ya hukumu za Sharia, inafahamika kuwa Sharia imewekwa kwa ajili ya masilahi ya waja, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} [AL-ANBIYAA: 107], kutokana na rehma imeelezwa ya kwamba Sharia ya mwisho ya Muhammad: Iwe inaleta masilahi na kuondoa uharibifu, kwa sababu rehma kwa upande wa Mwenyezi Mungu ni wema upole na usaidizi, athari hizi zote zinapelekea Sharia kujengwa kwenye msingi wa masilahi, kwa sababu wema hauwi wema ikiwa mwema atamuamrisha mweye kufanyiwa wema jambo au kumkataza kitu kilicho kinyume na masilahi yake na kupingana au amri na katazo vikiwa havina masilahi wala uharibifu.

Katika hilo Imamu Al-Baidhawy anasema: “Utafiti umeonesha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka hukumu zake kwa masilahi ya waja, ikiwa ni utukuzaji na wema” ([24]).

Na Imamu Shatwiby anasema: “Uwekaji Sharia unazingatia masilahi ya waja kwa wakati wa sasa na baadaye kwa pamoja….kauli yenye nguvu tuliyoikubali kuhusu Sharia ni kuwa imewekwa kwa masilahi ya waja….ikiwa utafati umeonesha hili, na ikawa mfano wa kadhia kama hii yenye faida kielimu, basi sisi tunapitisha moja kwa moja kuwa jambo endelevu katika fafanuzi zote za Sharia” ([25]).

Ikiwa imethibiti hivyo basi suala la hukumu za Sharia linakuwa ni kukusudia kufikia haya masilahi, na masilahi hayo ni yanayoelezewa na makusudio ya Sharia, na haya makusudio yanapita katika hukumu za Sharia Takatifu kama mtiririko wa maji katika uwa.

Na makusudio sio ibara tu ya alama inainuliwa, bali yenyewe ni tafaiti katika tafiti za elimu ya misingi ya fiqhi, na makusudio haya ni yenye taratibu zake na viwango vyake vya Kisharia inayofanya kazi, na wala hayajajengwa kwa dhana na wema tu.

Hili swali lililotajwa hata kama litakuwa jipya katika muundo wake isipokuwa Wanachuoni wameelezea madhumuni yake na wakajibu kwenye maelezo yao juu ya aina za masilahi, na yenyewe inagawanyika kwenye aina tatu:

Aina ya Kwanza: Masilahi yameonekana na sharia kwa kuyazingatia, kwa kupatikana asili ya Kisharia ambayo inaonesha aina ya masilahi, mfano: Kumdhamini mwizi kwa thamani ya kilichoibwa, ikiwa itatekelezwa kwake adhabu ni kukemewa na vitendo vya uadui, kwa sababu Sharia imeshuhudia aina yake kwa hukumu yake ya kutoa dhamana kwa mporaji kwa kosa lake.

Imamu Ghazaly amesema: “Ama yaliyoshuhudiwa na Sharia kwa kuyazingatia; hayo ni hoja, na mwisho yanarejea kwenye kipimo” ([26]).     

Aina ya Pili: Masilahi Sharia imeshuhudia kubatilisha kwake, kwa kuwepo tamko linaonesha hukumu inayopinga hukumu ambayo inaelezea masilahi yanayodaiwa.

Na sababu ya kubatilisha hii aina ni kuwa imehukumu kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya masilahi anayofikira mwanadamu kwa mtazamo wake ([27]).

Mifano yake: Ni kusema kuwa mtoto wa kike ni sawa sawa na mtoto wa kiume katika mirathi kwa sababu ya usawa wao katika undugu kwa mrithiwa, na kwa vile mtoto wa kike amekuwa anashirikiana na mume wake katika matatizo ya maisha, hivyo usawa wa mtoto wa kiume na wa kike ni kwa upande huu, haya masilahi Sharia imeshuhudia kuyabatilisha kwa kuwepo tamko la kuwa mtoto wa kiume ni sawa na nafasi ya watoto wawili wa kike.

Aina ya Tatu: Masilahi haikufahamika mazingatio ya Sharia au kufuta kwake, kwa maana Sharia haikuzingatia jinsi ya ukaribu, bali imezingatia jinsi ya mbali, na wala haikufahamika kufuta kwake kwa upande wa Sharia, nayo huitwa “Masilahi ya moja kwa moja” ([28]).

Haya maneno yao yanashiria jibu la swali, ikiwa muradi wa makusudio katika ibara ya (Makusudio ya Sharia), makusudio huzalisha hukumu kinyume na sehemu ya hukumu za Kisharia, kila makusudio au masilahi yanayoingia katika hukumu za Kisharia kwa kufutwa masilahi yanakuwa yamefutwa au makusudio danganyifu.

Chanzo cha hukumu ndio chanzo cha makusudio kwani vyote viwili ni Sharia, na ibara ambayo siku zote inatajwa na Wanachuoni wakati wa kuongea kwao kuhusu hakimu ambaye ni moja ya nguzo za hukumu ya Kisharia ni: “Kwa hakika Hakimu ni Mwenyezi Mungu” ([29]), na katika maana yake: “Hakuna anayefahamu vizuri hukumu isipokuwa ni kwa upande wa Mwenyezi Mungu” ([30]), maana zake: “Hakimu ni Sharia na wala si akili” ([31]), madai ya kufanyia kazi makusudio peke yake hayo ni kwa upande wa kuamini baadhi ya maandiko pasi ya maandiko mengine, kwani Sheikh Twahir Ibn Ashuur Mwanachuoni Mhakiki anasema kwenye tafasiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa upande wa wana wa Israil:

{Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila fedheha katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda} [AL BAQARAH: 85], kwa maana ni namna gani mumekusudia kwenda kinyume na Torati katika kuendesha mvita dhidi ya ndugu zenu na kuwapeleka kuwa fidia wa mateka wenu? Na kufuta kukaitwa imani na kufuru kwa njia ya maneno ya kuazima ili kuchafua kinachofananishwa, na kuonya kukusudia kwenda kinyume na maandiko yanayoweza mpelekea muhusika kwenye ukafiri, limekuja neno “Munamini” katika hali ya upingaji, ikiwa ni kuelezea kuwa kukusanya kati ya mambo mawili haiwezekani, nayo ni kuonesha kuwa wamekaribia kupinga haramu ya kuwatoa kwao, au huenda walipinga hilo, na wakapinga yale yaliyokuwa na amri ya moja kwa moja katika dini ([32]).

Na Sharia yote haigawanyiki, kuifanyia kazi ya kuitenganisha na makusudio ambayo Sharia imeyazingatia kisha kuyaondoa bila ya kuzingatia matumizi maalum ya Sharia; inachukuliwa ni kuizushia Sharia na matumizi mabaya ya makusudio, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:

{Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za Shetani; hakika yeye kwenu ni adui wa wazi} Al-Baqarah: 208. Kundi la Maimamu waliotangulia kama vile Ibn Abbasi, Mujahid, Twaawus, Ibn Zaid, Adhihak, Akrama, Qatada na Sudyy – kwa maana ya Uislamu.

Al-Hafidh Ibn Kathiir anasema katika tafasiri yake: “Mungu Mtukufu anatoa amri kwa waja wake waliomuamini na kumsadikisha Mtume wake wachukuwe pande zote za Uislamu na Sharia zake, na kufanyia kazi amri zake zote pamoja na kuacha makatazo yake yote kadiri wanavyoweza kufanya hivyo….na kuna miongoni mwa wafasiri waliosema: Ingieni katika Uislamu nyinyi nyote, kauli ya kwanza ndio sahihi, nayo ni kuwa wameamrishwa kufanyia kazi pande zote za Imani na Sharia ya Uislamu, nazo ni nyingi sana basi wanazoziweza” ([33]).

kusema kuwa inawezekana kutekeleza makusudio ya Sharia na wala hukumu za Sharia ni kauli ya hovyo, kwa sababu makusudio yakitofautiana na hukumu yanakuwa upotofu, na tumeona kuwa ukina wa kuchukuwa msingi huu umefikia kwa baadhi ya watu kuchafua misingi thabiti na kuondoa maandiko ya Kisharia kwenye maudhui yake na kuyafanya maandiko ya kihistoria kufanya kwake kazi ni kwa muda na sehemu ambayo yameonekana, na kufanya kazi sehemu ya hukumu za Kisharia – kama vile adhabu kwa mfano – kwa jina la Sharia ni udanganyifu kwenye Sharia, na kuwa si lazima kushikamana na maandiko yenyewe bali kwa roho yake na makusudio yake tu, hawa ndio wale walioitwa na Dr. Yusuf Al-Qardhawy: “Wakwamishaji wapya” ([34]), jambo la kushangaza zaidi kuwa hawa wanakwamisha maandiko ya Sharia Tukufu na hukumu zake kwa madai ya kuchunga masilahi ya waja, kana kwamba maandiko haya na hizo hukumu vimekuja kupingana na hayo masilahi, hakuna shaka kuwa Sharia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu haikuja isipokua kufikia masilahi na kukamilisha makusudio, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kujua zaidi waja wake na kile chenye masilahi kwao na kuwafaa: {Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari}.

Mwanachuoni Ibn Qayyim anasema katika kitabu cha Iilaam Al-Muwaqiin: “Hakika Sharia ujenzi wake na msingi wake ni hukumu na masilahi ya waja katika kuishi na siku ya mwisho, nayo yote ni uadilifu, yote ni rehma, yote ni hekima, masula yote yaliyotoka kwenye uadilifu kwenda kwenye uovu, yaliyotoka kwenye huruma na kuwa kinyume chake, kutoka kwenye masilahi na kuwa uharibifu, kutoka kwenye hekima na kuwa uovu basi hivyo si katika Sharia hata kama kutaingia maelezo: Kwani Sharia ni uadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na rehma zake kwa waja wake, kivuli chake katika ardhi yake, na hekima zake zenye kumuonesha Yeye na ukweli wa Mtume wake S.A.W ni dalili timilifu zaidi na kweli zaidi, nayo ni nuru yake ambayo kwa nuru hiyo huangazia wenye kuona, uwongofu wake ambao wameongoka waongokaji, ponyo lake kamili ambalo lenye dawa ya kila maradhi, njia yake iliyonyoka ambayo mwenye kuifuata atakuwa amefuata njia iliyonyoka sawa sawa, nayo ni utulivu wa macho na uhai wa moyo pamoja na ladha ya roho; yenyewe ni uhai lishe dawa nuru pongyo na zuio, kheiri zote zilizopo ni zenye kunufaika nayo, na kila upungufu kwenye vilivyomo sababu yake inatokana na kuipoteza Sharia, lau Sharia isingebaki basi dunia ingeharibika na kukunjika ulimwengu, nayo ni zuio kwa watu na nguvo za ulimwengu, na kwa Sharia hizo Mwenyezi Mungu hushika mbingu na ardhi kutodondoka, ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atataka kuiharibu dunia na kuukunja ulimwengu basi ataondoa Sharia zilizopo, kwani Sharia ambayo Mwenyezi Mungu amemleta Mtume wake S.A.W ndio nguzo za ulimwengu na nguzo za mafanikio na furaha duniani na Akhera” ([35]).

Ambalo utukufu wake unakuja na wala haiwezekani kuingiza ndani yake mtaalam ni kusema kufanyia kazi makusudio kunazingatiwa kwa upande wa kuimarisha utungaji Sharia ambapo hakuna andiko, na hili linakuwa kwa upande wa kufanyia kazi aina ya tatu katika aina za masilahi ambayo tumeyataja hapo mwanzo, nayo ni: Masilahi ambayo hayakufahamika mazingatio ya Sharia au kufutwa kwake, nayo huitwa “Masilahi yasiyozingatiwa wala kufutwa” na sababu ya kuitwa kwake hivyo ni kwamba yenyewe hayajazingatiwa na Sharia au kufutwa kwa andiko maalum au lenye maana hiyo” ([36]).

Bali ikiachwa huru kwa umma katika kupangilia mambo ya maisha yao kisiasa kiuchumi na kijamii, kunaweza kuwa makusudio muhimu yaliyonyamaziwa kabisana Sharia ([37]).

Hilo limeelezewa na baadhi ya Wanachuoni wa siasa za Kisharia, kuwa hufanyiwa kazi na mkuu wan chi “Anakuwa na watu waliokaribu zaidi na mafanikio na kuwa mbali zaidi na uharibifu, hata kama haijawekwa na Mtume S.A.W wala kuteremshiwa ufunuo” ([38]).

Imekuwa kawaida kwa upande wa katiba nchini Misri tokea mahakama za kikatiba zilipotokewa na sheria kuwa zisihukumu kwa katiba Sharia yanazokwenda kinyume na makusudio ya Sharia au masilahi ambayo yanasimamiwa na Sharia ([39]).

Ni hukumu zipi zinakusudiwa kutekelezwa?

