Hukumu Zinazohusiana Na Utoaji Mimb...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu Zinazohusiana Na Utoaji Mimba

Question

Hukumu Zinazohusiana Na Utoaji Mimba

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na swala na salamu zimshukie Bwana wetu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na waliomfuata, na baada ya hayo...

Suala la kuhifadhi kizazi ni miongoni mwa makusudio makuu ya Sharia yaliyoamrishwa kuhifadhiwa, ili jamii ya wanadamu iendelee kuwepo, kuujenga ulimwengu, na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Miongoni mwa njia za kuhifadhi kizazi ni: Kuhifadhi roho ya mwanadamu katika kila hatua ya kuumbwa kwake, na kutokiuka, na hatua ya kwanza kati ya hizi ni kuwa bado ni mtoto mchanga ndani ya tumbo la mama yake.

Na kwa kuzingatia hali halisi inayobadilika tunayoishi, na kuibuka kwa mielekeo inayoudai uhuru wa mwanawake – katika wakati wowote na chini ya kivuli chochote – wa kutoa mimba yake; kwa kuzingatia kwamba ana uhuru kamili katika hali hii, na pamoja na udhaifu wa dhamira ya kidini na ya kimaadili katika mioyo ya watu, yote haya na mengine yalilazimu ushiriki kwa kueleza baadhi ya hukumu za kisheria zinazohusiana na utoaji mimba katika utafiti huu mdogo.

Utafiti huu unahusika na utoaji mimba wa hiyari unaotokea kwa kutaka mwanamke mjamzito mwenyewe, au kwa kitendo cha wengine kutokana na ombi lake au kwa ridhaa yake. Ama utoaji mimba wa kulazimishwa au wa papo hapo unaotokea kwa sababu ya maradhi, haukufafanuliwa kuwa halali au haramu. Kwa sababu hakuna mtu anayehusikana katika hilo, na vivyo hivyo kutoa mimba kwa wengine kwa sababu ya uadui dhidi yake hakuna uhusiano wowote hapa; Kwa sababu hakuna tofauti juu ya uharamu wake na kustahiki adhabu na faini kutokana na uadui.

Tumeugawanya utafiti huu katika utangulizi, dibaji, sura tatu na hitimisho.

Katika utangulizi kuna: Kutaja umuhimu wa suala, kuhariri mada ya utafiti, na kuelezea mbinu ya kuandika.

Dibaji inajumuisha mambo mawili: ya kwanza: ufafanuzi wa utoaji mimba, na ya pili: ni wakati gani roho inapulizwa ndani ya kiinitete?

Sura ya kwanza anuani yake ni: Hukumu ya kutoa mimba baada ya roho kupulizwa.

Sura ya pili inaitwa: Hukumu ya kutoa mimba kabla ya roho kupulizwa bila ya udhuru, nayo ina sehemu mbili: ya kwanza: katika Madhehebu za Wanachuoni kuhusu kutoa mimba kabla ya roho kupulizwa bila ya udhuru, na ya pili: Katika ushahidi wa Madhehebu na majadiliano yao, na uzito wa ushahidi huu.

Sura ya tatu ina anuani: Hukumu ya kutoa mimba kwa udhuru, nayo ina sehemu tatu: ya kwanza: kutoa mimba kutokana na uzinzi, ya pili: Kutoa mimba kwa mwanamke aliyebakwa, na ya tatu: Utoaji mimba wa kijusi kilichoharibika.

Kisha hitimisho, ambalo lilijumuisha matokeo muhimu zaidi ambayo tulifikia mwishoni mwa utafiti, na orodha ya marejeleo.

Katika utafiti wetu, tuliegemea katika kusambaza Madhehebu na rai na kuzihusisha na wenye rai hizi juu ya vitabu vilivyoidhinishwa, na vile vile utafiti wa kisasa juu ya suala hilo, kwa kufuata mbinu ya kisayansi katika kutaja na kujadili ushahidi na vipengele vya ushahidi, kwa kuzihusisha Aya tukufu, na kuzitoa Hadithi tukufu za Mtume kutoka katika mitazamo yao sahihi.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu, Mkarimu, atuongoze kwenye njia iliyo sawa, na Abariki utafiti huu na uwe na manufaa.

Dibaji:

Dibaji ina masuala mawili: Kwanza ni: Maana ya utoaji mimba, ya pili: Ni wakati gani roho hupuliziwa ndani ya kiinitete?

Ya Kwanza: Maana ya utoaji mimba:

Utoaji mimba katika lugha ni kutoa mimba, nayo ni kuondolewa kwa haraka kwa kitu kutoka mahali pake. Husemwa tumemtoa mtu kwenye kitu, yaani tumemtenga kwa kutumia nguvu na kitu hicho. Ngamia alitoa mimba ikiwa alimtupa mtoto wake.

Katika kitabu kiitwacho Al-Misbah Al-Munir: “Mwanamke alitoa mimba, akamtoa bila ya kukamilika umbaji.

Na tukiangalia maana ya kutoa mimba katika istilahi, tunakuta kwamba Wanachuoni wa Fiqhi wanatumia neno hilo la kutoa mimba kwa maana ile ile iliyotajwa katika lugha. Husemwa kuwa: Kutoa mimba ni kuondoa mimba kabla ya kumaliza kipindi cha ujauzito.

Mara nyingi huelezwa utoaji mimba kwa visawe vyake: Kama vile kuharibika kwa mimba, na kuzaa mtoto aliyekufa.

Ya Pili: Ni wakati gani roho hupuliziwa ndani ya kiinitete?

Wanachuoni wa Fiqhi waliamua kwamba roho inapaswa kupuliziwa ndani ya kiinitete baada ya siku mia moja na ishirini. Na hilo linatokana na Hadithi Sahihi iliyopokelewa kutoka kwa Abdullah. Ambapo amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa ametusimulia: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika riziki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), matendo yake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘matendo ya watu wa Peponi hadi ikawa baina yake na Pepo ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘matendo ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘matendo ya watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘matendo ya watu wa Peponi akaingia Peponi”.

Ilipokelewa katika Hadhithi nyingine inayoonekana kupingana na Hadithi hii iliyotajwa hapo awali kutoka kwa Hudhaifah Ibn Usayd Al-Ghifari amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akisema: “Kikifikia kizazi (mimba) siku arubaini na mbili, Mwenyezi Mungu Mtukufu anakitumia Malaika, akakitia sura, na akaumba masikio yake na macho yake na ngozi yake na nyama yake na mifupa yake (kwa amri ya Mola wake), kisha husema (Malaika): “Ewe Mola wangu! (Jee! Huyu atakuwa) mwanamume au mwanamke?” Akakimalizia Mola wako anavyopenda na Malaika akaandika. Kisha husema (Malaika): “Lini Mola wangu! (Jee! Wakati gani itakuwa) ajali yake? Akamwambia Mola wako anavyopenda na Malaika akaandika. Tena husema (Malaika) “Vipi Mola wangu! (Jee! Itakuwaje) riziki yake? Akamhukumu Mola wako anavyotaka na Malaika akaandika.” Kisha Malaika hutoka na kitabu cha matendo yake mkononi mwake na wala hawezi kuongeza zaidi ya yaliyoamirishwa wala hapunguzi”.

Katika Hadithi ya kwanza, kuna taarifa kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humtuma Malaika baada ya siku mia moja na ishirini, na katika Hadithi ya pili, kuna kauli kwamba Malaika hutumwa baada ya siku arubaini, basi Hadithi hizi mbili zinawezaje kuunganishwa?

Imamu Ibn As-Swalah akajibu hivi na kusema:

Malaika hutumwa zaidi ya mara moja kwenye tumbo la uzazi. Hutumwa mara moja baada ya siku arubaini za mwanzo, kwa mujibu wa ushahidi wa Hadithi ya Hudhaifah Ibn Usayd, pamoja na maneno yake katika mapokezi yake ambayo ni mengi, hivyo anaandika riziki yake, ajali yake (muda wake wa kuishi), matendo yake, hali yake katika uovu au wema, na kadhalika. Kisha Malaika hutumwa baada ya siku arubaini ya pili, basi humpulizia roho kwa mujibu wa ushahidi wa Hadithi ya Ibn Masuod na Hadithi nyingine, kisha inapingana na Hadithi ya Hudhaifah aliposema katika baadhi ya mapokezi yake alipotaja kutumwa kwa Malaika baada ya siku arubaini za mwanzo: “akakitia sura, na akaumba masikio yake na macho yake na ngozi yake na nyama yake na mifupa yake (kwa amri ya Mola wake), kisha husema (Malaika): “Ewe Mola wangu! (Jee! Huyu atakuwa) mwanamume au mwanamke?”

