Mke Kujizuia Kulala Kitandani Pamoja na Mumewe.
Question
Mke akiwa amegombana na mumewe kisha akakataa kulala naye kitanda kimoja, je jambo hili linakubalika? Kwa kuzingatia kwamba sababu ya kukataa kwake ni kuwa mumewe anamtaka kila mara, naye mke huwa analalamikia tabu azipatazo za kuihudumia nyumba na watoto mchana kutwa, na pia matamanio yake huwa yako mbali tofauti na mumewe. Nini kifanyike? Je mke akiongea na mumewe kwa jeuri atapata adhabu ya moto?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mume ana haki kwa mkewe kama ambavyo mke ana haki kwa mumewe, na hukumu za kisheria haziangalii namna kama hii (iliyotajwa hapa) ambayo kila mmoja anajivutia upande wake kihoja na kumuona mwingine kuwa ana makosa, na kuifanya Dini iwe ni njia ya kumkandamiza mwenziwe na kupata mahitaji yake bila ya kutekeleza wajibu wake ambao analazimika kuutimiza. Maisha ya ndoa yamejengeka kwa msingi wa utulivu, upendo, huruma na kuchunga zaidi hisia za upande wa pili kuliko hata kujengeka kwake (ndoa) kwa kutaka haki. Na kwa mujibu wa tabia njema alizotufundisha Mtume (Rehma na amani zimshukie) mke anapaswa kumuogopa Mwenyezi Mungu juu ya haki za mumewe na aelewe kuwa kutangamana nae kwa wema na kumvumilia ni katika milango ya kuipata pepo.
Na kama ilivyokuwa ni katika mambo ya halali ya kujistarehesha ambayo mwanamke hapaswi kumzuia mumewe, na wala hapaswi kumuonesha mume wake kuwa ana nafasi ya mwisho katika mambo anayoyapa umuhimu. Naye mume anatakiwa achunge sana udhaifu wa mkewe na tabu azipatazo katika kuitunza nyumba yake mchana kutwa pamoja na kuwalea watoto, na awe mume mwenye huruma na asimbebeshe mkewe asiyoyaweza. Hizi ndizo hisia za kweli wanazotakiwa kuhisiana wote wawili, wanandoa katika kutimiza wajibu wao na kusimamia matakwa ya Mwenyezi Mungu yanayowawajibikia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
