Umuhimu wa michezo ya viungo vya mwili
Question
Ni zipi mitazamo ya Sharia ya Kiislamu kwenye michezo ya viungo vya mwili kwa watoto?
Answer
Sharia ya Kiislamu imehimiza kuwafunza watoto michezo yenye manufaa na michezo muhimu ambayo huonesha mielekeo yao kifikra na kuonesha uwezo wao, jambo linalopelekea kuanzisha michezo ya viungo vya kimwili kwa mtoto, hivyo anaweza kuwa na nafasi chanya katika kuhudumia dini yake na jamii yake, kutoka kwa Ibn Omar R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:
“Wafundisheni watoto wenu michezo ya kuogelea na kurusha mkuki….” Hadithi imepokewa na Baihaqy katika mlango wa Imani.