Kuruhusu Jiahadi inakusudiwa binafs...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuruhusu Jiahadi inakusudiwa binafsi au ni njia ya kufikia mambo mengine

Question

Je, kuruhusu Jiahadi inakusudiwa binafsi au ni njia ya kufikia mambo mengine?

Answer

Kusudio la kuruhusu Jihadi si kwa ajili ya kuruhusu mapigano, bali ni kwa ajili ya kuwa njia mojawapo njia na mbinu za kuzuia uadui na kujikinga na udhalimu na uadui dhidi ya umma, bila ya kujali sababu na visingizio vya uadui huo ikiwa ni dini au kupora mali zake, kwa hiyo tunaona Aya nyingi za Qur'ani Tukufu zilizotaja hukumu ya Jihadi zilitaja wazi sababu ya kuruhusu Jihadi, mfano wa hayo kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote} [At-Tawbah: 36], sababu ya kuruhusu mapigano kwa mujibu wa Aya hii ni kujibu na kuzuia uadui, kwa hivyo washirikina wasingaliwavamia waislamu zama ya Mtume (S.A.W.) Mwenyezi Mungu Asingaliagiza Waislamu kufanya Jihadi, kwa kuwa Jihadi ndiyo njia ya kuzuia dhuluma, lakini dhuluma haikuwepo, hivyo ndivyo maana ya kwamba Jihadi ni wajibu kwa namna ya kuwa njia siyo lengo lenyewe, kama ilivyo kuondoa udhalimu na kusimamisha uadilifu, kinyume na hayo, magaidi wanadhani kuwa Jihadi ni wajibu pasipo na sababu maalumu, hivyo kwa mujibu wa mtazamo wao huu, basi Muislamu anatakiwa kuwa katika vita muda wote!

Share this:

Related Fatwas