Sharia ambayo inakusudiwa kurejewa na kutekelezwa ikiwa itathibiti kuwa sio yenyewe inayofahamika kufanyia kazi makusudio mkabala na kupuuza hukumu za Kisharia, linakuja swali ni zipi hukumu ambazo zinakusudiwa kutekelezwa, na Wanachuoni Waislamu kati yao kuna tofauti, hivyo ni uelewa upi ambao utarejewa? Na ni madhehebu gani yatategemewa?

Kabla ya jibu la swali hili ni lazima kuelezea kwanza masuala ya hukumu za moja kwa moja na zile za kudhani, kwani hukumu za Kisharia zinagawanyika kwenye hukumu zilizokubalika moja kwa moja na zile hukumu za kufikiriwa, hukumu zilizokubalika moja kwa moja ni zile zinazohusiana na maswala ambayo wamekubaliana Waislamu, ambapo hakuna nafasi ya kufanya jitihada, mfano: Ulazima wa swala tano, kutoa zaka, kufunga mwezi wa Ramadhani, uharamu wa uzinifu, uharamu wa riba, dhuluma na maovu, na hukumu za kufirikiwa ni zile ambazo dalili yake inatokana na dhana ni sawa sawa kwa upande wa dalili, mifano yake ni mingi, na hukumu hizi ni sehemu ya jitihada.

Inawezekana jambo asili yake likawa ni lenye kukubalika moja kwa moja, lakini likawa la kufikiriwa katika ufafanuzi wake, kama vile riba, hakuna tofauti kwa upande wa uharamu wake na yenyewe ni katika madhambi makubwa, lakini kunatofauti kwa mfano katika kuuza kitu ([40]), miongoni mwa Wanachuoni wamesema: Ndani yake kuna shaka ya riba, na shaka katika hili kwa hakika ipo ([41]), miongoni mwao wamesema: Yenyewe ni njia ya kusalimika kuingia katika riba ([42]).

Kwa maelezo hayo: Hakuna tatizo katika kundi la kwanza nalo ni hukumu za moja kwa moja, ambapo hakuna tofauti kabisa, na linabakia kundi la pili nalo ni hukumu za kufikiriwa, na hili linawezekana kwa mtawala aliyepewa mamlaka ya kutunga sheria kuteua katika Fiqhi pana ya Kiislamu madhehebu ya Wanajitihada kile anachokiona kinafikia masilahi ya umma, na katika yaliyopitishwa Kifiqhi: Kiongozi kutumia kwa wananchi kinachowapa masilahi ([43]), na uteuzi wa kiongozi unaondoa tofauti, ikiwa kiongozi atateua kauli katika kauli za Wanajitihada katika masuala miongoni mwa masuala yenye tofauti na kuwalazimisha wananchi wake kuzichukuwa amri hizo basi inakuwa ni lazima kwao kufuata katika hilo, Wanachuoni wamezungumza kuhusu kanuni hii na kutoa maelezo mengi kwenye hilo miongoni mwao: Imamu Al-Qurafy katika tofauti, tofauti ya sabini na saba kati ya kanuni ya tofauti ya masuala ya jitihada kabla ya hukumu ya kiongozi na kati ya kanuni ya masuala ya jitihada yanaondoa tofauti na kupitishwa kauli moja baada ya hukumu ya kiongozi, kauli hiyo ndio hukumu iliyotolewa na kiongozi kwenye hali za Kisharia, akasema: “Fahamu kuwa hukumu ya kiongozi katika masuala ya jitihada huondoa tofauti na aliyetofauti na madhehebu yake hurejeshwa kwenye madhehebu ya kiongozi na fat’wa yake hubadilika baada ya hukumu ya kiongozi kutoka kuwa kwake kauli sahihi kwa madhehebu ya Wanachuoni” ([44]).

Na Mwanachuoni mhakiki Sheikh Mustafa Zarka anasema ndani ya kitabu chake cha Utangulizi wa Fiqhi: “Jitihada ya Kiislamu imepitisha kwa mkuu wa nchi kuanzia Khalifa au asiyekuwa Khalifa kuweka mpaka wa kuenea kwa hukumu za Kisharia na utakelezaji wake, au kuamuru kufanyia kazi kauli dhaifu yenye kupewa nguvu ikiwa masilahi ya wakati yatahitaji hilo na kuwa ni kauli yenye nguvu ambayo inapaswa kufanya kazi, na hilo limeelezewa na Wanachuoni wetu kufuatana na kanuni ya: “Masilahi yaliyoletwa na Sharia” na kanuni inayosema: “Hukumu hubadilika kwa kubadilika zama”, na maandiko ya Wanachuoni katika milango tofauti inaonesha kuwa mamlaka ikiwa zitaamua jambo la sehemu ya jitihada  - kwa maana: Linalokubali jitihada, lisilogongana na maandiko ya moja kwa moja katika Sharia – amri yake inakuwa ni lazima kuheshimiwa na kutekelezwa Kisharia, ikiwa baadhi ya makubaliano yamezuia masilahi ya yaliyojitokeza yaliyo lazimu kuchungwa hilo, na makubaliano hayo yakawa ni halali kutekelezwa Kisharia, basi kwa kuzuia kwake yanakuwa ni batili na kusimamishwa kwa mujibu wa amri” ([45]).

Ama masuala mapya na matukio ya sasa – ambayo ni matunda ya mabadiliko endelevu ya maisha kwa pande zake mbalimbali, upande wa vitu, upande wa watu, upande wa matukio, upande wa fikra na upande wa mifumo – hakuna jukwaa la jitihada na kutaka msaada wa watu wa mitazamo kupitia kazi za kitaasisi hukutana wazoefu wa mambo ya Sharia na elimu mbalimbali, hili ndani ya nchi yetu lipo sawa na Jopo la tafiti za Kiislamu na Ofisi kuu ya Mufti wa Misri kwa upande mmoja, na Academi zake za tafiti za kisayansi, mfano: Kituo cha Taifa cha tafiti, Kituo kikuu cha Takwimu na mfano wake kwa upande mwengine, na hilo ili kufahamu hali halisi kwa usahihi zaidi, kisha kutafiti masuala haya mapya tafiti za kielimu hutolewa ufafanuzi wa maandiko na kuchunga makusudio makuu ya Sharia na kununi zake kuu kukitegemewa katika hilo pande za kimtazamo na jitihada zenye kuzingatiwa ([46]).

Hukumu za Kisharia na sheria za sasa:

Ikiwa hukumu za moja kwa moja zenye kufahamika zimethibiti, na kuwa mkuu wa nchi ana haki ya kuteua madhehebu ya Wanajitihada kile anachona kinafikia masilahi, na katika maswala ya matukio hutegemewa jitihada za upande uliopewa jukumu hilo, hapa swali lengine linakuja, nalo ni je hilo linalazimu sisi kuvunja sheria ya sasa na kuanza kuasisi sheria mpya?

Jibu: Kabla ya kujibu swali hili ni lazima tufahamu asili ya sheria, na hapo tutahusisha sheria za kiraia na sheria za jinai, kwa sababu mijadala mingi mara nyingi huzungumzia sheria hizi mbili kuliko sheria zengine.

Mtazamo unaovuka asili ya sheria ya kiraia:

Ama sheria ya kiraia ya Misri asili yake mkusanyiko wa sheria za mwaka 1883 ambazo zimewekwa na Mwanachuoni Al-Hanafy Muhammad Qadary Basha na kuandikwa kwa lugha ya Kifaransa, kisha zikatafasiriwa kwa lugha ya Kiarabu, watu wengi wakadhani kuwa Misri imetekeleza sheria ya Kifaransa, lakini sio hivyo, imekuja katika kifungu cha kwanza cha sheria kuwa, haipingi haki yeyote iliyopitishwa katika Sharia ya Kiislamu, kifungu hiki kimendelea kuwepo mpaka mwaka 1908, ambapo sheria ilipitiwa tena, imekuja – kwa mujibu wa mhadhiri wa vikao vya mijadala – kuondoa ibara hii inayohusiana na Sharia, ambapo imepita robo karne bila ya kupingwa na yeyote kipengele chochote ndani ya sheria hii, kisha marehemu Dr. Abdulrazak Basha As-Sanhuury alikuja na kuongoza tume ya kielimu ili kufanya kazi ya kurekebisha sheria hii, mpaka ikamalizika na kuanza kufanya kazi mwaka 1949, kisha akafanya kazi ya kusherehesha katika kitabu chake kikubwa kilichoitwa “Al-Wasiitw” chenye juzuu kumi, akielezea humo kila chanzo kilipochukuliwa kwenye Sharia ya Kiislamu, na akataja kuwa uundaji umetegemea Sharia mbalimbali kumi na sita, na fikra ya Sanhuury ilikuwa Vitabu vya Sharia havifai kuundia sheria mpya za kisasa, hilo halikuwa kupinga Sharia, bali mfumo wa uandishi wake na kuandikwa kwa hukumu zake ndani ya vitabu vya fiqhi na kuendana kwake na wakati ([47]).

Sanhuury anasema katika sheria za kiraia za Kimisri: “Yaliyokuja katika sheria miongoni mwa maandiko inawezekana kutoa hukumu za Sharia ya Kiislamu pasi ya matatizo yeyote makubwa, ni sawa sawa limepatikana tamko au halijapatikana, kwani hakimu anakuwa kati ya mambo mawili: Ima atekeleze hukumu zisizopingana na misingi ya Sharia ya Kiislamu, au kutekeleza Sharia yenyewe ya Kiislamu” ([48]).

Katika makala yake kuhusu sheria za kiraia za nchi za Kiarabu anasema: “Sisi tumefupisha kufuata sheria hizi kwa kuzingatia kuwa hizi ndio lengo la kuboresha fiqhi ya Kiislamu, hatuwezi kuwa tumetengeneza kitu, na inakuwa ni bora kufuata moja kwa moja sheria za Kimagharibi… kilichowajibu ni kufanya tafiti Sharia ya Kiislamu tafiti ya kina kwa mujibu wa misingi ya utengenezaji wake, wala haifai kutoka kwenye misingi hii kwa madai kuwa mabadiliko yanapelekea huku kutoka”.

Anasema: “Ambalo tunalitaka katika utafiti wa fiqhi ya Kiislamu kwa mujibu wa msingi ya utengenezaji wake mpaka tunapata sheria mpya inayokubaliana na wakati ambao sisi tumo…sheria ya kudumu nchini Misri na Iraq bali na nchi zote za Kiarabu, ni sheria ya kiraia ya Kiarabu ambayo itatoholewa kutoka Sharia ya Kiislamu baada ya kuboreshwa” ([49]).

Ikiwa Sanhuury anaelezea faida za sheria ya kiraia na kuainisha sehemu ndogo wala hatambui riba, na anatofautisha ndani ya kitabu chake cha: “Vyanzo vya haki” kati ya faida ya kuzungusha mtaji ni ambao moja ya vitenda kazi vinne (Ardhi-Utawala-Kazi-Mtaji) anajaribu kuifanya sheria yote ya kiraia si sehemu inayotokana na Sharia ([50]), hata kama hatukubaliani na hii tofauti yake anabakia kuwa haalalishi riba na kuitengenezea sheria bali anapinga sifa ya riba kwa sura yeyote pamoja na kukubali asili ya uharamu wake na kuzuiliwa kwake.

Na Sheikh Sayyid Abdalla Hussein R.A ambaye alimpinga vikali Sanhuury na kumjibu kwa majibu makali alitunga kitabu kingine jina lake: “Uwiano katika Sharia za kiraia za mbinguni na zile za kutungwa” kisha kikachapwa kwa jina: “Uwiano wa Sharia kati ya sheria za kiraia za kutengenezwa na Sharia za Kiislamu” kikiwa na juzuu nne, Sheikh Taidy katika hiki kitabu alifanya kazi ya kulinganisha sheria ya kiraia ya Kifaransa misingi na kanuni kwenye madhehebu  ya Imamu Maliki, kwa kuzingatia kuwa sheria hii ndio msingi wa kanuni ya utungaji sheria za kuwekwa, akamalizia kuwa tisa ya kumi ya hizo sheria zinakubaliana na madhehebu ya Imamu Maliki, akaelezea sababu ya hilo kuwa athari hizi ni za zamani, zinarejea wakati wa Andulus ilipokuwa kitivo cha elimu marejeo watu wa Ulaya wanazama katika nuru na elimu, madhehebu ya Imamu Maliki yakaeleza utungaji wao wa sheria wakati huo kwa njia hii ([51]).

Sheria ya jinai na mipaka ya adhabu za Kisharia:

Ama sheria ya jinai, yenyewe imekuwa ikikosolewa sana kuliko sheria zengine, kwa kukosekana adhabu ambazo Sharia ya Kiislamu imekuja nazo dhidi ya muuaji mzinifu mwizi na wengine, na mpangilio wake wa adhabu zengine, mpaka ibara ya: “Utekelezaji Sharia” imekuwa ndani ya ufahamu wa watu wengi na katika baadhi ya fasihi za kisasa ni sawa sawa na kufanya kazi adhabu na kuzitekeleza, ukweli ni kuwa Sharia ni pana zaidi ya adhabu, na adhabu ni sehemu ya Sharia.

