Mke Hupewa Jina la Familia ya Mume....

Egypt's Dar Al-Ifta

Mke Hupewa Jina la Familia ya Mume.

Question

Ndoa katika Ufaransa inampa mke jina la mumewe, mtazamo wa Dini ni nini kuhusu suala hili? Je, ni kosa kama Muislamu akifanya hivyo ? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Katika desturi ya Magharibi kama binti hakuolewa, basi jina lake linaunganishwa na jina la baba yake na familia yake, lakini kama akiolewa, jina lake linaongezwa na jina la familia ya mumewe, hivyo ni kumfahamisha kuwa ameolewa kwa istilahi inayofahamika katika lugha zao kuwa ameolewa kama vile ; Mrs au Madam nk. Basi huongezwa jina la familia ya mumewe ni kama tunaposema “Mwanamke fulani ameolewa na mmoja wa familia fulani”, kwa hivyo, hali hii ni aina ya kufahamika kwa mwanamke kwa mujibu wa mila na desturi zao, na aina ya kufahamika ni nyingi, kama tunaposema: Ikrima mtumwa wa Ibn Abbas, au kupitia kazi, kama vile; Al-Ghazzali, yaani anayefanya katika kazi ya kusuka nyuzi, au pengine kujulikana kwa jina la utani, kama vile; Al-Araj yaani kilema, na Al-Jahidh; na wakati mwingine hunasibishwa na jina la mama yake ingawa baba yake anajulikana, kama vile ; Ismail Ibn Ulaiyah. Na pengine kumfahamu mwanamke kwa kuongeza jina la mumewe kama ilivyotajwa katika Qur`ani Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mke wa Nuhu na mke wa Lut'i}[AT TAHREM 10], {Mkewe Firauni}[AT TAHREM 11], na imepokelewa kutoka kwa Bukhari na Muslim kutoka Hadithi ya Abi Said Al-Khudry R.A. kuwa Zainab mkewe Ibn Masud R.A alikuja ili kuomba ruhusa ya Mtume S.A.W. Akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu ni Zainab anaomba ruhusa, akasema : Zainab nani ? akaambiwa: Zainab mkewe Ibn Masud, akasema: “Naam mwambie karibu”, akaambiwa karibu.

Kilichopigwa marufuku kwa mujibu wa Sharia ni kwamba mtu anachukua jina la asiye baba yake, kwa matamshi ya uana, na pengine jambo hili linaenezwa katika baadhi ya pahala au katika baadhi ya hali, na baadhi ya wakati linakuwa kama jambo la kawaida, na hakuna ubaya katika jambo hili muda wakuwa haipelekei kuchukua jina ambalo Sharia imekataza, nao ni kuchukua jina la uana la asiye baba yake. Vile vile jambo hili halizingatiwi ni kujifananisha kulikokatazwa na Sharia, kwa sababu kujifananisha kulikokatazwa na Sharia ni lazima kuwepo masharti mawili: Liwe jambo la kujifananisha limekatazwa kisharia na awe mwenye kutenda tendo hili amekusudia kuiga linalokatazawa kwa Sharia. Ikiwa moja ya masharti mawili halijatekelezwa, basi mwenye kutenda tendo hili halaumiwi kwa mujibu wa Sharia ; dalili ya hivyo ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Muslimu(624) kutoka kwa Jabir Ibn abdullah R.A alisema: Mtume S.A.W aliumwa, tukaswali nyuma yake naye ameketi, akageuka kwetu akatuona tumesimama, akatuashiria tuketi, tukaketi, alipomaliza Swala akasema: “Mmekuwa karibu ya kuwaiga Waajemi na Warumi; walikuwa wanasimama mbele ya Wafalme wao wakati ambapo wafalme wameketi, kwa hivyo, mfuateni Imamu wenu ; akiwa anaswali hali ya kuketi chini, salini hali ya kuwa mmeketi”. Ingawa masahaba waliwaiga Waajemi na Warumi katika kitendo hiki lakini hawakukusudia kuwaiga, kwa hivyo wasifu wa kuiga umeondoka.

Kwa hivyo, Ibn Najm Al-Hanafi alisema katika kitabu cha [Al-Bahrur Raiq 2/11]: “Jua kwamba uigaji wa Watu wa Kitabu hauchukiwi katika hali zote, tunakula na tunakunywa kama wanavyofanya, lakini uigaji unaokatazwa ni uigaji mbaya uliokusudiwa tu”. Hakuna katika kupewa jina la familia ya mume kwa mkewe kukanusha uwana wake kwa baba yake, lakini ina maana ya kumpambanua mwanamke huyo kama ilivyotajwa hapo juu.

Sababu ya kufanana na uharamu hapa ni kufuta neno la “Ibn” kati ya jina la mwana na baba yake, na hali hii japokuwa inawezekana kuwa kuondoshwa neno la Ibn ni kwa ajili ya kupunguza tu, lakini jambo hili limesababisha kuchanganya katika majina. Kwa hivyo, kuna baadhi ya mashirika rasmi yalitoa wito kufutwa majina ya kunasibisha kwa sababu yanachanganyika uana kati ya majina mawili ya kunasibisha, kwani hali ya kufuta kwa neno la “Ibn” kati ya jina la mwana na baba yake ilikuwa jambo la kawaida tu. Kwa hivyo, hakuna kitu kibaya katika kuongeza jina la kupewa la familia ya mume kwa mkewe katika jamii ambayo ilizoea hali hii, kwani mke huyo hufahamika kuwa ameolewa kwa kuongeza neno la Mrs au Madam kabla ya jina lake. Wakati ambapo jambo hili halipinganin na Sheria, hakuna kitu kibaya kama tukifanya hivyo.

Sheria Tukufu ilizingatia mila na desturi za jamii zikiwa hazipingani nayo. Kwa hivyo, Wanavyuoni wa Fiqhi walisema: “Desturi inazingatiwa”, Sheria haikuwataka Waislamu kuasi desturi za jamii zao au kuzipinga, ili kuwaunganisha katika jamii zao na wasijitenge nazo, ili waweze kuishi na kulingania kwa ajili ya Dini iliyo sahili pasipo na migogoro yeyote na pasipo na kupingana na msingi miongoni mwa misingi ya Sheria.    

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas