Jinsi ya kuoga kutoka katika hali y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Jinsi ya kuoga kutoka katika hali ya janaba

Question

Mke ni mfanyakazi, na nywele zake ni za aina ya Afro, hivyo anazihudumia nywele zake kwa kuzitengeneza kwa mtaalamu wa nywele kila baada ya siku kumi na tano. Muulizaji anataka kujua hukumu ya kisheria kuhusu jinsi mke wake atakavyotwaharisha mwili wake ili aweze kutekeleza ibada ya Swala, kwa kuwa maji yanaharibu nywele zake. Hivyo, mke huyu haoshi nywele zake isipokuwa anapokwenda kwa mtaalamu wa nywele, yaani kila baada ya wiki mbili.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Inavyojulikana katika Fiqhi ya Hanafi, ni lazima kupangusa nywele kwa maji wakati wa kutia udhu, lakini katika hali ya kujitwaharisha kutokana na janaba, hedhi, au nifasi, ni lazima maji yafike kwenye mizizi ya nywele na kwenye ngozi ya kichwa. Na hakuna haja ya kufumua misuko ya nywele ikiwa zimesukwa. Katika tukio linalohusiana na Swali hili, tunasema kwa mleta swali kwanza: Hairuhusiwi kisheria kwa mwanaume kumruhusu mke wake kwenda kwa msusi kabisa; kwa sababu nywele za mwanamke ni tupu (faragha) na hazipaswi kuoneshwa wala kuangaliwa na mtu asiye kuwa mume wake. Zaidi ya hayo, ni haramu kwa msusi wa nywele kumgusa au kumtengenezea nywele mke wa mtu mwingine. Hali hii si ya kimaadili kwa mwanamke mcha Mungu, ambaye hapaswi kuonesha nywele zake wala kwenda kwa mtaalamu wa nywele kumtengenezea. Ikiwa alifanya hivi, basi ametenda kosa kubwa.

Hii ni ikiwa msusi ni wa jinsia ya kiume. Na mke wa muulizaji ni lazima apanguse nywele zake kwa maji wakati wa kutia udhu, vinginevyo udhu wake hautakuwa sahihi kisharia. Ama kuhusu kujitwaharisha kutokana na hedhi, nifasi, na janaba, ni lazima maji yafike kwenye mizizi ya nywele na kwenye ngozi ya kichwa, bila kujali athari zitakazotokea. Bila ya hivi twahara yake haitotimia. Kutokana na hayo, tunapata jibu ikiwa hali ni kama alivyoeleza muulizaji.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas