Kumwombea dua marehemu kwa kusema: ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwombea dua marehemu kwa kusema: "Ee Mwenyezi Mungu, mjaalie makazi yake kuwa Peponi"

Question

Ni hukumu gani katika kmwuombea dua marehemu kwa kauli: "Ee Mwenyezi Mungu, mjaalie makazi yake kuwa Peponi"? Watu wengine hudai kwamba neno "makazi" (MATHWA) ni maalumu kwa Jehanamu na adhabu, na kwamba maneno "sehemu pa kupumzika (Mustaqar) "  na "mafikio (Al- Maawaa)" ni maalumu kwa Pepo na Neema.

Answer

Kuombea marehemu kwa kauli, "Ee Mwenyezi Mungu, m mjaalie mkazi yake kuwa Pepo," ni halali kulingana na Sharia ya Kiislamu, kwani hakuna madhara katika kutumia neno "makazi (Mathwaa)" pamoja na Pepo katika dua, iwe kwa mtazamo wa Kiislamu au wa kilugha.

Madai kwamba maneno "makazi (Al-Maawaa)" au "mafikio (Mathwaa)" ndiyo maneno pekee sahihi ya kutumia kwa ajili ya Pepo, badala ya "sehemu pa kupumzika," si sahihi na ni kinyume na matumizi ya maneno haya katika Qur`ani Tukufu, ambapo yanapatikana katika sehemu kadhaa pamoja na Pepo na Moto.

Maelezo

Inapendekezwa katika Uislamu kumwombea marehemu rehema na msamaha na kwamba Mwenyezi Mungu Amwingize Peponi. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah(R.A). kwamba Mtume (S.A.W) amesema: "Mtu anapofariki, amali zake hukoma isipokuwa mambo tatu: sadaka ya yenye kuendelea, elimu yenye manufaa, au mtoto mwema anayemwombea dua." imepokewa na Muslim. Kwa hivyo, Wanazuoni wamesema: "Thawabu ya dua huwafikia waliofariki, kama vile sadaka..."

Kuhusu baadhi ya watu kukataza kuombea waliofariki kwa kauli "Ee Mwenyezi Mungu, mjaalie makao yake kuwa Peponi," wanadai kuwa neno "makao (Mathwaa)" ni maalumu kwa Moto, kwa sababu Mwenyezi Mungu Anasema: { Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanao takabari?} [Az-Zumar: 60], na kwamba neno " sehemu pa kupumzika (Mustaqar) " au "hifadhi" ni maalumu kwa Pepo, kama Mwenyezi Mungu Anavyosema: { Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazi bora na mahali penye starehe nzuri} [Al-Furqan: 24], na Anasema: {Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake} [An-Nazi'at: 41].

Jibu la madai haya, tunasema: Hii ni kauli ya uongo isiyo na ushahidi wowote unaoithibitisha, kwa sababu maana za maneno "makazi," "mafikio," na "hifadhi" zinazunguka katika dhana moja, ambayo ni: hali, nyumba, au sehemu pa kuishi, iwe sehemu hapo ni Pepo au Moto. Qur`ani Tukufu imetumia maneno haya sambamba na Pepo na Moto katika sehemu kadhaa, ikiwemo:

Kwanza: Ambapo yanatumiwa yakiambatanishwa na Moto na adhabu:

- Mwenyezi Mungu Anasema: {Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua} [Al-An'am: 128]

- Na Akasema: {Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi!} [An-Nahl: 29].

- Na Akasema: { Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. } [Al-Furqan: 65-66].

- Na Anasema: { Basi ama yule aliye zidi ujeuri,  Na akakhiari maisha ya dunia, Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!} [An-Nazi'at: 37-39].

Pili: Sehemu ambapo yanatumiwa yakiambatanishwa  na Pepo na Neema:

- Mwenyezi Mungu Anasema kwa ulimi wa Aziz wa Misri: {Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makaazi ya hishima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu.} [Yusuf: 21].

- Na Mwenyezi Mungu Anasema kupitia maneno ya Yusuf A.S: {Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewa} [Yusuf: 23].

- Na Akasema: {Hao ndio watakao lipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo maamkio na salamu.  Wadumu humo - kituo na makao mazuri kabisa} [Al-Furqan: 75, 76].

- Na Akasema: {Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,  Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!  } [An-Naziat: 40-41].

Tunapata Faida kutokana na yaliyotangulia:

1- Kumwombea marehemu kwa kauli, "Ee Mwenyezi Mungu, mjaalie makazi yake yawe Peponi," ni halali kulingana na Sharia ya Kiislamu.

Hakuna tatizo lolote kutumia neno "makazi (Mathwaa)" pamoja na Pepo katika dua, si kwa mtazamo wa kidini wala wa kilugha,  Kwa hakika, Qura`ni Tukufu imelitumia katika sehemu kadhaa pamoja na Pepo na Moto.

3. Dai kwamba maneno "ma'wa" (hifadhi) au "mustaqar" (makazi) ndiyo maneno pekee sahihi ya kutumia kwa Pepo, badala ya "muthaw", ni ya uongo na si sahihi, kwani Qur`ani Tukufu imetumia maneno haya katika sehemu kadhaa sambamba na Pepo na Moto.

Share this:

Related Fatwas