Akakimalizia Mola wako anavyopenda na Malaika akaandika...mpaka mwisho wa Hadithi hiyo. Inajulikana kuwa umbo hilo haliwi katika siku ya arubaini ya pili; Kwani huwa ni donge la damu katika siku hizi, lakini umbo hilo liko karibu na kipindi cha kumpulizia roho, na hivyo tukaeleza kwa uwazi katika baadhi ya mapokezi ya Hadithi za Hudhaifah mbali na Hadithi Sahihi.

 Na namna ya kujibu mkanganyiko huu ni: kuwa na maana ya usemi wake: “akakitia sura” kwa maana ya kukitia sura kwa maneno na maandishi, si kwa vitendo, yaani akataja kukitia sura na akaandika hivyo. Na dalili ya usahihi wa jambo hili ni kuwa kuumbwa mwanamume au mwanamke ni pamoja na sura zilizotangulia, na akasema kuhusu kuumbwa kwake kuwa mwanamume au mwanamke: “Basi Mola wako Mlezi akakimalizia anavyopenda na Malaika akaandika … mpaka mwisho wa Hadithi hii”

Vile vile kunatofauti kutoka katika Hadithi ya Ibn Masoud kwamba imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kwa maneno haya, ambayo ni: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). 

Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika riziki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), matendo yake, mtu muovu au mwema, basi roho hupuliziwa ndani yake.” Basi kauli yake: “Kisha Malaika hutumwa kwake” kwa kutumia neno kisha ambalo lina maana ya kuchelewesha kwa kuandika mambo manne mpaka baada ya siku arubaini ya tatu, na Hadithi ya Hudhaifah Ibn Usayd inahukumu kwamba Malaika anaandika mambo hayo baada ya siku arubaini ya mwanzo.” Njia ya kutoka kwa mkanganyiko huo ni: kufanya kauli yake: “Kisha Malaika hutumwa kwake, naye anaamrishwa, naye huandika” inaambatanishwa na kauli yake: “Hukusanywa umbo lake ndani ya tumbo la mama yake siku arubaini” kama hilo katika kauli yake Mwenyezi Mungu, {Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi * Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.} (AR RUUM: 17, 18).

Imamu al-Nawawiy amesema: “Kauli yake: “Kisha hutumwa Malaika” Inaonekana kuashiria kwamba kutumwa kwake kutatokea baada ya siku mia moja na ishirini. Katika mapokezi mengine yanayofuatia hayo, Malaika anaingia kwenye tone baada ya kukaa tumboni kwa siku arubaini au arubaini na tano, akisema: Ewe Mola Mlezi, ni muovu au ni mwema? Na katika mapokezi ya tatu: “Tone lilipopita siku arubaini na mbili, Mwenyezi Mungu humpelekea Malaika akakitia sura na akaumba masikio yake, macho yake na ngozi yake.” Na katika mapokezi ya Hudhayfah Ibn Usayd: “Hakika tone hukaa tumboni kwa siku arubaini, kisha Malaika huikabidhi.”

Katika mapokezi mengine: “Malaika ambaye kazi yake ni shughuli za uzazi ikiwa Mwenyezi Mungu akipenda huumba kitu, kwa karibu zaidi ya siku arubaini.” Na akataja Hadithi hiyo, na katika mapokezi ya Anas: “Mwenyezi Mungu Amemtuma Malaika, hivyo anasema: Ewe Mola Mlezi tone, Ewe Mola Mlezi pande la damu, Ewe Mola Mlezi kipande cha nyama. Wanachuoni walisema: Njia ya kuunganisha mapokezi hayo yote ni kwamba Malaika ana wajibu wa kuzingatia hali ya tone, na kwamba husema, "Ewe Mola, hili ni pande la damu, hiki ni kipande cha nyama" kwa wakati wake uliowekwa. Kila wakati anaposema yaliyompata kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Anajua zaidi, Malaika ana maneno yake na mwenendo wake katika kila wakati; Nayo ni kwamba:

Mwenyezi Mungu anapoumba tone kisha kuwa donge la damu, ambalo ni elimu ya kwanza ya Malaika kwamba huyo ni kiinitete; Kwa sababu si kila tone inakuwa kiinitete, na hiyo ni baada ya siku arubaini ya kwanza, na wakati huo riziki yake, muda wake wa maisha yake, kazi yake, uovu wake, au wema wake huandikwa, basi Malaika ana mwenendo mwingine katika wakati mwingine, ambao ni kukitia sura na kuumba masikio yake, macho yake, ngozi yake, nyama yake, mifupa yake, na kwamba ni mwanamume au mwanamke.

Hivyo ni katika siku ya arubaini ya tatu, nao ni muda wa kuwa pande la nyama na kabla ya kupitia siku hizi arubaini, pia kabla ya kupuliziwa roho ndani yake; Kwa sababu hali ya kupuliziwa roho haitokei mpaka baada ya kukamilika sura yake, na kuhusu kauli yake katika mojawapo ya mapokezi: “Kama tone ikipitia muda wa usiku wa arubaini na mbili, Mwenyezi Mungu humpeleka Malaika, naye akaitia sura yake, kuumba masikio yake, macho yake, ngozi yake, nyama na mifupa yake, kisha akasema: “Ewe Mola, Jee huyo ni mwanamume au mwanamke?” Kisha Mola wako Mlezi husema anachotaka na Malaika hukiandika, Kisha akasema: “Ee Mola Mlezi, muda wake katika maisha, Kisha Mola wako Mlezi husema anachotaka na Malaika hukiandika. Na akataja riziki yake pia. Al-Qadhi na wengineo wakasema: Hadithi hii haiko kwa hakika yake na wala si sahihi kuifahamu kwa hakika yake.

Kwa sababu hali ya kutia sura baada ya siku arubaini ya kwanza haipatikani kwa kawaida, lakini hufanyika katika siku ya arubaini ya tatu, ambayo ni kipindi cha kuwa donge la nyama, kama Mwenyezi Mungu alivyosema: {Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo (12) Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti (13) Kisha tukaumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaimba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji (14)} [AL MU'MINUUN:12-14].

Kisha Malaika ana taswira nyingine, nao ni wakati wa kupulizwa roho baada ya siku arubaini ya tatu anapokamilisha miezi minne. Wanachuoni wameafikiana kuwa hali ya kupulizwa roho haikutokei mpaka baada ya miezi minne, na ikatokea katika mapokezi ya Al-Bukhari: ““Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake. Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika riziki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), matendo yake, mtu muovu au mwema. Kisha hupuliziwa roho (yake)”.

  Al-Qadhi na wengineo wakasema: Kinachokusudiwa kwa kumtuma Malaika katika mambo haya ni amri yake kwao na kutenda vitendo hivi. Vinginevyo, imetajwa katika Hadithi kwamba Malaika ambaye kazi yake ni shughuli za uzazi na kwamba anasema: Ewe Mola Mlezi, tone la damu, Ewe Mola Mlezi, pande la damu”. Al-Qadhi amesema: Na kauli yake katika Hadithi ya Anas: “Na Mwenyezi Mungu akitaka kuhukumu kuumba, husema: Ewe Mola Mlezi, mwanamume au mwanamke?”

Haipingani na yale tuliyowasilisha, na sio lazima kwake kusema kwamba hivyo ni baada ya kipande cha nyama, lakini ni mwanzo wa maneno na kuelezea kuhusu hali nyingine, kwa hivyo akaeleza mwanzoni hali ya Malaika pamoja na tone, kisha akaeleza kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kuonesha uumbaji wa tone kama ni donge la damu, ni hivi na hivi, halafu kinachomaanishwa na yale yote yaliyotajwa ya riziki, muda wa maisha yake, uovu, wema, matendo, uume na uke, hali hii inadhihiri kwa Malaika na kumwamuru kutekeleza na kuandika. Vinginevyo, Hukumu ya Mwenyezi Mungu imetangulia hapo, na ujuzi Wake na mapenzi Yake kwa hayo yote yalikuwepo katika umilele, na Mwenyezi Mungu ndiye Anajua Zaidi.”