Kabla ya kuchambua sheria ya makosa ya jinai ni lazima kuangalia mambo mawili:

La Kwanza: Ni upande wa historia inayohusiana na hiyo sheria, kumekuwa na mijadala mingi mwishoni mwa karne ya kumi na tisa, ikizungumzia kuepukana kwake na masuala ya utekelezaji adhabu, ikaibuka kadhia inayofahamika “Zama za Shaka” na zama ambayo tunaishi pamoja na kupanuka kwake na kubadilika majukumu ya watu na uchache wa masharti ya utoaji ushahidi ambao umekubaliwa na Wanafiqhi kumeifanya zama hii kuwa ni zama ya shaka ([52]), na kanuni inasema: Adhabu huondoka kwa uwepo wa shaka, katika Hadithi Tukufu Mtume S.A.W anasema:

 “Acheni kutekeleza adhabu kwa Waislamu kadiri muwezavyo, ikiwa mutakuta kwa Muislamu sehemu ya kutokea basi muacheni huru, kwani kiongozi kukosea kutoa msamaha ni bora zaidi kwake kuliko kukosea kutoa adhabu” ([53]). Na Omar Ibn Khattabu akasema: “Kukwamisha adhabu kwa kuwepo shaka ni jambo nilipendalo sana kwangu kuliko kutekeleza adhabu kwa kuwepo na shaka” ([54]).

Tofauti ni kubwa kati ya kutofanya kazi adhabu kwa sababu ya kutoamini uhalali wa Sharia ya Kiisalmu na uhalali wake katika kuhukumu, na kati ya kutofanya kazi kwa sababu anayoiona mwenyezi ni kizuizi cha kutofanya kazi Kisharia, pamoja na kuamini jinai ya vitendo hivi na dhambi za mtendaji wake, na kuwa Sharia ndio haki.

Usimamishaji huu katika mtazamo wao ni sawa na yaliyokuja katika kuondoa Amiri wa Waumini Omar Ibn Khattabu mwaka wa njaa adhabu ya kukata mkono iliyothibiti kwa kauli ya Mola Mtukufu:

{mwizi mwanamme na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima} [AL MAIDAH: 38].

Na kutoka kwa Omar amesema:

 “Hakatwi mkono wakati wa matezo na kipindi cha njaa” ([55]).

Na imepokelewa maana yake kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kumkata mkono mwizi ndani ya zama za njaa” ([56]).

Hali ya njaa ni sehemu ya dharura na mahitaji, ndipo Omar akaishusha hali ya dharura sehemu ya ugawaji na ikawa uwepo wa hali hii ni shaka inayotosheleza kuondoa adhabu ya kukatwa mkono mwizi, na hii ni kutanguliza masilahi ya kulinda viungo ambavyo ni sehemu ya makusudio ya kulinda nafsi zaidi ya masilahi ya kulinda mali katika hali hii maalum ([57]).

Hili kwa Omar halikuwa kupinga uhalali wa kutekelezwa adhabu wala kukwamisha Sharia, bali ilikuwa ni ishara ya utekelezaji Sharia kwa masharti yake, na miongoni mwa masharti ya Sharia ni kukumilika hali maalum ikiwa itakosekana hali hiyo basi adhabu haiwezitekelezwa, huu ni mtazamo wa Sharia na wala si vyengine ([58]).

Imamu Ahmad amesema kuwa hakuna kukata mkono wa mwizi ndani ya kipindi cha mwaka wa njaa ([59]), Ibn Qayyim amesema: “Imamu Ahmad amekubali kuondoka adhabu ya kukata mkono katika kipindi cha njaa”. Al-Auzai pia amesema, na hiki ni kipimo na mahitaji ya kanuni za Sharia, kwani mwaka ukiwa ni mwaka wa njaa na shida watu huzidiwa na mahitaji hivyo mwizi hukaribia kwa dharura hii kuhitaji angalau kitakacho ziba njaa yake….na hii ni sehemu ya shaka inayo ondoa adhabu ya kukata mkono kwa mwenye kuhitaji, nayo ni shaka yenye nguvu zaidi kutajwa na Wanachuoni….na mwaka wa njaa huwa wengi sana watu wenye kuhitaji na kutenzwa nguvu, ni vigumu kutenganisha mtu mwenye kujitosheleza na mwizi hivyo kumekuwa na shaka kubwa mwenye kustahiki adhabu na yule asiyestahiki” ([60]).

Hoja hii na sababu hii ya kutotekelezwa adhabu ni sawa sawa ikiwa ni jitihada sahihi au yenye makosa imeendana na usahihi, na sawa sawa tunakubaliana nayo au hatukubaliani nayo, lakini inatulazimisha katika hali zote tuifahamu, na kuelewa ndiyo ambayo imehukumu ufahamu wa wazee walioweka sheria za jinai, ni tofauti kubwa kati ya ufahamu na kujengea.

Majaribio ya sasa katika kutekeleza adhabu na maswali muhimu:

Jambo la pili ambalo ni lazima kusimama kwenye hilo na kufanya utafiti wakati wa kuzungumzia sheria za makosa ya jinai na kadhia ya utekelezaji wa adhabu za Kisharia ni utafiti jaribio kwa nchi zote za sasa za Kiislamu ambazo zimetamka juu ya utekelezaji wa adhabu ni majaribio mawili tu: Jaribio la kwanza ni jaribio la Mamlaka ya Kiarabu ya Saudi Arabia, ambapo hutekelezwa Sharia ya adhabu kwa njia ya moja kwa moja ya mahakama ya Kisharia bila ya kutumia maandiko ya sheria iliyotengenezwa katika sura ya sheria ya adhabu ya kosa la jinai, na utekelezaji wa adhabu wa Saudi Arabia ni jambo linaloendelea, na wala hakuna wito wowote au muelekeo wenye kuathiri ili kufuta Sharia hizo au kuzisimamisha kufanya kazi au kuzigandisha, pamoja na kuwepo baadhi ya miito kutoka kwa wapingaji wa mfumo wa kiutawala wanaotoa wito wa udhibiti wa hatua na kuelezea mfumo wa sasa hauna uadilifu, na kushambulia haki za binadamu.

