Mke wa Baba ni Haramu Kuoa
Question
Ipi hukumu ya kisharia ya mke wa baba kuwa ni haramu? Je, inajuzu kwangu kusafiri na kuwa peke yangu na mama yangu wa kambo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ibn Qudamah katika “Al-Mughni” amesema: “Mwanaume ameharamishwa kuoa mke wa baba yake, awe yuko karibu au mbali, mrithi au la, kwa damu au kwa kunyonyesha. Kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita} Al-Baraa’ibn A’zib akasema: “Nilikutana na ami yangu naye alikuwa na bendera: Nikasema: Unataka kwenda wapi? Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amenituma kwa mtu aliyemwoa mke wa baba yake baada ya kifo chake, ili nimpige shingo yake au nimuue. Imepokelewa kutoka kwa Al-Nasa’i. Katika mapokezi mengine, amesema: Nilikutana na ami yangu Al-Harith Ibn Amr, naye alikuwa na bendera, na akataja Hadithi kwa njia hii. Imepokelewa kutoka kwa Saeed na wengineo. Haijalishi ikiwa ni mke wa baba yake au mke wa babu yake mzaa baba au babu yake mzaa mama, awe wa karibu au wa mbali. Hakuna tofauti baina ya Wanavyuoni juu ya jambo hili tunalolijua.
Inajulikana kutokana na hayo hapo juu kwamba mama wa kambo ni haramu kabisa kuolewa, na kwamba hili ni suala la makubaliano baina ya Wanavyuoni.
Kwa hiyo, ni haramu kuoa mke wa baba, na inajuzu kusafiri naye na kuwa peke yake naye.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
