Kuboresha mwonekano wa meno ili yaonekane vizuri wakati wa kucheka
Question
Ni nini hukumu ya kidini kuhusu kupunguza nafasi kati ya meno (kubana meno) na kuyafanyia marekebisho ili kuboresha mwonekano wake yaonekane vizuri wakati wa kucheka?
Answer
Kupunguza nafasi kati ya meno (kuyabana meno) kulikokatazwa ni kule kunakofanywa kwa lengo la kuonekana kijana zaidi na kuongeza urembo na uzuri tu, hii ni kwa sababu kuna udanganyifu, na kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
Ama ikiwa ni kwa lengo la matibabu, kuficha kasoro, na kuboresha mwonekano wa meno, basi inaruhusiwa kisharia na haina neno, ikiwa mtu anahitaji kurekebisha meno yake kwa sababu ya mwonekano mbaya au ugonjwa uliyoasiri meno hayo, basi hakuna ubaya.
Maelezo
Mwenyezi Mungu amemkirimu mwanadamu juu ya viumbe vingine vyote.
Mwenyezi Mungu Amesema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu}[Al-Israa: 70]. Pia Amesema: {Hakika tumemuumba mtu katika umbo lilio bora kabisa} [At-Tin: 4]. Na Akasema: {Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakutieni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na kwake ndio marejeo} [At-Taghabun: 3].
Sharia imetuhimiza kusafisha meno, kuondoa uchafu, na kufanya harufu ya kinywa iwe nzuri. Mtume S.A.W. amesema: (Mswaki ni usafi kwa kinywa na ni radhi kwa Mola)[1]; hadithi hii inaonyesha kupendekezwa kwa kutumia mswaki, hii ni kwa sababu mswaki husafisha kinywa na huleta radhi za Mwenyezi Mungu kwa anaefanya hivyo.
Hukumu ya suala la kurekebisha meno inatofautiana kulingana na kusudio (nia), kama ifuatavyo:
Kwanza: Ikiwa lengo ni kuonekana kijana zaidi na kuongeza urembo na uzuri: Jambo hili ni Haramu kisharia; hii ni kwa sababu linahusisha udanganyifu na kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, jambo ambalo limekatazwa kubadilisha umbile kwa namna inayoashiria kupinga kile alichokadiria Mwenyezi Mungu huhesabika kuwa ni kazi ya Shetani.
Mwenyezi Mungu amesema: {…na nitawaamrisha, basi bila ya shaka watabadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu…} [An-Nisa: 119].
Mtume (S.A.W). amesema: ((Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wanaojichora tatuu na wanaochorwa, na wanaopunguza nyusi, na wanaopunguza nafasi kati ya meno kwa ajili ya urembo, wanaobadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu))[2]. maandiko haya yanaonesha kuwa mambo hayo yote ni haramu kwa sababu Mtume (S.A.W.) amewalaani wafanyao hilo, na hairuhusiwi kumlaani mtendaji wa jambo lililo halali.
Pili: Ikiwa lengo ni matibabu ya ugonjwa, au kurekebisha mwonekano mbaya, au kuondoa kasoro (kama jino moja kuwa refu kuliko mengine):
Jambo hili linaruhusiwa kisharia, na halichukuliwi kama kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu kwa sababu zifuatazo:
Inaingia chini ya amri ya kutafuta matibabu ambayo Mtume (S.A.W.) amehimiza kwa kusema: ((Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha maradhi na dawa, na akaweka dawa ya kila ugonjwa, basi jitibuni, wala msijitibu kwa haramu))[3]. Na imepokewa kutoka kwa Usama bin Sharik amesema: ((Mabedui walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwani hatujitibu? Akasema: Ndiyo, enyi waja wa Mwenyezi Mungu, jitibuni ; kwani hakika Mwenyezi Mungu hakuweka ugonjwa ila ameuwekea na shifaa (ponyo) —au alisema: dawa— isipokuwa ugonjwa mmoja tu. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi huo? Akasema: Uzee (ukongwe).)) Imepokelewa na At-Tirmidhi.
Kulingana na kanuni ya kisheria isemayo: "Dhara huondolewa" Kurekebisha meno katika hali hii husaidia kuondoa madhara ya kimwili na kisaikolojia yanayompata mtu kutokana na mwonekano mbaya wa meno yake.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia: kwa mambo mawili:
Ni haramu kurekebisha meno ikiwa lengo ni kuonekana mdogo na kuongeza uzuri tu.
Inaruhusiwa kurekebisha meno ikiwa lengo ni matibabu, kuficha kasoro, au kuboresha mwonekano wenye hitilafu.
[1] Imepokelewa na Annasaiy
[2] Imepokelewa na Bukhary na Muslim.
[3] Imepokelewa na Abou Dawoud.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