Sura ya Kwanza:

Hukumu ya Utoaji Mimba Baada ya Roho Kupulizwa

Hakuna tofauti yoyote baina ya Wanachuoni wa Fiqhi kuhusu uharamu wa kutoa mimba baada ya roho kupulizwa. Wao Walikubaliana kwa kauli moja kwamba utoaji mimba baada ya roho kupulizwa ndani ya kiinitete ni haramu. Na wakasema: kuwa hali hii ni kuua bila kutofautiana.

Katika kitabu cha Haashiyat Ibn Abidin, kimojawapo cha vitabu vya Imamu Hanafi, amemnukuu kutoka kwa Al-Dhakhira: “Mwanamke akitaka kutoa maji ya uzazi baada ya kufika katika tumbo la uzazi, walisema: Muda wa kupulizwa roho ukipita, haijuzu kwake, na kabla ya kipindi hicho Mashekhe wametofautiana juu yake, na kupulizwa kunakadiriwa kuwa siku mia moja na ishirini kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume (S.A.W)”.

Na kinachoidhinishwa na madhehebu ya Imamu Malik ni kwamba kutoa mimba ni haramu kabisa kabla ya kupulizwa roho, na hiyo ni moja kwa moja baada ya tumbo la uzazi hushika manii, hivyo ni jambo la kipaumbele uharamu baada ya kupulizwa roho.

Imeelezwa katika vitabu vyao: “Hairuhusiwi kutoa manii yalioko katika tumbo la uzazi, hata kabla ya siku arubaini, na ikiwa roho imepuliziwa ndani yake, ni haramu kwa maafikiano”.

Ibn Jazi anasema katika Sharia za kifiqhi: “Ikiwa tumbo la uzazi likishika manii, haijuzu kuyagusa, na mbaya zaidi yatakapo jiumba, na mbaya zaidi kuliko hilo ikipuliziwa roho ndani yake, basi ni kuiua nafsi kwa kauli moja”.

Katika vitabu vya mabwana watukufu wa Imamu Shafi, tunapata kwamba walisema: Rai ambayo ni sahihi kabisa ni uharamu wa kutoa mimba baada ya kupuliziwa roho.

Na Sheikh Al-Ramli anasema katika kitabu cha Nihayatul Muhtaj: “Ama kuhusu hali ya kupulizwa roho na kipindi kinachofuata mpaka kuzaa, hakuna shaka juu ya uharamu”.

Sikuona katika vitabu vya Imamu Ibn Hanbal katazo la wazi la kutoa mimba baada ya siku mia moja na ishirini, na huu ni wakati wa kupulizwa roho. Hata hivyo, kauli yao ya kuruhusiwa kutoa mimba katika kipindi cha tone bila ya vipindi vilivyo baada yake, hata ikiwa ni kabla ya kupulizwa roho, inafahamika kutokana nayo kuwa ni uharamu wa kutoa mimba baada ya kupulizwa roho na hivyo ni hali ya kipaumbele.

Katika maelezo ya kitabu cha Al-Muntaha cha Al-Bahwati: “(Inaruhusiwa kwa mwanamume kunywa dawa iliyo halali inayozuia kujamiiana) kama kafuri, kwa sababu ni haki yake (na halali pia kwa mwanamke kuinywa kwa kuondoa manii na kupata hedhi), kwa kuwa kikanuni asili ni halali mpaka ipokelewe hukumu ya kuharamisha, na wala haikupokelewa hukumu ya uharamu.”

Kwa hivyo, kutoa mimba baada ya kupulizwa roho ni haramu kwa mujibu wa Sharia. Hayo ni kwa sababu inahesabika kuwa ni kuua nafsi kwa dhulma, na Mwenyezi Mungu amesema: {Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki.} [AL AN'AAM: 151] na kiinitete kilichomo ndani yake roho imepuliziwa na kimekuwa nafsi, kwa hivyo hairuhusiwi kuishambulia nafsi hiyo.

Isipokuwa katika hali moja tu ambapo utoaji mimba unaruhusiwa baada ya kupulizwa roho, ambayo ni kesi ya kutoa mimba kwa dharura. Ili kuhifadhi maisha ya mama kutokana na hatari halisi ya kuishi kwa ujauzito. Ambapo maisha ya mama yawe katika upande wa mizani na maisha ya kiinitete yawe katika upande mwingine wa mizani, hivyo kuna ubora wa kuhifadhi maisha ya mama; Kwa sababu maisha yake ni ya hakika na yamethibitishwa mbele yetu, tofauti na kiinitete.

Kuhusiana na hili, Sheikh Mahmoud Shaltut anasema: “Ikithibitika kutoka kwenye njia ya kuaminika kwamba kuishi kwake (yaani kwa kiinitete) baada ya utambuzi wa uhai wake (yaani baada ya miezi minne kupita tangu mwanzo wa ujauzito) bila shaka husababisha kifo cha mama, basi Sharia ya Kiislamu pamoja na kanuni zake za jumla inaamrisha kufanya madhara madogo.” Ikiwa kuishi kwa kiinitete ni kifo cha mama, na hana njia ila ni kutoa mimba yake, basi kutoa mimba yake katika hali hiyo ni maalumu na wala haifai kumtoa mhanga kwa ajili ya kukiokoa kiinitete, kwa sababu mama yake ndiye asili yake, na maisha yake yametulia, na ana bahati ya kujitegemea katika maisha, na ana haki na wajibu, na baada ya haya yeye ndiye nguzo ya familia, na si jambo la busara kumtoa mhanga kwa ajili ya uhai wa kiinitete ambao haukujitegemea, na haukupata haki wala wajibu wowote”.

Kwa hivyo, inakuwa wazi kuwa utoaji mimba unaruhusiwa kwa ajili ya kuhifadhi maisha au afya ya mama, chini ya masharti yafuatayo:

1- Kuwepo kwa ulazima wa utoaji mimba, kama vile kuishi kwa kiinitete ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke kunatishia maisha ya mama yake au kudhuru afya yake kwa dhahiri, madhara makubwa ambayo hayawezi kustahimili mpaka wakati wa kujifungua, na hali hii haiwezi isipokuwa kwa kutoa mimba.

2- Kuthibitisha kuwepo kwa ulazima huu kwa njia ya kuaminika, kwa hivyo sio udanganyifu.

3- Kuamua ulazima wa kutoa mimba ili kuokoa maisha ya mama au kuhifadhi afya yake, angalau madaktari wawili wazuri na wenye ujuzi wa Kiislamu.

Lakini ikiwa hakuna dharura ya kweli kwa hili, bali ni dharura ya kudhaniwa, basi hairuhusiwi kumdhuru kiinitete.

Sura ya Pili:

Hukumu ya Kutoa Mimba Kabla ya Kupulizwa Roho Bila ya Udhuru

Mada ya kwanza:

Madhehebu ya wanazuoni kuhusu kutoa mimba kabla ya kupulizwa roho bila udhuru.

Wanachuoni wa Fiqhi walitofautiana kuhusiana na hukumu ya kutoa mimba kabla ya kupulizwa roho kwa mujibu wa Madhehebu yafuatayo:

Madhehebu ya kwanza:

Yameharamisha kabisa kutoa mimba tangu mwanzo wa kurutubishwa na kuingia katika tumbo la uzazi, na hairuhusiwi kutoa manii baada ya kutulia ndani ya tumbo la uzazi. Kwa sababu yanaelekea katika kutunga mimba.

Hii inaungwa mkono na Madhehebu ya Imamu Malik. Katika Al-Sharh Al-Kabiir cha Sheikh Al-Dardir: “Hairuhusiwi kutoa manii yaliopo katika tumbo la uzazi hata kabla ya siku arubaini, na ikiwa roho itapuliziwa ndani yake, ni haramu kwa maafikiano.”

Sheikh Al-Dusouki alisema katika maelezo yake ya chini kwa maelezo yaliyotangulia: “(Kauli yake: hata kabla ya siku arubaini) haya ndiyo yaliyokubaliwa”.

Haya ni maneno ya mwanasheria Ali Ibn Musa kutoka Madhehebu ya Imam Abu Hanifa. Katika Haashiyat Ibn Abidin: “Na imepokelewa kutoka kwa Al-Dhakhira kwamba mwanamke akitaka kutoa mimba kabla ya muda ambao roho imepuliziwa ndani yake inajuzu kwake kufanya hivyo au la?

Wanazuoni wametofautiana juu ya hilo, na mwanasheria Ali Ibn Musa alikuwa akisema: Inachukiza hivyo, kwa sababu maji ya uzazi baada ya kutumbukia tumboni yamekusudiwa uhai, hivyo yana hukumu ya uhai, kama katika yai lililokamatwa kwenye pahala patakatifu.

Na kuchukiza hapa ni kuharamisha, kama ilivyo wazi kutoka kwa hoja. Hii ndiyo rai ambayo ni sahihi zaidi kwa mujibu wa Ibn Hajar Al-Haytami kutoka kwa Wanazuoni wa Shafi - kama katika Al-Tuhfa, na itakuja baadae -; Kwa sababu tone, baada ya kukaa, huwa na sura ambayo ni tayari kwa kupulizwa roho.

Ni kauli ya Imamu Al-Ghazali, na Ibn Al-Imad pia kutoka kwa wanazuoni wa Shafi.

Imam Al-Ghazali katika kitabu cha Al-Ihyaa anasema baada ya kutaja uhalali wa kutoa manii nje, amesema: “Hili – yaani kutoa manii nje – si sawa na kutoa mimba, kwa sababu suala hilo ni uhalifu dhidi ya kiumbe kilichopo, na pia ina viwango, na viwango vya kwanza vya kuwepo ni kwamba manii hufika tumboni na kuchanganyika na maji ya uzazi ya mwanamke na kujiandaa kupokea uhai na kuiharibu hali hiyo ni jinai. Iwapo likiwa pande la damu na donge la nyama, basi hivyo ni jinai kubwa zaidi, na ikiwa roho ikipuliziwa ndani yake na sura ilikuwa sawa, basi jinai huzidi ukubwa wake zaidi, na uchafu mkubwa zaidi katika uhalifu huu baada ya kutengana donge la nyama lililo hai”.

Na imekuja katika kitabu cha Tuhfat Al-Muhtaaj msisitizo wa maneno ya Al-Ghazali: “Na katika kitabu cha Al-Ihyaa katika mada ya kutengwa kuna dalili kwamba ni haramu suala hilo, na rai hii ni sahihi zaidi; kwa sababu baada ya kutulia kwa tone, inaongoza kwenye kuumbwa ambako huko tayari kupulizwa roho, na wala sio kutengwa

Na ikatajwa katika kitabu cha At-Tuhfa pia: “Na wametofautiana katika kusababisha kutoa mimba ambayo haikufikia kikomo cha kupulizwa roho ndani yake, nayo ni siku mia moja na ishirini, na hukumu yake ni haramu kwa mujibu wa Ibn Al-Imad na wengineo kutokiuka”, Vile vile Ibn Al-Jawzi na Ibn Taymiyyah kutoka kwa Hanbali wamesema hivyo.

Al-Mardaawiy ametaja katika kitabu cha Al-Insaf kutoka kwa Ibn Al-Jawzi kuwa ni haramu suala hilo ambapo amesema: “Inajuzu kunywa dawa ya kutoa manii, akaitaja katika kitabu cha Al-Wajiyz, na akawasilisha hivyo katika Al-Furu'. Pia Ibn Al-Jawzi amesema katika hukumu za wanawake kwamba suala hilo ni haramu”.

Ibn Taymiyyah anasema: “Kutoa mimba ni haramu kwa maafikiano ya Waislamu, na ni sehemu ya mauwaji ambayo Mwenyezi Mungu amesema juu yake: {Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa (8) Kwa kosa gani aliuliwa? (9)} [AT-TAKWEER: 8,9], Vile vile Mwenyezi Mungu amesema: {Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini} [AL-ISRAA:31]”.

Na aliyesema haya miongoni mwa Wanachuoni wa Fiqhi kuzuia utoaji mimba baada ya kuwa donge la damu na pande la nyama.

Madhehebu ya pili:

Inaruhusiwa kutoa tone kabla ya kuwa donge la damu na pande la nyama.

Rai hii ndiyo iliyofuatwa na Wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal; ambapo waliruhusu mwanamke kunywa dawa ya halali ili kutoa tone siyo pande la nyama, kwa hiyo katika kitabu cha Muntaha Al-Iradat na maelezo yake kwa Al-Bahwati: “(Na inaruhusiwa kwa mwanamme kunywa dawa ya halali inayozuia kujamiiana) kama kafuri, kwa sababu ni haki yake (na inaruhusiwa kwa mwanamke kuinywa hivyo hivyo) yaani inajuzu (kutoa tone na kupata hedhi), kwani asili yake inajuzu mpaka kutajwa kwa dalili ya uharamu wake. Lakini hakuna dalili ya uharamu huu.”

Al-Bahwati anasema katika kitabu cha Al-Rawd Al-Murabba’: “Inajuzu kwa mwanamke kutoa tone kabla ya siku arubaini kwa dawa”.

Na imetajwa katika kitabu cha Al-Insaf kwa Al-Mardawi: “Inajuzu kunywa dawa ya kutoa tone la manii. Ameitaja rai hiyo katika kitabu cha Al-Wajiyz, na akaiwasilisha hivyo katika Al-Furu”.

Ibn Rajab amesema: “Mwenzetu walisema kwa uwazi kwamba kiinitete kikiganda damu haijuzu kwa mwanamke kukitoa, kwa sababu tayari kimekuwa kiinitete, tofauti na tone ambayo bado halijaganda, na huenda lisiwe kiinitete.”.

Matini yaliyotangulia - ya wafuasi wa Madhehebu haya - yanaonesha wazi ruhusa ya kutoa mimba wakati wa siku arubaini za kwanza za ujauzito, ambayo ni hatua ya tone, na kukataza kwa utoaji mimba wakati wa hatua mbili za kuganda (donge la damu) na kiinitete (pande la nyama).

Haya ni maneno ya Abu Al-Hasan na Al-Lakhmi kutoka kwa w\Wanazuoni wa Madhehbu ya Imamu Malik.

Na ikatajwa katika maelezo mafupi ya Khalil kwa Al-Kharshi: “Na aliyoyataja sheikh huyu yalipokelewa kutoka kwa Abi Al-Hassan nayo ni kwamba inajuzu kutoa tone kabla ya siku arubaini.” Na Al-Adawi akatoa maelezo katika kuhusu maelezo hayo, akisema: “Al-Lakhmi anakubaliana naye.”

Na Sheikh I’lish amesema katika Fatwa zake: “Na Al-Lakhmi peke yake ndiye aliyeruhusu kutoa kilichomo tumboni kutoka kwenye maji ya uzazi kabla ya siku arubaini”.

Nayo ni mtazamo wa baadhi ya wafuasi wa Imamu Shafi; kitabu cha Nihaayat Al-Muhtaaj kwa Al-Ramli: “Al-Muhib Al-Tabari amesema: Wanazuoni wametofautiana kuhusu tone kabla ya kukamilika siku arubaini kwa kauli mbili: Ikasemwa: Hukumu ya kutoa na kuua kwa mimba haithibitiki, na ikasemwa: hairuhusiwi na haijuzu kuiharibu mimba au kuitoa baada ya kutulia katika tumbo la uzazi”.

Madhehebu ya tatu:

Ruhusa ya kutoa mimba katika hatua za tone na kuganda siyo kiinitete.

Haya ni maoni ya baadhi ya wafuasi wa Madhehebu ya Imam Shafi, Al-Karabisi kaisimulia kutoka kwa Abu Bakr Al-Furati. Katika kitabu cha Nihaayat Al-Muhtaaj kwa Al-Ramli: “Al-Zarkashi amesema: Na katika maoni ya baadhi ya watu wema, Al-Karabisi alisema: Nilimuuliza Abu Bakr Ibn Abi Said Al-Furati kuhusu mtu ambaye alimpa mjakazi wake kinywaji ili kutoa mimba yake kuiharibu mimba. Akasema: Maadamu ni tone la manii au pande la damu, inaruhusiwa kwake kufanya hivyo Mwenyezi Mungu akipenda”.

Madhehebu ya nne:

Inaruhusiwa kabisa kutoa mimba kabla ya roho kupulizwa.

Rai hii imefuatwa na wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, Imamu Shafi, Ibn Aqiil na Ibn Abdel Hadi kutoka kwa Wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal.

Ama katika Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa: basi mwenye kuangali katika vitabu vyao ataona kwamba semi za wengi wao zinaonesha kizuizi cha kuruhusiwa kwa kutobainisha chochote kutoka katika kuumbwa kwa kiinitete, lakini walitafsiri hili kuwa ni uumbaji wa sehemu au ukamili wa kiinitete ambacho hakitokei kabla ya roho kupulizwa, na kwamba kuonekana kwa sura yake ndani ya kiinitete kunaonesha kwamba roho ilipulizwa ndani yake hapo kabla; Ibn Al-Hammam amesema katika Sharh Al-Hidaya: “Je, inajuzu kutoa mimba baada ya kutokea ujauzito? Inajuzu maadamu hakijaumbwa chochote kutoka humo, basi zaidi ya sehemu moja wamesema: Na hii haitokuwa mpaka baada ya siku mia moja na ishirini, na hili linahitaji kuwa walikusudia kwa kuumbwa ni kuipulizia roho, vinginevyo ni makosa; Kwa sababu kuumbwa hupatikana kwa kutazama kabla ya kipindi hiki

Na Ibn Abidin ametaja katika maelezo yake ya chini juu ya mkataba wa Al-Faradi: kwamba Wanachuoni wa Fiqhi wa Madhehebu walisema: “Inajuzu kwake kutoa damu maadamu mimba hiyo ni kiinitete au ni donge la damu ambayo hakuna kiinitete kilichoumbwa, na wakakadiria muda huo kuwa ni siku mia moja na ishirini, lakini wakaruhusu hilo kwa sababu bado si binadamu.”

Hata hivyo, basi sharti la kuhalalisha suala hilo, ni kutopoteza haki za mume na mke, maana yake ni kwamba haijuzu kwa mtu kando/mtu wa mbali kutoa mimba ya mke isipokuwa kwa idhini yake na idhini ya mumewe. Ikiwa alifanya hivyo kwa kosa dhidi ya mama, basi lazima alipe fidia iliyokadiriwa na wale wenye uzoefu, na hawalazimishi kulipa fidia. Kwa sababu kwao fidia si wajibu ila kwa yule aliyepuliziwa roho. Vivyo hivyo, ikiwa mke akitoa mimba yake bila idhini ya mume wake, atakuwa amefanya dhambi, na lazima pia alipe fidia. Kwa sababu mume ana haki ya kiinitete, hata ikiwa roho haijapuliziwa ndani yake. Lakini uharamu hapa haukuwa wa kuua kiinitete chenyewe, bali ni kwa ajili ya kupoteza haki ya mwingine bila idhini yake.

Ama kwa Madhehebu ya Imamu Shafi; imekuja katika maelezo ya chini kwa Al-Bajirami juu ya kitabu cha Al-Iqnaa katika muktadha wa kuzungumzia mzozo katika kuruhusiwa kwa kutoa tone baada ya kutua tumboni, akasema: “Na imekubaliwa kuwa haiharamishwi ila baada ya kupulizwa roho”.

Sheikh Al-Qalyubi amesema: “Ndio inajuzu kutoa tone, hata kwa dawa, kabla roho haijapuliziwa ndani yake kinyume na maoni ya Al-Ghazali.”

Mwanachuoni Al-Ramli amesema katika maelezo yake ya Al-Minhaj, baada ya kutaja rai ya Imam Al-Ghazali na mtazamo wake kuhusiana na uharamu wa kutoa mimba: “Rai iliyo sahihi zaidi ni kukatazwa kabisa kwa kutoa kiinitete baada ya roho kukipuliziwa ndani yake, na inaruhusiwa hivyo kabla ya kipindi hicho.”.

Rai ile imefuatwa na Ibn Aqiil na Ibn Abdel Hadi kutoka kwa wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal.

Ama kauli ya Ibn Aqiil, Ibn Muflih ameipokea katika kitabu cha Al-Furu’ pale aliposema: “Na katika sanaa ya Ibn Aqiil: Walikhitalifiana waliotangulia kuhusu kutoa nje manii, na baadhi ya watu wakasema: Hii ni Mawu’dah (msichana aliyezikwa hai) kwa sababu anakata kizazi. Akakanusha hayo, na akasema: Mawu’dah ni baada ya vipindi saba tu, akasoma {Na kwa yakini tumemuumba mtu} mpaka {Kisha tukamfanya kiumbe mwingine} Akasema: Na hii imetoka kwake Mwanachuoni mkubwa, na uchunguzi mzuri kama alivyosikia {Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa (8) Kwa kosa gani aliuliwa? (9)} [AT-TAKWIIR: 8,9] na akasoma {atapoulizwa kwa kosa gani aliuliwa}. Ndiyo inayofanana zaidi na hali, na yenye ufasaha zaidi katika kukemea, na hili ndilo ambalo roho imepuliziwa; Kwa sababu yale ambayo roho haikupuliziwa hayafufuki, basi inafahamika kwamba haikatazwi kutoa tone”

Mada ya pili:

Dalili za Madhehebu na Majadiliano yao, na Rai Iliyo Sahihi Zaidi

Dalili za madhehebu ya kwanza – isemayo kwamba ni haramu kabisa kutoa mimba tangu mwanzo wa kutunga na kuwa pande la nyama katika tumbo la uzazi, na kwamba hairuhusiwi kutoa tone baada ya kutua ndani ya tumbo la uzazi –:

Wafuasi wa Madhehebu hii wametoa dalili zifuatazo:

Dalili ya kwanza: Kwamba kutoa mimba ni kosa dhidi ya kiumbe kilichopo, na viwango vya kwanza vya kuwepo ni kufika manii katika tumbo la uzazi na kuchanganyikana na maji ya mwanamke, na kujiandaa kuukubali uhai na kukiuharibu kiinitete hiki ni jinai. Tulisema msingi wa sababu ya kuwepo katika suala la kufikia manii kwenye tumbo la uzazi, si kwa suala la kutoka kwake kutoka kwa mrija wa mkojo (urethra). Kwa sababu mtoto hakuumbwa kutokana na manii ya mwanamume peke yake, bali kutokana na wanandoa wote wawili, ima kwa maji ya mume na maji ya mke.

Dalili ya pili: Kwamba maji baada ya kufikia ndani ya tumbo la uzazi, basi yanakuwa na uhai, kwa hiyo yana hukumu ya uhai, kama katika yai la mawindo katika Makka. Iwapo mtu ambaye ni mwenye kuingia katika Ihram akivunja yai la mawindo wakati wa hali yake ya Ihram atalipa dhamana;

Kwa sababu asili ya kuwinda ni haramu kwa kwa mwenye kuhirimia kuua, kwani Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo} [AL-MAIDAH: 95],

Basi anapoadhibiwa aliyenunja mayai ya kuwinda, si kidogo kuliko yule mke aliyeyatoa maji hayo bila ya udhuru baada ya kufika katika tumbo la uzazi ni dhambi; Kwa kupima kuleta sababu ya uumbaji wa kiinitete.

Dalili za Madhehebu ya pili - isemayo kwamba inaruhusiwa kutoa tone bila donge la damu na pande la nyama:

Wafuasi wa Madhehebu hii wametoa dalili zifuatazo:

Dalili ya kwanza:

Ikiwa kiinitete kitakuwa donge la damu, haijuzu kwa mwanamke kutoa; kwa sababu kilikuwa tayari ni kiinitete, tofauti na tone, ambalo bado halijaumbwa, na huenda halijaumbwa na kuwa mtoto, hivyo kutoka hapa inaruhusiwa kutoa; kwa sababu hakuna uharamu kwake.

Dalili ya pili:

Kwamba hukumu ya kutoa tone haithibitishi, hivyo inaruhusiwa kuitoa.

Dalili ya tatu:

Hatua ya tone ni tofauti na ile inayokuja baada yake; katika hatua ile, kiinitete bado hakijaanza kuumbwa. Mwanzo wa uumbaji huanza baada ya siku arubaini ya kwanza; kama katika Hadithi ya Hudhayfah Al-Ghifari, hukumu ya hatua zilizo baada yake ni tofauti na hukumu ya hatua iliyo kabla yake.

Dalili za Madhehebu ya tatu - Isemayo kwamba kutoa mimba kunaruhusiwa katika hatua za tone na donge la damu siyo katika hatua ya kuwa pande la nyama:

Sikusoma dalili maalumu kwa rai hii, isipokuwa inaweza kuonekana “mtazamo wa rai hii kutoka kwa: Kiinitete katika hatua ya kuwa pande la nyama kimeanza hatua ya kuumbwa kwake, na baadhi ya viungo vyake vinaonekana, tofauti na hatua mbili za tone na donge la damu, hakionekani kuwa katika hali ya kuumbwa, na kwa hiyo hakuna dhambi katika kutoa mimba katika hatua mbili hizi”.

Rai hii inajadiliwa na ukweli kwamba kiinitete, ingawa katika hatua zake za mwanzo hakuna chochote cha uumbaji wake kinachoonekana, hii haina maana kwamba inaruhusiwa kukitoa; Kwa sababu hatua hii ni mwanzilishi wa uumbaji wa mwanadamu, lau hatukutoa mimba yake, angekuwa mwanadamu ambaye yuko hai.

 

Dalili za Madhehebu ya nne - isemayo kwamba inaruhusiwa kabisa kutoa mimba kabla ya roho kupuliziwa ndani yake:

Wafuasi wa Madhehebu hii wametoa dalili zifuatazo:

Dalili ya kwanza:

Kiinitete katika hatua za kabla ya kupuliziwa roho basi bado si mwanadamu ili hukumu za mwanadamu zithibitishwe kwake, hukumu hizi ni kama vile; uwajibu wa kumtunza, na uharamu wa kumdhuru, kwa hivyo utoaji wake hauzingatiwi kuwa ni jinai, na kwa hiyo hakuna uharamu ndani yake.

Katika Haashiyat Ibn Abidin: “Inajuzu kwa mwanamke kutoa damu maadamu mimba bado pande la nyama au donge la damu ambayo bado hakuna kiungo kilichoumbwa. Wanazuoni wakakadiria muda huo kuwa ni siku mia moja na ishirini, lakini wakaruhusu hilo kwa sababu kiinitete bado si mwanadamu.”.

Dalili ya pili:

Kiinitete ambacho roho yake haijapuliziwa katika wakati huo haiitwi mauaji ya mimba. Kwa sababu mauaji ya mimba yanakuwa katika mwili ambao roho imepuliziwa ndani yake, hili linabainishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa (8) Kwa kosa gani aliuliwa? (9)} [AT-TAKWIIR: 8,9], msichana aliyezikwa hai hataulizwa isipokuwa atakapofufuliwa, na hatafufuliwa isipokuwa roho itakapopulizwa ndani yake, basi kiinitete ambacho roho yake haijapuliziwa hakitafufuka, vile vile haikatazwi kutoa mimba katika hali hiyo - Ibn Aqiil alisema kuwa inaruhusiwa kutoa mimba kabla ya roho yake kupulizwa ndani yake.

Majadiliano ya Dalili:

Majadiliano ya Dalili za wafuasi wa Madhehabu ya nne:

Kiinitete katika hatua za kabla ya kupuliziwa roho basi bado hakijawa mwanadamu ili kithibitishiwe hukumu za mwanadamu, hukumu hizi ni kama vile; uwajibu wa kumtunza, na uharamu wa kumdhuru, kwa hivyo utoaji wake hauzingatiwi kuwa ni jinai, na kwa hiyo hakuna uharamu ndani yake. Rai hii inajadiliwa kwamba hata kiinitete kikiwa bado si mwanadamu, basi ni “mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu”.

Na ikiwa tutakubali kwamba kukidhuru kiinitete kabla ya roho yake kupuliziwa hali hii haiitwi mauaji ya mimba, bali ni kukidhuru kiumbe kilichopo tayari, nacho ni katika hatua za kuumbwa, hatua ya kwanza ni kwamba tone hufikia tumbo la uzazi na kuchanganyika na maji ya mwanamke na kujiandaa kukubali uhai na kuharibu maji hayo ni jinai. Ikiwa maji hayo yakawa pande la nyama na tonge la damu jinai hiyo itakuwa kubwa zaidi, na kama roho ikipuliziwa ndani yake na sura yake ilikamilika jinai hilo litakuwa kubwa sana baada ya kutengana ambapo yuko hai.

Majadiliano ya Dalili za wafuasi wa Madhehabu ya tatu:

Kiinitete katika hatua ya kuwa pande la nyama kimeanza hatua ya kuumbwa kwake, na baadhi ya viungo vyake vinaonekana, tofauti na hatua mbili za tone na donge la damu, na hilo linajadiliwa kwa namna ambayo dalili za wafuasi wa Madhehebu ya nne zilivyojadiliwa: kwamba kiinitete, ingawa katika hatua zake za mwanzo hakionekani chochote katika kuumbwa kwake, hii haimaanishi kuwa inaruhusiwa kutoa mimba. Kwa sababu kiinitete bado ni kianzio cha uumbaji wa wanadamu, lau hatukutoa mimba yake, angekuwa mwanadamu ambaye yuko hai.

Majadiliano ya Dalili za wafuasi wa Madhehabu ya pili:

Dalili hizi zinajadiliwa kwa namna zilivyojadiliwa dalili za rai ya nne, ambayo ni:

Kiinitete kiko bado katika hatua ya tone, ijapokuwa kinatofautiana na hatua zinazokifuata, kwani bado haijaumbwa mimba, isipokuwa bado ni kianzio cha uumbaji wa wanadamu, lau hatukutoa mimba yake, angekuwa mwanadamu ambaye yuko hai.

Na kama tukikubali kwamba kukidhuru kiinitete kabla ya hatua ya kuwa tone hali hii haiitwi mauaji ya mimba, bali ni kudhuru kiumbe kilichopo tayari, nacho ni katika hatua za kuumbwa, kama ilivyotajwa hapo awali na Imam Al-Ghazali katika majadiliano ya dalili za wafuasi wa Madhehebu ya nne.

Rai inayochaguliwa:

Rai inayochaguliwa kwetu kutokana na rai za wafuasi wa Madhehebu ya Wanachuoni wa Fiqhi ni ile iliyowaendea wale wanaosema kuwa ni haramu kutoa tone na kuiharibu bila ya udhuru; kwa sababu dalili zao walizowasilisha, na kwa sababu tone katika tumbo la uzazi imethibitishwa kuwa ni kiinitete; kiinitete kilielezewa hivyo muda wote kilipokuwa tumboni mwa mama yake, na kiliitwa hivyo kwa sababu ya kufichwa kwake, hivyo kulidhuru tone kwa kulitoa kunathibitishwa kuwa ni kukidhuru kiinitete.

Na kwa sababu asili ni kwamba utoaji mimba ni ufisadi na uharibifu, na hukumu ya uharibifu inatofautiana kulingana na kitu kilichoharibiwa. Uharibifu unaweza kuwa wajibu ikiwa madhara yameharamishwa kutumiwa, au ikiwa madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake, na hiyo ni kama: Kuangamiza wanyama wanaoshambulia, ambao wana madhara na sio manufaa. Uharibifu unaweza kuharamishwa ikiwa kitu kilichoharibika ni chenye manufaa au faida yake ni kubwa kuliko madhara yake. Muislamu hana haki ya kuharibu moja ya viungo vyake bila ya haja, na hana haki ya kuharibu mali yake na kuitoa katika hali ya uadilifu na kuipeleka katika hali ya ufisadi bila ya udhuru. Hana haki ya kuua mnyama wake, wala kuharibu chakula chake au nguo zake, ikiwa hakuna haja au ulazima wa kazi hii.

Hapana shaka kwamba kiinitete kinachoumbwa katika tumbo la uzazi la mama, na kitakuwa katika hatua ya kuwa donge la damu na kuumbwa, tayari kinapulizwa roho baada ya muda fulani, kinaweza tu kuainishwa katika mambo yenye manufaa, na hakiwezi kuainishwa katika mambo yenye madhara. Basi kukitoa bila haja ni haramu.

Kwa hivyo, uharamu wa utoaji mimba kabla ya roho kupulizwa ni lazima kwa yale tuliyoyataja katika asili ya kuangamiza vitu vilivyo hai au vilivyokufa, na asili hii isivunjwe isipokuwa kwa dalili.