Jaribio la pili ni hali nchini Pakistani na Sudani na moja ya majimbo nchini Nigeria, Malysia na Irani ambazo sheria yake imeruhusu adhabu za Kisharia, na tayari imesimamishwa utekelezaji wake nchi Pakistani, na imesimamishwa kufanya kazi baada ya utawala wa An-Numairy nchini Sudani, na imesimamishwa kufanya kazi nchini Irani na Malysia, na kufanya kazi ndani ya baadhi ya majimbo nchini Nigeria na kuhamasishwa nchi hizi mbili kufanya kazi adhabu za Tazir “za mtazamo wa hakimu” badala ya kutekeleza Sharia za adhabu, tofauti na uhalifu ambao unalazimisha adhabu ya kunyongwa.

Hapa kunaibuka maswali mengi muhimu:

Ni ipi sababu iliyopelekea kuwepo utulivu katika jaribio la kwanza – Jaribio la Saudi Arabia – na je ni utulivu wa kweli imara?

Na kili kilichopelekea nchi za jaribio la pili kutaja adhabu hii katika sheria zao kinadharia tu bila ya kutekelezwa kivitendo? Je kumewekwa vikwazo? Je sababu ni kukosekana kukamilika masharti ya kufanya kazi Sharia za adhabu? Ikiwa jibu ndio je hili limetokea kwenye adhabu zote ndani ya nchi zote kwa watuhumiwa wote? Au sababu kile kinachotajwa (Hali ya Kimataifa)? Au kumepelekea kwenye utekelezaji wake vitu vilivyofanya wasimamishe kabisa kwa mizani ya masilahi na uharibifu na kutangulizwa kuondolewa kibaya zaidi kati ya viwili?

Je kinachoitwa (Matatizo ya pande nne) ambayo hali hii inapitia – nayo: “Uwepo wa mifumo ya kisiasa iliyojifunga na kandamizi, na mamlaka kidini zimegawanyika, na mahitaji yenye mgongano, wananchi wamekosa elimu na kuchukuliwa kwa kushikamana na kwa dhati na Uislamu, lakini kushikamana kwa hisia na jazba” – kunatengeneza kizuizi cha kweli kwenye kutekeleza adhabu za Kisharia kama vile baadhi ya wanafikra wa sasa wanavyosema?

Ikiwa tutataka kuchukuwa jaribio la kwanza je adhabu hutekelezwa mara moja au kwa awamu katika utekelezaji wake? Na nini maana ya awamu? Na je kuna muda uliozingatiwa au ni jambo tu la uonavyo?

Na je inawezekana kutegemea baadhi ya rai za sasa ambazo zinazungumzia kuhusu adhabu ya kupigwa mawe kuwa inafaa kuwa taazir (rai ya hakimu) na wala sio adhabu, kama Sheikh Mustafa Zarqa anavyosema, kwa upande wa kuiba: Hakima ana hiyari kati ya moja ya mambo matatu: Kutoa adhabu ya kifungo, au kumlipisha mwizi faini na kurudisha alichoiba, na mwisho anaweka kutoa hukumu ya kukata mkono, kama vile Sheikh AbdulMutaal Swaidy anavyosema, kwa upande pia wa kuritadi: Ni kuwa mwenye kuritadi hauliwi bali siku zote atatakiwa kutubia.

Maswali mengine pia yanaelezwa kwenye jaribio la kwanza, miongoni mwa maswali hayo: Je kushindwa masharti ya ushahidi ndio sababu pekee ya kusimamisha utekelezaji wa adhabu katika zama zetu kwa mtazamo wenu? Ni nini ikiwa watashuhudia wengi ambao haiwezekani kuhusishwa na uongo? Ni nini pia ikiwa kuna kukiri ambako hakuhitaji dalili?

Je hukumu zenu kuwa zama za shaka ni sehemu ya kushushwa matatizo sehemu ya kusaidia mahitaji ya watu mpaka kusahau kuwa kwake kipindi cha matatizo na hilo kuwa ni sababu ya kuondolewa adhabu hata kwa upande wa hali zilizopita?

Je sababu ya kupuuza nchi zilizobaki za Kiislamu ambazo zinafika idadi yake nchi hamsini na sita kadhia ya utakelezaji adhabu katika Sharia zake ni kwa vile zama za shaka au kuna sababu nyengine?

Je ni lazima kurekebisha uchumi na kufikia usawa na uadilifu wa kijamii kabla ya utekelezaji wa adhabu za Kisharia kama wanavyodai baadhi ya watu au hili ni uharibifu hauangaliwi?

Maswali yanahitaji majibu na utafiti wa kimaudhui wa kina kutoka kwa watu wenye weledi, ili tuweze kunufaika na haya majaribio yote, na baada ya hapo tuwe na msimamo wa Kisharia wenye matumaini ndani ya wakati wetu wa sasa.

Marekebisho ya Sharia ni kujenga si kubomoa:

Baada ya maelezo hayo kinachobakia ni kusema kuwa si lazima kabisa kauli ya kutekeleza Sharia kwa sura iliyoelezewa kubomoa sharia za sasa hivi na kuanza kutengeneza sheria mpya, kwa sababu sheria za hivi sasa kwa ujumla wake hazitokani na rai iliyonukuliwa kutoka madhehebu ya wanajitihada katika Fiqhi ya Kiislamu, na watengenezaji sheria wamechukuwa muundo wao kutoka muundo wa sheria za Kimagharibi, katika hili sheria haitoki katika kiini mbali na kuwa kwake dhaifu kwenye rai za Wanafiqhi au kuwa na mazingatio mengine ya Kisharia, pindi sheria za mahakama mchanganyiko mahakama za kiraia zilipoondolewa mwaka 1875 na mwaka 1883, na Al-Azhar ikaunda tume ya Wanachuoi wa madhehebu nne ili kuzipitia na ikandaa ripoti iliyoeleza: “Sheria hizi na vipengele vyake ima zikubaliane na maelezo ya moja ya madhehbu nne au zisizipingane na maelezo, au zenyewe zizingatiwe upande wa masilahi yaliyoletwa ambayo inafaa kufanya jitihada kwa kuchunga masilahi ya watu” ([61]).

Jambo la lazima ni kuangalia vipengele ambavyo vinadaiwa kwenda kinyume na Sharia na kufikishwa kwa Wasomi waandamizi wa Sharia, baada ya uamuzi itaangaliwa ikiwa tofauti imethibiti basi vitafanyiwa marekebisho au kubadilishwa kwa vipengele vyengine, mwisho jambo halitahitaji isipokuwa baadhi ya mabadiliko ya Kisharia katika baadhi ya maudhui zinazojadiliwa na bunge – baada ya kurejea kwa Wasomi wa Sharia – sambamba na masilahi ya umma.

