Kutoa Zaka Mali Iliyohifadhiwa kwa ajili ya Ndoa
Question
Ninaweka sehemu ya mshahara wangu ili kununua mikufu na bangili za dhahabu kwa mabinti zangu ili niviuze baadaye na viwasaidie katika maandalizi ya ndoa. Je! Inapasa Zaka katika pesa hiyo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Makusudio ya aliyeuliza katika ibara yake “Ili kununu mikufu na bangili za dhahabu kwa mabinti zangu” kwa sababu atawapa hii mikufu na bangili kama zawadi, Fatwa iliyotolewa katika mapambo ya wanawake ambayo ni dhahabu iliyoandaliwa kwa ajili ya mapambo, ni kwamba havitolewi Zaka; na haya ni Madhehebu ya Jamhuri ya Wanazuoni isipokuwa Madhehebu ya Hanafi, na hata Madhehebu ya Hanafi ni kwamba katika sharti la kupasa Zaka ya mali ni kufikia kiwango na kuzungukiwa na mwaka kuwa imezidi katika mahitaji ya asili, mali iliyoandaliwa kununua mahitaji asilia hakuna zaka katika mali hiyo; kwa sababu mwenye mali yake hajatosheka nayo, bali mali hiyo ni katika mahitaji yake ya lazima, na mahitaji ya msichana katika ndoa yake yanazingatiwa kuwa ni katika mahitaji ya muhimu, na Mwenyezi Mungu Anasema: {Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi}[Al-Baqara, 219], nacho kilichozidi katika mahitaji ya mtu na famili yake, na Mtume S.A.W. anasema: “Hakuna sadaka isipokuwa kwa kile kilichotosheleza” imepoekelewa na Ahmad, na hii pia imepokelewa na Bukhari kwa maana yake, na wameifasiri Wanazuoni kuwa ni mahitaji ya msingi kwa kuwa: “Ni yale ambayo yanampelekea mwanadamu kuangamia kwa uhakika, nyumba, vifaaa vya kivita, mavazi ya kipindi cha kiangazi au kipindi cha baridi, au kwa kukadiria: kama deni; kwa mdaiwa anahitajika kulipa deni lake kwa alicho nacho katika kiwango cha Zaka ili kuepuka kifungo ambacho ni kuangamia. Akiwa na pesa ambayo anatakiwa kuitoa katika mahitaji atakuwa kama yule ambaye hana pesa; kama ilivyokuwa kwa maji yaliyoandaliwa kwa kiu anakuwa kama aliyekosa maji, kunajuzu kwake kutayammamu” maneno haya kutoka katika Hashia ya Ibn Abdin.
Na ikiwa makusudio katika ibara hii ni kwamba anajinunulia mwenyewe kwa ajili ya mabinti zake, linaashiriwa hilo na kauli yake: “Ili niviuze baadaye”; kwa namna yeye hamiliki kuuza anachomiliki mabinti zake, bali huenda wakazitumia mabinti zake kwa namna moja au nyingine, basi ni haramu kwake hilo; kwa sababu kanuni ya kisharia inasema: kilicho haramu kukitumia ni haramu kukihifadhi, dhahabu ni miongoni mwa vitu ambavyo ni haramu kwa wanaume kuvitumia, basi ni haramu kwao kuihifadhi, na hapo inapasa Zaka kwa rai ya jamhuri ya Wanazuoni, lakini haipasi Zaka kwa rai ya Madhehebu ya Hanafi, kwa yaliyotangulia kuyasema.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
