Kuituhumu jamii kuwa ni jamii ya Ja...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuituhumu jamii kuwa ni jamii ya Jahiliya (Upotofu)

Question

Je, kuwepo kwa baadhi ya makosa na maasi katika jamii fulani ni sababu ya kuituhumu jamii hiyo kuwa ni jamii ya Jahiliya (Upotofu)?

Answer

Makundi ya kigaidi yalitumia dhana ya jahiliya katika maandishi yao wakikusudia sifa ya kukufuru kwa umma kwa ujumla na hasa wasiowafuata, hiyo ndiyo dalili kuu ya upotofu wa fikra za watu hao, ambapo wanatumia dhana hii kwa kuashiria jamii isiyoendana na fikra zao bila ya kujali msimamo wa jamii yenyewe kutokana na masuala ya imani, jambo ambalo halikubaliki kwa wataalamu wa Waislamu hata kidogo isipokuwa wafuasi wa makundi haya, na ukweli ni kwamba Uislamu ni imani iliyo thabiti na imara isiyoondolewa kwa maasi na maovu, bali uelewa huu ni kinyume na yaliyokuja nayo Qur`ani na Sunna, Mwenyezi Mungu Amesema: "Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote" [Az-Zumar: 53], na: "Na anayetenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu" [An-Nisaa: 110], naye Mtume amesema katika Hadithi nyingine: "Mambo matatu ni miongoni mwa misingi ya Imani; kutomuudhi anaye kariri kuwa hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, kutomhukumu ukafiri kwa dhambi, wala kutomhukumu kutoka kweye Uislamu kwa kitendo fulani" [Imesimuliwa na Abu Dawood], kwa hiyo haikubaliki kabisa kuzituhumu jamii za kiislamu kwa ukafiri (jahiliya) kwa baadhi ya madhambi na maovu yaliyopo katika jamii husika, bali kufanya hivyo hupinga mafundisho ya Sharia.

Share this:

Related Fatwas