Kuna juhudi zilizotangulia katika maswala ya utungaji Sharia inawezekana kunufaika nayo na kurejea, mradi mpya zaidi wa kisheria wa Dr. Swaufy Abi Twalib ambaye aliuanza mwaka 1978 na kutaka msaada wa Jopo la Wanachuoni wa Al-Azhar pamoja na Wasomi sheria haki na wengine mpaka kazi ikakamilika mwaka 1983 na kuchapishwa ndani ya juu saba, na kufikishwa kwenye bunge la wakati huo lakini haikupitishwa.

Makusudio ni kuwa mfumo wenye faida kivitendo ni mfumo wenye kujenga na sio kubomoa, na huo ndio mfumo thabiti, kipindi ilipoundwa tume ya kutengeneza katika mwaka 1923 ilikuwa katika jumla wa wajumbe wake ni pamoja na Mwanachuoni Muhammad Bakhit Al-Mutwii Mufti wa zamani wa Misri, na ilikuwa katika jumla ya maelezo yake yale yaliyokuja katika taarifa fupi ya kikao cha pili kilichokaliwa tarehe 13/4/1922 kauli yake: “Ni sawa sawa katika katiba au sheria za uchaguzi hatujaribu kuunda uzushi ambao haupo katika sheria za kikatiba za mataifa na sheria hizi zote tunazo, tume yetu haitaongeza kazi zaidi ya kurekebisha baadhi ya maandishi yake ili kuendana na nchi yetu” ([62]).

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Na shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu.

 

[1] Kitabu cha Sunani Al-Kubra 10/179 chapa ya Dar Al-Kutubil-Ilmiyah.

[2] Tafasiri ya At-Tawabary 70/22 chapa ya Taasisi ya Risala.

[3] Angalia kitabu cha An-Nihayah cha Ibn Al-Athiir 2/460, chapa ya maktaba ya Al-ilimiyah, pia angalia kitabu cha Taaji Al-Aruusi cha Zaidiy 21/259. 260 chapa ya Daru Al-Hidaya.

[4] Kitabu cha Taaji Al-Aruus 11/292 ukurasa wa 451 chapa ya Taasisi ya Risala.

[5] Kitabu cha utangulizi wa sheria cha Dr. Mahmoud Abdulrahman 1/139 chapa ya Dar An-Nahdha Al-Arabia.

[6] Kitabu cha rufaa ya jinai 24/2/1975, mjumuiko wa hukumu za rufaa 26 ukurasa wa 158.

[7] Kitabu cha Taji Al-Arusa 31/510.

[8] Angalia hilo katika kitabau cha Ghayaatul-Wusuuli cha Sheikh wa Uislamu Zakaria Al-Answary ukurasa wa 6,7 chapa ya Al-Halaby. Na kitabu cha Usuulul-Fiqhi cha Sheikh Zuheir 1/69 – 71 chapa ya Dar Al-Baswair.

[9] Angalia kamusi ya Lisaanu Al-Arabu 3/353, 354. Na kitabu cha Taaji Al-Aruus 9/36.

[10] Imenukuliwa ndani ya kitabu cha Taajul Al-Aruusa 9/36, 37.

[11] Kitabu cha Al-Ibhaaj 3/55.

[12] Angalia kitabu cha Al-Muwafakat 2/8.

[13] Kitabu cha Al-Muwafakati 1/38.

[14] Kitabu cha Al-Muwafikat 2/10, 11.

[15] Angalia kitabu cha Al-Ashbaha wa Nadhahir cha Imamu Suyutwy ukurasa wa 88.

[16] Angalia kitabu cha Burhan 2/924, 925.

[17] Kitabu cha Al-Muwafakati 2/12.

[18] Angalia sherehe ya kitabu cha Kaukabu Al-Muniir 4/167, 168.

[19] Kitabu cha Al-Mustasfy ukurasa wa 174.

[20] Tafasiri ya Twabary 21/512.

[21] Angalia kitabu cha Latwaaif Al-Ishaarat cha Abdul Hamid Qudus ukurasa wa 9 chapa ya Al-Halaby, tafiti katika somo la Usuulu-Fiqhi isiyokuwa ya Imamu Abu Hanifa, kitabu cha Shaikh wetu Marehemu Al-Husainy Yousuf Shaikh ukurasa wa 25.

[22] Sharia: Ni asili ya neno la Kisariani kwa maana ya rura, kisha likahamishwa kwenye kadhia jumla kwa upande ambao hutolewa hukumu ndogondogo wenye kama kakuli ya Watu wa Sarufi ya Lugha: Mtendaji anakuwa na irabu ya dhamma ya Dhumma, na mtendewa anakuwa na Irabu ya fat;ha, na huitwa kadhia hiyo: Asili na Kanuni, na hayo matawi ya hukumu, na kutoa katika asili hizo matawi, kisha yakawa yanatumika na pia kukusudiwa maana iliyotajwa hapo juu, nayo ni maana kuu ya sheria, na ina maana nyengine maalum kwa wasomi wa sheria, nayo ni: Mkusanyiko wa sheria zinazotolewa na mamlaka ya kutunga sheria ndani ya nchi, na sababu ya maana hii kuwa ni maalum ni kuwa utungaji Sharia uliyotajwa haukuwa isipokuwa ni chanzo kimoja cha sheria katika jumla ya vyanzo vengine vingi. Angalia kitabu cha makusudio makuu ya Sharia ukurasa wa 734, utangulizi wa elimu ya sheria ukurasa wa 16.

[23] Amesema ndani ya kamusi ya Al-Wasiitwu 2/550 chapa ya Dar Ad-Daawa: “Utekelezaji ni masuala na kadhia kufuata kanuni za kielimu au kisheria au mfano wake”.

[24] Kitabu cha Minhaaji Al-Wusuul ukurasa wa 60.

[25] Kitabu cha Al-Muwafakati 2/6, 7.

[26] Kitabu cha Al-Mustaswfy ukurasa wa 173, 174.

[27] Kitabu cha Al-Mahsuul cha Imamu Razy 6/162.

[28] Angalia kitabu cha Al-Mahsuul cha Imamu Razy 6/162/163, na kitabu cha Nihayatul-Suul cha Sheikh Bakhit 4/91 – 98, pia kitabu cha Nadharia ya masilahi cha Dr. Hussein Hamid Hassan ukurasa wa 15 – 17.

[29] Kitabu cha Talwiih 2/244,

[30] Kitabu cha Ghayatul-Wusuul ukurasa wa 7.

[31] Kitabu cha Minhaaj Al-Wusuul cha Baidhaqy ukurasa wa 13.

