Kukutana mwanamke na mwanamume chumba kimoja kazini
Question
Ni ipi hukumu ya kukutana mwanamke na mwanamume katika chumba kimoja kazini?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hakuna kizuizi kisharia kuwepo mfanya kazi wa kiume na mwenzake wa kike kazini katika chumba kimoja, ikiwa chumba hakikufungwa au katika hukumu ya faragha, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Asikae faragha mwanamume na mwanamke isipokuwa pamoja Mahrim” imepokelewa na Bukhari.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