Hukumu hii ni ya awali, isipokuwa kwamba kuishi kwa kiinitete ni hatari halisi kwa mama, ambapo tunasema kuwa inaruhusiwa kukitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

Sura ya Tatu:

Hukumu ya Utoaji Mimba Kutokana na Udhuru

Mada ya kwanza: utoaji mimba kutokana na uzinzi:

Rai Tuliyochagua kwa ajili ya Fatwa katika suala hili ni kwamba hairuhusiwi kutoa mimba inayotokana na uzinzi, iwe ni kabla au baada ya kupulizwa roho, isipokuwa inapokuwa kuishi kwa kiinitete ni hatari ya uhakika kwa mama, ambapo tunasema kwamba inajuzu kukitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

Dalili ya rai hiyo ni Hadithi ya Ma’iz na Al-Ghamidiyah; Katika yale yaliyopokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Buraida kutoka kwa baba yake:- isemayo: Al-Ghamidiyah akaja akasema, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Nimezini, basi nitakase, na akamrudisha. Ilipofika kesho, Al-Ghamidiyah akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa nini umenirudisha? Labda umenirudisha kama ulivyomrudisha Ma’iz, maana naapa kwa Mwenyezi Mungu nina mimba. Mtume (S.A.W) akasema: “Hapana, basi nenda mpaka ujifungue.” Alipozaa, akamletea mvulana akiwa amevaa nguo, na akasema: Huyo ndiye niliyemzaa. Mtume (S.A.W) akasema: “Nenda ukamnyonyeshe mpaka umuachishe.” Alipomwachisha kunyonya, alimletea tonge la mkate mkononi mwake na akasema: “Huyu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimemwachisha kunyonya, na anakula chakula. Basi yule mtoto akakabidhiwa kwa mwanamume Muislamu, kisha akaamrisha kuchimbiwa shimo usawa wa kifua chake, na akaamrisha watu wampige mawe, basi Khalid Ibn Al-Walid akaleta jiwe na kulirusha katika kichwa chake, na damu ikachuruzika juu ya uso wa Khalid, hivyo akamtukana, hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akamsikia hivyo, akasema: “Subiri, Khaled, naapa kwa Mwenyezi Mungu  Ambaye roho yangu imo mkononi Mwake, yule mwanamke alitubu kweli  Lau mwenye dhambi kubwa sana angetubu kama alivyotubu yeye, angesamehewa.” Kisha akaamuru aswaliwe, na akazikwa.

Na dalili kutokana na Hadithi hii: kwamba Mtume (S.A.W) hakumweleza ikiwa mimba yake ilikuwa katika miezi ya mwanzo – yaani: katika kipindi ambacho roho ilikuwa bado haijapuliziwa ndani ya kiinitete – au baada ya hapo – yaani: katika kipindi ambacho roho ilipuliziwa ndani yake – na ikiwa hukumu itatofautiana kulingana na jambo hili, basi Mtume (S.A.W) atamwuliza. Lakini Mtume (S.A.W), hakufafanua, kwa hiyo hii inaonesha uharamu wa jumla wa kutoa mimba ya mwanamke mzinzi wakati wowote wakati wa maisha ya kiinitete. Na hiyo inatokana na kanuni ya Usuul isemayo: Kuacha kuuliza katika hadithi ya kadhia pamoja na kuwepo uwezekano hupelekea hali ya ujumla katika kusema na kuboresha dalili. Na uwezekano hapa upo, je, kiinitete wakati huo roho yake ilipuliziwa au la? Hata hivyo, Mtume (S.A.W), hakumwuliza, kwa hivyo hii inaashiria ujumla wa hukumu hii ya mambo mawili, kabla au baada ya roho kupulizwa.

Imamu Al-Nawawiy amesema: “Ndani yake – yaani katika Hadithi hii – kwamba mwanamke mjamzito asipigwe mawe mpaka ajifungue, iwe mimba yake ni ya zinaa au vinginevyo, na hili limeafikiwa kwa kauli moja, kisije kikauliwa kiinitete chake. Kadhalika ikiwa adhabu yake ni kuchapwa akiwa mjamzito, hakupigwa mijeledi kwa kauli moja mpaka alipojifungua.

Mada ya pili: kutoa mimba kwa mwanamke aliyebakwa:

Kubaka katika lugha maana yake ni unyang'anyi, inasemekana: kumnyang'anya mtu kwa nguvu, na kumnyang'anya mtu: akachukua mali yake kwa nguvu na kwa dhuluma, hivyo ni mnyang'anyi, na kutoka hapa ikasemwa: Mwanamume alimbaka mwanamke mwenyewe ikiwa amezini naye kinyume na mapenzi yake, na akambaka yeye mwenyewe pia, na ni sitiari nzuri.

Maana ya kiistilahi kwa neno “ubakaji” hapa haitokani na maana ya kilugha, ambayo inakusudiwa kumlazimisha mwanamke kufanya uzinzi bila ridhaa yake.

Hivyo basi, nini maana ya suala letu hili: Hukumu ya kutoa mimba katika tumbo la uzazi la mama yake, kabla ya wakati wake, kwa nia ya kumuondoa, ikiwa ni tunda la ubakaji wa mama huyo, kumaanisha hali ya ubakaji na ya kulazimishwa ilitokea kwake, si kwamba kitendo hicho kilitokea kutoka kwake mwanamke, na ni sawa kama mhalifu alilazimishwa au ilikuwa kwa hiyari yake isivyo haki.

Kwa hiyo, inatoka nje ya mada ya suala letu: Hukumu ya kutoa mimba ya uzinzi, ambayo ni tunda la uasherati wa hiari kwa pande zote mbili, kama ambavyo inatoka hukumu ya kutoa mimba ya kubakwa kwa mwanamke, ikiwa ubakaji huu ulitokana na kitendo cha mwanamke huyo tu, au ulikuwa kwa msaada wake kutoka kwa wengine; Kwa sababu mchanganyiko kati ya masuala hayo mawili (kiinitete cha uzinzi na kiinitete cha kubakwa mwanamke) ni utiifu wa mwanamke na chaguo lake la tendo ambalo matunda yake na matokeo yake ya asili mara nyingi hutengeneza kiinitete, hivyo uchaguzi wake wa tendo hilo lilikuwa chaguo la matunda yake.

Ama suala letu linahusika na hukumu ya kiinitee cha ubakaji alichofanyiwa mwanamke, iwe mhusika alijitolea kwa hiari au kwa kulazimishwa; Kwa sababu mwanamke si mtiifu kwa tendo, kwani hataki tendo au athari yake pamoja, na ikiwa jambo hilo lilikuwa mikononi mwake, tendo hilo lisingefanyika, hivyo kiinitete kisingekuwepo.

Rai Tuliyochagua kuhukumu juu ya suala hili ni kwamba inajuzu kutoa mimba kabla ya siku mia moja na ishirini kupita tangu mwanzo wa ujauzito - yaani katika kipindi cha kabla ya kupulizwa roho - na ni haramu baada ya kupita kwa siku mia moja na ishirini - yaani baada ya kupulizwa kwa roho - isipokuwa ikiwa kuishi kwake ni hatari ya uhakika kwa mama.

Dalili ya kuruhusiwa kwa utoaji mimba - katika hali hii - kabla ya roho kupulizwa ndani yake ni: kuondoa madhara yaliyosababishwa kwa mwanamke aliyebakwa; Na kanuni ni: “Madhara yanaondolewa”, imesemwa: “Madhara hayaondolewi kwa madhara”, tukasema: Tunazingatia ubaya mkubwa kati ya hayo mawili kwa kufanya ubaya mdogo tu, na kanuni ni: “Ikiwa maovu mawili yanapingana, kubwa zaidi yao huzingatiwa kwa kufanya dogo lake”, na katika picha hii inaonekana kwamba madhara ya kutoa mimba ni chini ya madhara ya kuishi kwake. Kwa sababu ya matokeo ya kukaa kwake kwa madhara ya kisaikolojia yanayoendelea na yanayohusiana na mwanamke aliyebakwa, na kile kinachoweza kusababishwa juu yake ya aibu ambayo hana kosa, na pia kuna madhara ambayo yanaweza kusababishwa kwa mtoto mchanga katika siku zijazo; Kwa sababu ni zao la ubakaji na si kosa lake pia; Kwa haya yote, tuliruhusu kutoa mimba kwa kiinitete kilichotokea kutokana na mwanamume huyo kumbaka mwanamke bila ridhaa yake kabla ya roho haijapuliziwa ndani yake.

Haya yote, pamoja na kuwepo kwa upanuzi katika Madhehebu zilizoidhinishwa za Sharia, yanaweza kuamuliwa katika kesi hii pia. Wanachuoni wa Madhehbu ya Imamu Abu Hanafi na Imamu Shafi wanathibitisha kuwa: Kutoa mimba kunajuzu kabisa kabla ya roho kupulizwa, hivyo inajuzu kuwafuata, na hakuna ukanushaji. Kwa sababu: “Halikataliwi jambo ambalo ndani yake kuna kutofautiana, bali linakanushwa jambo lililokubaliwa.” - kama ilivyothibitishwa.

Haikusemwa kuwa haijuzu kutoa mimba kabla ya roho kupulizwa pia, kwa mujibu wa Hadithi ya Al-Ghamidiyah. Kwa sababu Mtume (S.A.W) hakumuuliza kama mimba yake ilitokana na zinaa kwa ridhaa yake au kwa kulazimishwa kwake, hivyo inaeleweka kutoka kwake kwamba kuharibika kwa mimba haijuzu katika hali zote mbili;

Hii ni kwa sababu muktadha wa Hadithi hii unaakisi haya. Al-Ghamidiyah alikuja kwa Mtume (S.A.W) akasema, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Nimezini, basi nitakase, wala hakusema: Nimelazimishwa kuzini. Kwa sababu inajulikana kuwa uzinzi wa kulazimishwa hauadhibiwi hapo kwanza. Ibn Qudamah amesema: “Hakuna adhabu kwa mwenye kulazimishwa kwa mujibu wa kauli ya Wanachuoni wengi”, na Imamu Al-Bukhari akaingiza katika Sahihi yake sura yenye kichwa: “Ikiwa mwanamke atalazimishwa kuzini, basi hakuna adhabu kwake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

{Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.} [AN-NUUR:33],

Na Al-Laith alisema: Nafeh aliniambia kwamba Safiyyah binti Abi Ubaid alimwambia kwamba mtumwa kutoka kwa watumwa wa Imarah alifanya mapenzi na mjakazi mmoja. Basi akamlazimisha mpaka akaondoa ubikira wake, basi Omar akamchapa adhabu yake na kumfukuza, na hakumpiga mjakazi yule kwa sababu tu alimazimishwa.

Al-Zuhri amesema kuhusu mwanamke mjakazi bikira anayeondolewa ubikiri wake na mwanamume huru: Hukumu hiyo inapimwa na bikira mjakazi kwa mujibu wa thamani yake na kupigwa mijeledi, na hakuna faini katika hukumu ya mjakazi asiye bikira, bali anaadhibiwa tu.

Ama kuhusu uharamu wa kutoa mimba ya mwanamke aliyebakwa baada ya kupuliziwa roho ndani ya mimba yake, ni haramu isipokuwa ikiwa kuishi kwake kutaleta hatari ya uhakika kwa mama yake. Hii ni kwa sababu kwa kupuliza roho ndani yake, basi kuharibika kwa mimba kunakuwa ni kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza kuiua isipokuwa kwa uadilifu.

Mada ya tatu: utoaji mimba ya kiinitete chenye ulemavu:

Inawezekana kiinitete chenye ulemavu ambao ulemavu wake ni mdogo au mkubwa.

Ikiwa ulemavu huo ni mdogo, kama ule unaotokea kwenye viungo, au kuchelewa kiakili (mtoto wa Kimongolia), au kuongezeka kwa baadhi ya viungo, basi katika hali hii haijuzu kuitoa, iwe kabla au baada ya kupulizwa roho ndani yake; kwa sababu ya dalili zilizotangulia za kukataza kabisa kutoa mimba, ulemavu huu mdogo hauzingatiwi sababu ya kuruhusiwa kwa jambo hili, ambalo liliamuliwa hapo awali na hukumu yake ni uharamu. Isipokuwa kuishi kwa kiinitete kutakuwa hatari halisi kwa mama, katika kesi hii tunasema kwamba inaruhusiwa kuitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

Ikiwa ulemavu ni mkubwa, ulemavu ambao kiinitete kina uwezekano mkubwa wa kutoweza kuishi baada ya kuzaliwa, au hitajio lake la kudumu la kiwango fulani cha utunzaji ambao ni vigumu kupatika kila wakati, na mifano ya ulemavu mkubwa: kiinitete kisicho na kichwa, au chenye kasoro na ugonjwa mkubwa wa moyo, au magonjwa makubwa ya damu. Hukumu katika kesi hii inakuja katika aina mbili:

Ya kwanza: Kwamba hii iwe kabla ya kupita siku mia moja na ishirini baada ya kushika mimba - yaani, kabla ya roho kupulizwa - na katika hali hii inaruhusiwa kutoa mimba ya kiinitete, kwa mujibu wa ushuhuda wa wataalamu wa kuaminika; Hili linatokana na kanuni ya Kifiqhi: “Ikiwa maovu mawili yanapingana, basi lililo kubwa zaidi kati yao linapaswa kuzimgatiwa kwa kufanya dogo lake.”

Ya pili: Kwamba ulemavu huu mkubwa uligunduliwa baada ya kupita siku mia moja na ishirini tangu mwanzo wa ujauzito - yaani, baada ya kupulizwa roho - na hali hii ni suala la mzozo; Hii inatokana na ugumu wa kubainisha jambo baya kubwa na dogo kati ya maovu mawili, rai tuliyoichagua ni: Kukataza kutoa mimba baada ya roho kupulizwa, hata ikithibitika kisayansi kuwa ina ulemavu, isipokuwa tu ikiwa kuishi kwake ni hatari kwa mama; hii ni kwa sababu kwa kupulizwa roho ndani yake, basi kuharibika kwa mimba kunakuwa ni kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza kuiua isipokuwa kwa haki.

Kwa kuzingatia hilo, uamuzi wa Baraza la Fiqhi la Kiislamu la Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu huko Makka Al-Mukarramah katika kikao chake cha kumi na mbili cha Rajab 15, 1410 Hijiria, ambapo ilisema: Haijuzu kutoa mimba ikiwa imefikia siku mia moja na ishirini, hata ikiwa na ulemavu, ikiwa hakuna hatari iliyothibitishwa kwa mama.

Hitimisho la utafiti na matokeo yake:

Mwishoni mwa utafiti huu, tunakuja kwenye baadhi ya matokeo:

1. Kuharamisha kabisa utoaji mimba baada ya kupulizwa roho, isipokuwa ikiwa uhai wake unaleta hatari kwa mama, ili uhai wa mama uwe katika mizani na uhai wa kiinitete uko katika mizani. Kwa sababu maisha yake mama ni ya hakika na yamethibitishwa mbele yetu, tofauti na kiinitete. Katika kesi hii, tunasema kwa kutoa mimba ya kiinitete; ili kuhifadhi maisha ya mama kutokana na hatari halisi ya kuishi kwa ujauzito.

2. Uharamu wa kutoa mimba kabla ya roho kupulizwa na kusababisha mbegu kutolewa na kuharibika bila ya udhuru. Ikiwa kubaki kwa kiinitete ni hatari ya uhakika kwa mama, basi katika hali hii tunasema inajuzu kukitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

3. Hairuhusiwi kutoa mimba itokanayo na uzinzi, iwe ni kabla au baada ya kupulizwa roho, isipokuwa ikiwa kuishi kwa kiinitete kunaleta hatari ya uhakika kwa mama, ambapo tunasema inajuzu kuitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

4. Inajuzu kutoa mimba ya mwanamke aliyebakwa kabla ya kupita siku mia moja na ishirini tangu mwanzo wa ujauzito - yaani, katika kipindi cha kabla ya kupulizwa roho - na ni haramu baada ya kupita siku mia moja na ishirini - yaani baada ya roho kupulizwa - isipokuwa ikiwa kuishi kwake ni hatari ya uhakika kwa mama.

5. Hairuhusiwi kutoa mimba yenye ulemavu mdogo, iwe kabla au baada ya kupulizwa roho, isipokuwa ikiwa kuendelea kuishi kwa kiinitete kunaleta hatari ya uhakika kwa mama, ambapo tunasema kwamba inajuzu kuitoa; ili kuokoa maisha ya mama.

Na ikiwa ulemavu ni mkubwa, na kuna uwezekano mkubwa kwamba kiinitete hakitaishi baada ya kuzaliwa, au kwamba itahitaji daima kiwango fulani cha huduma ambayo ni vigumu kupatikana katika hali endelevu, basi inaruhusiwa kutoa mimba. kabla ya siku mia moja na ishirini kupita tangu ujauzito - yaani, kabla ya kupulizwa kwa roho - kwa ushuhuda wa wataalamu wanaoaminika. Na haijuzu kuitoa mimba baada ya kupita kwa siku mia moja na ishirini tokea mwanzo wa ujauzito - yaani baada ya kupulizwa kwa roho - isipokuwa kama kuna hatari fulani katika kuendelea kuishi kwake kwa mama.

Na Mwenyezi Mungu ndiye Aliye juu na mjuzi Zaidi, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.

Utafiti huu umeandikwa na / Mustafa Abdul Karim Muhammad 20/7/2009 BK

Share this:

Related Fatwas