[32] Kitabu cha Tahrir na Tanwiir 1/591 chapa ya Dar Tunisia.

[33] Tafasiri ya Qurani Tukufu 1/565, 566 chapa ya Dar Twiiba.

[34] Kati ya makusudio makuu na sehemu ya maandiko, utafiti uliowasilishwa kwenye kongamano la makusudio ya Sharia kwenye madhehebu ya Kiislamu, taasisi ya Furqan London Mardh 2005 ukurasa wa 4. Kupitia kitabu cha: Nafasi ya makusudio katika Sharia za sasa, kitabu cha Dr. Muhammad Sulaim Al-Awaasw ukurasa wa 14 chapa ya Taasisi ya Furqan kwa ajili ya urithi wa Kiislamu.

[35] 3/11, 12, chapa ya Dar Al-Kutubil-Al-ilmiya.

[36] Kitabu cha Usuulul-Fiqhi cha Sheikh Muhammad Mustafa Shalaby ukurasa wa 297.

[37] Makusudio ya kunyamaza kwa Sharia kitabu cha Dr. Muhammad Sulaim Al-Awaas ukurasa wa 42, chapa ya Taasisi ya Al-Furqan ya urithi wa Kiislamu,

[38] Haya maneno ya Abi Wafaa Ibn Aqiil Ibn Hambaly, ameyanukuu kutoka kwa Ibn Qayyim katika kitabu cha njia za hekima ukurasa wa 12 chapa ya Dar Al-Bayan.

[39] Kitabu cha Nafasi ya makusudio katika Sharia za sasa cha Dr. Muhammad Al-Awaadh ukurasa wa 25.

[40] Ni mtu kuuza kitu anachomiliki kwa malipo ya baadaye, lakini anakinunua sasa hivi kwa bei iliyopo, na ikaitwa uuzaji huu ni uuzaji kitu, kwa sababu mnunuzi wa bidhaa kwa malipo ya baadaye anachukuwa badala yake kitu kwa maana pesa hivi sasa: Angalia kitabu cha Al-Miswbahul-Muniir cha Al-Fayyuumy ukurasa wa 441 chapa ya Maktaba Al-Ilmiya, na angalia kitabu cha Asnaa Matwaalibu cha Sheikh wa Uislamu Sheikh Zakaria 2/41 chapa ya Dar Al-Kutubil-Islaamiy.

[41] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Al-Kaasany 5/199 chapa ya Dar Al-Kutubil-Ilmiya.

[42] Angalia kitabu cha: Al-Miswabaah Al-Muniir ukurasa wa 441.

[43] Kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhwair cha Imamu Suyutwy ukurasa wa 121 chapa ya Dar Al-Kutubil-Ilmiya.

[44] Kitabu cha Al-Furuuku 2/103 chapa ya Aalamul-Kutubi.

[45] 1/215 chapa ya Dar Al-Qalam. Na angalia ukurasa wa 217, ambapo kinaeleza kuwa hilo linapitishwa kwa kutolewa na mkuu wa nchi, akiwa ni mkuu peke yake kwa maana ya (Rais wa nchi) au kundi kwa maana ya (Bunge)

[46] Jambo la kutajwa ni kuwa Ofisi kuu ya Mufti wa Misri imefanya makubaliano mengi ya mashirikiano (Protocol) na Taasisi nyingi na Academi za tafiti za kisayansi mfano: Kituo cha taifa cha tafiti, Chuo Kikuu AinuShams, Ofisi kuu ya vitabu ya Misri, Chuo cha huduma za kijamii, Banki Kuu na taasisi zengine, jambo ambalo linaipa haki Ofisi ya Mufti kunufaika na ushauri wa Taasisi hizi na kunufaika pia na uzoefu wa kielimu na ujuzi pindi unapohitajika, kila upande na weledi wake, na hilo ni kwa ajili ya fat’wa itoke kwa msingi wa kielimu inayojengwa kwa taswara sahihi inayofungamana na hali halisi, ni muhimu kuwa fat’wa inaundika na hukumu ya Kisharia pamoja na hali halisi, inawezekana kutafautiana kwa tofauti za wakati sehemu watu na hali.

[47] Kitabu cha Tajruba Al-Misria cha Sheikh wtu Dr. Ally Jumaa ukurasa wa 35, 36, 37, chapa ya Nahdhwatu Masri, utangulizi uhakiki wa kitabu cha Uinganishi wa utungaji Sharia chapa ya Dar Us-Salaam.

[48] Sheria ya kiraia kazi za maandalizi 1/20, kupitia kitabu cha Mikwamo ya utekelezaji wa Sharia ya Kiisalmu cha Dr. Omar Al-Ashqy ukurasa wa 129 chapa ya Dar Nafaais.

[49] Jarida la Mahakama (Chama ya wanasheria nchini Iraq) toleo la 1, 2 la September mwaka 1962. Kupitia: Jaribio la Misri ukurasa wa 39.

[50] Kitabu cha Jaribio la Kimisri ukurasa wa 38, 41.

[51] Angalia: Kitabu cha Uwiano wa Sharia 1/50, 62.

[52] Kitabu cha Tajruba Al-Masria ukurasa wa 41, 42.

[53] Sunani Al-Baihaqy 8/413.

[54] Kitabu cha Muswannifu cha ibn Abi Shaiba 5/511 chapa ya Maktabatul-Rushdi.

[55] Yamepokewa na Abdulrazak katika kitabu chake 10/242 chapa ya Maktab Al-Islaamy kutoka kwa Yahya Ibn Abi Kathiir.

[56] Imepokelewa na Abu Nuaim katika kitabu cha Historia ya Aswbahan 1/375 chapa ya Dar Al-Kutubil-Ilmiya kutoka kwa Abi Amama Al-Baahily.

[57] Ni utafiti wa Uzamili kitengo cha masomo ya Sharia ya Kiislamu kitivo cha masomo ya haki Chuo Kikuu Alexandria.

[58] Kitabu cha Jaribio la Kimisri ukurasa wa 42.

[59] Kitabu cha Al-Inswaaf cha Mardawey 10/277 chapa ya Dar Ihyaau Turaath Al-Araby.

[60] Kitabu cha Iilaam Al-Muwaqiina 3/17.18.

[61] Mifumo ya hukumu na utawala katika Sharia ya Kiislamu na sheria za kuwekwa ukurasa wa 18, 19. Kupitia vikwazo vya utekelezaji Sharia Dr. Al-Ashqar ukurasa wa 127.

[62] Kitabu cha: Dini na nchi…jaribio la Kimisri cha Dr. Al-Awas ukurasa wa 7.

Share this:

Related Fatwas