Umri wa Kukoma Hedhi na Kuzaa

Egypt's Dar Al-Ifta

Umri wa Kukoma Hedhi na Kuzaa

Question

Ni upi umri wa kukatika hedhi kwa mke, na umri wa kuzaa kisharia?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mwenyezi Mungu Anasema: {Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi}[Al-Talaq, 4]. Aya imebainisha kwamba eda ya wanaweke waliokoma hedhi au ambao hawapati hedhi kabisa kwa umri wao kuwa mdogo au amefikia umri wa kupata hedhi,, basi eda yao ni miezi mitatu tangu kuachika, na wanazuoni wametofautiana katika umri wa kukoma hedhi kama ifuatavyo:

Katika Madhehebu ya Hanafi: Mwanamke aliyekoma hedhi ni yule aliyefikia miaka hamsini na tano, na hii ndio kauli inayotolewa Fatwa, na kuna kauli nyingine.

Na katika Fiqhi ya Malik: Kwamba umri wa kukoma hedhi ni miaka sabini, na kati ya miaka Hamsini mpaka sabini hurejewa wanawake wenye uzoevu, na wengineo pale itakapokuwa damu inayotoka kwa mwanamke ni damu ya hedhi au nyingine.

Na katika Fiqhi ya Shafi mwanamke aliye liyekoma hedhi ni yule aliyefikia miaka sitini, na hii ndio kauli sahihi zaidi kwao.

Na katika Fiqhi ya Imamu Ahmad: Mwanamke aliekoma hedhi ni yule aliefikia miaka hamisini na tano na damu ya hedhi ikakata, na itachukuliwa kauli yake katika kukatika damu ya hedhi au kutoka, na atasadikishwa akidai kuiona damu ya hedhi katika umri huu Pamoja na kutaja alama zake, na ataapa kiapo cha Yamini kwa kutaka amkasirikie akiwa hatamuamini katika madai yake. Mwanamke anayekaa eda akiwa amefikia muda wa kukoma damu ya hedhi, kwa kawaida anakuwa hawezi kuzaa, kutokana na kukatika damu ya hedhi, mwanamke anakuwa anaweza kuzaa kuanzia kubaleghe kwake na anasimama kikawaida anapokoma hedhi, na hutofautiana kati ya mwanamke na mwingine, na Mwenyezi Mungu Anasema: {Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza}[Ash-Shouraa, 49: 50]. Na Amesema: {Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.  Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua} [Al-Dhariyat, 24: 30].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas