Baadhi ya sifa za makundi potofu kama yalivyotajwa katika Sunna za Mtume
Question
Je, Sunna za Mtume zimezungumzia sifa za makundi ya Khawariji na wenye fikra potofu?
Answer
Kwa hakika, Sunna za Mtume imezungumzia kijumla kuhusu baadhi ya sifa ambazo zikipatikana kwa watu huwa alama ya kumwelekeza muumini awe na tahadhari nao na kutowafuata, kwa kuwa watu wenye sifa hizo huwa wenye fikra potofu walio mbali na mafunzo ya dini, katika Hadithi iliyosimuliwa na Abi Idriis Al-Khawlany kuwa amemsikia Hudhaifa Bin Al-Yaman akisema: "watu walikuwa wakimmuliza Mtume (S.A.W.) kuhusu heri, lakini mimi nilikuwa namuuliza kuhusu shari kuhofia kupatwa nayo, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika tulikuwa katika zama za ujahili iliyo na shari nyingi, Mwenyezi Mungu Akatuletea heri hiyo, Je, inawezekana kupatikana shari baada ya heri tuliyo nayo?! Akasema Mtume: Ndiyo, tena inayo fitina kubwa, nikamuuliza: fitina ipi? Akasema: Watu watafuata sunna ambayo si sunna yangu, na kuongoka kwa uongofu ambao si wangu, unaweza kuwatambua na kuwakataa, nikasema: Je, baada ya heri hiyo huwa shari? Akasema: Ndiyo, watu wanaowavuta wengine kuangamizwa motoni yeyote atakaewajibu hutupwa motoni, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tafadhali tubainishie, akasema: ni watu miongoni mwetu wanaozungumza maneno yetu, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nisihi nifanyaje nikiwapata?! Akasema Mtume: uwe na jamaa ya Waislamu na Imamu wao, nikasema: Je, Waislamu wa wakati huo wakiwa hawana Imamu na jamaa, nifanyaje? Akasema Mtume: Basi jiepushe na makundi haya yote hata ukikosa njia zote isipokuwa kushikilia mzizi wa mti mpaka ufe, basi fanya hivyo" Imekubaliwa na wote.
Maana ya fitina hapa ni kutoongoka uongofu sahihi unaozingatiwa katika dini, kwa sababu ya kuchanganyika kwa yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, kama ilivyo katika kauli yake Mtume (S.A.W.): "watu huwa wanafuata sunna ambayo si sunna yangu, na kuongoka kwa uongofu ambao si wangu, unaweza kuwatambua na kuwakataa" kwa maana ya kukataa wanayoyafanya wakidai kuwa hayo ndiyo dini.