Uharamu wa kumwoa mke wa baba

Egypt's Dar Al-Ifta

Uharamu wa kumwoa mke wa baba

Question

Ni nini hukumu ya kumwoa mke wa baba? Je, inaruhusiwa kusafiri na mke wa baba na kuwa naye faraghani?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Qudamah katika kitabu chake "Al-Mughni": "Ni haramu kwa mwanaume kumuoa mke wa baba yake, awe wa karibu au wa mbali, mrithi au si mrithi, kwa nasaba au kwa kunyonya; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Wala msioe wale ambao baba zenu waliwaoa katika wanawake, isipokuwa yaliyokwisha pita} [An-Nisaa: 22], naye Al-Baraa binAazib amesema: “Nilikutana na mjomba wangu akiwa na bendera, nikamuuliza: Unaelekea wapi? Akasema: Amenituma Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kwa mtu aliyeoa mke wa baba yake baada ya (baba yake kufariki), ili nimpige shingo yake – au: nimuue” (Imepokewa na An-Nasa’i). Na katika riwaya nyingine alisema: “Nilikutana na baba yangu mdogo Al-Harith bin ‘Amr akiwa na bendera...” kisha akasimulia habari hiyo pia. Imepokelewa na Sa’id na wengineo. Na ni sawa katika hili mke wa baba au mke wa babu wa upande wa baba au wa upande wa mama, iwe wa karibu au wa mbali, ambapo hakuna tofauti baina ya Wanazuoni waliotangulia katika jambo hili ambalo tunalijua" Mwisho wa nukuu.

Kwa hiyo, imebainika kutokana na maelezo yaliyotangulia kuwa mke wa baba ni haramu milele (kuoa kwake), na hilo ni kwa makubaliano ya Wanazuoni wote.

Kwa msingi huo, wewe ni mahramu kwa mke wa baba yako, na inakubalika kusafiri naye na kuwa naye faragha.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas