Kuweka Qur’ani Tukufu iliyorekodiwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuweka Qur’ani Tukufu iliyorekodiwa kumsubirisha mteja (Waiting tone)

Question

Kisomo cha Qur`ani Tukufu kinawekwa katika simu ya kumsubirisha mteja aliyepiga simu katika shirika letu, mteja anasikiliza Qur`ani Tukufu mpaka atakapohudumiwa, hukumu ya hili nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Qur`ani Tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo Ameyateremsha kwa Mtume wake bora zaidi wa viumbe bwana wetu Muhammad S.A.W., na tumeamrishwa kuiheshimu na kuitukuza na kuamiliana nayo vizuri tofauti na tunavyoamiliana na kitu kingine; haiguswi isipokuwa na mtu aliyetaharika na hadathi kubwa na ndogo kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. Hapana akigusaye ila walio takaswa} [Al Waqiaa:77-79]. Pia hakujuzu kuweka kitabu juu ya msahafu; kwa sababu Qur`ani Tukufu inakuwa juu wala haiwi chini ya chohote, na ubora wa maneno ya Mwenyezi Mungu ni kama ubora wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake. Hivyo basi si sahihi wala si adabu kuiweka sehemu kama hizi; kwa sababu ina utukufu wake unaotukataza kufanya hivyo {Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.}. [ Al Hajj: 32], Pamoja na yale ambayo yanaweza kutokea katika kukatiza aya na kuharibu maana, na wakati mwingine kugeuza maana pale inaposimama kwa ajili ya kumjibu mteja.

Na kunawezekana badala yake kuweka kasida za kumsifu Mtume S.A.W., ama maneno ya Mwenyezi Mungu yana utukufu wake na umaalumu katika kushughulika nayo.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas